Friday, 27 December 2024

SHANGWE ZA SIKUKUU SHINYANGA IMEAMKA! DR SAMIA JUMBE HOLIDAY BONANZA KUTIKISA!

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Katika kusherehekea mapumziko ya mwisho wa mwaka, mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe ametangaza rasmi kuanza kwa mashindano ya DR SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA 'Shinyanga Imeamka!' yatakayofanyika katika wilaya ya Shinyanga. 

Mashindano haya yatakuwa na michezo mbalimbali, huku zawadi za kuvutia zikitolewa kwa washindi.

Akitangaza mashindano hayo pamoja na kukabidhi jezi kwa timu zitakazoshiriki katika mashindano ya mpira wa kikapu leo, Ijumaa, Desemba 27, 2024, Mratibu wa mashindano hayo, Jackline Isaro, amesema mashindano yatafanyika tarehe 31 Desemba 2024 kuanzia asubuhi katika uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga.

Michezo Itakayoshiriki

Mashindano ya DR SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA yatakuwa na michezo mingi, ikiwemo mpira wa kikapu, bao, karata, drafti, msusi mwenye kasi zaidi, mbio za baiskeli, Netball, wavu, PS Game, mchezo wa kufukuza kuku, kushindana kula, pull table na muziki.

Michezo mingine, kama vile mchezo wa bao, karata, drafti, na msusi mwenye kasi zaidi tayari imezinduliwa na mashindano hayo yatafikia tamati siku ya Desemba 31, 2024.

Lengo la Mashindano

Mratibu Jackline Isaro amesema kuwa lengo kuu la mashindano haya ni kufufua michezo mkoani Shinyanga na kutoa fursa kwa wachezaji na wadau wa michezo kuonyesha vipaji vyao. 

Isaro amesisitiza kuwa michezo ni muhimu kwa jamii kwa sababu inachangia afya, furaha, na pia ajira.

“Lengo la michezo hii ni kuonesha vipaji vya vijana wetu mkoani Shinyanga, na tunaamini kupitia mashindano haya tutapata wachezaji bora ambao watakuwa na nafasi ya kuendelezwa. Tunajua pia kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anahimiza michezo, na kupitia mashindano haya, tunatarajia kukuza michezo na vipaji katika mkoa wetu,” amesema Isaro.


Zawadi kwa Washindi

Mashindano haya yatatoa zawadi nono kwa washindi, ikiwa ni pamoja na fedha taslimu, ng'ombe, mchele na kreti za soda. Kwa mfano: Mchezo wa mpira wa miguu kati ya Upongoji Sports Club na Upongoji Stars: Mshindi atapata shilingi milioni moja, ng'ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 10 za soda na Mshindi wa pili atapata shilingi 500,000, ng'ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 10 za soda.

Mchezo wa Mabingwa wa Wilaya (Rangers FC vs Ngokolo FC), Mshindi atapata shilingi 500,000, ng'ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 10 za soda, Mshindi wa pili atapata shilingi 300,000, ng'ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 10 za soda.

Mchezo kati ya Bodaboda FC vs Bajaji FC, Mshindi atapata shilingi 500,000, ng'ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 7 za soda na Mshindi wa pili atapata shilingi 300,000, ng'ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 7 za soda.

Pia, mashindano ya mbio za baiskeli kwa wanaume na wanawake yatakuwa na zawadi kwa washindi kutoka nafasi ya kwanza hadi ya kumi

Washindi wa michezo mingine kama bao, karata, drafti, na msusi mwenye kasi zaidi pia watapata zawadi ya shilingi 100,000 kila mmoja.

Kwa upande wa Mpira wa pete, mshindi wa kwanza atapata shilingi 500,000, kreti 7 za soda, na mchele kilo 50, huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi 300,000, mchele kilo 50, na kreti 7 za soda.

Zaidi ya hayo, zawadi za shilingi 100,000 zitatolewa kwa washindi wa pull table, huku mashindano ya kufukuza kuku na kushindana kula yatatoa zawadi za shilingi 20,000 kwa washindi.

Wito kwa Wanashinyanga

Mratibu Jackline Isaro ametoa wito kwa wanajamii wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezo hii. Alisisitiza kuwa hakutakuwa na kiingilio kwa michezo yote, hivyo ni fursa nzuri kwa watu wa Shinyanga kuungana pamoja na kusherehekea mapumziko ya mwaka kwa njia ya michezo.

“Tunawaalika Wanashinyanga wote kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezo hii ambayo itaanza rasmi Desemba 31, 2024 kuanzia asubuhi katika uwanja wa CCM Kambarage. Hakutakuwa na kiingilio cha aina yoyote,” amesema Isaro.

Mashindano ya DR SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA ni fursa muhimu kwa kuendeleza michezo mkoani Shinyanga na kutangaza vipaji vya vijana. Pamoja na burudani ya michezo, zawadi za kuvutia zinatoa motisha kwa washiriki na kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za kijamii zinazochangia maendeleo ya afya na ustawi wa watu.



Mratibu wa ashindano ya DR SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA, Jackline Isaro akielezea kuhusu mashindano hayo

Share:

BARRICK NORTH MARA YAPELEKA SHANGWE YA SIKUKUU KWA VITUO VYA KULEA WATOTO NA JAMII


Katika kuadhimisha sikukuu za mwisho wa mwaka zinazoendelea, Mgodi wa Barrick North Mara, umetoa zawadi kwa makundi mbalimbali yenye mahitaji kwenye jamii katika wilaya za Tarime na Serengeti ikiwemo vituo vya kulea watoto yatima, na wazee wa kimila ili kuwezesha makundi hayo kusherekea kwa furaha sambamba na kudumisha uhusiano mwema.

Wazee wa kimila kutoka koo 12 wamekabidhiwa zawadi mbalimbali za sukari, mchele,mafuta ya kupikia na Ng'ombe wa kitoweo ili washerehekee sikukuu na wanaukoo wenzao katika vijiji wanavyotoka.

Mgodi wa North Mara kila mwaka umekuwa na utamaduni wa kukumbuka makundi mbalimbali kwenye jamii na kuyapatia zawadi mbalimbali wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya hususani vituo vya kulea watoto yatima na wenye changamoto za kijamii,wagonjwa na wazee wa mila kutoka vijiji mbalimbali vinavyozunguka mgodi huo.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha ATFGM Masanga wilayani katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Barrick North Mara baada ya mgodi huo kukabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu kwenye kituo hicho.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Masanga wakifurahia zawadi wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi za Sikukuu.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Wazee wa kimila wakifurahia zawadi mbalimbali baada ya kukabidhiwa walipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa mgodi huo
Wazee wa kimila wakifurahia zawadi mbalimbali baada ya kukabidhiwa walipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa mgodi huo
Share:

AJALI YA BASI, NOAH YAUA WATU 9

 Watu 9 wamefariki dunia Wilaya Rombo Tarekea Mkoani Kilimanjaro,baada ya Basi la Ngasere kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Noah.

"Nimesikitishwa na taarifa ya vifo vya ndugu zetu 9 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea katika barabara ya kutoka Tarekea, Wilaya ya Rombo kuelekea mji wa Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro. 

Ninawaombea marehemu wapumzike kwa amani. Ninatoa salamu za pole kwa wafiwa, ndugu na jamaa, na ninawaombea majeruhi wapate nafuu kwa haraka.

Nasisitiza madereva kuendelea kuwa makini na waangalifu zaidi barabarani, huku Jeshi la Polisi likiendelea na kazi ya kusimamia sheria za usalama barabarani wakati huu wa mwisho wa mwaka"_ Rais Samia Suluhu Hassan
Share:

Thursday, 26 December 2024

Video Mpya : KACHELENG'WA - NIMEPOTEA

 

Share:

ISSA GAVU ATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA MICHEZO MBALIMBALI - UNGUJA


Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka Mkoa kusini Unguja Mhe. Issa Ussi Gavu ambaye ni Katibu wa Oganazesheni wa CCM Taifa (MCC) ametoa zawadi mbalimbali za medali, vikombe na fedha kwa washindi walioshinda kwenye mashindano ya waendesha baiskeli, mchezo wa bao, karata, kukimbiza kuku nk.

Kabla ya kuanza kwa mashindano hayo wananchi wa Jimbo hilo na viongozi mbalimbali wa Chama walianza kwa matembezi ya amani kuhamasisha kuelekea miaka 61 ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi Januari 12 mwaka 2025.

Wakizungumza kwenye tamasha hilo wananchi hao wameshukuru Serikali ya CCM Chini ya Rais Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi na Mwakilishi wa Jimbo hilo kwa kuwaletea maendeleo na kutimiza zaidi ya asilimia 95 ya ahadi zake katika kipindi cha muda wake wa uongozi na kutekeleza ilani ya CCM ikiwemo barabara, afya, elimu na fursa za uchumi kwa vijana na wanawake.

Mashindano hayo yamefanyika ikiwa ni kuelekea miaka 61 ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DESEMBA 26, 2024

Share:

Wednesday, 25 December 2024

JENISTA MHAGAMA AKABIDHI GARI LA WAGONJWA KWA KITUO CHA AFYA MUHUKURU


Na Regina Ndumbaro - Ruvuma

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Ndugu Simoni Kapinga, amemuwakilisha Mheshimiwa Jenista Mhagama, Mbunge wa Songea Vijijini na Waziri wa Afya, katika kukabidhi gari la wagonjwa kwa Kituo cha Afya cha Muhukuru kilichopo katika Wilaya ya Songea Vijijini.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Ndugu Kapinga amewahimiza wananchi wa Kata ya Muhukuru kutumia gari hilo pindi panapozuka dharura za kitabibu.

Amesema gari hili litasaidia katika kusafirisha wagonjwa wanaohitaji huduma za haraka, hususan akina mama wajawazito na watoto, wanaohitaji kufikishwa kwenye hospitali kubwa ya mkoa.

Kwa upande wake, Dkt. Emanuel Tandewa, Daktari wa Kituo cha Afya cha Muhukuru, ameelezea historia fupi ya kituo hicho kilichozinduliwa mwaka 1968.

Amesema changamoto kuu wanayokutana nayo ni ukosefu wa gari la wagonjwa, jambo ambalo limekuwa likiwawia vigumu akina mama wajawazito na watoto kupata usafiri wa haraka.

Dkt. Tandewa ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zake, hasa kwa kumteua Mheshimiwa Jenista Mhagama kuwa kiongozi ambaye ameonyesha uthubutu na kujitolea kwa ajili ya wananchi wenye uhitaji.

Aidha, Dkt. Tandewa ametoa wito kwa viongozi wengine kujitokeza na kujitolea kwa hali na mali katika kuboresha huduma za kijamii, hususani katika vituo vya afya na shule, ili kuhakikisha maendeleo ya huduma za afya na elimu kwa wananchi wa maeneo ya vijijini.

Hii ni juhudi muhimu katika kuboresha huduma za afya na kuhakikisha kuwa wananchi wa Kata ya Muhukuru wanapata huduma bora za afya kwa wakati.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger