Wednesday, 15 January 2025
ZIARA YA DC MTATIRO KIJIJI KWA KIJIJI YAZIDI KUFICHUA MAZITO... AKERWA PESA ZA WANANCHI KUCHEZEWA UPAUAJI JENGO LA ZAHANATI
WIZARA YA NISHATI YAWASILISHA UTEKELEZAJI WA BAJETI 2024/2025 KATIKA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI

MAANDALIZI YA MKUTANO WA NISHATI WA WAKUU WA NCHI AFRIKA (MISSION 300) YAMEFIKIA ASILIMIA 95- DKT. BITEKO
Tuesday, 14 January 2025
Tanzia : MKUU WA WILAYA YA MBOZI ESTER MAHAWE AFARIKI DUNIA
AJALI YA LORI YAUA WATU 11 WAKISHUHUDIA AJALI NYINGINE, 13 WAJERUHIWA TANGA
Watu 11 wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebeba saruji kufeli breki na kugonga watu mashuhuda wa ajali ya gari dogo aina ya Coaster Tata katika kijiji cha Changombe, kata ya Segera, wilayani Handeni, mkoa wa Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha kwa sababu waliofariki walikuwa wakijaribu kuwasaidia majeruhi wa ajali ya awali.
Kwa mujibu wa taarifa, lori hilo lenye namba za usajili T 680 BQW, likiwa linatokea Tanga, lilishindwa breki na kuwakumba watu waliokuwa pembezoni mwa barabara, kusababisha vifo vya watu 11 papo hapo na kujeruhi wengine 13.
Mkuu wa Mkoa ametoa pole kwa familia za marehemu na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi wote. Aidha, ametoa wito kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali nzuri ya kiufundi ili kuepusha ajali za namna hii.
Monday, 13 January 2025
HUYU NDIYE SAID LUGUMI, HISTORIA YAKE YA KWELI
Bilionea Saidi Lugumi sio jina geni Nchini, huyu sio mtoto wa mjini, sio Kiongozi na huenda kwenye familia yake hakuna historia ya mwanasiasa zaidi ya marehemu baba yake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Magu.Ni kijana kutoka Jijini Mwanza, Wilaya ya Magu mwenye Elimu ya darasa la Saba pekee, hana Elimu ya kutisha lakini usishangae ukisikia Lugumi ni Daktari (PhD) udaktari wa heshima kwakuwa anastahili hilo kwa kiwango kikubwa kutokana na namna anavyojitoa kwa jamii.
Tofauti na Wafanyabiashara wengine, ukisikia habari zao mitandaoni ni mambo tofauti lakini kwa Lugumi imekuwa tofauti sana ambapo mwishoni mwa mwaka 2024 mwezi Disemba aliibua mjadala katika mitandao ya kijamii baada ya kuonesha sehemu ya nyumba anazojenga kwaajili ya watoto Yatima anao walea katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Bilionea Saidi Lugumi anaeleza kwa sasa kuna watoto yatima zaidi ya 800 kutoka maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam ambao anawahudumia kwa kila kitu ikiwemo chakula, mavazi, malazi, elimu, afya l, na hiyo inatokana na wito alionao kutoka kwa Mwenyezi Mungu na si vinginevyo.
Desemba 25, 2024 katika kusherekea sikukuu ya Krismasi alijumuika na watoto wake mtaa wa Msufini, wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kushirikinao dua na kisomo maalum sambamba na kushirikinao chakula cha pamoja alichokiandaa kwa ajili yao
Sambamba na hilo, katika kuboresha makazi yao Lugumi alisema kwa sasa anajenga majengo sita (6) ya ghorofa huku malengo yakiwa ni kujenga ghorofa nane (8) kwa ajili ya watoto hao, kwenye maeneo tofauti ya jiji hilo, ambapo jengo moja kati ya hayo linajengwa eneo hilo la Msufini.
"Hii ni nyumba yao (jengo la ghorofa), nyumba kama hizi ziko sita (6) lakini tumeanzia hapa kwa sababu nyumba hii iko mbioni kumalizika, chakula tutakula na wao hapa, na wenyewe wameweza kuwa na furaha kuona sehemu yao, kila kituo kinatarajiwa hakitazidi kukaa watoto 100, unaona nyumba kama hii ni watoto 100 tu na kwa namna Mungu anavyonijaalia nitazidi kuongeza, kwa sasa tumepanga nyumba kama tatu na nyingine tumenunua lakini bado hazitoshi", alisema Lugumi.
Lugumi anaeleza kuwa alianza kulea watoto hao na alipata maono hayo mnamo mwaka 2013 ambapo ni takribani miaka 12 sasa na amesisitiza kuwa yuko tayari apoteze kitu chochote lakini sio kuwapoteza watoto hao.
Kila Kituo kuna madaktari na maafisa Ustawi wa Jamii ambao wapo kwaajili ya kuwahudumia watoto hao ukiachana na suala la mavazi na malazi watoto hao wanasomeshwa mpaka ngazi za juu za Elimu na kuendelea na maisha yao na wengine hupatiwa mitaji ya Biashara huku wengine wakianza ajira zao.
Lugumi anasimulia kuwa sio kwamba siku zote wanapitia raha na wanae, kuna vipindi hali inakuwa sio nzuri na wanalazika kula wanachokipata.
Viongozi wa Dini wamepongeza juhudi za Lugumi, akiwemo Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' wa Kanisa la Inuka Uangaze amempongeza mfanyabiashara Lugumi kwa kujenga maghorofa matano kwa ajili ya watoto yatima.
“Ninampongeza Lugumi, ni jambo jema lenye roho ya kumcha Mungu,” alisema Mwamposa.
Majengo hayo, yanayotarajiwa kukamilika Machi mwaka huu, yatanufaisha zaidi ya watoto 800 wenye mahitaji maalum jijini Dar es Salaam.
Saidi Lugumi ni mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania, anayejulikana zaidi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Lugumi Enterprises Limited.
Lakini pia kupitia kampuni ya Tactical Defencs (T) Limited ni wakala wa makampuni makubwa ya silaha duniani.
Lakini pia, kampuni yake inajihusisha na huduma za uchapishaji wa vifaa vya ki-ofisi, teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) na hajawahi kuwa na Biashara nyingine tofauti na ilivyodaiwa kuwa anajihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Maisha yake binafsi Lugumi amekuwa sio Mtu wa kuweka wazi sana familia yake, lakini amewahi kukiri kuwa na watoto Saba (7) ambao ni wa kwake wa kuwazaa na wapo sehemu tofauti tofauti, huku akikanusha taarifa za kuwahi kumuoa binti aliyedaiwa kuwa ni familia ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Saidi Mwema.
SERENGETI BYTES YATOA ORODHA YA WATANZANIA 100 WALIOCHOCHEA MABADILIKO KATIKA MWAKA 2024
Toleo hili la pili linajumuisha wasifu wa watu 100 walioleta mchango mkubwa katika nyanja tofauti. Wakurugenzi wa Serengeti Bytes wanasema jarida hili si tu njia ya kuwaenzi bali pia jukwaa la kuhamasisha Watanzania kuungana katika kujenga taifa lenye ustawi.
“Orodha ya mwaka huu inaonyesha utofauti wa vipaji na kazi za kipekee zinazofanywa na Watanzania kutoka sehemu mbalimbali,” amesema Kennedy Mmari, Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Bytes. “Hawa ni watu wanaoonesha kwa vitendo kuwa mabadiliko yanawezekana kupitia bidii, ubunifu, na kujituma.”
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Serengeti Bytes, Michael Mallya, ameongeza kwa kusema: “Kila aliyeingia katika orodha hii ni ushuhuda wa nguvu ya maono na kushirikiana. Kupitia hadithi zao, tunalenga si tu kusherehekea mafanikio yao bali pia kuhamasisha ushirikiano wa kitaifa katika kuchochea maendeleo.”
Jarida hili limeandaliwa kwa umakini kupitia mchakato ulioshirikisha mapendekezo ya umma, tathmini za wadau, na utafiti wa kina. Kila hadithi inaelezea mchango wa wahusika katika kuboresha maisha ya watu na kujenga jamii zenye ustawi endelevu.
Kwa mujibu wa Serengeti Bytes, mpango huu unalenga zaidi ya kusherehekea mafanikio ya mtu mmoja mmoja, bali pia kuhamasisha mshikamano wa kitaifa. “Jarida hili ni njia mojawapo ya kuleta pamoja fikra na maono ya mabadiliko. Tunataka kila Mtanzania atambue kuwa anaweza kuchangia kujenga taifa lenye nguvu na fursa kwa wote,” ameongeza Mmari.
Orodha hii imegawanywa katika makundi tisa ikigusa sekta mbalimbali ikiwemo Serikali na Uongozi wa Umma, Biashara na Ujasiriamali, Teknolojia na Uvumbuzi, Sekta ya Azaki na Maendeleo, Sekta ya Tafiti na Taaluma, Vyombo vya Habari, Michezo, Sanaa na Burudani, Afya na Ustawi pamoja na Wadau wa Maendeleo wa Kimataifa.
“Katika tolea la mwaka 2024 tumeongeza kipengele cha Wadau/Marafiki wa Maendeleo ya Tanzania kwa lengo la kutambua mchango mkubwa wa watu ambao si raia wa Tanzania lakini wamekuwa na mchango unaostahili kutambuliwa kwa upekee.” ,amehitimisha Mallya.
Jarida linapatikana kwa njia ya kielektoniki. Kwa maelezo zaidi au kupata nakala yako, tembelea https://changemakers.co.tz/ au wasiliana na Serengeti Bytes kupitia hello@serengetibytes.com.





































