Saturday, 29 March 2025
UJENZI WA STENDI YA MABASI MADABA KUANZA RASMI APRILI
Friday, 28 March 2025
THE RUNNERS TANZANIA YAZINDUA MSIMU WA TANO WA ABSA DARCITY MARATHONI 2025
JE, UMEWAHI KUDHULUMIWA?, PATA HAKI YAKO SASA!
Naitwa Amani kutokea Babati, unajua hakuna kitu kibaya maishani kama kudhulumu mali ambayo sio yako, kuna watu mikosi haiondoki katika maisha yao kutokana na dhuluma walizozifanya huko nyuma.
Nasema hivyo kwa sababu Baba yetu aliamua kununua magari mawili kwa ajili ya watoto wake ili hapo baadaye tusije kuteseka katika maisha, haya magari ni mabasi kwa ajili ya usafiri na kila mmoja alipewa lake.
Basi niliamua kukodisha bus langu wakati naendelea na masomo na fedha niliyopata nilikuwa nalipa nayo ada ya chuo na matumizi mengine, dereva niliyempa gari langu alikuwa mwaminifu, kila mwisho wa wiki alinitumia fedha yangu kama tulivyokubaliana.
Sasa baada ya kumaliza chuo nilitaka kuchukua bus langu, hivyo nilimpaa taarifa hiyo, cha kusikitisha ni kwamba alikataa na kudai bus lile ni lake na kwamba nilimkodisha kwa makubaliano ya kumuuzia akifikisha kiwango fulani cha fedha.
Kubwa zaidi nilishangaa sana pale alipoamua kutoa nyaraka kuwa anamiliki bus lile, ugomvi ulikuwa mkubwa hadi Baba yangu alikuja lakini bado aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa gari ni mali yake.
Binafsi nilitaka kwenda mahakamni kufungua kesi, lakini rafiki yangu mmoja Leornad aliniambia kuna mtu mmoja anaitwa Kiwanga Doctors anaweza kunisaidia na kupata mali yangu bila kusumbuka sana.
Leornad alinipa mawasiliano ya Kiwanga Doctors kutokea Migori nchini Kenya na kuniambia niwasiliane naye mara moja, nilimpigia na kueleza shida yangu hiyo iliyokuwa inanisumbua, aliniambia nisijali kwani ndani ya siku chache mwenyewe atarudisha gari langu maana ameshafanya dawa, find lost items spell.
Baada ya siku chache yule dereva alinipigia simu akiwa hoi kitandani hata kuzungumza kwake ilikuwa kwa shida sana, aliniomba msamaha sana na kuniambia nikachuke gari langu. Nami nilienda nikachukua gari na kuweza kuendelea na biashara zangu na sasa nimepiga hatua kubwa kimaendeleo.
Tukio hilo ni la miaka mitano iliyopita, nimelikumbuka na kuandika stori yake hapa kwa sababu yule dereva hivi karibuni kanipigia simu na kusema tangu wakati ule kila akipata gari aendesha kwa ajili ya biashara anapata ajali, anaona kama imekuwa ni mkosi kwake.
Aliomba msamaha kwa mara ya pili na kuniambia nimuondolee mkosi huo, mimi nilichofanya ni kumpatia namba ya Kiwanga Doctors na kumtaka awasiliane naye na kumueleza changamoto yake.
Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.
KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MPANGO NA BAJETI YA OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2025/26

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa Mwaka wa fedha 2025/26 baada ya kupitia mafungu yote yaliyo chini ya ofisi hiyo na kujiridhisha.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo amezungumza hayo tarehe 27 Machi, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma alipokuwa akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo mara baada ya Wajumbe wa Kamati kujadili na kuridhia taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.
“Kamati imejadili na kuridhia kupitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa Mwaka wa fedha 2025/26, niwapongeze kwa maandalizi mazuri yenye uwazi, Kamati inawaasa kuwa na matumizi mazuri ya fedha pale zitakapopitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti ambapo tunaamini mtafikia malengo ya kuwatumikia watanzania kwa maendeleo ya nchi. Mhe. Kyombo amesema.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kwa kuwa na majadiliano mazuri na ofisi anayoiongoza ambayo wanaamini yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa majukumu yao kupitia bajeti hiyo.
Mhe. Mwenyekiti, nitoe shukrani za dhati kwa niaba ya ofisi ninayoiongoza mara zote tumepokea maoni, ushauri na michango mbalimbali kutoka katika Kamati yako inayolenga kuboresha Utumishi wa Umma nchini kwa lengo la kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na Utumishi wa Umma uliotukuka.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya ofisi hiyo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema Kamati hiyo imekuwa msaada mkubwa wa kuiongoza Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa kuwapatia maarifa mengi kutoka kwa Wajumbe wote wa Kamati hiyo yenye kuboresha utendajikazi.
Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kwa Mwaka wa fedha 2025/26 umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, Maelekezo ya Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22-2025/26).




Thursday, 27 March 2025
PAC YAISHAURI TEMESA KUONGEZA KASI YA USIMAMIZI MRADI WA KIVUKO KIPYA MAFIA NYAMISATI
UKATILI WA KIJINSIA NA MAAMBUKIZI YA VVU: CHANGAMOTO ZINAZOKUMBA WANANDOA NA JAMII YA KALENGA

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katika kijiji kidogo cha Kalenga kilichozungukwa na milima ya Iringa, hali ya kiuchumi imekuwa ikileta changamoto kubwa katika ndoa na familia. Miongoni mwa matatizo yanayojitokeza ni vitendo vya ukatili wa kijinsia na maambukizi ya virusi vya UKIMWI vinavyofanywa kwa maksudi.
Hii ni kutokana na wanawake ambao wamekuwa wakinyima waume zao haki ya tendo la ndoa kutokana na changamoto za kifedha, hali inayosababisha migogoro ya familia na jamii kwa ujumla.

Wakati hali hii inashika kasi, wanawake wengi katika Kata ya Kalenga wameshtumiwa kwa kunyima waume zao haki ya tendo la ndoa kwa kigezo cha kukosa fedha. Hali hii inatokea hasa wanapoingia katika matatizo ya kifedha, ambapo wanawake wanapinga kutoa unyumba hadi wapate kiasi fulani cha fedha.
"Mwanamke anaweza kumwambia mumewe, bila kiasi cha shilingi 20,000, basi sikupi tendo la ndoa, anavaa suruali na kujifunga mfuko wa sandarusi ili mumewe asimshike" alieleza Rose.
Hii ni changamoto kubwa kwa wanandoa katika Kata ya Kalenga, ambapo hali ya kiuchumi inavyozorota, ndivyo vitendo vya ukatili vinavyozidi kukithiri.
Wanandoa wanapokosa kushughulikia migogoro yao kwa njia za kiraia au za kiutu, wanageukia mikakati hatari ya kulipiza kisasi, jambo ambalo lina madhara makubwa kwa afya na ustawi wa familia zao.
Elimu na Huduma kwa Jamii: Njia ya Kupambana na Ukatili
Kituo cha Taarifa na Maarifa, kilichoanzishwa miezi sita iliyopita, kimekuwa na jukumu kubwa la kutoa msaada kwa wanandoa na familia zinazokumbwa na changamoto za kiuchumi na ukatili wa kijinsia.
Hadi sasa, kituo kimepokea kesi sita zinazohusiana na migogoro ya ndoa, vipigo, ulawiti, na kunyimana tendo la ndoa, pamoja na matatizo mengine yanayohusiana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Rose Wisiko alieleza kwamba, licha ya changamoto nyingi, wananchi wamekuwa na muitikio mkubwa katika kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kutokana na elimu waliyoipata.
"Wananchi wamejua haki zao, na sasa wanajua ni wapi pa kwenda pindi wanapojikuta katika hali ya ukatili," alisema Rose, akisisitiza kuwa kituo hicho kinatoa huduma kwa usiri ili kuhakikisha kwamba waathirika wanapata msaada bila aibu.
Kwa upande mwingine, katika Kata ya Mabogini mkoani Kilimanjaro, Hatangimana Justine, Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa, alisema kuwa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia inatolewa katika vijiji vyote vya kata hiyo.
Mikutano ya vijiji, klabu za watoto, na shule za msingi na sekondari ni sehemu muhimu ya kufikisha ujumbe huu kwa jamii.

Hatangimana alisisitiza kwamba lengo la elimu hii ni kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa wa kuchukua hatua stahiki wakati wanapokutana na vitendo vya ukatili.
"Tunataka jamii iwe na uwezo wa kuchukua hatua mara moja, na hivyo kuzuia madhara makubwa yanayotokana na ukatili wa kijinsia," alisema.
Changamoto za Kimasai: Dhana za Kijadi na Elimu
Hata hivyo, changamoto kubwa katika baadhi ya maeneo ni dhana za kijadi zinazohusisha jamii za Kimasai, ambazo mara nyingi haziruhusu watoto wa kiume, hasa wa kwanza, kupata elimu.
Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya Mgagao, mkoani Kilimanjaro, kimekuwa kikipambana na dhana hii, kuhakikisha watoto wote wanapata haki ya elimu bila kujali jinsia au umri.
Beatrice Msofe, Mwenyekiti wa Kituo hicho, alisema kuwa jamii ya Kimasai bado inakutana na changamoto kubwa katika kumfundisha mtoto wa kike au wa kiume.
"Tunajitahidi kubadilisha mtindo huu wa kijadi ili kuhakikisha kwamba kila mtoto anapata haki ya elimu," alisema Beatrice.
Kuhamasisha Jamii: Msingi wa Maendeleo na Ustawi wa Familia
Kama ilivyo katika maeneo mengine ya nchi, elimu kuhusu ukatili wa kijinsia ni muhimu kwa jamii. Katika maeneo kama Kalenga na Mabogini, kutoa elimu ya haki za binadamu na jinsi ya kushughulikia changamoto za kifedha ni hatua muhimu katika kupambana na ukatili wa kijinsia.
Hii si tu inasaidia kupunguza matukio ya vurugu na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, bali pia inachochea maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla.
Kwa kuwa jamii inaendelea kukabiliana na changamoto hizi, ni dhahiri kuwa elimu na ushirikiano wa viongozi wa kijiji na serikali utakuwa msingi wa kufanikisha mabadiliko chanya.
Majukumu ya kila mmoja katika kulinda haki za binadamu na kuhakikisha usalama na afya ya familia ni muhimu katika kujenga jamii imara na yenye ustawi.




















