Wednesday, 30 April 2025
TIJA KWA NCHI NDIYO KIPAUMBELE CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA (LNG)- DKT. BITEKO
Tuesday, 29 April 2025
WAZIRI MKUU : SERIKALI ITAENDELEA KULINDA UHURU WA HABARI KWA VITENDO, WAANDISHI TUMIEMI AKILI MNEMBA KWA UWAJIBIKAJI
👉Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Asisitiza Akili Mnemba Isaidie, Isiwe Kikwazo kwa Uhuru wa Habari
👉Serikali Kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa Vitendo
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa vyombo vya habari kwa vitendo na si kwa maneno, akisisitiza matumizi sahihi ya akili mnemba (Artificial Intelligence) kama chachu ya uwajibikaji na si kikwazo kwa waandishi wa habari.
Akizungumza jijini Arusha leo Aprili 29, 2025 wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (World Press Freedom Day 2025) ,yenye kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “Uhabarishaji katika Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari”, Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa wanahabari kutumia akili mnemba kwa weledi na kuzingatia ukweli wa taarifa wanazotoa.
“Akili Mnemba itumike kama nyenzo kwa waandishi wa habari na siyo kikwazo. Mjitahidi kuitumia vizuri kwa uwajibikaji, kutoa taarifa sahihi na zenye kuzingatia maadili ya taaluma. Serikali kwa kushirikiana na Wadau tunaendelea na mchakato wa kutengeneza sera kuhusu Akili Mnemba ”, amesema Waziri Mkuu.Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Mhe. Majaliwa ametaka vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, haki na wa uwazi akihimiza utoaji wa taarifa sahihi, zinazojenga amani na mshikamano.
Aidha, amevitaka vyombo vya habari kuendelea kuelimisha na kuhabarisha jamii kuhusu maendeleo ya taifa, kwa kuzingatia ukweli na uadilifu.
Waziri Mkuu ameeleza kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kulinda uhuru wa vyombo vya habari kwa vitendo siyo maneno, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji wa taarifa na uhuru wa kujieleza.







.jpeg)









































