Saturday, 8 March 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 8,2025



Magazeti















Share:

Friday, 7 March 2025

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI WAASWA KUWAHAMASISHA WANANCHI


Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari kutoka halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam leo Machi 07,2025.

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari kutoka halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam leo Machi 07,2025.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akifafanua jambo.


Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba ya kufunga mafunzo hayo
Na. Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwahamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao.

Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari kutoka halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ya nadharia na vitendo namna ya kutumia vifaa vitakavyotumika kwenye zoezi hilo ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari mkoani humo ambao utaanza tarehe 17 hadi 23 Machi, 2025.

“Mnahimizwa kuhamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao,” amesema Jaji Mbarouk.

Ameongeza kuwa Tume inatarajia kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika watu watakaokuwa wamepatiwa kadi watakuwa ni wapiga kura halali.

“Jukumu la uhamasishaji linawahusu moja kwa moja ninyi watendaji, kwa kushirikiana na wadau wengine katika maeneo yenu kupitia nyenzo mlizo nazo,” amesema Jaji Mbarouk.

Amewasisitiza kuhakikisha kuwa sambamba na kuwahamasisha wananchi wasambaze mabango waliyopewa na Tume kwenye maeneo yao ya kiutendaji ili wananachi wapate habari za kina kuhusu zoezi hilo.

“Mabango na vipeperushi mtakavyopewa na Tume mvisambaze mapema katika kata zote zilizopo katika halmashauri zenu na kutokea huko yafike vituoni ili iwe rahisi kwa wapiga kura na wadau wengine kujua vituo viko wapi,” amesema.
Jaji Mbarouk amewaasa kuwa licha ya shughuli nyingi za kiutendaji walizonazo watendaji hao wafuatilie kwa karibu zoezi hilo na kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha kuwa linafanikiwa.

Kuhusu watumishi wa vituoni, Jaji Mbarouk amesema “ni vyema kuwasisitiza watendaji walio chini yenu kuzingatia matumizi ya lugha nzuri pamoja na kufanya kazi vituoni muda wote hata kama hakuna waombaji wanajitokeza.”.

Katika hatua nyingine Jaji Mbarouk amewakumbusha watedaji hao kuhusu uwepo wa mawakala wa vyama vya siasa na kuwasisitiza kuhusu umuhimu wa kuwapa ushirikiano kwa kuwa ni wadau muhimu.

“Wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura hivyo wapewe ushirikiano,” amesema.
Share:

TUTAENDELEA KUTENGENEZA SERA RAFIKI KUVUTIA UWEKEZAJI SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA - KAMISHNA SHIRIMA


📌 Asema Sekta ya Mafuta nchini imeimarika

📌 Ataja miradi ya kimkakati ujenzi wa mabomba ya gesi na mafuta

Kamishna wa Petroli, Goodluck Shirima amesema kuwa, Tanzania  imejipanga vyema  kutengeneza sera rafiki zitakazozidi kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya Mafuta na Gesi Asilia ambazo zitawezesha pia kupata mitaji ya kuendesha Sekta kwa ufanisi.

Kamishna Shirima amesema hayo  leo jijini Dar es Salaam wakati wa  Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25) linalofanyika kwa  Siku Tatu jijini Dar es Salaam.

“ Katika  Mkutano wa EAPCE’25 tumejadili kuhusu umuhimu wa kuwa na mikataba ambayo ina uwazi, inayotabirika na yenye manufaa kwa nchi na kwa wawekezaji. Mabenki na taasisi za kifedha zipo tayari na zina hamu ya kufadhili miradi hii, sisi kama Serikali jukumu letu ni kutengeneza mazingira sahihi kupitia sera zetu na sheria.” Amesema Shirima

Kuhusu Sekta ya Mafuta nchini, amesema kuwa imeimarika kwani mafuta yapo na yanapatikana kwa bei himilivu na kwamba sasa bei ya kushushia mafuta kwenye bandari zote zinafanana kwa lengo la kupunguza gharama kwa Watanzania.

Kuhusu mkondo wa kati wa petroli, Shirima amesema kuwa Serikali inaendelea kuwa na miradi ya kimkakati ya usafirishaji mafuta na gesi ambapo Serikali ya Tanzania na Zambia ziko kwenye mazungumzo ili kujenga bomba jipya la kusafirisha mafuta ambalo litasaidia kusambaza mafuta pia katika sehemu ambazo linapita kama vile Morogoro, Njombe na Mbeya.

Ameongeza kuwa, kuna mazungumzo yanaendelea na Serikali ya Uganda ili kujenga bomba la kusafirisha mafuta safi kutoka Tanzania kwenda Uganda na pia ujenzi wa bomba la gesi kwenda nchini humo ambalo pia litasambaza gesi sehemu ambazo linapita.

Amesema kuwa chini ya uongozi madhubuti wa Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko  miradi hiyo itatekelezwa kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, Mhandisi Joyce Kisamo kutoka Wizara ya Nishati amesema kuwa mkutano huo ambao umeendeshwa kwa mafanikio umehudhuriwa na Viongozi wa Ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya Mawaziri, Makatibu pamoja na Wataalam wabobezi wa Sekta kutoka nchi 6 za Afrika Mashariki.




Share:

BUWSSA NA MIKAKATI YA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI KUTOKA ASILIMIA 64 HADI 32



Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

MKURUGENZI Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda Bi. Ester Gilyoma ameeleza Mikakati ya kupunguza Upotevu wa maji katika mjinhuo ambapo amesema mwaka 2021 upotevu ulikuwa asilimia 64 lakini kwasasa ni asilimia 32 kutokana na maboresho ya bomba chakavu na ubadilishaji wa mita goi goi.

Bi Ester ameyasema hayo mapema Leo hii Jijini Dodoma Machi 6,2025 wakati akizungumza na Wanahabari akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan.

Na kuongeza kuwa upotevu wa maji wa asilimia 64 ulitokana na mtandao wa bomba chakavu uliojengwa kutoka mwaka 1972 lakini Serikali ya awamu ya sita ilitoa fedha na kufanya matengenezo ya bomba hizo pamoja na mita.

"Upotevu wa maji kwa 2021 ulikuwa wastani wa asilimia 64 kutokana na mtandao wa bomba chakavu uliojengwa kuanzia mwaka 1972,baada ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita za kutoa fedha na kubadili bomba chakavu na mita goi goi upotevu wa maji kwasasa ni asilimia 32 na unaendelea kushuka kutokana na jitihada zinazoendelea kufanyika".

Aidha amesema kuwa tangu awamu ya sita kuingia Madarakani Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda imepitishiwa
miradi ya thamani ya TShs 28,180,572,033.71 na Tshs 11,894,976,776.81 taryari zimepokelewa
na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea.


Mamlaka hiyo pia imenufaisha wakazi 195,848 mwaka 2024 kati ya hao Asilimia 85 yenye sawa na wakazi 165,613 wamepata huduma ya maji ya bomba Kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt samia.

Ambapo amebainisha chanzo cha maji hayo kuwa ni ziwa vikitoria ambapo kuna umbali wa kilomita 24.8 kutoka katika kijiji cha Nyabehu na uzalishwaji wake ni wastani wa mita za ujazo 2976m3 kwa siku.

Pamoja na kupambana na usafi wa mazingira kwa sasa Mamlaka ya maji safi Bunda inaujenzi wa mradi wa miundombinu ya majitaka katika eneo la Butakale ,kwa ajili ya usafi wa mazingira na mradi utakamika ndani ya mwaka huu wa fedha 2024/2025.

Vile vile Mwenyekiti wa bodi ya maji safi bunda Bwana Jushua chacha Merumbe, ameeleza kuwa hali iliyopo sasa hivi bunda ni bora kuliku hapo awali pia amesema kwa kata 13 zilizopatiwa maji zinaendelea kutumia na kufurahia huduma hiyo ambayo awali ilikuwa ni changamoto kwa wakazi wa mji wa Bunda.
Share:

RC MACHA AWASISITIZA WANAWAKE KUJITOKEZA KUSHIRIKI FURSA ZA KIUCHUMI.



Na. Paul Kasembo, MSALALA DC

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewasihi wanawake na wasichana mkoani Shinyanga kujitokeza kwa wingi kushiriki katika fursa mbalimbali za kiuchumi na ujasiriamali zinazojitokeza ili kujiimarisha kiuchumi.


RC Macha ameyasema haya Machi 6, 2025 kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika Kata ya Bugarama, Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na Viongozi wa Taasisi za Serikali na Binafsi,Watumishi pamoja na wanachi, maadhimisho yenye Kaulimbiu “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”.


“NIchukue fursa hii kuwahimiza wanawake na wasichana wote kujitokeza kushiriki katika fursa mbalimbali za kiuchumi na ujasiriamali zinazojitokeza ili kujiimarisha kiuchumi”, amesema RC Macha.


Aidha RC Macha ameongeza kwa kuwasihi wananawake kutumia nishati safi ya gesi na umeme ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuifanya Tanzania iwe na matumizi ya nishati safi na utunzaji wa mazingira.


Akiwasilisha taarifa fupi ya shughuli zilizofanyika kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake kwa siku 3, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson amesema kuwa wamefanikiwa kushirikiana na wajasiriamali 15, Taasisi takribani 9 zimeshiriki maonesho na kutoa huduma, zoezi la ugawaji miti ili kutunza mazingira pamoja na kongamano kubwa la wanawake ambapo wanawake takribani 466 walihudhuria na kupata elimu ya masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi mkoani Shinyanga Dkt. Regina Malima ameshauri kuanzishwa kwa sera na mikakati ya kuwakwamua wanawake na wasichana kiuchumi sambamba na utoaji elimu endelevu ili wafahamu fursa zilizopo za kuwawezesha kiuchumi.


Maadhimisho ya Siku ya Wanawake mkoani Shinyanga yamehitimishwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Anamringi Macha ambaye ndiye mgeni rasmi ambapo yaliambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo maandamano, kutembelea mabanda ya maonesho pamoja na utoaji hundi za mikopo ya Serikali ya asilimia 10 kwa vikundi kwenye Halmashauri.

Share:

Thursday, 6 March 2025

WANAWAKE WASISITIZWA KUGOMBEA NA KULETA ULINGANIFU KATIKA NGAZI MBALIMBALI ZA UONGOZI

 



NA NEEMA NKUMBI- MSALALA

Wanawake wanatakiwa kuhudhuria na mabinti zao katika makongamano ya wanawake ili kujifunza na kuwajengea uwezo katika maisha.


Hayo yamesemwa Machi 5, 2025, na Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mkoa wa Shinyanga, Regina Malima, katika kongamano la Wanawake lililofanyika Bugarama, Halmashauri ya Msalala, Mkoani Shinyanga.


"Tunakubali kuwa wanaume ni kichwa cha familia na pia wana mamlaka, lakini kuwa na uchumi mzuri hakukufanyi kuacha majukumu yako kama mwanamke," amesema Malima.


Mbunge wa Viti Maalumu, Santiel Kirumba, amesema kuwa kila mwanamke ana uwezo wa kuwa kiongozi, na kwamba wanawake wanapaswa kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.


"Mwanamke ana uwezo wa kuongoza familia, hivyo anatakiwa pia kuwa na nafasi katika uongozi wa taifa," amesema Kilumba.


Mwezeshaji wa afya ya akili ameeleza kwamba katika jamii tunayoishi, kuna matarajio yanayoleta athari kubwa kwa wanawake, ikiwa ni pamoja na watoto kulazimishwa kuolewa, vipigo, na maneno yasiyostahili, Hali hii inaathiri sana afya ya akili ya wanawake, na inasababisha msongo wa mawazo.


Mwezeshaji huyo amebainisha njia za kuondokana na changamoto za akili, ikiwa ni pamoja na kupata muda wa kulala, kufanya mazoezi mara kwa mara yanayoendana na afya zao, kuwa na mahusiano chanya, na kuchangamana na watu wanaofaa katika maisha yao.


Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga, Lydia Kwesigabo, amesisitiza kuwa wazazi wanatakiwa kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto, kuimarisha mahusiano mazuri kati ya wazazi, na kutoa adhabu sahihi kwa watoto.

"Ukali wa kupitiliza husababisha watoto kuwa waongo," alisema Kwesigabo.


Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Rehema Edson, ameonyesha takwimu za ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi, akisema kuwa katika ngazi ya uongozi kuanzia Mkuu wa Mkoa, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Idara, Watendaji wa Kata na Watendaji wa Kijiji, wanaume ni 1497 sawa na asilimia 86%, huku wanawake wakiwa ni 243 tu, sawa na asilimia 14%.


Rehema amesisitiza umuhimu wa wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuweka ulinganifu na usawa katika suala la uongozi.


Kongamano hili la wanawake limebeba kauli mbiu inayosema, "WANAWAKE NA WASICHANA 2025; TUIMARISHE HAKI, USAWA NA UWEZESHAJI," ikiwasisitiza wanawake na wasichana kuongeza juhudi katika kukuza haki, usawa, na uwezo wao katika jamii.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger