Saturday, 16 August 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 16,2025

Magazeti ya leo

   
Share:

Friday, 15 August 2025

MIMI NDIYE NILIWAHI KUANDIKIWA WASIFU WA KIFO HOSPITALINI, LEO NAWAAMBIA SIRI YA KUPONA

Hospitali moja kubwa jijini Dar es Salaam iliwahi kuandaa wasifu wa kifo kwa mgonjwa ambaye madaktari walithibitisha hakuwa na matumaini ya kupona tena. Wauguzi waliambiwa kuwa muda wowote wangehitajika kutoa taarifa rasmi ya kifo. 

Familia yake ilishaandaa jeneza na michango ya mazishi ilianza kutumwa. Lakini kwa mshangao wa kila mtu, mgonjwa huyo aliamka, akapata nafuu ya ghafla, na leo hii anaendesha biashara yake mwenyewe akiwa na afya tele.
Share:

MRADI WA KUTATUA CHANGAMOTO YA NDOA ZA UTOTONI KUPITIA MILA NA DESTURI WAZINDULIWA MZUMBE

Mradi wa RE - EMPOWER wazinduliwa Chuo Kikuu Mzumbe.

******

Chuo Kikuu Mzumbe, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Antwerp cha nchini Ubelgiji wamezindua rasmi mradi wa Kuwezesha mabadiliko chanya ya mila na desturi katika Kukabiliana na ndoa za utotoni nchini Tanzania (RE-EMPOWER) ambao umelenga kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na kimazingira ambazo zimebainika kuwa ni vichocheo vya ndoa za utotoni nchini Tanzania.

Uzinduzi wa Mradi huo umefanyika Agosti 14 katika ukumbi wa Maekani , Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Wataalamu wa ustawi wa jamii, wanataaluma, pamoja na viongozi wa dini na serikali, Kamishna wa Ustawi wa Jamii,

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Kamishna wa Ustawi wa jamii Dkt. Nandera Mhando amesema kuwa ni muhimu kudumisha mila na desturi kwani ndizo zinastawisha jamii , lakini mradi huu unatoa fursa ya kushirikisha jamii katika kutatua changamoto za ndoa za utotoni wakati huo huo ukuendeleza mifumo bora ya kijamii

Aliongeza kuwa tafiti zinazofanywa ndani ya mradi huu zinatoa ushahidi wa kisayansi unaosaidia serikali na wadau kupanga sera na mikakati inayolenga matokeo halisi ya jamii na kuwasisitiza Wadau wote kushiriki vyema katika utafiti huo ili kupata majawabu sahihi ya changamoto ya ndoa za utotoni

Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Allen Mushi, alisisitiza kuwa mradi wa RE-EMPOWER unalingana na kauli mbiu ya chuo hicho inayosema "Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu" kwa kuwa unalenga kutatua changamoto halisi kupitia tafiti zinazotoa maarifa na suluhisho chanya kwa sera na mikakati ya maendeleo.

Aidha Prof. Mushi alisisitiza kuendeleza ushirikiano kati ya Mzumbe, Chuo Kikuu cha Antwerp, na wadau wengine na kusema kuwa jambo hilo litaongeza ubora wa kitaaluma na kuimarisha nafasi ya chuo katika viwango vya kimataifa.

Awali, Dkt. Seraphina Bakta ambaye ni Mtiva wa Kitivo cha Sheria, alielezea kwa kina umuhimu wa mradi huu wa miaka mitano katika kushughulikia matatizo ya ndoa za utotoni yanayosababishwa na tabia na mazingira na kubainisha jinsi mradi huo ulivyolenga kutoa suluhisho na fursa kwa Wanataaluma kutoka chuo Kikuu cha Antwerp na Chuo kikuu Mzumbe kufanya tafiti zinazohusiana na ndoa za utotoni na masuala ya kijamii yanayohusiana na sheria.

Mratibu wa Mradi huo Dkt. Isabelle Zundel kutoka Chuo Kikuu cha Antwerp, alisema:

"Tunafurahia kushirikiana na Chuo Kikuu Mzumbe katika mradi huu unaolenga kutoa matokeo chanya katika kuzuia ndoa za utotoni. Mradi huu ni mfano wa jinsi elimu, utafiti na jamii vinaweza kuunganishwa kuleta mabadiliko yanayohitajika."

Mradi wa RE-EMPOWER ni kielelezo cha jinsi ushirikiano kati ya vyuo vikuu, serikali, jamii na wadau wa kimataifa unavyoweza kuleta mabadiliko chanya ya kijamii. Kwa kushirikisha maarifa, tafiti na mila za kienyeji, mradi huu unatoa mwanga wa matumaini kwa vijana, unasaidia kupunguza ndoa za utotoni, na unaweka msingi wa jamii yenye afya, elimu bora, na usawa wa kijinsia.
Mfawidhi (MC) ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Wakili Bernadetha Iteba akiongoza itifaki na utambulisho wakati wa uzinduzi wa mradi wa RE - EMPOWER
Mtiva wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Seraphina Bakta akiwakaribishawashiriki kwenye uzinduzi wa mradi wa RE - EMPOWER
Mratibu wa Mradi kutoka Chuo kKikuu cha Antwerp Dkt. Isabelle Zundel akielezakuhusu malengo ya mradi, muda wa utekelezaji na namna mradi unavyotekelezwa kwakushirikiana na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mradi wa RE - EMPOWER
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. William Manyama akitoa nenowakati wa uzinduzi wa mradi wa RE - EMPOWER
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Allen Mushi akieleza umuhimu waushirikiano wa kimataifa kati ya Mzumbe, Chuo Kikuu cha Antwerp na wadau wenginewakati wa uzinduzi wa mradi wa RE - EMPOWER
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. Nandera Mhando akizindua mradi wa RE - EMPOWER na kusisitiza kuwa mradi huo unatoa fursaya kushirikisha jamii katika kutatua changamoto za ndoa za utotoni na kuendelezamifumo bora ya kijamii
Baadhi ya wahadhiri wa chuo kikuu mzumbe na wadau mbalimbali wa nje walioshirikiuzinduzi wa mradi wa RE - EMPOWER
Mgeni rasmi wa uzinduzi wa mradi wa RE - EMPOWER ambaye pia ni kamishna waUstawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. Nandera Mhando (katikati) akikabidhiwa zawadi ya kumbukumbu na Mtiva wa Kitivo cha Sheria Dkt. Seraphina Bakta (kulia) wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Share:

WIZARA YAANIKA MKAKATI KUENDELEA KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA,YAPONGEZA JUHUUDI ZA ORYX GAS


Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Nishati imesisitiza kuwa imeweka mkakati wa kuhakikisha wananchi wote wanatumia nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo yamekuwa na madhara ya kiafya na kimazingira huku ikiwapongeza wadau wakiwemo Oryx Gas kwa kushiriki kikamilifu katika kufanikisha mkakati huo.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Nishati Safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Nolasco Mlay wakati wa uzinduzi wa kampeni ya maalum ya Gesi Yente na Oryx Gas yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi yakupikia kwa Watanzania wote.

“Usipotumia nishati safi ya kupikia kuna madhara makubwa kiafya na kimazingira, tunaweza kuona wenyewe siku hizi watu wengi wamekata miti kwasababu wanatumia kwa ajili ya kupikia mkaa na kuni.

“Hivyo tunahama kutoka kutumia nishati isiyo safi ya mkaa na kuni na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia, ndio maana wadau kama ORYX GAS na wadau wengine wanashirikiana na Serikali ambayo imekuja na mkakati ifikapo 2034 asilimia 84 ya Watanzania tuwe tumehamia kwenye nishati safi ya kupikia.

“Na ukweli ORYX wanatusaidia sana kwasababu wako Tanzania nzima na mpango wao ni kuendelea kushiriki kikamilifu kuhakikisha mkakati wetu ifikapo 2034 wananchi asilimia 84 wawe wanatumia nishati safi ya kupikia na tuachane na matumizi ya kutumia kuni na mkaaa.

“Kama Serikali tukisaidiana na wadau kama ORYX tunahakikisha tunaweka ruzuku kwenye gesi ili kila mwananchi aweze kumudu kununua gesi,kutumia na kumudu gesi inapoisha.Wananchi waelewe tunapozungumzia nishati isiyo safi ndio nishati ukitumia inakuathiri kiafya,”amesema Mlay.

Amesisitiza Serikali pia inamkakati wa kupunguza kodi katika bidhaa za nishati safi kwani kodi inapokuwa juu na bei ya bidhaa hizo inakuwa kubwa huku akifafanua tayari kuna mkakati ambao umeanza na kuna rasimu ambayo imeshapelekwa kwa ajili ya mchakato utakaowezesha bidhaa za nishati safi ya kupikia zishuke bei ili kıla Mwananchi amudu.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoit amesema wameendelea kuwahamasisha Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia kwani tafiti zinazonesha maelfu ya familia bado zinategemea kuni,mkaa na mafuta ya taa kwa kupikia hali inayoongeza magonjwa katika Mfumo wa hewa na uharibifu wa mazingira.

“Tunaishi kipindi ambacho afya ya jamii na mazingira yetu inahitaji kulindwa zaidi ya wakati mwingine wowote. Kuna maelfu ya familia bado hutegemea kuni, mkaa, na mafuta ya taa kwa kupikia, hali inayoongeza hatari ya magonjwa ya njia ya hewa, uharibifu wa mazingira, na gharama kubwa za maisha kwa muda mrefu.

“Kupitia kampeni ya Gesi Yente, tunalenga kurejesha mitungi ya gesi iliyopakiwa majumbani na isiyotumika sokoni, na kuirudisha kwenye matumizi. Mitungi hii siyo ya kupuuzwa ni rasilimali muhimu ambayo inaweza kusaidia familia nyingi kupikia kwa usalama, kwa haraka, na kwa gharama nafuu.”

Pia amesema kupitia kampeni hiyo Oryx Gas itakuwa inatoa zawadi mbalimbali kwa washindi katika kampeni hiyo na miongoni mwa zawadi zitakazotolewa ni kama vile pikipiki, baiskeli, seti ya sufuria, mabegi ya shule.

Pamoja na hayo amesisitiza huu ni wakati wa kuamka kama taifa na kumuunga mkono kiongozi wetu wa taifa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuipeleke nchi viwango vingine kwenye suala la nishati safi.

“Tunawahimiza Watanzania wote kama una mtungi wa gesi ulioiacha nyumbani ni wakati wa kuuleta tena sokoni, ni wakati wa kuutumia tena na ujishindie zawadi kemkem.Na kwa wale ambao bado hawajaanza kutumia gesi tunawahamasisha kuchukua hatua na waanze kutumia gesi.Tunaweza kujenga taifa linalotumia nishatisafi, salama, na rafiki kwa mazingira.”
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 15,2025




























Share:

Thursday, 14 August 2025

MKE WA PILI ALIJIFANYA MCHA MUNGU KUMRITHI MUME WANGU LAKINI MIMBA ZAKE ZOTE ZILITOKA



Nisingeamini kama mtu anaweza kuja kuvuruga ndoa ya miaka 12 kwa kuhubiri ‘Mungu ameniambia nitakuwa mke wako’. Lakini ndivyo ilivyotokea. 

Mie ni mke wa ndoa ya kwanza, tulibarikiwa na watoto watatu, maisha yetu yalikuwa ya kawaida ila ya amani. Mume wangu alikuwa mcha Mungu, lakini alivyoanza kuhudhuria maombi kwenye kanisa jipya, alianza kubadilika taratibu.
Share:

MKURUGENZI WA ELIMU KWA MLIPAKODI TRA ATEMBELEA OFISI YA RC SIMIYU KUIMARISHA UHUSIANO MWEMA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha akizungumza na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo pamoja na Meneja wa TRA mkoani humo Bw. Joseph Mtandika wakati Mkurugenzi Kayombo alipomtembelea ofisini kwake.

**********

Na Mwandishi wetu, Simiyu

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu kwa lengo la kuimarisha uhusiano na kuomba ushirikiano zaidi katika kuhakikisha kuwa TRA inatimiza majukumu yake ya ukusanyaji mapato ya serikali.

Akizungumza mara baada ya kumtembelea Mkuu wa Mkoa huo ofisini kwake, Mkurugenzi Kayombo alisema kwamba, kuimarisha uhusiano kati ya TRA, viongozi na wadau ni moja ya mkakati mahususi katika kujenga ushirikiano na wadau hao ili kufanikisha jukumu zima la ukusanyaji wa kodi.

“Moja ya mikakati tuliyonayo kama TRA ni kuhakikisha tunakuwa na uhusiano mzuri baina yetu, walipakodi, viongozi wa serikali na wadau mbalimbali. Mkakati huu umetusaidia kujenga ushirikiano na kupata maoni juu ya namna bora ya kukusanya kodi kwa ufanisi”, alisema Bw. Kayombo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha, amesema kuwa, sasa hivi kuna mabadiliko makubwa ndani ya TRA ambapo ameipongeza kwa kujenga uhusiano mzuri na wadau tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

“Kwa sasa TRA ina uhusiano mzuri na walipakodi pamoja na wadau kuliko hapo awali na hii ndio sababu mojawapo ambayo imewasaidia kuvuka lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha uliopita. Ofisi yangu itaendelea kutoa ushirikiano ili kuiwezesha TRA kutekeleza majukumu yake ya ukusanyaji mapato kwa ufanisi”, alieleza Mhe. Macha.

Naye, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo ameipongeza TRA mkoani Simiyu kwa kujenga ushirikiano na wadau ndani ya mkoa huo hali ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko kwenye ofisi za viongozi na kurahisisha utendaji kazi wa viongozi husika.

Mkurugenzi Richard Kayombo baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu pia alipata nafasi ya kuongea na watumishi wa TRA mkoani humo kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwahimiza kuzingatia maadili ya utumishi wa umma pamoja na kufanya kazi bidii.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha akizungumza na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo pamoja na Meneja wa TRA mkoani humo Bw. Joseph Mtandika (hawapo pichani) wakati Mkurugenzi Kayombo alipomtembelea ofisini kwake.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha (hayupo pichani) wakati Mkurugenzi Kayombo alipomtembelea Mkuu wa Mkoa ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha akizungumza na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano Bw. Richard Kayombo pamoja na Meneja wa TRA mkoani humo Bw. Joseph Mtandika (hawapo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano Bw. Richard Kayombo na Meneja wa TRA mkoani humo Bw. Joseph Mtandika wakati walipomtembelea ofisini kwake.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo ofisini kwa Katibu Tawala huyo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo akizungumza na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano Bw. Richard Kayombo pamoja na Meneja wa TRA mkoani humo Bw. Joseph Mtandika (hawapo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake.
Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishashaji) wa Mkoa wa Simiyu Bw. Juma Topera (mwenye suti ya kijivu), Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano Bw. Richard Kayombo (kushoto) na Meneja wa TRA mkoani humo Bw. Joseph Mtandika wakifurahia jambo wakati Mkurugenzi Kayombo alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger