Monday, 10 February 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 11, 2025

Share:

WASIRA AMJULIA HALI GACHUMA KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amemjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu yaTaifa (NEC), Ndugu Christopher Gachuma ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Bugando jijini Mwanza.

Ndugu Gachuma amelazwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali ya gari jana katika Kijiji cha Gesarya, Kata ya Lung'abure, wilayani Serengeti Mkoa wa Mara alipokuwa akielekea katika Ziara ya Makamu Mwenyekiti Wasira.

Majeruhi mwengine katika ajali hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ndugu Kemilembe Ruta pamoja na dereva wa gari hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya hospitali hiyo, majeruhi wote wa ajali hiyo wanaendelea vizuri.

Ndg Wasira amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ambapo kesho atahutubia mkutano mkubwa utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.

Share:

SERIKALI YA MTAA MUUNGANO YAONESHA MUELEKEO CHANYA KWENYE MAENDELEO


Na Mariam Mohamed Amry

MWENYEKITI wa Mtaa wa Muungano kata ya Goba Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, mkoani Dar es Salaam, Isack Maduhu amelezea mikakari mipya ya utendaji na hatua zilizochukuliwa katika sekta mbalimbali za kijamii ndani ya Mtaa wake ikiwepo Afya , Elimu , Miundombinu ya Maji na kadhalika.

Akizungumza na wananchi Februari 9, 2025 kwenye mtaa wake, Maduhu amesema kutakuwa na ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Muungano ambayo itarahisisha ufanisi wa huduma ya Afya kwa wananchi.

Amesema kutatolewa vyandarua vyenye dawa kwa watoto chini ya Mwaka Mmoja na wajawazito kwa hati punguzo ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria.

Aidha amesisitiza kuwa Serikali ya Mtaa inayotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitahakikisha kinajenga jamii yenye Afya bora, katika kipindi cha mwaka 2024 - 2029.

Katika Sekta ya Elimu ameunda utaratinu wa ziara wa kutembelea shule za awali, Msingi na Sekondari kuangalia majengo na maziingira yake.

Pamoja na hayo Maduhu amewahakikishia wananchi wa Mtaa wa Muungano kufanyika kwa ujenzi na upanuzi wa Miundombinu ya maji ili waweze kupata maji safi na salama .

"Mpaka sasa wananchi wameishaanza kuchukua fomu kwa ajiri ya kuonganishiwa huduma ya maji na na tayari mabomba yameshakabidhiwa katika shina namba nne na shina namba tano". Amesema Maduhu

Kwa upande wake Mwakilishi wa TARURA, Mkandarasi Cavine Lugendo amesema wamechukua hatua ya kuomba fedha ili kudhibiti athali za mvua zilizotokea mwaka jana na hadi mwaka huu mwanzoni na kuharibu Miundombinu ya barabara na Madaraja.
Share:

ALIYETAPELIWA SH32.7 MILIONI ATOA USHUHUDA WA MATUMAINI

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Charity, amewataka wananchi kuhakikisha wanajiepusha na biashara ya kupata utajiri wa haraka baada ya kudaiwa kupoteza Sh32.7 milioni kwa kampuni iliyomlaghai.

Kulingana na ripoti, alidai alikubaliana na kampuni hiyo kwamba wangemuongezea fedha zake mara 10, hivyo hakusita kwani aliwekeza kiasi chote cha Sh32.7 milioni ili kuona kama dili hilo lilikuwa halali kwani ofa hiyo ilikuwa tamu na hakuwa tayari kuiacha. 

"Mwanzoni kila kitu kilikuwa sawa, pesa ziliendelea kuingia na jinsi zilivyozidi kuja, ndivyo nilivyoendelea kuwekeza kwao bila kujua kuwa wameniwekea mtego wa kunipeleka shimoni." alisema Charity.

Kwa maneno yake mwenyewe, alifichua kuwa alifikia hatua ya kuamua kuwekeza kiasi cha Sh32.7 milioni baada ya kuhakikishiwa usalama wa fedha zake kwa kupewa wadhamini wa haraka ila mwisho wa siku walitoweka katika mazingira yasiyoeleweka.  

Hakuwa tayari kukubali ukweli kwamba alikuwa ametapeliwa Sh32.7 milioni ndani ya siku chache. Alijaribu kuripoti kisa hicho kwa Polisi lakini kuwatafuta matapeli hao, haikuwa kazi rahisi kama Polisi walivyomwambia. 

Alibaki na jambo moja tu la kufanya ambalo lilikuwa ni kukubaliana na ukweli kwamba alikuwa ametapeliwa. Anasema rafiki yake mmoja alimwambia atafute msaada kutoka kwa waganga wa jadi aitwaye Dr Bokko. 

Alipewa mawasiliano yake +255618536050  kisha kumpigia na kufika katika ofisi zake, Charity alimueleza Dr Bokko kila kitu kilichotokea hadi kutapeliwa Sh32.7 milioni katika mazingira ambayo hata yeye mwenyewe alikuwa haelewi.  

Basi alifanyiwa matambiko ya kichawi ambayo yamekuwa akirejesha mali zote ambazo zimekuwa zikichukuliwaa kwa njia ambayo sio halali ikiwemo utapeli. 

Baada ya siku chache fedha zake zilirejea kwani wahusika walijisalimisha wenyewe kwa Polisi huku wakisema kukaa na fedha hizo haiwezekani kutokana na majanga ambayo walikuwa wakikumbana nayo. Ilibainika kuwa hii ilikuwa biashara ambayo walikuwa wakifanya kwa muda mrefu.

Charity alifika kituo cha Polisi na kukabidhiwa fedha zake zote kiasi cha Sh32.7 milioni , huku matapeliwa wale wakichukulia hatua kali za kisheria. Hata hivyo, ukweli ni kwamba bila Dr Bokko hasingepata fedha zake na matapeli hao wangeendea kuwaibia watu kila siku.


Share:

Sunday, 9 February 2025

SIMBACHAWENE AUNGANA NA FAMILIA YA LOWASA KWENYE IBADA YA SHUKRANI



Na Barnabas Kisengi Arusha

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene leo February 09,2025 ameungana na wanafamilia, viongozi wa chama, serikali na wananchi katika Ibada ya shukrani ya Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Monduli mkoani Arusha, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Taifa lilipompoteza kiongozi huyo.

Akizungumza kwa niaba ya Familia ya Hayati Edward Lowassa, Mwanae ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wote waliokuwa pamoja tangu Baba yao alipofariki hadi hivi sasa huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa wa kuwa pamoja na familia hiyo tangu Baba yao alipoanza kuugua hadi umauti ulipomkuta

"Kwa unyenyekevu mkubwa ninawaomba Watanzania wote tuendelee kumuenzi Hayati Edward Lowassa kwa yale yote mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake" amesisitiza Fredrick Lowassa

Naye, Baba Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dkt. Solomon Masangwa ameitaka familia hiyo kuzidi kumuangukia Mwenyezi Mungu katika kila jambo wanalolifanya.










Share:

VITUO VYA MFANO VYACHOCHEA TEKNOLOJIA YA UCHENJUAJI KWA CIP


 
*Serikali yakusanya zaidi ya bilioni 3.3 kupitia Vituo vya Mfano


*Uzalishaji wa Madini ya dhahabu waongezeka

*Wachimbaji waiomba STAMICO kuongeza mitambo ya uchenjuaji

*Vituo vingine kujengwa Tanga, Lindi na Kahama

Imeelezwa lengo la Serikali la kuanzisha Vituo vya Mfano kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uchimbaji bora kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini limefaniliwa kwa kiasi kikubwa baada ya wachimbaji wengi nchini kuhamia na kuanzisha teknolojia ya Uchenjuaji wa kutumia (CIP) badala ya mialo ambayo imesaidia kuongeza tija kwenye shughuli zao na  kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Hayo yamebanishwa na Mshauri Elekezi katika shughuli za uchimbaji mdogo,  Mkurugenzi wa Kampuni ya Tan Discovery Consultant Company Limited na mjenzi wa vituo hivyo, Mhandisi Rogers Sezinga wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Madini baada ya kuvitembelea vituo hivyo.

Ameongeza kwamba, vituo vya mfano vimesaidia kuongeza mzunguko wa uuzaji madini kwenye masoko jambo ambalo limepelekea Serikali kupata taarifa za wachimbaji hao na hivyo kuwawezesha kupata mikopo kwenye baadhi ya taasisi za fedha hapa nchini.

‘’ Nikiwa mshauri elekezi, nimekuwa nikipata maombi mengi kwa ajili ya ujenzi wa CIP hizi kutoka maeneo mbalimbali nchini. Hadi sasa nimejenga CIP zaidi ya 10 na hapa kama mnavyoniona naendelea na ujenzi wa CIP nyingine, hivyo vituo hivi vimeongeza tija baada ya watu kujifunza. Wito wangu, wachimbaji wazitumie ili kuachana na matumizi ya zebaki na zitaongeza vipato vyao na kodi za Serikali,’’ amesema Sezinga.

Mbali na kuanzishwa CIP,  vituo hivyo vimewavuta wakazi  wanaozunguka vituo hivyo na wachimbaji kujikita kwenye shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu baada ya kutoa elimu kwa vitendo kuhusu namna bora ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini kwa wachimbaji wadogo.

Vituo  vya mfano vilijengwa na Serikali kupitia Wizara ya Madini  katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kilichopo kijiji cha Katente Wilayani Bukombe, Lwamgasa- Geita na Itumbi-Chunya, vinasimamiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) likisimama kama mlezi wa wachimbaji wadogo.

Aidha, mbali na mafunzo ya uchimbaji na uchenjuaji, vituo hivyo vinatoa huduma za uuzaji wa vilipuzi, kemikali, uchomaji wa kaboni ambapo mpaka sasa Vituo hivyo vimekusanya zaidi ya bilioni 3.3 zikitokana na kodi mbalimbali na mrabaha  tangu kuanzishwa kwake Mwaka  wa Fedha  2019- 2020.

Kwa upande wake,  Msimamizi wa Kituo cha Mfano cha Katente ambaye pia ni Mratibu wa Vituo vya Mfano vya Katente-Bukombe,  Lwamgasa-Geita na Itumbi-Chunya, Mhandisi Tiberio Lucian Kaduma amesema Serikali kupitia STAMICO imejenga Vituo hivyo katika maeneo yenye madini kwa lengo la kumsaidia mchimbaji mdogo kupata maarifa ya uchimbaji na uchenjuaji bora na wenye tija.

Aidha, Mhandisi Kaduma amesema Vituo vya Mfano ni sehemu mahususi ya kuwapatia wachimbaji wadogo mafunzo ya nadhari na vitendo ili kukuza ujuzi, maarifa na elimu kuhusu uchimbaji salama na utunzaji wa mazingira.

Mhandisi Kaduma amesema Vituo hivyo vimesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa kuhusu uchimbaji salama ikiwemo uchenjuaji wa kutumia teknolojia ya sayanaidi katika uchenjuaji na kuachana na matumizi ya zebaki inayo haribu mazingira.

‘’Serikali kupitia STAMICO inampango wa kujenga vituo vya mfano vingine katika mikoa ya Kimadini ya Tanga Lindi na Kahama ili kuwasaidia wachimbaji wadogo kufanya shughuli za uzalishaji madini kwa faida na kuongeza tija kwenye Pato la Taifa.

Pamoja na mambo mengine, Mhandisi Kaduma ametoa wito kwa wachimbaji madini kote nchini kuvitumia Vituo vya Mfano kwa ajili ya maendeleo yao na kutumia huduma zinazotolewa na Vituo hivyo ikiwemo uuzaji wa vilipuzi na kemikali zinazotumika katika uchenjuaji madini ili kujiongezea wigo na ufanisi katika shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini nchini.

Kwa upande wake, mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu wa Katente namba 1, Max Thomas Kajoro ambaye ni mnufaika wa kituo hicho, ameishukuru Serikali kupitia STAMICO kwa kujenga Kituo cha Mfano cha Katente ambacho kimemnufaisha kwa kiwango kikubwa baada ya kupeleka mawe yake kwa ajili ya kuchakata na kupata dhahabu  nyingi zaidi ya matarajio yake ambapo ametoa wito kwa wachimbaji wengine kutumia Kituo hicho kwa ajili ya maendeleo yao.

‘’Kituo cha mfano Katente ni suluhisho na msaada mkubwa kwa wachimbaji wadogo ambapo mimi binafsi kimenisaidia kununua mashamba, gari, pikipiki, kujenga nyumba, kusomesha watoto na kukidhi kuhudumia familia yangu,’’ amesema  Kajoro.


Naye, Mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu wa Katente namba 2, Simon Sospeter Dittu ameipongeza Serikali kwa kujenga Kituo hicho katika eneo hilo ambapo amenufaika kwa kupata elimu ya uchimbaji salama na ushauri wa uchimbaji bora ikiwemo kutunza mazingira na elimu ya utambuzi wa maeneo yenye tija katika uchimbaji wa madini ambapo kwa sasa anazalisha kwa faida kupitia mgodi wake.

Kwa upande wake, Mchimbaji mdogo Pamela James amelipongeza Shirika la STAMICO kwa kuwalea vyema  na kuwapa mafunzo ya uchimbaji na uchenjuaji kwa vitendo jambo ambalo  limewasaidia wachimbaji wengi kuachana na mila potofu za kutumia waganga na badala yake kutumia utaalamu waliyopatiwa na kujipatia faida ambapo kwa sasa mama huyo ameajiri zaidi ya wafanyakazi 50 katika shughuli zake za uchimbaji.

Aidha, Pamela ametoa wito kwa STAMICO kupanua wigo wa uzalishaji kwa kufunga mitambo mikubwa zaidi ili kupunguza foleni ya wateja, muda na kuongeza uzalishaji tofauti ya ilivyo sasa.


Share:

KAMPUNI YA FIT GROUP KUTOKA NIGERIA KUWEKEZA NCHINI


WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) umepokea wawekezaji kutoka Kampuni ya FIT Group kutoka nchini Nigeria. Ujio wao ni wa mara ya pili ambapo wawekezaji hao wamekuja kuona maeneo ya uwekezaji yanayomilikiwa na TBA kwa ajili ya kuyaendeleza kwa njia ya ubia. Ziara yao nchini imeambatana na kufanyika kwa kikao kati yao na TBA pamoja na kutembelea maeneo ya uwekezaji.

Katika Kikao hicho wawekezaji hao kutoka FIT Group walipokea wasilisho la mpango wa uendelezaji na kuonyeshwa fursa za uwekezaji zilizopo kwenye meneo hayo pamoja na kuyatembelea.

Akizungumza baada ya kutembelea maeneo ya Magomeni Kota, Kindondoni Manyanya Kota pamoja na Ilala Mchikichini Kota jijini Dar es Salaam, Mshauri Elekezi wa Kampuni hiyo Bw. Godbless Safugha amesema kuwa kikao na ziara hiyo imetoa nafasi ya kuona Mpango wa Uendelezaji wa maeneo pamoja na miradi inayotekelezwa na TBA.

“Tunatarajia kufanya uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki, lakini tumevutiwa zaidi na Tanzania hasa maeneo mazuri ya TBA katika jiji la Dar es Salaam na Dodoma ambayo yanatoa fursa ya uwekezaji hasa katika Sekta ya majengo”.

Pia Bw. Godbless amesema kuwa uwekezaji huo unatarajia kugharimu kati ya dola za marekeni milioni 30 mpaka 40 na kutoa ajira zaidi 10,000 kwa vijana wa Kitanzania.

Vile vile Bw. Godbless amesema kuwa wanatarajia kusaini Hati ya Ushirikiano (MoU) kati ya Kampuni yao ya FIT Group na TBA ndani ya muda mfupi ujao kabla ya kusainiwa kwa mikataba ya uendelezaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Bw. Fredy Mangula amesema kuwa ziara ya Kampuni ya FIT Group imekuwa na tija na kuwa TBA inaendelea kuwakaribisha wawekezaji wengine wa ndani na nje ya nchi kutembelea maeneo ya uendelezaji yaliyopo katika mikoa yote nchini ili waone fursa za uwekezaji zilizopo kutokana na changamoto ya upungufu wa nyumba bora za makazi katika mikoa hiyo.

Vile vile Bw. Mangula amesema kuwa kuja kwa wawekezaji hao ni matokeo ya utekelezaji wa agizo lililotolewa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Machi 21, 2022 wakati wa ufunguzi wa nyumba za waakazi 644 katika eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.
Share:

Saturday, 8 February 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARI 9, 2025







Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger