Monday, 24 February 2025

AFARIKI KWA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME AKIJARIBU KUIBA NYAYA ZA TRANSFOMA SHINYANGA



Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kijana aliyejulikana kwa jina la Daniel Mussa Mageni (27) mkazi wa Kitangili Manispaa ya Shinyanga amefariki dunia kwa kukosa hewa baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akijaribu kuiba nyaya katika Transfoma iliyopo katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mashuhuda wanasema kuwa Daniel mkazi wa Kitangili Shinyanga Mjini aliyezaliwa Kilulu wilaya ya Bariadi Mkoa wa Shinyanga amekutwa amefariki katika Transfoma iliyopo jirani na Zahanati ya Isela kata ya Samuye leo asubuhi Februari 24,2025, huku baiskeli aliyotumia kusafiria na vifaa alivyokuwa akivitumia kukata nyaya vikiwa eneo la tukio. 
Sehemu ya waya uliokuwa tayari umekatwa 

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isegeneja, bi. Amina Hamis Bwire amesema mwanaume huyo amebainika kupoteza maisha dunia majira ya saa mbili asubuhi baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akijaribu kujuhumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Mhandisi Mwandamizi wa TANESCO Mkoa wa wa Shinyanga, Anthony Tarimo akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga amesema kijana huyo amefariki dunia wakati akiingilia njia ya umeme mkubwa katika Transfoma hiyo.

“Kitaalamu ameingilia njia ya umeme mkubwa, ameingilia usalama wa Transfoma akapata ajali hiyo. Alikuwa anajaribu kuiba nyaya za shaba zinazolinda usalama wa Transfoma”,ameeleza Mhandisi Tarimo.
Mhandisi Anthony Tarimo

Mhandisi Tarimo amewataka wananchi kuwa waangalifu na kuacha vitendo vya kuhujumu miundombinu ya umeme, akisisitiza kuwa ulinzi wa miundombinu hiyo ni jukumu la kila mmoja. 

“Ulinzi wa miundombinu ya umeme ni jukumu letu sote, toeni taarifa kuhusu wanaohujumu. Pia wananchi epukeni kusogea kwenye Transfoma na njia za umeme kwani ni hatari. Ukiangalia hata hapa kwenye hii Transfoma kuna onyo kabisa kwamba ni HATARI”,amesema Mhandisi Tarimo.

Amewahimiza wananchi kutoa taarifa pale wanapobaini uhujumu na uharibifu wa miundombinu na kuepuka kukaribia maeneo ya Transfoma, kwani ni hatari kwa maisha.

“Kwa upande wa usalama, miundombinu ya umeme ni hatari na tunapaswa kuepuka kujihusisha nayo kwa namna yoyote ile. Tunaomba wananchi wawasiliane na mamlaka husika pale wanapobaini watu wanaohujumu miundombinu,” ameongeza.

Jeshi la Polisi na Madaktari wamefika kwenye eneo la tukio kwa uchunguzi wa awali na mwili wa marehemu ulichukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Wakazi wa Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiangalia mwili wa Daniel Mussa Mageni (27) aliyefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme alipojaribu kuiba nyaya katika Transfoma.
Wakazi wa Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiangalia mwili wa Daniel Mussa Mageni (27) aliyefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme alipojaribu kuiba nyaya katika Transfoma.
Wakazi wa Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiangalia mwili wa Daniel Mussa Mageni (27) aliyefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme alipojaribu kuiba nyaya katika Transfoma.
Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Share:

MITENDEWAWA YABAHATIKA KUPATA MRADI MKUBWA WA UMEME

Kaimu Afisa Habari wa Huduma kwa Wateja TANESCO Ruvuma Emma Ulendo akizungumza na wananchi wa Mitendewawa
 
Afisa Habari na Uhusiano Tanesco Mkoani Ruvuma Allan Njiro akizungumzia namna ya kulinda miundombinu ya umeme katika kijiji cha Mitendewawa

Wananchi waliojitokeza kupata elimu ya jinsi ya kupata fomu ya maombi ya kupata umeme Mitendewawa



Na Regina Ndumbaro - Ruvuma

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Ruvuma limeendelea na ziara yake ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme. 

Ziara hiyo imefanyika katika kijiji cha Mitendewawa, kata ya Mshangano, ambako wananchi walipata fursa ya kufahamu hatua mbalimbali za kuhakikisha wanapata na kutumia umeme kwa usahihi.

Afisa Habari na Uhusiano wa TANESCO mkoani Ruvuma, Allan Njiro, amesema kuwa mradi mkubwa wa umeme umefanikiwa kutekelezwa katika kijiji cha Mitendewawa.

 Hata hivyo, mradi huo ulipitia changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vifaa maalum, hali iliyopelekea ucheleweshaji wa kukamilika kwa wakati uliotarajiwa. 

Pamoja na hayo, amewashukuru wananchi wa Mitendewawa kwa kuwa wavumilivu wakati wa utekelezaji wa mradi huo.

Njiro ameongeza kuwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya umeme, kijiji cha Mitendewawa kimebahatika kufungiwa transfoma mbili kwa ajili ya matumizi ya wananchi. 

Ameeleza kuwa kwa wale ambao bado hawajapata huduma ya umeme, mpango wa kuendelea na mradi mwingine upo na unatarajiwa kutekelezwa ifikapo mwezi Julai.

Aidha, amewakumbusha wananchi kuwa ni jukumu lao kuhakikisha miundombinu ya umeme inatunzwa vizuri ili kuepusha hasara kubwa inayoweza kutokea. 

Amewataka kuepuka ukataji miti kiholela karibu na nyaya za umeme na kuwa makini na matapeli wanaoweza kuwalaghai katika upatikanaji wa huduma hiyo. 

Pia, ameonya kuwa uharibifu wa miundombinu ya umeme husababisha hasara kubwa kwa serikali na kuwanyima wananchi huduma ya umeme.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Habari wa Huduma kwa Wateja TANESCO Ruvuma, Emma Ulendo, amewashauri wananchi kuhakikisha wanafanya wiring kwa kutumia vifaa bora. 

Ameeleza kuwa maombi ya kuunganishiwa umeme yanaweza kufanywa kupitia ofisi za TANESCO Ruvuma au kwa njia ya mtandao kwa kutumia mfumo wa "NIKONEKTI" unaorahisisha ujazaji wa fomu. Pia, amesisitiza umuhimu wa kulipa ada za umeme kupitia benki au simu ili kuepuka udanganyifu.

Ulendo ameongeza kuwa wale ambao bado hawajafanya wiring wanapaswa kutuma maombi haraka ili waweze kufanikisha upatikanaji wa huduma hiyo. 

Ameeleza kuwa umeme una faida nyingi, ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya ardhi na kurahisisha shughuli za biashara na maendeleo mengine ya kiuchumi.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mshangano, Samweli Mbano, ameishukuru TANESCO mkoani Ruvuma kwa jitihada zao za kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya umeme. 

Ameeleza kuwa elimu hiyo itawasaidia wananchi kuutumia umeme kwa usalama na kuhakikisha miundombinu inatunzwa ipasavyo.

Mbano pia ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhakikisha wananchi wa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya umeme. 

Ameeleza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Share:

KATAMBI AANZA ZIARA YAKE KATA KWA KATA SHINYANGA MJINI…WAJUMBE WA CCM WAKUMBUSHWA KUTETEA CHAMA NA VIONGOZI WAO


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Wajumbe na wanachama wa Chama cha Mapinduzi jimbo la Shinyanga Mjini wametakiwa kutetea na kuyasemea mazuri yanayofanywa na viongozi wa chama chao ili waweze kuendelea kutekeleza ilani ya chama hicho.

Hayo yamebainishwa leo Februari 23, 2025 wakati wa ziara ya kata kwa kata ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi yenye lengo la kukijenga chama na kusikiliza kero za wananchi ndani ya jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha amewahimiza wajumbe hao kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi na kuwakumbusha wajibu wao katika kuyasema mazuri yaliyofanywa na viongozi wa chama hicho na kuwatetea kwenye majukwaa dhidi ya watu wanaowakashifu.

"Tuendelee kuwahamasisha wasio wanachama kujiunga na chama chetu ili ifikapo Oktoba tuweze kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi wa kuwachagua viongozi wetu, lakini pia twendeni tukayaseme yale waliyofanya viongozi wetu ikiwemo wabunge, madiwani na Rais wetu kupitia majukwaa mbalimbali. Yanayosemwa juu ya viongozi wetu tuwe mstari wa mbele kuwatetea ili kuwapa moyo wa kuendelea kukitumikia", amesema Hamisa Chacha.

Diwani wa kata ya Kizumbi Mhe. Ruben Kitinya ameeleza ukuaji wa kasi wa kata hiyo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, umeme na maji na kumshukuru Mbunge Katambi kwa kuwapigania wananchi na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka minne huku akimuomba Mheshimiwa Mbunge kuwashika mkono katika ukamilishaji wa jengo la zahanati ya Bugayambelele ambalo ujenzi wake umeanzishwa na wananchi.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi amesema kwa sasa Shinyanga imepiga hatua kubwa katika maendeleo sambamba na ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyake vya mapato na kufikia bilioni 5 hadi 6 na kuweka wazi miradi iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka 4 ndani ya jimbo la Shinyanga kwenye sekta zote.

"Ahadi nyingi zilizoahidiwa na ilani ya Chama Cha Mapindizi zimeendelea kutekelezwa, tumejenga shule mpya 10 za msingi na sekondari ndani ya miaka 4 lengo ni kutoa elimu ya uhakika, fursa na ajira kwa vijana, lakini pia ujenzi wa vyuo vikuu na vya kati, uhimalishaji wa huduma za afya nao pia umeendelea kuimarishwa",


"Ni lazima tuwe na miundombinu bora ili kufanya manispaa ya Shinyanga kuwa Jiji, tunazidi kuiba serikali kufanya ukarabati wa miundombinu yetu iliyoharibiwa na mvua, dhamira yetu ni kusambaza mtandao wa barabara za lami utakaounganisha kata zetu sambamba na ujenzi wa uwanja wa ndege lengo ni kuongeza mapato na shughuli za uzalishaji ndani ya manispaa ya Shinyanga ili kupiga hatua na kuwa Jiji na haya yote yanafanywa na serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ", ameongeza Katambi.

Nao baadhi ya wananchi walimpongeza Mbunge Katambi kwa kazi kubwa ambayo ameifanya, huku akimuomba awatatulie changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo iliharibiwa na mvua,kufikisha umeme kwenye maeneo ambayo bado, pamoja na umaliziaji wa maboma ya Zahanati yaliyosalia.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dk. Elisha Robert akijibu swali la ukamilishaji wa Zahanati kwenye Mkutano wa hadhara kata ya Kizumbi amesema kwanza anamshukuru Mheshimiwa Rais Samia pamoja na Mbunge Katambi, kwa kupunguza idadi ya maboma ya vituo na zahanati ambayo yalikuwa bado hayajakamilika kuliwa na Maboma 16,lakini 6 yamekamilishwa na yanatoa huduma, huku Zahanati mbili ya Mwagala na Mwamagunguli zipo hatua za mwisho za ukamilishaji.

Mheshimiwa Mbunge Patrobas Katambi Februari 24,2025 anaendelea na ziara yake Katika Kata ya Mwamalili na Oldshinyanga ambapo leo ameanza ziara hiyo kwenye kata ya Kizumbi na Ibinzamata,

Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Said Bwanga akizungumza wakati wa ziara hiyo.Diwani wa kata ya Kizumbi Mhe. Ruben Kitinya akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Diwani wa kata ya Ibinzamata Mhe. Ezekiel Sabo akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha akizungumza wakati wa ziara hiyo ya kata kwa kata.



Miongoni mwa wananchi akiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara kata ya Kizumbi.
Miongoni mwa wananchi akiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara kata ya Kizumbi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi akijibu kero za wananchi kwenye mkutano wa hadhara kata ya Kizumbi.Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye Mkutano kata ya Ibinzamata.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria Mkutano katika kata ya Ibinzamata.
Share:

Sunday, 23 February 2025

CCM YAISHIKA PABAYA ACT WAZALENDO ZANZIBAR

 
Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 
Chama Cha Mapinduzi  (CCM) kimemshangaa Makamu   Mwenyekiti  wa ACT  Wazalendo , Ismail Jussa Ladhu , kwa kukosa  vipimo na maarifa ya kisiasa huku  akiendelea kuwadangaya  wananchi kwa kuponda Maendeleo yalioletwa na SMZ 

CCM imemtaka Jussa   kutozichezea akili  za wazanzibari kwani maendeleo  anayoyaponda  yako sanjari na ahadi  zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi  ya ACT  mwaka 2020/2025.

Siri hiyo imefichuliwa  na Katibu  wa Kamati Maalum ya NEC  Zanzibar  Idara  ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis  Mbeto Khamis ,  aliyesema baadhi ya ahadi  zilizotekelezwa na SMZ chini ya  Rais  Dkt.  Huseein  Mwinyi  , zimo katika Ilani ya ACT Wazalendo .


Mbeto  akionyesha kumshangaa Jussa ,amesema yalioahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2020- 2025,  yanafanana na ahadi za  ACT,  hivyo ni kituko  kumsikia Jussa akibeza ujenzi  wa shule  za Maghorofa.

Akitoa mfano , amesema katika kifungu cha 4.3  kuhusu Michezo, Sanaa na Burudani ,  ukurasa wa 39,  ilani  ya ACT, kama kingeingia ikulu , kiliahidi kuimarisha maeneo ya mapumziko kwa kushiriana na vikundi vya Wanawake na Vjana ili kuongeza ajira.

Pia Mbeto  amekitaja kifungu cha 3.2.1 cha ilani  ya ACT, imeahidi endapo  kingeshinda uchaguzi , kingeboresha Miundombinu ya huduma za  Afya kwa kujenga Zahanati ,Vituo vya Afya na kuzijengea  uwezo hospitali  za Wilaya na Mikoa.

"Nimewahi kusema  mahali fulani Jussa kifikra na kiitikadi  hana tofauti na kibaraka wa zamani  huko Zimbabwe  Ian  Douglas Smith  .Kazi yake kubwa ni kupinga mema yote ya kimaendeleo kwa Afrika na watu  wake", ameeleza Mbeto.

Katibu  huyo Mwenezi , amesema  juhudi za kimkakati na kisera zilizofanywa na Serikali ya Rais  Dk. Mwinyi  kupitia ilani ya CCM mwaka  2020 - 2025, ametekeleza kwa ufanisi mkubwa   sekta za  Elimu,  Uwekezaji, utalii Michezo ,Sanaa na Afya ,tena kwa kiwango cha juu.

"Jussa na ACT  msiwafanye wananchi wa Zanzibar hawajui malengo  yenu . Mmeshindwa kutekeleza mradi  wenu wa siri acheni kuburuza wananchi   .Rasilimali na Maliasili za Zanzibar zipo , zitawanufaisha wazanzibari si vinginevyo ",amesema Mbeto.

Kwa muktadha huo ,CCM imewataka wananchi  wa Zanzibar  na wafuasi wa ACT, kuamka na kuyatafakari maneno ya Jussa kila anapotamka kwani ameamua kuwa  komedi wa kisiasa   akiamini atawachekesha walionuna.

'Serikali ya awamu ya nane  imejenga Viwanja vya soka vya kisasa  , imeimarisha  studio za  Sanaa na Wasanii. Zimejengwa Shule za Msingi,  Sekondari,  Vyuo  vya Amali  ,Zahanati , hospitali  za wilaya na Mikoa", amesema  Mbeto. 

Mbeto amemtaka Jussa kama kweli yeye si kibaraka ,ajitokeze akanushe kama ACT haikuahidi  ahadi hizo.

Amesema CCM kupitia ilani yake ya uchaguzi mwaka 2020 hadi 2025  chini ya serikali ya Rais  Dkt.  Mwinyi imetimiza wajibu wake .

"Wana ACT  wasidanganywe na Ian Smith  . Waisome ilani yao ya uchaguzi mwaka 2020 -2030 waone kama yaliotekelezwa na SMZ kama si yale yaliomo  kwenye ilani yao  . Jussa si kibaraka  tu ni kiongozi  mawenge", amesisitiza Mbeto

Share:

MKE AANGUA KILIO BAADA YA MUMEWE KUTEMBEA NA MAMA YAKE!

Kulikuwa na drama na zogo katika mtaa wa Tom Mboya Estate, Kisumu nchini Kenya baada ya mwanaume mmoja aliyeoa kufanya tukio lisilo la kawaida wala kutarajiwa na wengi kwani jamaa huyo alitembea na Mama mkwe wake. 

Tukio hilo limewaacha wengi wakijiuliza imekuwaje kwa watu siku hizi kwani wanaume hawaonekani tena kuwaheshimu wakwe zao kama ilivyokuwa hapo awali, yaani miaka ya nyuma. 

Hapo awali, mwanaume Mwafrika hakuweza hata kulala usiku mmoja kwa wakwe zake, watu wengine wanaamini inatakiwa hata jua lisitue mwanaume ukiwa bado upo katika kijiji cha wakwe zako. 

Nandera na Sam walikuwa wameoana kwa miaka mitatu. Wakiwa wenyeji wa jiji la kando ya ziwa, walikuwa na nyumba nzuri huko Kisumu na kuishi maisha mazuri tu. 

Kutokana na mahitaji ya kazi, iliwalazimu kujenga nyumba nyingine jijini Nairobi ambapo Nandera alifanya kazi kwa bidii kubwa ili kuweza kuitunza familia yake. 

"Tuna pesa, lakini sio nyingi, Mungu ametubariki kwa magari mawili, nyumba mbili na familia yenye hali nzuri. Ninampenda mume wangu, lakini alikuja kunishangaa kwa njia ambayo sikuamini na kuelewa. Lakini sasa tuko sawa.” alisema Nandera. 

Mwanamke huyo alikiri kwamba ingawa kila kitu kilionekana kuwa sawa, ila chini kabisa ndoa yao ilikuwa imegonga mwamba, na urafiki wao ulikuwa unakufa.

Alishuku kuwa Sam hakuwa mwaminifu kwa ndoa yao lakini hakuwa na ushahidi. Sasa miezi minne iliyopita, Sam alikuwa katika kile alichokiita mkutano wa kibiashara mjini Kisumu. Alipanda ndege Ijumaa jioni kabla ya mkutano uliopangwa kufanyika Jumatatu.

Kwa kuwa Nandera pia alikuwa nje kikazi wikendi hiyo, alipanga kumshangaza mume wake kwa mlo wa kitamaduni wa hali ya juu baadaye Jumatatu hiyo jioni.

Aliendesha gari Jumatatu hiyo asubuhi hadi Kisumu. Alipofika, alipitia soko la karibu la Kibuye, ambako alinunua viungo, samaki, na mboga, kisha akaelekea nyumbani ambapo ilikuwa umbali wa chini ya kilomita 4 tu.

Ilikuwa yapata saa 1 usiku alipofika akiwa ameongozana na dada yake. Kwa kushangaza, madirisha ya nyumba yalikuwa wazi. "Sam hajifunzi kamwe, anapenda kuacha madirisha wazi," alimwambia dada yake.

Alipokaribia mlangoni wakati akitafuta ufunguo, alipigwa na butwaa ambapo aliona jambo la kushangaza. Mama yake alikuwa bize kitandani na mume wake.

"Huu ndio mkutano uliokuwa unazungumzia Sam?", alifoka, Yaani unakula hadi mama yangu aki Sam. Mama, unafanya nini hapa? Hii ni nyumba yangu. ili ni kosa". 

Wawili hao hawakuweza kusema lolote. Nyuso zao zilikuwa zimekosa nuru kwa aibu. Nandera alishindwa, kwa hiyo alikimbia nje na kuanza kulia.

Matokeo ya fumani hilo yanakuja wiki moja baada ya Nandera kuwaambia Kiwanga Doctors kwamba anashuku kuwa mume wake alikuwa akimdanganya. Kwa kutumia uchawi wenye nguvu, waganga hao wa mitishamba waliwawekea mtego, naye akaingia humo.

Lakini sasa Nandera alikuwa anakula zaidi ya alivyoweza kutafuna. Alirudi kwa waganga hao na kutafuta ushauri zaidi; aliwaambia hataki kumuacha mume wake licha ya tukio hilo baya.

Kiwanga Doctors aliitazama hali yake na kumshauri kuachana na dawa za uzazi wa mpango zenye homoni alizokuwa akitumia kwani zinamfanya kukosa hamu ya tendo la ndoa hadi mume wake kwenda nje.

Ukiona mambo hayaendi kama unavyotaka, basi usisite kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba +254 769 404965, wataalamu hawa wamesaidia watu wengi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. 


Share:

SIMBACHAWENE AWAITA OFISINI VIONGOZI WA VIJANA WA 'NETO'


Na Mwandishi Wetu - Morogoro

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene ameipongeza timu inayosimamia mchakato wa ajira za Ualimu kwa namna wanavyoendesha zoezi hilo kwa uadilifu na ufanisi.

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo tarehe 22 Februari, 2025 wakati alipotembelea na kukagua timu inayosimamia mchakato wa ajira za Ualimu Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) Mkoani Morogoro.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwaita ofisini kwake Dodoma kwa mazungumzo Viongozi wa vijana waliojitambulisha kwenye andiko lao kuwa ni “Non Employed Teachers Organisation (NETO)” wenye umoja wao kupitia mitandao ya Kijamii.

“Nimesoma Makala yao yenye kichwa cha habari Ombi la Wahitimu wa Ualimu Vyuo mbalimbali Nchini kati ya mwaka 2015-2023 kwa Serikali, andiko lao ni zuri na linaeleweka ingawa linahitaji ufafanuzi zaidi, hivyo ninatoa wito kwa vijana hao kuja ofisini Dodoma kwa mazungumzo” alisisitiza Mhe. Simbachawene.

Aliongeza kuwa amewasiliana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda na Viongozi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI na wamekubalina kushiriki mazungumzo hayo wakati kundi hilo litakapokuwa tayari.

Mhe. Simbachawene amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaongozwa kwa kuzingatia misingi ya Falsafa ya 4R  (Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga Upya), hivyo kwa moyo wa upendo amewakaribisha ili kupata maridhiano katika jambo wanaloona haliko sawa. 

Aidha, amesema kuwa kuanzia tarehe 14 Januari hadi terehe 24 Februari,  2025 Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (UTUMISHI), Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia; Wizara ya Afya; Tume ya Utumishi wa Walimu, Ofisi za Wakuu wa Mikoa yote na wataalamu mbalimbali kutoka katika Taasisi za Umma inaendesha usaili wa kada za Ualimu.

“Usaili huu una lengo la kujaza nafasi elfu kumi na nne mia sita na arobaini na nane (14,648) zilizotolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kupunguza uhaba wa walimu nchini” alifafanua Mhe. Simbachawene.

Naye, Msimamizi wa Kituo hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bibi. Hilda Kabissa amesema kuwa zoezi linaendelea vizuri na Sekretarieti ya Ajira inaendesha usaili wa aina tatu, Usaili wa kuandika (Aptitude Test), Usaili wa vitendo (Practical) na Usaili wa mahojiano ya ana kwa ana (Oral Interview) kwa kuzingatia mahitaji ya kada au nafasi inayotakiwa kujazwa.

Share:

Saturday, 22 February 2025

IJUE SIRI YA AJABU NYUMA YA MAFANIKIO YA WENGI


Yeye sio tu mzee anayengojea simu ya mwisho, hakuwa amekata tamaa, akiwa pale nyumbani, Babu yangu alitaka kutoa njia ya mwisho na muhimu katika maisha, ni ujumbe ambao alikuwa ameufikiria kwa muda mrefu.

Tulikusanyika huku tukitumaini kupata kila alichosema, kwanza, alituonya dhidi ya kuitikia kila aina jambo, alisema kufanya hivyo kutamaanisha kuwa tutakuwa tunafanya mambo kulingana na kile watu kinachotokea.

"Wakati unapohisi hofu zaidi, ndio wakati wa kufanikiwa, urahisi hautakufanya ukue, unajua kadiri unavyopinga mabadiliko, ndivyo unavyozidi kudumaa kimaisha na kiuchumi," alisema Babu.

Alituonya dhidi ya kupuuza mila na maadili yetu na kukumbatia maisha ya kisasa tu ambayo yameletwa na nchi za magharibi, alisema mila zetu ni ukumbusho wa pale tulipotoka kwamba bila hizo mila tungepotea kabisa.

Pia alisisitiza juu ya umuhimu wa kuomba msaada kwa watu wengi ambao ni sahihi haswa wakati shida hiyo inahitaji akili zaidi ya moja kutatuliwa.

Aliendelea kwa kusema kuwa wakati wa shida alikuwa na watu kadhaa ambao wangeweza kumpa ushauri na msaada ambao utamkwamua kutoka kwenye shida hiyo na mara zote alikuwa akifanikiwa.

Anasema alipotaka kupanua biashara yake na kujitosa katika ujenzi wa nyumba, alikwenda kutafuta huduma za mganga wa jadi maarufu kama Kiwanga Doctors ambao walimsaidia kupata fedha zake nyingi za kuikuza.

Babu alitabasamu huku akisimulia jinsi biashara yake ilivyokua ndani ya muda mfupi tu, ndipo akanunua kipande chake cha kwanza cha ardhi huko Upperhill Nairobi.

Anasema kwa msaada wa Kiwanga Doctors, himaya yake kibiashara ilikua kubwa sana, na sasaa anahitaji kukabidhi ufalme huo mikononi mwetu maana ndio vijana wenye nguvu kwa sasa lakini tusisahau kuwa karibu na Kiwanga kwani wanaweza kuongeza bahati katika kazi zetu.

"Ninajua jinsi hii inaweza kuonekana kuwa ngumu lakini ichukueni kutoka kwa mzee niliye na uzoefu. Ikiwa haifanyi kazi, kamwe nisingewaambia muwasiliane na Kiwanga Doctors, namewaambia hivyo kutokana najua wapi aliponitoa," alisema Babu yetu.

Wapigie sasa Kiwanga Doctors kwa namba +254 769 404965.
Mwisho.

Share:

DKT. MPANGO AITAJA STAMICO MFANO BORA UTEKELEZAJI MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUPIKIA


* Mageuzi Makubwa ya STAMICO Yapelekea Kujitegemea Kiuchumi

Mbeya,

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, amepongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kuwa mfano bora wa utekelezaji wa ajenda ya matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia nchini.

Amesema kuwa STAMICO imeonyesha mwelekeo sahihi kupitia uzalishaji wa mkaa mbadala uitwao Rafiki Briquettes, unaotokana na makaa ya mawe.

Dkt. Mpango amesema hayo, leo, Februari 21, 2025 wakati akifunga mkutano wa mafunzo wa 109 wa watayarishaji wa Vipindi vya Elimu kwa Umma (WASHITIRI) kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) chini ya Uenyekiti wa STAMICO uliofanyika katika Ukumbi wa City Park Garden uliopo Jijini Mbeya.

Serikali Yajizatiti Kuboresha Upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia

Dkt. Mpango ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia kwa lengo la kuboresha afya za wananchi na kulinda mazingira. Amesema kuwa Serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 8.68 kwa ajili ya upatikanaji wa nishati hiyo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Taifa wa kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa wa miti ambao unachangia uharibifu wa mazingira.

“Matumizi ya nishati safi ya kupikia ni moja ya vipaumbele vya Taifa letu. Tunataka ifikapo mwaka 2034, angalau asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi, kama vile gesi asilia, umeme wa jua, na mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes unaotengenezwa na STAMICO,” amesema Dkt. Mpango.

Taasisi za Umma Zatekeleza Agizo la Serikali Kuhama kutoka Kuni na Mkaa

Dkt. Mpango amefafanua kuwa tangu Serikali ilipotoa katazo kwa taasisi zote za umma zinazohudumia watu wasiopungua 100 kwa siku kuacha matumizi ya kuni na mkaa wa miti, tayari taasisi 506 zimekwishaanza kutumia nishati safi ya kupikia. Amezitaka taasisi nyingine zinazobaki kuhakikisha zinaharakisha mchakato wa kuhama ili kulinda afya za watumiaji na kusaidia juhudi za uhifadhi wa mazingira.

“Natoa wito kwa taasisi zote za umma zinazohudumia watu wasiopungua 100 kwa siku, kuhakikisha zinafuata maelekezo haya haraka iwezekanavyo. Serikali iko imara katika kuhakikisha mabadiliko haya yanafanikiwa kwa manufaa ya taifa letu,” amesisitiza Makamu wa Rais.

Mageuzi Makubwa ya STAMICO Yapelekea Kujitegemea Kiuchumi

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse, akiwasilisha maendeleo ya shirika hilo, ameeleza kuwa kutokana na mageuzi makubwa ya kiutendaji, STAMICO sasa limeanza kujitegemea kiuchumi na kwamba Shirika hilo linakusanya mapato ya takriban shilingi bilioni 85 kwa mwaka kutokana na shughuli zake mbalimbali, ikiwa ni ongezeko kubwa kulinganisha na miaka ya nyuma.

Dkt. Mwasse amesema kuwa, katika juhudi za kuongeza uzalishaji wa Rafiki Briquettes, STAMICO imeagiza mitambo mipya mikubwa yenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa siku, ambayo tayari imewasili nchini na imeanza kufanya kazi. Mitambo hiyo itasaidia kuongeza upatikanaji wa mkaa mbadala na kuwafanya wananchi wengi zaidi kuachana na matumizi ya mkaa wa miti.

Wanawake na Samia Wapewa Uwakala wa Usambazaji wa Rafiki Briquettes

Katika hatua nyingine, Shirika la STAMICO limeingia ubia na Taasisi ya Wanawake na Samia, kwa kuwapatia uwakala wa usambazaji wa Rafiki Briquettes. Taasisi hiyo, ambayo inafanya kazi katika mikoa 20 ya Tanzania Bara na mkoa mmoja wa Zanzibar, imetambuliwa kwa juhudi zake za kuwawezesha wanawake kushiriki katika sekta ya nishati safi.

Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, amekabidhi rasmi vyeti vya uwakala kwa wawakilishi wa wanawake hao kutoka mikoa ya Songwe, Iringa, Njombe, na Ruvuma. Aidha, jumuiya ya wazazi kutoka Mbinga na wafanyabiashara wa Soko la Mwanjelwa pamoja na Mkoa wa Mbeya walipokea vyeti hivyo kwa kutambua mchango wao katika kusambaza Rafiki Briquettes.

Shule ya Sekondari ya Wasichana Loleza Yapokea Majiko ya Kisasa kutoka STAMICO

Kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya nishati safi katika taasisi za elimu, Makamu wa Rais Dkt. Mpango amekabidhi majiko matatu ya kisasa kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Loleza jijini Mbeya. Majiko hayo, ambayo yana uzito wa kilogramu 50 kila moja kutoka STAMICO yanatarajiwa kupunguza gharama za nishati shuleni hapo na kuboresha mazingira ya upishi kwa wanafunzi.

Juhudi za Serikali na wadau kama STAMICO zinaonyesha dhamira thabiti ya kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kubwa katika matumizi ya nishati safi. STAMICO kupitia uzalishaji wa Rafiki Briquettes na uwezeshaji wa wanawake katika usambazaji wa bidhaa hizo, Tanzania imepanga kuachana na matumizi ya kuni na mkaa wa miti kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2034.

Mkutano huo umefanyika chini ya Kaulimbiu ya “Tumia Nishati Safi, Tunza Mazingira”
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger