Sunday, 15 December 2024

WAHITIMU CHUO CHA UHASIBU ARUSHA WAKUMBUSHWA KUTUMIA TAFITI ZAO KUSAIDIA JAMII

 

Wahitimu wa chuo cha uhasibu Arusha  wapatao 5854, wamekumbushwa kutumia tafiti zao walizozifanya wakiwa chuo ili ziweze kusaidia jamii na taifa kwa ujumla. 

Akizungumza katika mahafali ya 26 ya mwaka 2024 Naibu waziri wa fedha (mb) Hamad Hssan Chande, amewataka kutumia changamoto  walizokutana nazo na kuzifanya njia ya kufikia mafanikio wanayoyatarajia

"Nawapongeza sana kwa hatua hii, lakini mkiaminiwa jiaminishe, mkawe na subira na kujifunza kuridhika, kuwa wavumilivu na kuacha tamaa ya kuharakia maisha, naamini mkizingatia haya mtafanikiwa na kutimiza ndoto zenu"

 " Sasa tanueni wigo wa taaluma zenu, kama mlivyotembelea SADC, fungueni matawi huko nina imani mtakubaliwa, na hatua hii itaongeza kiwango cha wanafunzi ili kufikia lengo" ,amekumbusha Chande

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha Profesa Eliamani Sedoyeka, amewatakia wanafunzi wote waliohitimu kozi mbalimbali heri na fanaka tele katika maisha yao baada ya kumaliza masomo, ambapo jumla ya wahitimu 5854 kati yao wanaume ni 3601 na wanawake 2253 kwa ngazi ya astashahada, stashahada, shahada na shahada za uzamili katika fani mbalimbali. 

Hata hivyo amewaasa wahitimu kuendelea kujituma, kutochagua kazi na kushirikiana na kila mmoja katika jamii ili kuendelea kujifunza mambo muhimu ya kujijenga na kuzingatia nidhamu ya pesa na muda. 

Katika namna hiyo ameishukuru serikali kwa kuwapatia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 40 kupitia mradi wa elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi(HEET), kwamba kupitia fedha hizo wanatarajia kujenga  songea, na baadhi ya majengo katika kampasi ya babati na arusha yakiwemo madarasa, maabara za kompyuta, jengo la utawala na kituo cha umahiri cha TEHAMA, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuendelea kuboresha na kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia. 

"Tumefanikiwa kutoa wahitimu wa kwanza katika kozi tatu za shahada na kozi moja ya shahada ya uzamili, kozi hizo za shahada ni shahada ya usalama wa mtandao, Shahada ya Uanagenzi katika usimamizi wa utalii na ukarimu, na shahada katika menejimenti ya maktaba na taarifa, kozi hizi tatu za shahada zilianza rasmi mwaka wa masomo 2020/2021"    amefafanua Profesa Sedoyeka. 

"Kipekee nimefurahi kuona  mmefikia hatua hii kubwa, ni imani yangu mtazidi kufanikiwa iwapo mtazingatia yale yote mliyoelekezwa na walimu wenu, nawakaribisha tena hapa chuoni kuongeza kiwango cha elimu sisi tuko tayari  kuwatumikia na nitawakumbuka sana" ameeleza Profesa Sadoyeka. 

Mwenyekiti wa baraza la uongozi wa chuo kikuu cha uhasibu Arusha  Mwamini Tulli, amesema chuo kimeweka mpango mkakati wa kuongeza idadi wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho, mikakati hiyo inaendana na ujenzi wa majengo mapya yanayokidhi vigezo vya watu wenye ulemavu na wale wasiokuwa na changamoto pamoja na ukarabati wa miundombinu mingine. 

"Mimi kama mama nasikia furaha kubwa kuona idadi ya wanawake wanaohitimu leo ni kubwa kiasi hiki, nawasihi mkatumie vizuri taaluma zenu ili mkalete mabadiliko katika jamii zenu, mzidi kuaminika na kuwafanya wazazi wenu kujivunia" amesema Tulli. 

Mwakikishi wa wanafunzi aliyehitimu elimu ya shahada ya kwanza katika chuo hicho, na Rais wa wanafunzi mstaafu Shafii Rajab ameushukuru uongozi wa shule, walimu na walezi kwa kuwasaidia na kuhakikisha leo wanatimiza ndoto yao ya kumaliza masomo.

"Kipekee nawapongeza wazazi wetu kwa kuamini katika kuwasomesha watoto wa kike, nafurahi maana ukisomesha mtoto wa kike umeikomboa jamii, lakini pia wazazi wetu mmefanya kazi kubwa ya kutulipia ada na kutushauri ndio maana leo tuko hapa tunafurahia matunda ya kujitoa kwenu", 

"Tunaahidi tutaenda kufanyia kazi kile tulichokipata, kwa maana ya kuwa wabunifu, kujituma, uadilifu na kuchangamkia fulsa zilizoko mtaani, nasema tumepikwa na tumeiva kutokana na elimu hii, hivyo tunategemea kujenga uchumi wetu na taifa kwa ujumla" amesema Shafii.















Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 15,2024

 

         
Share:

Saturday, 14 December 2024

WAANDISHI DAR ES SALAAM WANUFAIKA NA ELIMU YA UDHIBITI WA EWURA

 

Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Bw.Titus Kaguo, akitoa mafunzo ya elimu ya udhibiti wa huduma za nishati na maj,uvunaji wa maji ya mvua na matumizi ya nishati safi kwa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) leo Disemba 13,2024.

.....

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo Tar.13 Desemba 2024, imefanya mafunzo kwa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) jijini Dar es Salaam, huku msisitizo ukiwa kwenye uvunaji wa maji ya mvua katika kukabiliana na upungufu wa huduma za maji katika maeneo mbalimbali.

Pia katika mafunzo hayo mkazo umetolewa katika kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia na kwenye magari.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw. Titus Kaguo, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Dkt. James Andilile, alisema lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo wanahabari kutoa taarifa za sekta ya nishati na maji kwa usahihi na kwa wakati kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Pamoja na uhamasishaji wa uvunaji maji ya mvua na matumizi ya nishati safi, mafunzo hayo pia yalijikita katika historia ya EWURA, shughuli za udhibiti wa sekta za umeme, petroli, gesi asilia na maji pamoja na mafanikio ya udhibiti tangu kuanzishwa kwa EWURA mwaka 2006.

Naye Katibu wa JOWUTA Bw. Suleiman Msuya aliishukuru EWURA kwa mafunzo hayo huku akitoa rai kwa waandishi wa habari kutumia elimu walioipata kutoa taarifa za nishati na maji kwa usahihi zaidi.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Bw.Titus Kaguo, akitoa mafunzo ya elimu ya udhibiti wa huduma za nishati na maj,uvunaji wa maji ya mvua na matumizi ya nishati safi kwa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) leo Disemba 13,2024.

Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki EWURA, Mhandisi. Mwanamkuu Kanizio, akijibu swali kuhusu sekta ya umeme wakati wa mafunzo hayo.

Baadhi ya waandishi wa habari wanachama wa JOWUTA, wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo leo.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw. Titus Kaguo, aliyekaa katikati,akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa JOWUTA mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya elimu ya udhibiti wa huduma za nishati na maj,uvunaji wa maji ya mvua na matumizi ya nishati safi kwa Wanachama hao leo Disemba 13,2024.

 
Share:

Friday, 13 December 2024

MWILI WA MWANAMKE ALIYESOMBWA NA MTO WAPATIKANA, WACHACHE WAMZIKA

Mwili wa marehemu ukiopolewa mtoni
Mwili wa Leah George (Nkwimba) mwenye umri wa miaka 44, mkazi wa mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga, aliyefariki dunia baada ya kusombwa na maji katika daraja la Machimu lililopo mtaa wa Tambukareli mjini Shinyanga, umezikwa leo katika makaburi ya Dodoma mjini Shinyanga.

Mazishi yamefanyika leo majira ya saa 11 jioni, na kuhudhuriwa na watu wachache wakiwemo ndugu wa marehemu kwa kuwa tayari ulikuwa umeshaharibika, hali iliyolazimu upitilizwe moja kwa moja makaburini na kuwanyima fursa watu waliokuwa wakisubiri nyumbani kwa ajili ya kuaga kabla ya mazishi kama ilivyo katika desturi za kijamii.


Kwa mujibu wa Afisa Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga Inspector Edward Seleman, ambaye alikuwa akiongoza kikosi cha kuutafuta mwili huo, amesema wameupata leo kwenye kijiji cha Mwagala (B) Kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga, baada ya kupewa taarifa na raia wema majira ya saa tatu asubuhi, ambapo waliukuta ukiwa umenasa kwenye mizizi ya mti uliopo kwenye ukingo wa mto.

Leah alifariki dunia Desemba 9, 2024, majira ya jioni, baada ya kusombwa na maji wakati akijaribu kuvuka daraja, kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga na kusababisha baadhi ya madaraja kufunikwa na maji.

Awali Mama mzazi wa Leah Bi. Rachel Faustine (72) aliiambia Redio Faraja kuwa, siku ya tukio mwanaye aliondoka nyumbani asubuhi na kwenda mtaa wa Tambukareli kwa shughuli zake, lakini hakurudi mpaka kesho yake Desemba 10, 2024, alipopigiwa simu na kuelezwa kuwa amesombwa na maji katika daraja la Machimu, wakati akijaribu kuvuka kurudi nyumbani baada ya mvua kukatika.


Alisema baada ya kupata taarifa hizo alishirikiana na majirani kuwataarifu viongozi wa mtaa, ambapo Mwenyekiti wa Mtaa huo alifika na kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na uokoaji ambalo lilifika eneo la tukio na kuanza kuutafuta mwili wa Leah bila mafanikio.


Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Bw. Solomon Nalinga Najulwa, amelishukuru Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa kushirikiana na wananchi kwa namna walivyofanya juhudi mpaka kufanikisha kupatikana kwa mwili huo, ambao wameutafuta kwa muda wa siku tatu bila kukata tamaa mpaka ulipopatikana na kuzikwa kwa heshima zote za kibinadamu.

Chanzo- Faraja Fm
Share:

SERIKALI YA TANZANIA YATEKELEZA MIKAKATI YA KUBORESHA HUDUMA ZA DHARURA

Share:

OFISI YA WAZIRI MKUU YATOA TAHADHARI DHIDI YA KIMBUNGA CHIDO

 


Share:

Thursday, 12 December 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 13, 2024

Share:

NILIVYOJIKUTA NAOA MZUNGU



Jina langu ni Mustafa kutoka Zanzibar nina miaka 29 sasa nikiwa ni Baba wa watoto watatu na mke mmoja ambaye na mpenda sana na yeye ameonyesha kunipenda tangu siku ya kwanza tunaanza mahusiano yetu.

Hata hivyo, hapo awali katika kutafuta mke wa kumuoa kuna wakati nilifikia kipindi na kusema huwenda nina mikosi katika maisha yangu, hiyo ni kutokana kila mwanamke ambaye nilikuwa namtongoza alikuwa akinikatalia ombo langu.

Sikujua sababu ni nini hasa maana kama ni mvuto wa sura ninao, nina kazi ya kunipa kipato kizuri tu cha kijikimu na kuendeleza maisha yangu na hata kumuhudumia mwanamke ambaye nitakuwa naye katika mahusino.

Ila sasa nina mke ambaye ni raia wa Canada, alikuja Zanzibar kutalii na ndipo aliweza kukutana na mimi na kuanzisha mahusiano, kukutana kwetu kulikuja baada ya mimi kuhaingaika sana kutafuta dawa za mvuto wa kimapenzi ambazo nilikuja kuzipata kwa Dr Bokko.

Mtu huyu nilikutana naye kupitia mitandao ya kijamii ambapo kwenye group moja la WhatsApp linalohusu mambo ya uchumba, dada mmoja alituma namba zake +255618536050 na kueleza Dr Bokko alifanikiwa lengo lake la kupata mume.

Nikiwa katika hali ya kukata tamaa, niliamua kupiga moyo konde na kumtumia Dr Bokko ujumbe mrefu kupitia WhatsApp nikimueleza kuhusu shida yangu. Haikuchukua muda ujumbe wangu ukawa umejibiwa na mchakato wa kutumiwa dawa ukawa umeanza.

Baada ya kupata dawa zangu nilianza kuzitumia nikiwa na matumaini tele, sasa siku moja nikiwa nakatiza maeneo ya mjini nilikutana na dada mmoja wa kizungu ambaye alikuwa anahitaji nyumba ya kufikia wageni, kutokana mimi nilikuwa ni mwenyeji wa pale, nilimsaidia kupata nyumba hiyo mara moja.

Aliniomba namba yangu ya simu na kuniambia atanitafuta siku inayofuata, sikuwa na mawazo kuwa anaweza kuja kuwa mpenzi wangu, nilikuwa najua tu anaweza kunipa kazi za hapa na pale na baadaye kupata fedha za kusukuma maisha.

Basi akanipigia tukakutana na kuzungumza sana, tukala na kunywa, tuliendelea kuzoeana hadi ikafika hatua za yeye kuonyesha dalili kuwa ananipenda.

Nilisita kumwambia kuhofia kuwa naweza kuharibu urafiki wetu, mwenyewe uvumilivu ulimshinda na kunitumia SMS kuwa ananipenda ana angependa niwe mume wake.

Na hatimaye tulianza mahusiano hadi kuja kufunga ndoa na sasa tumejaliwa kupata watoto watatu wa kiume, maisha ni mazuri sana, watu wengi wanauliza nimefanya nini hadi nikaweza kumuoa, siri ya ushindi wangu ni Dr Bokko. Mpigie kwa namba +255618536050.



Share:

Tuesday, 10 December 2024

KATIBU MWENEZI CCM DODOMA AWASIHI WANANCHI KUENDELEA KUWA WAMOJA KATIKA KUPIGA VITA UMASIKINI ADUI WA MAENDELEO




Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Tanzania ikiwa inaadhimisha miaka 63 ya Uhuru wake,Katibu wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Jawadu Mohamed amewataka wananchi kuendelea kuwa na umoja na mshikamano katika kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na kuhakikisha kuwa taifa linaendelea kupiga hatua kubwa katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Aidha ameeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru kuwa ni pamoja na kuondoa ujinga, maradhi na umasikini vitu vilivyokuwa kama adui wa maendeleo nchini.

Hayo yameelezwa leo December 9,2024 Jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika ambapo amesema kuwa chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kuleta mabadiliko makubwa na ya kudumu kwa wananchi wake na kwamba mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya chama hicho na wananchi.

Ameeleza kuwa hatua muhimu zimepigwa katika kuboresha huduma za afya, elimu, na kubuni fursa za kiuchumi kwa wananchi na kwamba Serikali imekuwa ikianzisha sera na miradi mingi ya kijamii ambayo imewezesha kupunguza umasikini na kuboresha maisha ya wananchi, hasa katika maeneo ya vijijini.

Katibu Mwenezi huyo ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka 63 ya uhuru, Serikali imefanikiwa kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa ya milipuko, kama vile malaria, kipindupindu na mengineyo ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya afya, kwa kujenga zahanati na vituo vya afya kila pembe ya nchi, na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote, hasa wale wa vijijini.

Kwa upande wa sekta ya elimu, Katibu Mwenezi huyo ameleza kuwa Tanzania imefanikiwa kutoa elimu bure kwa watoto wote, ambapo karibu kila mtoto nchini anapata elimu ya msingi na sekondari.

"Ndani ya miaka hii 63 ya Uhuru tumeshuhudia mapinduzi makubwa kwenye sekta ya elimu,Serikali imejenga shule mpya, kuajiri walimu wengi, na kuongeza rasilimali za elimu ili kuhakikisha kuwa kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu bora,

“Leo hii, tunajivunia kuwa na idadi kubwa ya wahitimu wa vyuo vikuu, wataalamu wa sayansi na teknolojia, na wataalamu wa afya, ambao wanachangia katika maendeleo ya taifa letu,” anafafanua

Ameleza kuwa kupambana na umasikini ni moja ya changamoto kubwa zilizokabiliana na taifa tangu kupata uhuru.

Hata hivyo, amesema kuwa juhudi za serikali katika kuboresha kilimo, viwanda, na miundombinu zimeleta matokeo chanya kwa wananchi.

"Kwa mfano, serikali imeimarisha mifumo ya kilimo cha kisasa na mikopo kwa wakulima, ikiwemo kuanzisha miradi ya maji na barabara, ili kuboresha maisha ya watu katika vijiji na miji midogo. Matokeo ya jitihada hizi ni ongezeko la uzalishaji wa chakula na bidhaa nyingine za kilimo, na hivyo kutoa fursa nyingi za ajira na kuongeza pato la taifa, "amesisitiza.

Hata hivyo amesema licha ya mafanikio hayo, bado kuna changamoto zinazokabiliana na nchi, lakini amesisitiza kuwa Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia malengo yake ya kuwa na uchumi wa kati na wa viwanda, huku wananchi wakinufaika na mafanikio hayo.

"Maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru ni nafasi nzuri ya kutafakari na kujivunia kile kilichopatikana,tunapaswa kuangalia mbele na kufanya kazi kwa juhudi ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu, huu ni wakati wa kujivunia mafanikio yetu, lakini pia ni wakati wa kuendelea kujitahidi kufikia malengo makubwa zaidi kwa ajili ya taifa letu na vizazi vijavyo,” amesema







Share:

NILIVYOMFUKUZA KAZI BOSI ALIYEKATAA KUNIONGEZA MSHAHARA

Jina langu ni Naomi kutokea Dar es Salaam, Tanzania, katika umri wangu nimekuja kujua katika hii dunia kuna watu ambao wana roho za ajabu sana, unaweza kukuta mtu anakuchukia na kukufanyia mambo ya ajabu na aibu bila kujua sababu hasa ni ipi.

Hadi kuna muda unajikuta unajiuliza kama ulishawahi kumkosea mahali?, hapana!, ulishawahi hata kumchukulia kitu chake?, hapana!, ulishawahi kumsema vibaya kwa watu, hapana, sasa chuki yote hii inatoka wapi?.

Haya ndio maswali niliyokuwa najiuliza mimi Nairobi kila mara baada ya Bosi wangu kuwa na chuki ya waziwazi kwangu, alifanya mambo mengi ya kunikomoa ikiwa ni pamoja na kuninyima likizo, kunikata mshahara kwa kosa ambalo hata sijafanya,

Nakumbuka kuna kipindi alishawahi kunikata Tsh50,000 kwa madai kuwa simekuwa siwajibiki vizuri katika kazi yangu, hadi wafanyakazi wenzangu walikuwa  wananionea huruma na kuamua kwenda kuniombea msamaha kama kuna sehemu nilimkwaza.

Aliwasikiliza na kuwaambia wakiendelea kufuatilia jambo hilo atawafukuza kazi wote, mfanyakazi mwenzangu aitwaye Grace aliniambia tuonane wikiendi inayofuata ana habari njema kwangu.

Basi wikiendi ilipowadia niliweza kukutana naye nyumbani kwake, tulizungumza mengi ila kubwa zaidi aliniambia anaweza kunisaidia kuhusu manyanyaso nayopata kwa Bosi wangu pale ofisini.

Nilimwambia itakuwa vizuri maana nilitakiwa kuongezwa mshahara takribani mwaka mmoja lakini Bosi hajafanya hivyo licha ya mkataba wangu kueleza hilo wazi wazi.

"Sasa sikiliza Dada yangu Grace, nakupa namba ya Dr Bokko, huyo mtalaamu ataweza kunisaidia kwa haraka, mimi pia aliwahi kunitoa katika changamoto moja kubwa huko nyuma," Grace aliniambia.

Basi Grace alichukua simu yake na kunitajia namba hii +255618536050 ya Dr Bokko ambaye nilimpigia pale pale nikiwa na Rose na kumueleza jinsi Bosi wangu amekuwa akinitesa na kugoma kuniongezea mshahara.

Dr Bokko aliniuliza maswali machache na kuniambia niwe na subra kwani muda wa siku tatu hali itakuwa shwari kabisa, nilikuwa na matumaini tele ya ushindi kutokana na habari kedekede nilizopewa kuhusu mtalaamu huyo.

Ghafla kesho yake kazini tulishangaa Mkuu wa Taasisi kaja ofisini kwetu na sio utaratibu wake kuja bila taarifa, ghafla ilitangazwa kuwa atakuwa na mkutano na wafanyakazi wote.

Katika ule mkutano Mkuu wa Taasisi alitangaza kumfukuza kasi Bosi kwa madai alikuwa akilazimisha kutoka kimapenzi na baadhi ya wafanyakazi pale ofisini jambo ambalo ni kinyume na maadili na kiapo alichoaapa kukisimamia.

Basi Bosi yule aliondoka kwa aibu kubwa na baada ya wiki alikuja Bosi mpya, huyu Bosi mpya anapenda wafanyakazi wote bila ubaguzi wowote.

Baada ya wiki moja aliniita ofisini kwake na kuniambia kuwa ameniongeza mashahara wangu mara mbili kwani mkataba wangu unaonyesha nilipaswa kuongezwa mshahara muda mrefu.

Kwa uzoefu wangu, Dr Bokko anaweza kukufanya kushinda bahati nasibu, kukupa mvuto wa kibiashara na mapenzi, kuwathibiti adui zako, kushinda kesi mahakamani, kubaina anayechepuka na mume au mke wako. Mpigie kwa namba hii +255618536050.


Share:

Video Mpya : MAHILI NG'WANA LUSI - BINADAMU

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger