Thursday, 11 September 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 11,2025

Magazeti

 
Share:

Wednesday, 10 September 2025

ZAWADI YA JEZI NA HADITHI YA BINTI WA DODOMA KATIKA SIMBA DAY 2025



✍️✍️Na Dotto Kwilasa

Simba Nguvu Moja , Kutoka Dodoma Hadi Mkapa, Moyo Wangu unajihisi uko Nyumbani!

Siku ya leo si ya kawaida ni Simba Day 2025 , siku ya sherehe, fahari, mapenzi ya dhati kwa klabu kubwa kuliko zote Afrika Mashariki, Simba Sports Club.

Lakini kwangu si tu Simba Day bali naitumia siku hii kutimiza ndoto kwa kuvaa jezi ya kipekee zawadi kutoka kwa rafiki yangu muhimu mno, rafiki ambaye sio tu Mwana Simba wa kweli, bali pia ni shabiki kindakindaki wa Simba.

Hii si jezi tu ni alama ya familia, ushindi, na mapenzi ya kweli.

Unajua ilikuwaje!..Siku moja kabla ya Simba Day, nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu akasema kwa sauti yenye utulivu lakini yenye nguvu kama nyimbo za hamasa uwanjani

“Nina zawadi yako, ni jezi ya Simba SC, ile orijino ya mwaka huu inakungoja!”

Nilishika simu, moyo ukagonga kwa kasi, macho yakalowa na ninavyopenda sasa Jezi ya Simba taarifa hii ilinifanya nijione Malkia kwa kupata zawadi ya ndoto ya maelfu ya mashabik lakini safari hii, ikawa yangu.

Nilipoishika kwa mara ya kwanza, nilihisi nguvu ya historia,rangi nyekundu iliwaka kama moto wa mapambano Nembo ya Simba iling’aa kama jua la asubuhi.

Nikaiweka kifuani nikasema,“Leo si Mwana Simba wa kawaida mimi ni Malkia wa Simba!”

Asubuhi Ya Simba Day ambayo ni leo September 10,2025 nmeamka na jezi yangu mpya, nikaiweka vizuri, nikaipasi kwa upendo tayari kabisa kwa safari ya kuelekea Dar kule ulipo ushabiki wa kweli.

Lakini kabla sijaanza safari yangu ya kuelekea Uwanja wa Benjamin Mkapa, nilijikumbusha jezi ya mwaka jana bado inang’aa kama dhahabu ya Geita.

Nikaona ni vema niivae alafu ile mpyaa niiache kwanza nitaitumia kwenye mechi za maangamizi nikiamini kuna kitu spesho ndani yake ambacho ni nguvu ya kumbukumbu.

Nikajipulizia perfume ya hali ya juu, si unajua ukivaa jezi ya mabingwa lazima uende na viwango vya mabingwa!

Nilipojitazama kwenye kioo nikasema:

“Leo naenda kutembea kama Malkia wa Simba si mchezo!”

Safari Kutoka Dodoma kuelekea Dar ikaanza nikiwa kwenye Bus, dereva akaniangalia akasema “Mwana Simba! Piga siti ya mbele hapa unapewa heshima yako!”

Nikaketi kama mjumbe wa CAF,Watu ndani wakaniangalia kana kwamba nimeingia na kombe la Ligi Kuu mikononi.

Nikajua moja kwa moja hii jezi ni tiketi ya VIP kila kona!

Mitani Dodoma, vijana wa boda boda wakapiga honi za ushangiliaji.

Wazee wa maskani wakanialika chai ya maziwa, wengine wakaomba picha niligeuka kuwa Lulu kwa sababu ya Jezi yaani Jezi ya zamani makali yaleyale.

Nikacheka, nikasema kimoyomoyo,“Mpango mzima upo kwenye hii jezi anayevaa anajua utamu wake.

Mwisho wa yote safari yetu ikaishia kwa Mkapa ilikuwa kama bahari ya damu nyekundu,Kila kona nyimbo, kelele, tabasamu,Nilihisi kuwa sehemu ya historia.

Mzee mmoja akanisogelea akasema, “Binti yangu, hiyo jezi si ya kawaida, ni alama ya mapambano,ni historia ya kila mwanasimba, na ni fahari ya wanawake wa Simba.

Nilibaki kimya, lakini moyo wangu ukapiga kelele za ushindi,kwa mara ya kwanza, nilihisi kuwa sehemu ya mabadiliko makubwa sehemu ya mapinduzi ya soka,sehemu ya Simba Day ya kweli.

Katika stori yangu hii kuna kitu Nimejifunza ambacho ni Kuwa Wanasimba wanapendana Sana kila utakapienda hata kama ni mgeni ukivaa jezi ya Simba lazima utapata wenyeji wako wakarimu.

Kitu kingine ni kwamba Mwana Simba wa kweli si kushangilia tu ni KUIISHI Simba,Jezi si vazi tu ni ishara ya kupendwa, kuaminiwa, na kuunganishwa na historia lakini kubwa zaidi ni kwamba Wanawake ndani ya soka wana nafasi ya juu tunavaa jezi kwa heshima na kuibeba kwa fahari ya Simba

Hii inanifundisha kwamba Jezi yangu sitaiweka kabatini tena,naitunza kama kumbukumbu ya siku ambayo niliheshimiwa, kupendwa, na kujiona kama sehemu ya familia kubwa ya Simba SC.

Na siku Simba Day nyingine itakapotajwa miaka ijayo, watu watasema,“Kulikuwa na binti mmoja kutoka Dodoma aliyevaa jezi kama malkia, na akaiandika historia kwa moyo wake wote.”

Mwisho wa yote historia inabaki kuwa Simba Nguvu Moja mwanzo wa urithi wa kweli!


Share:

Tuesday, 9 September 2025

JUBA TO HOST HISTORIC WBC AFRICA MUAYTHAI CHAMPIONSHIP BELT ON SEPTEMBER 27

 

The stage is set for one of Africa’s most electrifying combat sports nights as South Sudan prepares to host the WBC Africa Muaythai Championship Belt at the Nyakuron Cultural Centre in Juba on Saturday, September 27, 2025.

The championship, regarded as a milestone event for African Muaythai, will feature high-profile bouts between top fighters from South Sudan and Tanzania, blending national pride, explosive action, and continental glory.

MAIN EVENT
South Sudan’s very own James Majok Gau will face Tanzania’s powerhouse Emmanuel Shija Kajala in a thrilling showdown. With speed, strength, and sheer determination on display, the two warriors will battle for the prestigious WBC Africa Muaythai Championship Belt — but only one will emerge victorious.

CO-MAIN EVENT
World Muaythai Champion Sky returns to his homeland after his sensational victory in Pattaya, Thailand (November 2024), where he shocked the world by defeating one of the greatest Dutch fighters in history. In Juba, he will square off against Tanzania’s Musa Said Munisi in what promises to be an explosive, emotional, and unforgettable fight.

UNDERCARD BATTLES
Fans will also witness South Sudan’s rising stars lighting up the ring, including:
Simon Sudan, Abednego “Boyka” Wize J, Eddy, Rambo, John, Johnson, Classic, Irene, Thai Leng, Musa Luwate, and more promising warriors showcasing the future of the sport.

EVENT HIGHLIGHTS

  • World-class Muaythai action on African soil.

  • Continental pride as South Sudan takes center stage.

  • A festival atmosphere with music, entertainment, and cultural showcases.

Organizers emphasize that this will be more than just a fight night — it will be a historic celebration of African combat sports and cultural pride.

📍 Venue: Nyakuron Cultural Centre – Juba, South Sudan
📅 Date: Saturday, September 27, 2025
Tagline: WBC Africa Muaythai Championship Belt – Power. Pride. Glory.


Share:

COLUMBIA AFRICA YAINGIA TANZANIA KWA KUINUNUA IST CLINIC



Columbia Africa Healthcare Limited imetangaza ununuzi wa IST Clinic, kituo maarufu cha huduma za afya kilichopo Dar es Salaam.

Kupitia ununuzi huu wa hisa kwa asilimia 100, Columbia Africa inaimarisha uwepo wake katika Ukanda wa Afrika Mashariki, ikiongeza Tanzania kwenye mtandao wake wa kliniki uliopo Nairobi, Kenya.

Ununuzi huu ni hatua muhimu katika mkakati wa Columbia Africa wa kupanua huduma bora, nafuu na zinazomlenga mgonjwa katika Afrika Mashariki. Baada ya mchakato wa muunganiko, IST Clinic itafanya kazi chini ya jina la Columbia Africa.


Kama sehemu ya dhamira yake ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya nchini Tanzania, wagonjwa wa IST Clinic wataendelea kupata huduma bila usumbufu, wakiendelea kuhudumiwa na timu ile ile ya madaktari waliowazoea, huku wakiwa sasa wanapata msaada wa utaalamu wa kimataifa kutoka Columbia Africa.


Muunganiko huu utafanya maboresho yafuatayo: Ubora wa Juu wa Huduma – kupitia utambulisho wa mifumo ya kitabibu yenye viwango vya kimataifa na kanuni za usalama kwa wagonjwa. Upatikanaji Bora wa Huduma – wigo mpana wa vipimo, mchakato wa tiba ulio rahisi, na huduma za kibingwa.


Huduma Kidijitali ili Kuondokana na mfumo wa Karatasi – mfumo wa kisasa wa usimamizi wa kliniki utakaoleta uharaka wa usajili, usalama wa kumbukumbu, na urahisi wa kufanya miadi na tabibu. Mwendelezo wa Huduma – timu iliyopo ya IST Clinic itaendelea kuwa kiungo muhimu cha utoaji huduma kwa wagonjwa. Programu Pana za Afya – upatikanaji wa huduma za kinga, programu za ustawi wa afya na utaalamu wa kimataifa.


"Tunafuraha kubwa kuipokea IST Clinic ndani ya familia ya Columbia Africa. Ununuzi huu si tu hatua ya ukuaji – bali ni ahadi ya kuleta huduma za afya za viwango vya kimataifa karibu na jamii za Tanzania, huku tukiendelea kudumisha mahusiano thabiti ambayo wagonjwa wameyajenga na madaktari wao," alisema Dkt. Sumit Prasad, Mkurugenzi Mtendaji, Columbia Africa.


Ype Smit, MD, Mwanzilishi na Mkurugenzi, aliongeza: "Kwa zaidi ya miaka 25, IST Clinic imekuwa ikitoa huduma zinazomlenga mgonjwa moja kwa moja jijini Dar es Salaam. Kujiunga na Columbia Africa kunatupa nafasi ya kuunganisha historia hii na mifumo ya kisasa ya kitabibu, teknolojia na viwango vya kimataifa vya huduma ili kuwatumikia wagonjwa wetu kwa ubora zaidi."


Tangu kuanzishwa mwaka 1997, IST Clinic imekua na kuwa mtoaji wa huduma za afya zenye ubora wa hali ya juu jijini Dar es Salaam, ikitambulika kwa huduma za kibinafsi na endelevu. Kupitia timu yake ya madaktari, wauguzi, maabara na wafamasia, IST Clinic imetumikia vizazi vingi vya familia na kuendelea kuwa mshirika anayeaminika wa afya nchini Tanzania.


Columbia Africa, ikiwa sehemu ya makampuni ya afya ya Columbia Pacific Management, inaleta uzoefu wa miongo kadhaa katika kuendeleza hospitali na vituo vya kutoela huduma za afya barani Asia, Afrika na China. Ujio wake Tanzania unaonesha zaidi dhamira ya kujenga mifumo endelevu ya afya katika maeneo yenye ukuaji wa haraka.


Kuhusu Columbia Africa



Columbia Africa Healthcare Limited ni kampuni binafsi ya huduma za afya yenye makao yake makuu Nairobi, Kenya. Inafadhiliwa na Columbia Pacific Management Inc., kampuni yenye makao yake Seattle, Marekani, yenye uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika kuendeleza huduma za afya na makazi ya wazee duniani. Columbia Africa inatoa tiba inayozingatia uthibitisho wa kisayansi kupitia mazingira ya kisasa, yenye ufanisi na kujali, yaliyobuniwa kukidhi mahitaji ya kiafya ya miji inayoendelea kukua barani Afrika.


Kuhusu IST Clinic


IST Clinic, iliyoanzishwa mwaka 1997, ni mtoa huduma za afya za kila siku iliyopatika katika eneo la Peninsula, Dar es Salaam, Tanzania. Inatambulika kwa huduma zinazomlenga mgonjwa na mwendelezo wa huduma, IST Clinic imejijengea sifa ya tiba ya kibinafsi, ubora wa kitabibu na kuaminika na jamii.

Share:

SHIDA SIYO MOMBO, SHIDA NI AMANI NA UTULIVU WA TANZANIA




Septemba 9, 2025

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam

Hivi karibuni kumekuwa na mtiririko wa taarifa mbalimbali za uzushi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Suleiman Mombo.

Taarifa hizo ambazo zinasambazwa kwa nia ovu na genge la watu waliopo nje ya nchi na wengine wa ndani ya nchi, zinafanya upotoshaji mkubwa kuhusu maisha binafsi na kazi ya mkuu huyo wa taasisi hii nyeti.

Wapotoshaji hao walianza kwanza kusambaza taarifa za uzushi kuhusu kifo cha mkuu wa usalama wa taifa wa Tanzania.

Walivyoona kuwa wameumbuka kuhusu uzushi huo, wakaibua upotoshaji mwingine kuhusu uadilifu wake.

Kwa asili ya kazi yake na maadili ya cheo chake, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (DGIS) hawezi kuitisha mkutano wa vyombo vya habari kukanusha upotoshaji huo.

Mwiko na maadili ya kazi yake yanamtaka akae kimya licha ya shambulio linalofanywa dhidi ya heshima na utu wake.

Je, lengo la kampeni hii chafu ya upotoshaji dhidi ya DGIS ni nini?

Jibu la swali hilo liko kwenye majira ambayo nchi inapitia sasa hivi na mageuzi makubwa ambayo Mombo ameyafanya ndani ya TISS tangu ateuliwe kuongoza idara hiyo mwezi Julai mwaka jana.

Kama ambavyo sote tunafahamu, Tanzania kwa sasa iko kwenye kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu.

Uchaguzi mkuu ni kipindi ambacho TISS inatakiwa kuwa macho pengine kuliko majira yoyote yale ili kuhakikisha utulivu, amani, na maendeleo endelevu ya taifa letu.

Maadui wa Tanzania waliopo nje na ndani ya nchi wanadhani kuwa wakiiteteresha TISS kwa tuhuma za uzushi dhidi ya kiongozi wake mkuu wanaweza kufanikiwa kuibuia taharuki nchini na kuhatarisha ulinzi na usalama.

Mombo anasifika kuwa na ujuzi mkubwa na ubobezi kwenye masuala ya operesheni za ujasusi, ikiwemo kufuatilia na kuzuia vitisho kama vile ugaidi, uhalifu wa kimataifa, na uvamizi wa nje.

Idara ya usalama wa taifa ni moja ya nguzo za msingi za nchi yoyote. 

Idara hii inawajibika kulinda maslahi ya taifa, kuhakikisha usalama wa raia, na kudhibiti vitisho vya ndani na nje vinavyoweza kuhatarisha utulivu wa nchi. 

Idara ya usalama wa taifa inalinda mipaka ya nchi na kuhakikisha usalama wa kitaifa na kuruhusu raia kuishi kwa amani bila hofu ya vitisho vya usalama.

Idara hii inasaidia kudumisha utulivu wa ndani kwa kupitia usimamizi wa sheria na utulivu, vyombo vya usalama huzuia machafuko, ghasia, na uhalifu unaoweza kusababisha kuvunjika kwa umoja wa taifa. 

Vilevile, idara hii inashirikiana na mamlaka nyingine za serikali kuimarisha mifumo ya ulinzi, kama vile ulinzi wa miundombinu ya umma na taasisi za serikali.

Pamoja na masuala ya usalama, idara ya usalama wa taifa pia ina jukumu la kuchangia uchumi wa nchi kwa kuhakikisha mazingira salama ya uwekezaji. 

Biashara na uwekezaji hustawi pale ambapo kuna amani na usalama, na hii inasaidia kukuza uchumi wa taifa kupitia ajira na mapato ya serikali.

Kwa maana hiyo, idara ya usalama wa taifa ni kiungo muhimu cha maendeleo ya nchi.

Bila usalama wa kitaifa, maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa hayawezi kufanikiwa. 

Ni wajibu wa kila raia kushirikiana na idara hii kwa kutoa taarifa za msingi na kufuata sheria ili kuhakikisha usalama wa taifa unadumishwa.

Hivyo basi, upotoshaji unaofanywa kwenye mitandao ya kijamii siyo shambulio kwa Mombo au TISS peke yake, bali ni shambulio linalolenga kuhatarisha amani, utulivu, usalama, ustawi na mustakabali mzima wa taifa.

Watanzania tusimame imara kuhakikisha kuwa genge la watu lenye nia ovu halifanikiwi kuiyumbisha nchi kwenye kipindi hiki cha uchaguzi na hata baada ya uchaguzi.

Mungu Ibariki Tanzania.
Share:

WAZIRI KOMBO AWASILI NCHINI UINGEREZA KWA ZIARA RASMI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahamoud Thabit Kombo, amewasili nchini Uingereza kwa ziara rasmi inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 8 hadi 12 Septemba, 2025. 

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano bora na wa kihistoria kati ya Tanzania na Uingereza.
  
Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Kombo atamwakilisha Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa kituo kipya cha Masuala ya Kimataifa cha *ODI Global* utakaofanyika Westminster, London, tarehe 9 Septemba 2025.

Akiwa London, Mheshimiwa Waziri Kombo pia atashiriki katika mfululizo wa vikao vya viongozi waandamizi wa Serikali ya Uingereza, Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika; pamoja na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Tabianchi.

Katika hatua nyingine ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, Waziri Kombo atakutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Ayorkor Botchwey, na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO), Mheshimiwa Arsenio Dominguez.

Aidha Waziri Kombo atafanya vikao na taasisi muhimu za Uingereza za fedha za maendeleo na uwekezaji, ikiwemo British International Investment (BII) na UK Export Finance (UKEF), pamoja na wawakilishi wa King’s Foundation
kama juhudi za kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza ambao ni msingi mkuu wa sera ya mambo ya nje ya Tanzania.

Ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi, Waziri Kombo atashiriki pia katika meza ya majadiliano ya kibiashara na makampuni teule ya Uingereza kwa ajili ya kubaini fursa katika biashara, uwekezaji, nishati safi, miundombinu, na sekta nyingine za kipaumbele.

Share:

Monday, 8 September 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 9,2025

Magazeti
 

Share:

TUME YAZITAKA TAASISI NA ASASI KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA KWA WELEDI


Na Mwandishi Wetu - Dodoma.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imezitaka taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi na weledi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 08 Septemba, 2025 wakati akifungua kikao kazi cha Tume na taasisi na asasi hizo kilichofanyika Mkoani Dodoma.

"Ni vyema mkafahamu kuwa kifungu cha 10(1)(g) na (h) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024 na kanuni ya 22 na 23 ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, zimeipa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi mamlaka ya kutoa elimu ya mpiga kura nchini, kuratibu na kusimamia taasisi na asasi zinazotoa elimu hiyo..

Hivyo, kazi mnayoenda kuifanya ni moja ya majukumu ya kisheria ya Tume na mnapaswa kuifanya kwa weledi na ufanisi mkubwa,” amesema.
Ndugu Kailima ameongeza kuwa, Tume inatarajia kuona kuwa, taasisi na asasi za kiraia zinatoa elimu iliyolengwa haswa kwa kutoa kipaumbele kwenye mambo ambayo yatawapa wananchi, wagombea na vyama vya siasa kwa ujumla uelewa wa namna ya kushiriki kwenye kampeni kwa amani na utulivu ikiwa ni pamoja na kupata uelewa mzuri wa utaratibu wa kupiga kura.

"Hatutarajii kabisa mtoe elimu ambayo italeta mkanganyiko kwenye jamii na kuiingiza nchi kwenye machafuko kama ilivyotokea katika maeneo mengine hapa Afrika na duniani kwa ujumla," amesema.

Amesisitiza kuwa taasisi na asasi hizo haziruhusiwi kuwapa watu wengine au taaisi au asasi nyingine vibali walivyopewa na kwamba vibali hivyo ni lazima vitumiwe na walengwa tu.

"Nyie ndio mabalozi wa Tume, hivyo, mhakikishe katika kipindi chote cha utekelezaji wa jukumu lenu la kutoa elimu, mnazingatia Katiba, sheria, kanuni na maelekezo ambayo Tume imekuwa ikiyatoa mara kwa mara," amesema.

Kikao kazi hicho kiliwaleta pamoja viongozi wa Tume na wawakilishi wa taasisi na asasi 164 zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa.

Mada zilizowasilishwa ni pamoja na Mwongozo wa Elimu ya Mpiga Kura wa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025, Sheria za Uchaguzi, Kura ya Rais Portal (Kura ya Rais Popote) na Mchakato wa Uchaguzi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger