Saturday, 13 September 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 13,2025

Magazeti

 
   

Share:

Friday, 12 September 2025

MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAONGEZEKA NCHINI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha.Felchesmi Mramba ameeleza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia nchinj yameongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 20.3 huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 80 ndani ya miaka 10, ambapo hadi sasa imebakia miaka 9.

Mha. Mramba ameyasema hayo Septemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililoandaliwa na kampuni ya Mwananchi kwa ushirikiano na Wizara ya Nishati pamoja na wadau mbalimbali likibebwa na kaulimbiu ya ‘Nishati safi ya Kupikia Okoa Maisha, Linda Mazingira.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mha. Mramba amesema “Nishati Safi ya Kupikia siyo jambo la kinadharia bali ni jambo linalohusu maisha, mazingira na uchumi huku msingi wake mkuu ukiwa ni kulinda afya, mazingira pamoja na maendeleo jumuishi.”

Aidha, Mhandisi Mramba ameendelea kuwahamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia akikumbusha kuwa, takwimu zinaonesha kuwa takribani watanzania 33,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya mfumo wa kupumua ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na uvutaji wa moshi unaotokana na matumizi ya nishati isiyo safi ikiwemo kuni na mkaa.

Ameeleza kuwa kutokana na athari hizo Serikali chini ya uongozi wa Rais, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia 2024–2034 uliozinduliwa mwezi Mei 2024 ambao utawezesha asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia.

Sanjari na hayo, Mha. Mramba amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa nishati safi ya kupikia kitaifa na kimataifa kwa Uongozi wake wa mfano na dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha kila Mtanzania anatumia nishati safi, salama na nafuu ya kupikia.

Share:

TEITI YAFANYA TATHMINI MGODI WA BARRICK NORTH MARA UNAVYOTEKELEZA SERA ZA CSR NA MAUDHUI YA NDANI ‘ LOCAL CONTENT’


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko, akizungumza na watalaamu kutoka TEITI waliotembelea mgodi huo.

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Timu ya wataalamu wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikali katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) ilitembelea Mgodi wa Dhahabu wa North Mara jana Septemba 11, 2025 kujionea mchango wake kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Eneo kubwa lililopewa kipaumbele katika ziara ya wataalamu hao ni Uwajibikaji wa Kamupuni kwa Jamii (CSR) na ushirikwasjwaji wa Watanzania (local content).

Msafara wa wataalamu hao uliongozwa na Mkuu wa Sehemu ya Utafiti kutoka TEITI, Andrew Eriyo.

“Lengo kubwa ni kutathmini utekelezaji wa sheria ya madini upande wa wa CSR na local content,” alisema Eriyo.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko, aliwakaribisha wataalamu hao wa TEITI katika mgodi uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.

“Karibuni sana, CSR ni suala la msingi, na tathmini kama hizi huwa zinasaidia sana kuboresha mambo kwenda vizuri zaidi,” alisema Lyambiko.

Mgodi wa North Mara unatumia mabilioni ya fedha kugharimia miradi ya maendeleo katika vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, huku suala la ‘local content’ nalo likipewa kipaumbele.

“Tuna miradi ambayo imekamilika na ambayo utekelezaji wake unaendelea. Mfano, kuna upanuzi wa mradi wa maji Nyangoto ambao ulitembelewa na Mwenge wa Uhuru hivi karibuni,” alisema Meneja Uhusiano wa Mgodi wa huo, Francis Uhadi.

Uhadi alitaja miradi mingine iliyokamilika kuwa ni pamoja na utengenezaji wa madawati zaidi ya 9,000 ambayo yamegawiwa kwenye shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya elimu.

"Madawati hayo yamegharimu shilingi milioni 800 za CSR", Uhadi alisema.

“Tuna miradi mingine mingi ya CSR, ukiwemo ujenzi wa zahanati, vyumba vya wagonjwa wa nje, madarasa na hata uzio katika shule,” aliongeza Uhadi.

Kuhusu suala la ‘local content’, mgodi huo unatoa kipaumbele kwa wazawa kwenye suala la ajira na fursa za kibiashara kwa jamii zinazozunguka mgodi huo unaoendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni tanzu ya Twiga Minerals.

“Mfano, tumeweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa kazi zisizohitaji stadi zozote wanapewa watu waliopo maeneo jirani na mgodi,” Uhadi alieleza.

Ujumbe huo wa TEITI ulitembelea pia miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa fedha za CSR na kuliridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na kampuni ya Barrick katika kuchangia maendeleo ya Watanzania.

"Mgodi wa Barrick North Mara umekuwa ni mdau wetu mkubwa na leo tumewatambelea kuangalia wanavyofanya kwenye eneo la CSR na local content," alisema mmoja wa watalaamu hao kutoka TEITI, Anastazia Ryoba.

Mbali na North Mara, Kampuni ya Barrick pia inaendesha Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga.

TEITI ni taasisi ya serikali inayohamasisha uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia ili kuhakikisha mapato yanayotokana na rasilimali hizo yanakuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya Watanzania na taifa kwa ujumla.
Kiongozi wa msafara wa wataalamu kutoka TEITI, Andrew Eriyo (wa pili kulia), wakitembelea miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa CSR wa Mgodi wa Barrick North Mara jana. Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano wa Mgodi huo, Francis Uhadi na wa kwanza kulia ni Mwanasheria wa TEITI, Julieth Moshi.
Kiongozi wa msafara wa wataalamu kutoka TEITI, Andrew Eriyo (wa pili kushoto), akijionea moja ya mazao yanayolimwa katika shamba darasa ambalo limeanzishwa na Mgodi wa North Mara kama sehemu ya juhudi za kuinua uchumi wa vijana katika kijiji cha Matongo, wilayani Tarime.
Timu ya watalaamu kutoka TEITI ikitembelea baadhi ya miradi ya CSR, ikiwemo ya elimu katika vijiji vilivyo jirani na mgodi wa North Mara jana.
Afisa Mchumi Mkuu kutoka TEITI, Tibenda Njoki, akisisitiza jambo katika ziara ya kutembelea mgodi wa North Mara.


Watalaamu kutoka TEITI wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa waandimizi wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara walipofanya ziara katika mgodi huo jana Septemba 11, 2025.
Share:

SIRI YA FULL POWER NA ZAT 50: UWEZO WA KIPEKEE KWA WANAUME

🌿✨ GREEN HERBAL CLINIC ✨🌿
💪 Nguvu zako, Fahari yako! 💪

🔥 TIBA ASILIA YA NGUVU ZA KIUME 🔥
🔋 FULL POWER – Kila kitu kinabadilika!

✅ Hurejesha nguvu za kiume kwa haraka na uhakika
✅ Huongeza hamu na furaha ya tendo la ndoa
✅ Hukusaidia kuchelewa kufika kileleni (hakuna haraka haraka)
✅ Huimarisha mzunguko wa damu na stamina – uko fresh muda wote!

🌿 Imetengenezwa kwa mimea tiba asiliaHakuna kemikali, hakuna madhara!


💥 ZAT 50 💥
💊 Mchanganyiko wa mimea tiba yenye nguvu

✅ Hurekebisha homoni za kiume
✅ Huongeza stamina ya mwili na nguvu za kiume
✅ Hujenga misuli na kuimarisha mwili
✅ Matokeo huanza kuonekana ndani ya siku chache tu!


📍 Tunapatikana: Zanzibar | Dar es Salaam | Shinyanga
📦 Tunatuma popote ulipo – dawa zinakufikia kwa usalama na haraka

📱 Piga/WhatsApp: +255 754 568767 / +255 717 702227
📸 Instagram: @greenherbalclinic

🌱 Bidhaa salama, asilia na zenye ubora
✔️ Hakuna madhara ya baadaye
✔️ Imejaribiwa na kuaminika

Share:

BODI YA ITHIBATI : WATU WALIOTAJWA KWA MAJINA YA EZEKIEL MOLLEL (MANARA TV) NA BARAKA LUCAS (JAMBO TV) WANAOSHIKILIWA POLISI SIO WAANDISHI WA HABARI


 
Share:

Thursday, 11 September 2025

MVUA ZA VULI KWA MWAKA 2025 KUTOKUWA ZA KURIDHISHA – TMA



Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kuwa msimu wa mvua za Vuli mwaka huu (Oktoba – Disemba 2025) unatarajiwa kuwa wa mvua za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya nchi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (IPCC), ametoa taarifa hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Septemba 11, 2025.

“Vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko usioridhisha wa mvua vinatarajiwa kutawala hasa katika pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki,” alisema Dkt. Chang’a.

Amefafanua kuwa mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza hadi ya pili ya Oktoba katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara na kaskazini mwa Kigoma, na baadaye kusambaa mikoa ya Pwani ya Kaskazini na nyanda za juu Kaskazini Mashariki kuanzia wiki ya kwanza ya Novemba.

Mvua hizo zinatarajiwa kuisha mwezi Januari 2026, huku vipindi vya joto kali kuliko kawaida vikitarajiwa kujitokeza katika msimu huo.

Dkt. Chang’a amesisitiza umuhimu wa wananchi kufuatilia utabiri wa kila siku, kila wiki na kila mwezi pamoja na tahadhari zinazotolewa na TMA kwa kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kutokea kwa muda mfupi.

Aidha, amebainisha kuwa TMA inaendelea kutoa utabiri wa msimu kwa ngazi ya wilaya. “Wilaya 86 zilizopo kwenye ukanda wa mvua mbili kwa mwaka, zitapatiwa utabiri wa kina wa maeneo madogo,” alisema.

Mamlaka hiyo imewataka wananchi, wakulima na wadau wengine waendelee kutumia taarifa hizi katika kupanga shughuli zao kwa ufanisi ili kuepuka athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa.






Share:

SHULE MPYA YA MAPINDUZI KUWAONDOLEA ADHA YA UMBALI WANAFUNZI




Na Mwandishi Wetu, Handeni

HALMASHAURI ya Mji Handeni mkoani Tanga imeandika historia mpya baada ya kukamilisha ujenzi wa Shule ya Amali ya Mapinduzi, hatua itakayowaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali wa kilometa 22 kila siku kufuata elimu katika Shule ya Sekondari Kwenjugo.

Mradi huo uliofadhiliwa na serikali kupitia Mpango wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) umegharimu zaidi ya Sh. milioni 584.2 na unatajwa kuongeza ufaulu pamoja na hamasa ya wanafunzi kushiriki kikamilifu masomo yao.

Akizungumza mara baada ya kukagua shule hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Maryam Ukwaju, ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika uboreshaji wa miundombinu ya sekta ya elimu.

“Nimpongeze sana Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwenjugo, John Rajabu, pamoja na Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Hadija Kingimali, kwa usimamizi mzuri hadi kukamilisha ujenzi wa shule hii. Hii ni hatua kubwa ya kuwaondolea adha watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu,” amesema.

Amesema kukamilika kwa shule hiyo kunatekeleza kwa vitendo dhamira ya serikali ya kuhakikisha elimu bora inapatikana karibu na jamii.

Pia ameelekeza kufanyike uthamini ili kuongeza eneo la shule hiyo kwa ajili ya viwanja vya michezo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Hadija Kingimali, alisema shule hiyo mpya ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 320.

“Tunatarajia shule zinapofunguliwa Septemba 15, wanafunzi 53 wa kidato cha kwanza waliokuwa wakisoma Sekondari ya Kwenjugo watahamishiwa rasmi kuendelea na masomo katika shule hii,” ameema Kingimali.

Awali, akisoma taarifa ya ujenzi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kwenjugo, John Rajabu, amesema mradi huo ulianza Septemba 27, 2024 kwa kujengwa majengo 13 ya kisasa yakiwemo maabara za kemia na biolojia pamoja na jengo la Tehama.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger