Thursday, 27 February 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 27,2025



 





Share:

Wednesday, 26 February 2025

WILDAF YAWAOKOA NA VITENDO VYA UKATILI ZAIDI YA WASICHANA 700 KUTOKA MIKOA YA SHINYANGA NA MARA, CANUCK YAAHIDI KUSHIRIKIANA NAO

Mkuu wa chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata Kahama (St Fransis Vacation Center) Father John akipokea zawadi kutoka kwa wahitimu wa mahafali ya 25 ya chuo hicho.


Shirika la Wanawake katika sheria na Maendeleo Barani Afrika(WilDAF) kwa kushirikiana na UN-FPA kwa ufadhili wa serikali ya Finland, kupitia mradi wa ‘Chaguo langu haki yangu’ limefanikiwa kuwaokoa mabinti balehe na vijana wamama zaidi ya 700 kutokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.


Afisa mradi wa mradi wa chaguo langu haki yangu Joyce Kessy katika mikoa ya Mara na Shinyanga amesema mradi huo unalenga kuwafikia mabinti balehe na wanawake vijana kati ya umri wa miaka 10-19 na 15 – 24, kuwalinda dhidi ya ukatili, ndoa na mimba za utotoni pamoja na ukeketaji kwa mkoa wa Mara.


Ameyazungumza hayo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mahafali ya 25 ya chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata Kahama (St Fransis Vacation Center) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo mabinti balehe na wanawake vijana zaidi ya 270 wamehitimu na kutunukiwa vyeti vyao tayari kwa kujiajiri/kuajiriwa.


Bi Kessy amesema mradi huo pia umelenga zaidi wenye ulemavu katika makundi hayo kwani wanaonekana kusahaulika zaidi na jamii, huku likiwa katika uhatarishi mkubwa wa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia.


Amesema WiLDAF kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la idadi ya watu ulimwenguni UNFPA kwa ufadhili wa serikali ya Finland, iliona suala kubwa ni kutoa nafasi kwa wale waliopo nje ya shule kujiunga na vyo vya VETA ikiwemo VTC Mwakata ili kujifunza fani tofauti tofauti ili wawe na uwezo wa kujiajiri, kuajiriwa ili kujikwamua kiuchumi hali itakayowasaidia kuepukana na vitendo vya ukatili.


“Kama tunavyofahamu kwamba uchumi duni unachangia kwa kiasi kikubwa sana vitendo vya ukatili, kwa hiyo sisi tunamwezesha binti kiuchumi, tunampa ujuzi, ili aweze kuinuka kiuchumi kama nyenzo ya kujikwamua dhidi ya vitendo vya ukatili” Alisema Kessy


Amesema wahitimu hao baada ya mafunzo wanawapatia vifaa kulingana na fani walizosomea ili waweze kutekeleza ujuzi wao kwa vitendo na kubadilisha maisha yao, na kwamba mabinti hao 787 wamefikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji wa mradi wa “Chaguo langu, haki yangu” uliotekelezwa katika wilaya mbili za mkoa wa Mara(Butiama na Tarime) na mbili za mkoa wa Shinyanga (Kishapu na Kahama).


Kati ya mabinti hao 263 wameshapatiwa vifaa na kwamba waliobaki wanakwenda kupatiwa vifaa vyao hivi karibuni kulingana na fani husika baada ya awamu hii ya mwisho kuhitimu, na kueleza kuwa mambo haya yote yanafanyika kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.


Akizungumza kwa niaba ya serikali ya manispaa ya Kahama, wakati wa mahafali hayo, afisa ustawi wa jamii kutoka manispaa hiyo Swahiba Chemchem alisema kuwa, serikali iko tayari kuwaunga mkono mabinti hao hata wanaporejea mtaani, sambamba na kuwaunganisha na fursa mbalimbali zitakazojitokeza.


Baadhi ya wahitimu Vaileth Charles mhitimu wa fani ya ushonaji kutoka Kishapu, aliishukuru WiLDAF kwa kuwawezesha kutimiza ndoto zao na kuwaomba waongeze muda zaidi wa utekelezaji wa mradi huo kwa mabinti wengi bad oni wahanga wa ukatili haswa mimba na ndoa za utotoni, sambamba na wao kutokuwa tegemezi.


Awali akisoma risala ya wahitimu kwa niaba ya wahitimu wenzake, kwa mgeni rasmi, ambaye ni afisa mahusiano wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu – Canuck Clarence Haule, mhitimu Debora Martin amelishukuru shirika la WiLDAF, uongozi wa chuo pamoja na serikali kwa kuwapatia fursa hiyo, ambayo imewasaidia kupata ujuzi mbalimbali, utakaowasaidia kujiajiri au kuajiriwa, huku wakiomba zinapotokea fursa mgodini hapo basi viongozi wasisite kuwapa kipaumbele.


Kwa upande wake Mwalimu wa chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata Kahama (St Fransis Vacation Center) Mwalimu Monica Daniel akisoma historia ya chuo hicho alisema kimeanzishwa mwaka 2003, na kilianzishwa na padreJoseph Elian aliyekuwa mkuu wa chuo chini ya mkuu wa shirika la Mt Fransisco wa sales.

Mwalimu Monica alisema chuo kimefanikiwa kuwajengea uwezo mzuri wanafunzi wao ikiwemo tabia njema za kiroho na kuishi katika hofu ya Mungu, lakini pia chuo kimefanikiwa kuwatafutia wanafunzi wao maeneo ya kujifunza kwa vitendo baada ya kuhitimu mafunzo yao.


Akizungumza kwenye mahafali hayo, mgeni rasmi ambaye ni afisa mahusiano wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Canuck iliyopo kata ya Mwakata Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga Clarence Haule, kwa niaba ya meneja mkuu wa kampuni hiyo ameahidi kuchangia mifuko 50 ya saruji, kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa uzio wa chuo hicho, ikiwa ni utekelezaji kwa vitendo dhima ya kurejesha sehemu ya faida yake kwenye jamii inayozunguka mgodi (CSR).


Haule amesema uwepo wa uzio chuoni hapo, utasaidia usalama kwa wanafunzi, mali za chuo na kuondoa migogoro itokanayo na mwingiliano kati ya wanakijiji na chuo, huku akiutaka uongozi wa chuo kuainisha aina za mashine na gharama zake ili mgodi uone namna ya kusaidia kufanikisha jambo hilo.


Akizungumzia changamoto ya maji inayokikabili chuo hicho pamoja na maeneo jirani, Haule amesema tayari mgodi umeanza mchakato wa kupata maji safi na salama kutoka ziwa Victoria, na chuo hicho ni miongoni mwa maeneo yatakayonufaika zaidi na ujio wa maji hayo, na kwamba yameshafikishwa kwenye mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kahama – KUWASA, na sasa wanasubiri utekelezaji wao.


“Tunatambua kuwa hapa kijijini swala la upatikanaji wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi na jamii na jamii bado ni tatizo, hivyo kampuni inawaomba wote kwa ujumla tuwe na subra kwa maana kampuni imekwishafikisha ombi la kufikishiwa huduma na KUWASA” Alisema Haule

Baadhi ya wanafunzi na wahitimu wa chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata Kahama (St Fransis Vacation Center), wakitoa burudani, wakati wa mahafali ya 25 ya chuo hicho
Mkuu wa chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata , Father John akizungumza wakati wa mahafali ya 25 ya chuo hicho.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 25 ya chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata Kahama (St Francis Vacation Center) ambaye ni afisa mahusiano wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Canuck iliyopo kata ya Mwakata Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga Clarence Haule kushoto, akiwa na mmoja wa wazazi wa wahitimu, wakiwatunza watumbuizaji.
mkurugenzi wa WiLDAF akizungumza na wahitimu pamoja na wazazi kwenye mahafali ya 25 ya chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata
Wahitimu wa fani ya umeme katika chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata Kahama (St Francis Vacation Center) wakionyesha kwa vitendo kile walichojifunza wakati wa mahafali ya 25 ya chuo hicho mbele ya mgeni rasmi ambaye ni afisa mahusiano wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Canuck iliyopo kata ya Mwakata Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga Clarence Haule.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 25 ya chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata Kahama (St Francis Vacation Center) ambaye ni afisa mahusiano wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Canuck iliyopo kata ya Mwakata Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga Clarence Haule kulia akitoa vyeti kwa wahitimu.
Matron wa chuo cha ufundi stadi Veta Mwakata Kahama (St Francia Vacation Center) Magreth Alimosa, akiongoza zoezi la ukataji wa keki ya mahafali ya 25 ya VTC Mwakata kwa wahitimu na wageni waalikwa.
Share:

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA WITO KWA WANANCHI WA CHIPOGOLO KUSHIRIKI MAENDELEO



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo wakati alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wananchi wa Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akiwa ameongozana na wananchi wa Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo mara baada ya kuwasili katika Kijiji hicho alipofanya ziara iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene (aliyevaa miwani) akisisitiza jambo kwa Viongozi wa Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo wakati Waziri huyo alipofanya ziara iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene (aliyenyanyua mikono) akielekeza jambo kwenye korongo linalohitaji kujengwa daraja katika Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo wakati alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Wananchi na Viongozi mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo wakati alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti Mstaafu wa Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo Bi. Grace Ndogwe akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo wakati akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo mara baada ya kuwasili wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Na. Mwandishi Wetu-Chipogolo


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametoa wito kwa wananchi wa Kijiji cha Chamsisili, Kata ya Chipogolo, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kushiriki shughuli za maendeleo katika kijiji hicho.

Mhe. Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ametoa kauli hiyo tarehe 25 Februari, 20245 akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata hiyo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Chamsisili, Mhe Simbachawene amewasisitiza wananchi wa Kijiji hicho kuweka nguvu kazi kubwa kwenye daraja wanalokusudia kujenga kufuatia korongo kubwa lililoko sehemu ya Kijiji hicho.

Naomba mshiriki maendeleo katika Kata yenu, adha tunayoipata kwa kutokushiriki maendeleo ni kubwa, hivyo tujitahidi kutumia nguvu zetu wakati Serikali inatafuta namna ya kufanya kupitia taasisi yake ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA). Amesisitiza Waziri Simbachawene.

Katika kuhakikisha ujenzi wa daraja hilo unatekelezwa kwa haraka, Waziri Simbachawene ameahidi kuchangia mifuko 300 ya saruji.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Chipogolo, Mhe. Kayanda Mwanika amemshukuru Waziri Simbachawene kwa kufanya ziara hiyo ambayo italeta chachu kwa maendeleo ya Kata hiyo.

Vilevile Mhe. Mwanika amempongeza Waziri Simbachawene kwa ahadi ya mifuko 300 ya saruji itakayoongeza nguvu kubwa katika kukamilisha daraja hilo na kuahidi kushirikiana nae pamoja na wananchi wa Kijiji hicho kwa lengo la kuleta maendeleo.
Share:

TUMIENI VYAKULA VYA ASILI ILI KUDHIBITI UDUMAVU

 






Na mwandishi wetu Muleba


Wadau wa lishe Wilayani Muleba Mkoani Kagera wametakiwa kushirikiana na Serikali kuhamasisha wananchi kula vyakula vya asili ambavyo vipo kwenye maeneo yao ili kuweza kudhibiti udumavu dhidi ya watoto katika Wilaya hiyo.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bi. Edina Kabyazi ametoa  kauli hiyo  kwenye kikao cha kamati jumuishi ya lishe ngazi ya Wilaya cha robo ya pili ya Oktoba hadi Desemba mwaka 2024/2025 ambacho kimefanyika Februari 25, 2025  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.


Bi. Edna Kabyazi amesema kuwa jukumu la uhamasishaji wa ulaji wa vyakula vyenye lishe sio la Watalaam wa afya pekee bali ni jukumu la kila mdau wa maendeleo kwani panahitajika nguvu ya ziada na kutokata tamaa lengo likiwa ni kuhakikisha kila kaya inakuwa na lishe bora.


Awali akiwasilisha taarifa ya lishe Afisa lishe Wilaya ya Muleba Dkt. Robson Tigererwa amesema kuwa wameweza kufanya kampeni ya ugawaji wa matone ya vitamin A na dawa za minyoo ambapo walilenga kuwapatia watoto 119,737 na wameweza kuwapatia watoto 119,440 sawa na asilimia 99.


Dkt. Tigererwa amesema kuwa pia pamefanyika upimaji wa hali ya lishe kwa watoto 53,881 wenye umri wa miezi sita hadi 59 ambapo watoto wenye hali nzuri ya lishe ni 50,649 sawa na asilimia 94, wenye hali hafifu ya lishe ni 3,017 sawa na asilimia 5.6 huku watoto wenye hali mbaya ya lishe wakiwa ni 216 sawa na asilimia 0.4.


Aidha amesema kuwa bado kuna changamoto ya baadhi ya wazazi kugoma kuwapeleka watoto kwenye zoezi la chakula dawa pamoja na ushiriki mdogo wa wanaume kwenye masuala ya lishe hasa kwenye mafunzo na mikutano.


Nao baadhi ya washiriki ambao ni Johanes Mtoka na Gaudini Gration wameshauri kuwepo kwa mashamba darasa kwenye shule za msingi na Sekondari ili kuondoa changamto ya  wa uhaba wa chakula shuleni ambao umekuwa ukipelekea baadhi ya wanafunzi kuwa na udumavu kutokana na kushinda njaa siku nzima.

Share:

Tuesday, 25 February 2025

NGEZE AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUPAMBANIA AFYA YAKE



Na Lydia Lugakila - Bukoba

Mwenyekiti wa Alat Taifa,Diwani wa kata ya Rukoma Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe, Murshid Hashimu Ngeze amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu hassan kwa namna alivyosimama katika kugharamia matibabu  yake alipopata ajali Mwaka 2022 iliyopelekea kukatwa mguu wake mmoja.

Mhe, Ngeze ametoa kauli hiyo katika dua Maalum ya Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumnusuru katika ajali mbaya ambayo imeenda sambamba kuliombea taifa hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu ujao iliyofanyika kata Rukoma Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera  ikiongozwa na viongozi mbali mbali wa dini na madhehebu.

"Namshukuru Rais Samia pamoja na wasaidizi wake kwa juhudi zao za kugharamia matibu yangu ndani na nje ya Nchi tangu nilipopata ajali iliyopelekea kuvunjika mguu  mmoja hadi kupelekea kukatwa" ,amesema Mwenyekiti  Alat Taifa.

Ngeze amesema Rais Samia ana upendo anajali anasikiliza na sio kwamba anaangalia miradi tu bali anaangalia Afya za Watanzania.

Ngeze amesema kupona kwake kuliimarika siku tatu alipokuja Makamu wa Rais wa Tanzania kumuona Hospitalini kwa maelekezo ya Rais Samia aliyemtaka aeleze nini anataka kufanyiwa ili Afya ikae sawa.

Aidha kiongozi huyo amewashukuru Madaktari waliohusika katika kutoa huduma ya matibabu bila kuchoka, Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya Taifa na Mkoa, taasisi za kifedha viongozi mbali mbali wa kiserikali pamoja na mtu mmoja mmoja ikiwemo familia yake  kwa namna walivyoshirikiana kutoa huduma mbali mbali katika kipindi hicho kigumu.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Privatus Mwoleka,  akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Halmashauri hiyo amesema wanamshukuru Mungu kwa uhai wa kiongozi huyo lakini pia wanampongeza Rais Samia kwa matibabu aliyoyapata nje na ndani ya Nchi kwani Rais Samia amegharamikia matibabu ya Ngeze kwa  asilimia 80.

Mkuu wa Wilaya Bukoba Erasto Sima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa amesema Kata ya Rukoma imekuwa mfano katika shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia Mwenyekiti Ngeze, ambaye amekuwa chachu ya kusimamia miradi inatekelezwa kwenye halmashauri hiyo yenye vijiji 94 kata 29.

Baadhi ya Viongozi wa dini waliongoza dua hiyo ni pamoja na Mchungaji Mathias Buberwa wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kaskazini Magharibi, Padre Achileus Rugemalia wa Poroko Ichwandimi pamoja na Sheikh Twahir Said wa Wilaya Bukoba.

Kwa pamoja wameliombea Taifa la Tanzania liendelee kuwa na amani umoja na mshikamano, ili viongozi wake wajaliwe rehema na busara katika kutekeleza majukumu yao kuanzia vitongoji hadi taifa na kuliepusha na migogoro mbalimbali.
Share:

TPA YAELEZA MAFANIKIO YAKE KWA KIPINDI CHA MIAKA MINNE



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema tangu Serikali ya awamu ya Sita iingie madarakani,mapato ya mamlaka hiyo yameongezeka kutoka shilingi trilion 1.1 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi shilingi trilion 1.475 Mwaka wa Fedha 2023/24.

Hayo yameelezwa leo jijini hapa February 24,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa TPA Plasduce M. Mbossa wakati akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Mamlaka hiyo (2021/22 – 2023/24) ikiwa ni mafanikio ya Mamlaka hiyo tangu Serikali ya awamu Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iingie madarakani.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/23 mchango wa sekta ya bandari ulikuwa Shilingi trilioni 10.8 sawa na asilimia 7.3 ya pato la Taifa lililokuwa Shilingi trilioni 148.3.

"Ongezeko hili la mapato limetokana na:Mapato ya matumizi ya bandari kuongezeka kutokana na ongezeko la shehena iliyohudumiwa bandarini
Mapato ya kuhudumia meli ambayo yameongezaka kutokana na ongezeko la idadi ya meli na ukubwa wa meli,Mapato ya mrabaha kwa tani au kasha linalohudumiwa na Kampuni ya DPW Dar es Salaam na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEGTL) pamoja na tozo la pango (Lease Rent) la maeneo ya bandari iliyolipwa na kampuni hizo kwenda Serikalini kupitia TPA, "amesema

Akizungumzia kuhusu utendaji wa kipindi cha Julai-Desemba, 2024
Katika kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2024/25 (Julai-Desemba, 2024)amesema jumla ya Shehena iliyohudumiwa na Bandari za TPA ni tani milioni 15.49 ambayo imezidi lengo lililowekwa la kuhudumia tani milioni 14.60 kwa asilimia 6.1, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 11.1 ikilinganishwa na tani milioni 13.94 iliyohudumiwa kipindi kama hiki mwaka uliopita (Julai-Desemba, 2023).

Amesema jumla ya Shehena ya Makasha iliyohudumiwa na Bandari za TPA ni Makasha TEUS 565,361, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 4.9 ikilinganishwa na shehena ya Makasha TEUS 539,013 iliyohudumiwa kipindi kama hiki mwaka uliopita (Julai-Desemba, 2023).

Mkurugenzi huyo pia amesema kuwa mamlaka hiyo ikiwa na dhamana ya kutangaza Bandari kimasoko (Promote),
Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Bandari (Safety and Security),
Kushirikisha na kusimamia Sekta Binafsi katika uendeshaji wa shughuli za Bandari (Landlord)kwa sasa ina simamia Bandari rasmi 131 zilizoko katika Bahari ya Hindi na Maziwa Makuu.

Akizungumzia hali ya utendaji wa TPA amesema imeboreka ambapo
Jumla ya Shehena iliyohudumiwa
Katika kipindi hiki jumla ya shehena iliyohudumiwa na TPA imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 15.23 kwa mwaka kutoka tani milioni 20.78 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi tani milioni 27.55 Mwaka wa Fedha 2023/2024.

"Jumla ya shehena iliyohudumiwa katika Bandari ya DSM iliongezeka kwa wastani wa asilimia 13.38 kwa mwaka kutoka tani milioni 18.67 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi tani milioni 23.98 Mwaka wa Fedha 2023/2024,ongezeko la shehena limetokea baada ya Serikali ya Awamu ya Sita kukamilisha miradi mbalimbali ya ujenzi na maboresho ya miundombinu ya Bandari nchini ikiwa ni pamoja na kukamilisha mradi wa maboresho na uendelezaji wa Bandari ya Dar es Salaam ,"amefafanua

Mbossa amesema Shehena ya Makasha Jumla ya shehena ya Makasha (Containers) iliyohudumiwa imeongezeka kwa wastani wa asilimia 12.9 kwa mwaka kutoka makasha (TEUs) 823,404 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi makasha (TEUs) 1,050,486 Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Aidha, jumla ya Shehena ya Makasha iliyohudumiwa katika Bandari ya DSM imeongezeka kwa wastani wa asilimia 10.7 kwa mwaka kutoka makasha (TEUs) 816,368 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi makasha (TEUs) 998,872 Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Amesema ongezeko la makasha katika Bandari ya Dar es Salaam limetokana na maboresho ya uendeshaji wa vitengo vya makasha vya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuviweka chini ya uendeshaji wa Sekta Binafsi wa Kampuni ya DP World Dar es Salaam na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL) ambazo zimewekeza kwa kufunga mitambo ya kisasa ya kuhudumia shehena pamoja na mifumo ya kisasa ya TEHAMA ya uingizaji na uondoshaji wa makasha bandarini.

Amesema ili kuongeza maboresho zaidi,Serikali kupitia TPA iliingia mikataba ya ushirikishaji na usimamizi wa sekta binafsi kwa ajili ya kuendesha Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi katika bandari hiyo.

"Shughuli za uendeshaji wa Kitengo Na. 1 cha Bandari ya Dar es Salaam gati
Shughuli katika kitengo hiki zilianza kukabidhiwa kwa awamu kwa Kampuni ya DP World Dar es Salaam mwezi Aprili 2024,Kampuni ya DP World Dar es Salaam inaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Uwekezaji ambao unakusudiwa kugharimu kiasi cha Dola za Marekani (USD) 250 Milioni (sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 675) kwa kipindi cha awali cha Mkataba cha Miaka mitano, "amesema

Amesema hadi sasa, Kampuni ya DP World imefanya uwekezaji wa awali katika maeneo mbalimbali ya uendeshaji ili kuboresha na kuongeza ufanisi wa huduma za bandari ambalo ni dhumuni kuu la kuingiwa kwa Mikataba kama ilivyoelezwa hapo awali.

Pia amesema Uwekezaji wa awali uliogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 214.42 umefanywa katika maeneo mbalimbali ikiwemo ununuzi na usimikaji wa mitambo krini za kisasa za kuhudumiwa shehena ya makasha uliogharimu Shilingi Bilioni 115.80 na Ununuzi na usimikaji wa mitambo nane inayotambulika kama “Rubber Tyred Gantry Crane-RTG” katika Gati Na. 1 la makasha la Bandari ya Dar es Salaam iliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 96;

Ununuzi wa ‘terminal tractors’ ishirini (20) ambazo hutumika katika kuhamisha na kusafirisha shehena kutoka eneo moja la bandari kwenda eneo jingine .

Vilevile amesema Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TPA inaendelea kutekeleza mapendekezo ya mpango kabambe ya maendeleo ya bandari nchini (2020 – 2045) na programu ya uboreshaji na uendeshaji wa bandari ambao ni mpango wa kitaifa (National Projects Management Information System – NPMIS) ambayo ilisajiliwa Oktoba, 2023 kwa jina la Tanzania Ports Development and Management Programme na kupewa namba ya mradi 4300.

"Katika Programu hiyo Serikali kupitia TPA itaenda kutekeleza miradi 10 ya kimkakati ikiwemo ya kupokelea na kuhifadhia mafuta SRT ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 17 na unagharimu dola za kimarekani million 265,Mradi huu ukikamilika utapunguza siku za kuhudumia meli zenye ujazo wa 150,000 DWT kutoka siku kumi (10) mpaka tatu (3),"amesema.

Ametaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa kituo cha reli na mtandao wake ndani ya bandari ya Dar es Salaam na unagharimu dola za kimarekani million 119.955 na kwamba ukikamilika utapunguza kiwango cha asilimia 98 cha shehena inayotoka bandarini kwa kutumia njia ya barabara na kupelekea kutatua tatizo la msongamano wa malori ndani na nje ya bandari.




Share:

NHC YAAGIZWA KUTOA GAWIO LA BILIONI 10 KWA SERIKALI

 


 ****

Na Mwandishi wetu 

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuweka lengo la kutoa gawio serikalini la bilioni 10 kwa mwaka Ujao wa fedha. 

Kauli hiyo ameitoa katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa NHC kilichofanyika mkoani Pwani mapema leo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mchechu awakumbusha wafanyakazi wa NHC kuwa umoja, upendo, na mshikamano katika utendaji wao wa kazi ni muhimu kwa maendeleo ya taasisi hiyo. 

Amesema kuwa, bila kushirikiana, taasisi hiyo itakuwa ngumu kufikia malengo yake ya kiuchumi.

"Miradi inayotekelezwa na NHC katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mtwara, Lindi, na Iringa inakaribia kukamilika, na italeta manufaa makubwa kwa taifa. Hivyo, ni muhimu wafanyakazi wa NHC kufanya kazi kwa bidii, kwa uwajibikaji na kwa umoja ili kufanikisha malengo haya," amesema Mchechu.

Mchechu ameongeza kuwa, wafanyakazi wa NHC wanapaswa kutokuwepo na majivuno na kutokuwa na utovu wa nidhamu katika kazi. 

Amesema kuwa maisha ni mafupi, na hivyo ni vyema wafanyakazi wa NHC kupendana na kufanya kazi kwa kujituma ili taasisi iweze kufikia malengo yake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Ahmad Abdallah, amewakumbusha wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa uwadilifu na katika muda uliotakiwa. 

Amesisitiza kuwa, ili taasisi iweze kufikia malengo ya kifedha yaliyowekwa, kila mfanyakazi anapaswa kuchangia kwa kiwango cha juu.

NHC imejipanga kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa nyumba na miundombinu katika mikoa mbalimbali, na Mchechu amesema kuwa, kama miradi hii itafanikiwa, itachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya taifa.








Share:

Monday, 24 February 2025

Video Mpya : ROGETI Ft. JINASA MADEBE - MJINI

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger