Tuesday, 10 December 2024

NGORONGORO WATHIBITISHA KUACHANA NA KUNI


-Wajitokeza kwa wingi kujipatia majiko ya gesi ya ruzuku

Wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha wameitikia wito wa kutumia Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda afya na kutunza mazingira.

Hayo yamedhihirika Desemba 8,2024 Wilayani Ngorongoro wakati wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa majiko ya gesi yanayotolewa kwa bei ya ruzuku ya 50% na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano na Kampuni ya Lake Gas wilayani humo.

Akizungumza wakati wa zoezi la usambazaji na uuzwaji wa majiko hayo ya ruzuku wilayani humo, Msimamizi wa Mradi wa REA Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro na Arusha), Mhandisi Gift Kombe aliwasisitiza wananchi kuzingatia elimu inayotolewa ya matumizi sahihi ya majiko hayo ili yaweze kuleta tija inayokusudiwa ikiwa na kuendelea kujaza mitungi hiyo pindi inapoisha.

Wananchi wilayani humo kwa nyakati tofauti walishukuru kwa kufikiwa na mradi na waliahidi kuwa mabalozi kwa wananchi wengine ambao hawakupata fursa ya kufika kupata huduma.

"Kwakweli hili ni jambo jema ila bahati mbaya si wananchi wote wameweza kufika hapa; tutaendelea kuhamasishana katika matumizi ya nishati safi ya kupikia," alisema Samwel Maganila mkazi wa Wasso Mashariki, Ngorongoro.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.
Share:

MGODI WA BARRICK NORTH MARA WAVILIPA VIJIJI VITANO MRABAHA WA SHILINGI BILIONI 2.1


Wenyeviti wa vijiji vilivyopo jirani na mgodi wa Barrick North Mara wakionyesha mifano ya hundi za malipo ya gawio la mrahaba la shilingi bilioni 2.1 lililotolewa na Mgodi huo, baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima (wa pili kulia waliokaa), katikati ni Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Apolinary Lyambiko.
Baadhi ya viongozi wa vijiji wakipokea hundi za gawio kutoka Waziri Doroth wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya viongozi wa vijiji wakipokea hundi za gawio kutoka Waziri Doroth wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akiongea na Wananchi katika hafla hiyo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara,Apolinary Lyambiko akizungumza
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akigawa majiko ya gesi kwa baadhi ya akina mama yaliyotolewa na Taifa Gesi kwa kushirikiana na Mgodi huo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akipata maelezo katika Banda la maonesho la Barrick North Mara wakati wa maonesho ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku 16 za kupinga vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa North Mara katika picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.

***

Mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara, kwa mara nyingine tena umevipatia vijiji vitano vilivyo jirani gawio la mrabaha la shilingi bilioni 2.1, ikiwa ni malipo ya robo ya tatu ya mwaka 2024.

Kiasi cha fedha zilizolipwa kwenye vijiji hivyo ni Genkuru (746,461,112), Nyangoto (581,176,695), Kerende (454,221,570), Nyamwaga (225,997,310) na Kewanja (98,350,773).

Wanufaika wa malipo hayo ni vijiji ambavyo vilikuwa na haki ya kuchimba dhahabu kwenye shimo la Nyabigena (ambalo ni sehemu ya mgodi wa North Mara) kabla ya Kampuni ya Barrick kukabidhiwa kuendesha mgodi huo kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals kuanzia mwaka 2019.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko, akiongea katika hafla ya kukabidhi fedha hizo amesema malipo hayo ya shilingi bilioni 2.1 yanafanya gawio la mirabaha iliyotolewa kwa vijiji hivyo kutokana na uzalishaji wa Aprili 2023 hadi Septemba 2024 kufikia shilingi bilioni 4.471.

Mifano ya hundi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.1 imekabidhiwa kwa viongozi wa vijiji hivyo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kitaifa Nyamongo wilayani Tarime, Mara.

Waziri Gwajima ameipongeza Barrick North Mara akisema utoaji wa gawio la mirabaha hiyo unasaidia kuboresha huduma za jamii na kuchochea maendeleo ya kisekta katika vijiji hivyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara amewataka viongozi wa vijiji vilivyopata fedha hizo za mrabaha kuhakikidha wanashirikisha wananchi kupitia mikutano halali kuibua na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati.

Nao wenyeviti wa vijiji vilivyopata mrabaha walishukuru na kuupongeza mgodi wa North Mara kwa namna unavyoendelea kuimarisha mahusiano na jamii inayouzunguka.

"Mgodi umekuwa na mahusiano mazuri na wananchi, hasa kwa kushirikiana katika nyanja za kimichezo na kimaendeleo, pia umekuwa ukitimiza wajibu wa kisheria kama Serikali inavyoelekeza, tunashukuru sana," amesema Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyangoto, Zakaria Machage.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Genkuru, Juma Elias ameushukuru mgodi huo na kuahidi kwenda kushirikiana na wananchi wake kupanga matumizi mazuri ya fedha walizopata kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 

"Fedha tunayo, sasa hakuna sababu ya kuchelewesha miradi," amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amekabidhi majiko 222 ya gesi kwa baadhi ya wanawake kutoka vijiji 11 vinavyozunguka mgodi wa North Mara.

Majiko hayo yametolewa na mgodi huo kwa kushirikiana na Kampuni ya Taifa Gas katika kuunga mkono jitihada za serikali za kumtua mama kuni kichwani na kumuepushia adha ya matumizi ya nishati ya kupikia isiyo salama kupitia kampeni ya Barrick na wadau wake katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizomalizika juzi.
Share:

TRA YATOA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WATU WENYE ULEMÀVU MKOANI TANGA


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

BAADHI ya watu wenye ulemavu Mkoa wa Tanga wameshindwa kurejesha mikopo ya asilimia mbili inayotolewa na halmashauri kwa kukosa elimu juu ya ufanyaji biashara na ulipaji kodi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Miradi kwa Viziwi Tanzania (UMIVITA) Ally Nassoro ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya elimu ya mlipa kodi kwa watu wenye ulemavu yaliyotolewa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Mkoa wa Tanga.

Amesema mikopo hiyo ni mzuri na inawasaidia sana katika kuendesha biashara zao na kujikwamua na umasikini, ambapo wengine wanafanikiwa kurejesha na baadhi kushinda huku wakiishia hata kuhama makazi yao.

"Wanaoshindwa kurejesha wanawanyima wenzao haki ya kupata mkopo, Sheria ya mkopo inasema kopa halafu rejesha, kwahiyo nikwambie wale wote ambao hawajalipa walipe ili wenzao wapqte" amesema.

Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba  elimu waliyopata itawanufaisha pakubwa kwani awali hawakuwa na uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayotokana na ulipaji wa kodi.

"Watu wenye ulemavu walikuwa hawaelewi kanuni au sheria zinavyosaidia katika kulipa kodi, lakini pia walikuwa na shida ya ulipaji wa kodi  na vipengele wanavyotakiwa kuvitumia, hivyo tumefurahi kupata elimu hii kwasababu itatusaidia kufuatilia ulipaji wa kodi kama inavyotakiwa" amesema.

Naye Ofisa Mkuu Msimamizi wa Kodi kitengo cha Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano Tanga, Flavian Byabato amesema kwa kushirikiana na UMIVITA wamewiwa kuwapa elimu ya kodi watu wenye ulemavu ili kuwaongeze uelewa.

"Siku ya leo ikiwa ni muendelezo wa TRA kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari na kutoa elimu ya kodi kwa wadau wetu ili waelewe zaidi masuala mbalimbali yanayohusiana na kodi, lakini pia ni katika kuendeleza nchi yetu kupitia maendeleo,

"Na maendeleo yanafika kutokana na kulipa kodi, kwahiyo tukawiwa kushirikiana na chama hiki kutoa hii elimu ya kodi kwa manufaa yao lakini pia na serikali" amesema Byabato.

Byabato amesema elimu waliyotoa ni pamoja na usajili wa biashara, kulipa kodi stahiki sambamba na hayo wamewajulisha haki ambazo wanazo katika masuala mbalimbali ya kodi ikiwemo kupewa taarifa na elimu ya kodi.

"Lakini wana haki ya kupewa hati safi ya ulipaji kodi baada ya kukamilisha taratibu mbalimbali ikiwemo matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki (EFD) na utoaji wa risiti,

"Tunashkuru kwamba wameitikia vema na tunategemea kuwa huu ni mwanzo wa hatua ya kukamilisha wajibu wao, tunategemea watakuwa walipaji waziri wa kodi na kuweza kueneza hii elimu ambayo wameipata" amesema.

Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la watu wenye ulemavu Mkoa wa Tanga (SHIVIAWATA) Subira Hoza amesema kabla ya kupata elimu hiyo watu wenye ualbino Mkoa walikuwa wanafahamu kuhusu elimu ya mlipa kodi kwa  asilimia 30.

"Lakini leo tumejifunza mambo mengi sana, hasa kuhusu ulipaji kodi kwa mtu mwenye kupata kiwango cha juu na chini, lakini pia kuhusu misamaha ya kodi, kwamba wapi wanapaswa kusamehewa na wapi walipe" ,amebainisha.








Share:

SERIKALI YA RAIS SAMIA KUZINDUA TUZO ZA UTALII NA HIFADHI

 
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeahidi kuendeleza juhudi za kukuza utalii ndani na nje ya nchi na Disemba 20,2024 itatoa tuzo za Utalii na Uhufadhi kwa wadau waliosaidia kukuza utalii nchini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam Disemba 9,2024 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Hassan Abbas wakati akitangaza kufanyika kwa uzinduzi wa Tuzo ya Utalii na Uhifadhi.

"Shughuli za tuzo zitakayofanyika Disemba 20 ,2024 jijini Arusha ambapo Tanzania kwa mara ya kwanza itatoa tuzo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ambao wanakumbukwa kwa kutoa mchango ulioiwezesha sekta hiyo ya utalii kuwa na mafanikio makubwa."


Katika hatua nyingine Dkt.Hassan Abbas amezungumzia Tuzo ambazo nchi imezipata duniani kwa kusema kuwa tuzo hizo zimetokana na Taifa kuwa na vivutio Bora kwa watalii wa ndani na nje ya Tanzania.


 Ametaja baadhi ya vivutio vya utalii nchini vinavyopendwa kuwa ni mbuga za wanyama kama Serengeti, Ruaha, Ngorongoro pamoja na kuwepo na makumbusho ya Taifa ambayo yamehifadhi vitu vya kale.

Share:

Monday, 9 December 2024

KATIBU MWENEZI CCM DODOMA AWASIHI WANANCHI KUENDELEA KUWA WAMOJA KATIKA KUPIGA VITA UMASIKINI ADUI WA MAENDELEO




Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Tanzania ikiwa inaadhimisha miaka 63 ya Uhuru wake,Katibu wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Jawadu Mohamed amewataka wananchi kuendelea kuwa na umoja na mshikamano katika kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na kuhakikisha kuwa taifa linaendelea kupiga hatua kubwa katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Aidha ameeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru kuwa ni pamoja na kuondoa ujinga, maradhi na umasikini vitu vilivyokuwa kama adui wa maendeleo nchini.

Hayo yameelezwa leo December 9,2024 Jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika ambapo amesema kuwa chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kuleta mabadiliko makubwa na ya kudumu kwa wananchi wake na kwamba mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya chama hicho na wananchi.

Ameeleza kuwa hatua muhimu zimepigwa katika kuboresha huduma za afya, elimu, na kubuni fursa za kiuchumi kwa wananchi na kwamba Serikali imekuwa ikianzisha sera na miradi mingi ya kijamii ambayo imewezesha kupunguza umasikini na kuboresha maisha ya wananchi, hasa katika maeneo ya vijijini.

Katibu Mwenezi huyo ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka 63 ya uhuru, Serikali imefanikiwa kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa ya milipuko, kama vile malaria, kipindupindu na mengineyo ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya afya, kwa kujenga zahanati na vituo vya afya kila pembe ya nchi, na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote, hasa wale wa vijijini.

Kwa upande wa sekta ya elimu, Katibu Mwenezi huyo ameleza kuwa Tanzania imefanikiwa kutoa elimu bure kwa watoto wote, ambapo karibu kila mtoto nchini anapata elimu ya msingi na sekondari.

"Ndani ya miaka hii 63 ya Uhuru tumeshuhudia mapinduzi makubwa kwenye sekta ya elimu,Serikali imejenga shule mpya, kuajiri walimu wengi, na kuongeza rasilimali za elimu ili kuhakikisha kuwa kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu bora,

“Leo hii, tunajivunia kuwa na idadi kubwa ya wahitimu wa vyuo vikuu, wataalamu wa sayansi na teknolojia, na wataalamu wa afya, ambao wanachangia katika maendeleo ya taifa letu,” anafafanua

Ameleza kuwa kupambana na umasikini ni moja ya changamoto kubwa zilizokabiliana na taifa tangu kupata uhuru.

Hata hivyo, amesema kuwa juhudi za serikali katika kuboresha kilimo, viwanda, na miundombinu zimeleta matokeo chanya kwa wananchi.

"Kwa mfano, serikali imeimarisha mifumo ya kilimo cha kisasa na mikopo kwa wakulima, ikiwemo kuanzisha miradi ya maji na barabara, ili kuboresha maisha ya watu katika vijiji na miji midogo. Matokeo ya jitihada hizi ni ongezeko la uzalishaji wa chakula na bidhaa nyingine za kilimo, na hivyo kutoa fursa nyingi za ajira na kuongeza pato la taifa, "amesisitiza.

Hata hivyo amesema licha ya mafanikio hayo, bado kuna changamoto zinazokabiliana na nchi, lakini amesisitiza kuwa Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia malengo yake ya kuwa na uchumi wa kati na wa viwanda, huku wananchi wakinufaika na mafanikio hayo.

"Maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru ni nafasi nzuri ya kutafakari na kujivunia kile kilichopatikana,tunapaswa kuangalia mbele na kufanya kazi kwa juhudi ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu, huu ni wakati wa kujivunia mafanikio yetu, lakini pia ni wakati wa kuendelea kujitahidi kufikia malengo makubwa zaidi kwa ajili ya taifa letu na vizazi vijavyo,” amesema







Share:

Video Mpya : MAHILI NG'WANA LUSI - BINADAMU

 

Share:

NGORONGORO WATHIBITISHA KUACHANA NA KUNI INAWEZEKANA


-Wajitokeza kwa wingi kujipatia majiko ya gesi ya ruzuku

Wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha wameitikia wito wa kutumia Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda afya na kutunza mazingira.

Hayo yamedhihirika Desemba 8,2024 Wilayani Ngorongoro wakati wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa majiko ya gesi yanayotolewa kwa bei ya ruzuku ya 50% na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano na Kampuni ya Lake Gas wilayani humo.

Akizungumza wakati wa zoezi la usambazaji na uuzwaji wa majiko hayo ya ruzuku wilayani humo, Msimamizi wa Mradi wa REA Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro na Arusha), Mhandisi Gift Kombe aliwasisitiza wananchi kuzingatia elimu inayotolewa ya matumizi sahihi ya majiko hayo ili yaweze kuleta tija inayokusudiwa ikiwa na kuendelea kujaza mitungi hiyo pindi inapoisha.

Wananchi wilayani humo kwa nyakati tofauti walishukuru kwa kufikiwa na mradi na waliahidi kuwa mabalozi kwa wananchi wengine ambao hawakupata fursa ya kufika kupata huduma.

"Kwakweli hili ni jambo jema ila bahati mbaya si wananchi wote wameweza kufika hapa; tutaendelea kuhamasishana katika matumizi ya nishati safi ya kupikia," alisema Samwel Maganila mkazi wa Wasso Mashariki, Ngorongoro.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.
Share:

Sunday, 8 December 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 9, 2024

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger