Sunday, 29 June 2025

AHMED SALUM : ASANTENI SANA SOLWA, TULIAHIDI NA TUMETEKELEZA!


Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Ally Salum - Asanteni Solwa, Tuliahidi na Tumetekeleza!



























Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 29,2025



Magazeti



Share:

Saturday, 28 June 2025

FRED ROMANUS AJITOSA KUWANIA UBUNGE JIMBO JIPYA LA ITWANGI


Kijana na mwanazuoni Fred Romanus kutoka Kijiji cha Mendo, Kata ya Ilola, ametangaza nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo jipya la Itwangi, mkoani Shinyanga.

Fred Romanus amesema amekuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuwatumikia wananchi kupitia nafasi ya Ubunge, akilenga kuwaletea maendeleo jumuishi na endelevu kwa makundi yote katika jamii.

“Ndoto yangu ni kuona kila mwananchi ananufaika na matunda ya uongozi bora. Naamini kupitia nafasi hii ya Ubunge, nitaweza kusukuma gurudumu la maendeleo kwa vitendo,” amesema Fred Romanus.

Kwa sasa, amesema sera na mikakati yake ya maendeleo itawasilishwa kwa wananchi katika siku zijazo wakati wa kampeni rasmi endapo chama kitampa ridhaa ya kugombea Ubunge.

Share:

Friday, 27 June 2025

SERIKALI YAJENGA VITUO 472 VYA POLISI HADI NGAZI YA KATA


Na Emmanuel Mbatilo

SERIKALI imeendelea kuliimarisha jeshi la polisi kwa kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza miundombinu, ambapo vituo vya polisi 472 vimejengwa hadi ngazi ya kata na shehia.

Ameyasema hayo leo Juni 27, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akitoa hotuba ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 Jijini Dodoma.

"Tumeboresha makazi ya askari na kununua vitendea kazi, ikiwemo magari na pikipiki, kwa ajili ya kazi za utawala na operesheni. Aidha, askari wapya 16,009 wameajiriwa, huku Maofisa,Wakaguzi na Askari 10,363 wakipandishwa vyeo". Amesema Rais Samia

Aidha ametoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwa kuzuia uhalifu.

"Kasi ya kuwabaini na kuwakamata wahalifu, na kuwafikisha Mahakamani imeongezeka. Jambo ambalo bado hatujafanikiwa vya kutosha ni ajali za barabarani. Lazima nazo tuendelee kuzitafutia muarobaini wake.

Pamoja na hayo Rais Samia amelielekeza Jeshi la Polisi kuongeza jitihada katika kukomesha matukio ya watu kupotea.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger