Monday, 25 August 2025

WALICHOKIFANYA WANANCHI WA WILAYA YA MULEBA KWA WALIOTEULIWA KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA MULEBA KASKAZINI NA KUSINI

Wananchi wa Jimbo la Muleba Kasikazini baada ya kumpokea ndugu Adonis Bitegeko mteuliwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini
Bwana Adonis Bitegeko aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kasikazini akizungumza baada ya kufika ofisi za chama cha Mapinduzi (CCM)

Na Mariam Kagenda _Kagera

Wananchi wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera wamejitokeza kwa wingi uwanja wa Ndege Bukoba kuwapokea walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Muleba Kusini na Muleba Kaskazini wilaya ya Muleba mkoani Kagera .

Wananchi hao baada ya kuwapokea wateuliwa wa nafasi hiyo ambao ni Adonis Bitegeko aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini na Dkt. Oscar Kikoyo Jimbo la Muleba Kusini waliwasindikiza kwa msafara wa magari na pikipiki mpaka kwenye ofisi za chama cha mapinduzi .


Baada ya Wagombea hao kufika ofisi za Chama hicho wameishukuru halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi kwa imani yao kubwa ya kuwateuwa kugombea nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika October 2025 na Wananchi ambao waliwachagua kwa kura nyingi katika uchaguzi wa Kura za maoni .


Leo Agosti 25 watachukua fomu za kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 2025 .

Ikumbukwe kuwa Adonis Bitegeko ndiye aliyeongoza katika Uchaguzi wa kura za maoni kwa Jimbo la Muleba Kasikazini kwa kupata kura 4392 na Dkt Oscar Kikoyo aliongoza kwa kupata kura 4710 .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Muleba Athumani Kahara amewahimiza wanachama wa chama hicho kuvunja makundi kwani kwa sasa kilichobaki ni kuwanadi Wagombea walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha wanatafuta ushindi wa kishindo wa Chama hicho.

Aidha amesema kuwa watafanya Kampeini za kistaarabu za kuhakikisha wanailinda amani na kujiepusha na vitendo vyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani katika kipindi cha Uchaguzi mkuu .
Dkt. Oscar Kikoyo aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kusini akizungumza na wananchi baada ya kufika ofisi za Chama Cha Mapinduzi.
Adonis Bitegeko akisaini kitabu cha Wageni katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Muleba
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Athumani Kahara( Aliyevaa Kanzu ) akiwa na wateuliwa wa nafasi ya Ubunge baada ya kufika ofisi za chama hicho.
Wananchi wa wilaya ya Muleba wakiwa uwanja wa Ndege kuwasubiri wateuliwa
Wananchi wakimpokea Adonis Bitegeko aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini
Share:

Sunday, 24 August 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 25,2025

 


Magazeti  

    

          

      

Share:

MIFUGO 148,172 KUCHANJWA HANDENI MJI KUDHIBITI MAGONJWA


 ‎
 ‎Na Mwandishi Wetu, Handeni ‎ ‎ 

Mifugo 148,172 katika Halmashauri ya Mji Handeni, mkoani Tanga, inatarajiwa kuchanjwa dhidi ya magonjwa ya kideri, sotoka na mapafu, kupitia kampeni ya kitaifa ya chanjo ya mifugo. ‎

 ‎Akizindua kampeni hiyo Agosti 22, 2025 katika Kata ya Malezi, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amewahimiza wafugaji wote wa Halmashauri hiyo wajitokeze kishiriki zoezi hilo la kitaifa ili kukabiliana na magonjwa ya mifugo. 

‎ ‎Kwa upande wake, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo, Aldegunda Matunda, amesema kati ya idadi hiyo ya mifugo; ng’ombe ni 38,006, mbuzi 25,356, kondoo 9,567 na kuku 75,243. 

‎ ‎Amesema Halmashauri hiyo inakadiriwa kuwa na wafugaji wapatao 34,484 na kwamba sekta ya mifugo imekuwa ikichangia asilimia 21.78 ya mapato ya Halmashauri kwa mwaka, sambamba na kuinua kipato cha wananchi. 

‎ ‎“Halmashauri imepokea mgao wa chanjo za ruzuku kutoka serikali kuu pamoja na vitendea kazi kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya mifugo. Tumejipanga kutoa elimu kwa wataalamu wetu walioko mashinani ili kusimamia zoezi hili ipasavyo,” amesema Matunda. ‎ ‎

Amebainisha kuwa chanjo zitakazotolewa ni ya homa ya mapafu kwa ng’ombe (CBPP), homa ya sotoka kwa mbuzi na kondoo (PPR), na kideri kwa kuku, katika kata zote 12 za Halmashauri hiyo. ‎

 ‎“Katika zoezi hili, mfugaji atachangia nusu ya gharama ya chanjo, huku utambuzi wa mifugo ukitolewa bure kabisa,” amesema
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger