Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele Septemba 19, 2025 ametembelea Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika Majimbo ya Uchaguzi ya Mbeya Mjini na Uyole na kupokea taarifa ya mkoa kutoka kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Jaji Mwambegele pia alipata fursa ya kutembelea kampeni za wagombea Ubunge wa chama cha CUF na CCM katika majimbo hayo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume,Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mbeya ambapo alisisitiza uadilifu wakati wa utendaji kazi wao.Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.










Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Septemba 19,2025 katika Viwanja vya Mabela.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe Lucy Thomas Mayenga akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa 31 wa Umoja wa Mabaraza ya Kitaifa Duniani (IPU) Mhe.Dr Tulia Ackson na Wananchi wa Wilaya hiyo mnamo Septemba 19,2025 katika Viwanja vya Mabela.
Mgombea Udiwani Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Joel Ndettoson kwatiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa 31 wa Umoja wa Mabaraza ya Kitaifa Duniani (IPU) Mhe.Dr Tulia Ackson na Wananchi wa Wilaya hiyo mnamo Septemba 19,2025 katika Viwanja vya Mabela.





































