Wednesday, 20 August 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 20,2025



Magazetini

















Share:

WOTE WALIKUWA WANASEMA SINA BAHATI KWENYE MAPENZI, SASA NIMEOLEWA NA BILIONEA MZUNGU



Walikuwa wananiita “mshenzi wa mapenzi.” Marafiki zangu wa karibu walinicheka kwa siri, wengine wakisema sijui kuchagua wanaume, wengine wakinihurumia kwa kimya. 

Katika familia, nilikuwa mfano wa “usiotakiwa kufuatwa”ndugu walinitumia kama somo kwa wadogo zangu, “msije kuwa kama dada yenu.”
Share:

Tuesday, 19 August 2025

WAFANYABIASHARA SHINYANGA WAIPONGEZA TRA KWA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI 2025


Baadhi ya wafanyabiashara katika mkoa wa Shinyanga wameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya mwaka 2025, ikiwemo hatua ya kufuta kodi kwa baadhi ya watoa huduma ndogo za kijamii kama waendesha bodaboda na mama lishe.

Zenaida Rweisunga, mfanyabiashara wa Shinyanga, amesema marekebisho hayo ni faraja kubwa kwa wananchi na yatapunguza mzigo wa kodi kwa watoa huduma wadogo, huku akishauri TRA kuendelea kusikiliza maoni ya wananchi hususan kwenye suala la kodi ya nyumba.

Naye Fadhili Machum, mwendesha bodaboda mjini Shinyanga, ameishukuru TRA kwa hatua ya kufuta kodi kwa waendesha bodaboda akisema itawapunguzia gharama na kuwapa nafasi ya kuboresha maisha yao.

Mabadiliko hayo yameelezwa kwa kina na Afisa Mkuu Msimamizi wa Kodi wa TRA, Hamad Mterry, wakati akitoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wa Shinyanga kuhusu sheria mpya za kodi zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Marekebisho haya yamelenga kurahisisha ulipaji kodi na kupunguza mzigo kwa watoa huduma wadogo ili kuongeza wigo wa walipa kodi kwa hiari,” alisema Mterry.

Kwa upande wake, Jackton Koy, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga, ameipongeza TRA kwa kushirikiana nao kupitia elimu ya kodi, huku akiwasihi wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya taifa.

“Ni muhimu TRA waendelee kutukaribisha karibu na kuwasikiliza wafanyabiashara. Kwa upande wetu, ni wajibu wetu kulipa kodi kwa hiari kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu,” alisema Koy.

Elimu hiyo imeonekana kuongeza uelewa kwa wafanyabiashara wa Shinyanga juu ya wajibu wao wa kulipa kodi, huku wengi wakiahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka hiyo kwa manufaa ya taifa.

Share:

WANANCHI WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE UCHAGUZI MKUU


Wananchi wametakiwa kujitokeza kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu kwani ni njia ya msingi ya kuhakikisha sauti zao zinasikika,na kuchagua viongozi wanaowapenda na wenye uwezo wa kuleta maendeleo na kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa NaCoNGO mkoa Morogoro na Mkurugenzi wa Tanzania Initiative for social and Economic Relief (TISER)Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Iniative for Social and Economc Relief (TISER),Otanamusu Nicholas wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro.

“Wananchi wote tunapaswa kutumia haki yetu ya kidemokrasia kwa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025”,ameeleza.

Nicholas amesema nchi yetu ya Tanzania ina amani na upendo wa kutosha,na hivyo katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wanapenda kuona amani inaendelea kuwepo na kuwapa nafasi kila mwenye haki ya kupiga kura kushiriki katika zoezi hilo.

“Kupiga kura ni haki ya kikatiba ya kila raia,kushiriki uchaguzi ni njia ya kutekeleza wajibu wa uraia na kuhakikisha sauti ya wananchi inasikika katika kuleta maendeleo”,amesema Nicholas.

Amesema viongozi watakaochaguliwa ndio watakuwa chachu ya kuleta maendeleo ndnai ya nchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu,kilimo na maji,hvyo kila mwananchi atambua kura yake ni muhimu sana na kujitokeza kwa wingi katika mchakato huo.


"Katika kipindi cha mchakato mzima wa uchaguzi tuepuke kauli za chuki,lugha mbaya,ambazo tunajua zinaweza kuleta sintofahamu kwa upande mmoja au mwingine na kusababisha vurugu za hapa na pale", amesema.

“Niwaombe wanasiasa,wagombea,tuepuke kauli za chuki,tunaponadi sera zetu jukwani tutumie lugha nzuri ambazo zitafanya sera zako kueleweka na kukubalika ndani ya jamii”,amesema.
Share:

WIZARA YA NISHATI YAJIVUNIA UTEKELEZAJI WA MIRADI SABA KATI YA 17 NCHINI


📌 Katibu Mkuu Nishati asema kati ya miradi hiyo saba, JNHPP imekamilika

📌 Asema EACOP imefikia asilimia 65 huku Serikali ya Tanzania  ikichangia  hisa za shilingi trilioni 1.12

📌Ruhudji na Rumakali tafiti zakamilika


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba amesema kuwa katika miradi ya kimkakati inayotekelezwa nchini Wizara ya Nishati inatekeleza takribani miradi saba.

Mhandisi Mramba ameyasema hayo Agosti 17, 2025 wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Vijana (YEE) ambao unagusa maeneo yanayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

“Miradi hiyo ni mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), Mradi wa kugeuza gesi kuwa kimiminika (LNG), Mradi wa utafutaji mafuta, Miradi ya umeme ya Rumakali na Ruhudji na utafiti wa mafuta eneo la Mnazi Bay North”, amesema Mha. Mramba.

Ameeleza kuwa katika miradi hiyo saba, mradi wa bwawa la kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere unaozalisha megawati 2,115 umekamilika na unaingiza umeme kwenye gridi ya Taifa.

Ameongeza kuwa mradi wa bomba la mafuta ghafi (EACOP) umefikia asilimia 65 na upo mbioni kukamilika, mradi wa LNG  upo katika hatua za mwisho na miradi ya umeme ya  Ruhudji na Rumakali tafiti zimekamilika.

Aidha, amesema Serikali ya Tanzania imeshachangia takribani shilingi trilioni 1.12 kwenye mradi wa EACOP kama hisa ya Tanzania katika mradi huo na kuna kampuni za kitanzania 200 ambazo zinatekeleza kazi mbalimbali katika mradi wa EACOP ambazo zitalipwa i jumla ya shilingi trilioni 1.325.

Mhandisi Mramba ametanabaisha kuwa mbali ya fursa za kiuchumi zinazopatikana pia wananchi wa maeneo ambayo  mradi ya umeme inayopeleka umeme EACOP itapita watanufaika kwa kuunganishwa na huduma ya umeme.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger