Friday, 22 November 2024

VETA KIHONDA YASISITIZA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WAHITIMU ILI KUJIAJIRI


-Mkurugenzi VETA Kanda ya Mashariki ahimiza ujasiriamali kwa vitendo

Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki, John Mwanja ameelekeza vyuo vya VETA Kanda ya Mashariki kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo kuwasaidia vijana kujiajiri baada ya kuhitimu mafunzo yao.

John Mwanja, ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 36 ya wanafunzi wa ngazi ya II katika chuo cha VETA Kihonda, yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho, tarehe 21 Novemba 2024.

Amewataka walimu na menejimenti za vyuo vya kuwasaidia na kuwasimamia wanafunzi kuanzisha vikundi, kupanga na kutekeleza mawazo ya kuanzisha makampuni madogo madogo wakiwa darasani, ili kuwazoesha kuungana na kufanya kazi kwa pamoja, kujiajiri na kutafuta soko la bidhaa zao.

“Hivyo, ni jukumu la menejimenti kuwasaidia wanafunzi waliojiunga kwenye vikundi vidogo vidogo kwa fani mbalimbali, kurasimisha vikundi hivyo ili bidhaa zitakazozalishwa ziweze kuingia sokoni,” Mwanja amesema

Mkurugenzi huyo, amesisitiza menejimenti kutoa mafunzo ya ujuzi yenye tija yanayolenga kuzalisha bidhaa zenye ubora kukidhi ushindani na kutafuta soko ili kupata marejesho ya bidhaa hizo kupitia fedha za mauzo.

Aidha, Mwanja ametaka bidhaa zinazotengenezwa na wanafunzi wakati wa mazoezi ya vitendo zitafutiwe soko na kama inashindikana kupata soko zitolewe kwa watu wenye mahitaji maalum badala ya kurundikana katika karakana.

Mkuu wa Chuo cha VETA Kihonda, Dkt. Salumu Ulimwengu, amewapongeza wahitimu na kuwataka Kwenda kutumia ujuzi katika kuwaendeshea maisha yao na kuwa mfano wa kuigwa na jamii itakayowazunguka.

“Nendeni mkawe mabalozi wazuri, mkatumie elimu ya ufundi stadi mliyoipata kuwaletea kipato,” Dkt.Ulimwengu amesema

Mahafali hayo yalijumuisha wahitimu 230 wa ngazi ya II wakiwemo wasichana 62 na wakiume 168 katika fani za Zana za Kilimo (wahitimu 25), Umeme wa magari (23), umeme majumbani (42), Bomba (37), Useremala (11), Uashi (21), Majokofu na Viyoyozi (32), Ushonaji (16), Ufundi magari (21), na Mitambo na Ukerezaji (16). Pia wanafunzi 132 wa udereva na kozi za muda mfupi wamehitimu
Share:

FURAHIA MAISHA NA GUTA ZA TOBOA , OIL ZA FLYING HORSE!

 


Share:

Thursday, 21 November 2024

JTC YATEMBELEA MTO MALAGARASI AMBAO NI SEHEMU YA MPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI

Mkuu wa timu ya wataalamu kutoka Burundi Mhe. Meja Jenerali Mbonimpa Maurice (aliyesimama mbele) pamoja na kiongozi wa timu ya Tanzania Bw. Samwel Katambi (aliyekaa mbele) na wataalamu wengine wakitoka kutembelea eneo la mto Malagarasi wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma wakati Kamati ya Pamoja ya Wataalamu wa Uimarishaji mpaka wa Tanzania na Burundi (JTC) ilipotembelea eneo hilo.

*****************

Na Munir Shemweta, WANMM KASULU

Kamati ya Pamoja ya Wataalamu ya Uimarishaji Mpaka wa Tanzania na Burundi (JTC) imetembelea Mto Malagarasi ambao ni sehemu ya mpaka wa kimataifa kati ya nchi hizo mbili ili kujionea hali halisi ya eneo hilo.

Uamuzi wa kutembelea eneo hilo la mto Malagarasi ni sehemu ya programu ya kikao cha JTC kinachoendelea katika halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.

Kikao hicho pamoja na mambo mengine kimepanga kutembelea katika vijiji vya Bukililo na Nyakayenzi upande wa Tanzania na kijiji cha Kamusha nchini Burundi.

Timu hiyo ya wataalamu ambayo kwa upande wa Tanzania iliongozwa na Mkurugenzi Msaidizi idara ya Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Samwel Katambi huku upande wa Burundi ikioongozwa na Meja Jenerali Mbonimpa Maurice ilitembelea eneo hilo la mpaka tarehe 20 Novemba 2024.

Lengo la kutembelea mpaka huo wa kimataifa ni kuwezesha JTC Kuandaa bajeti na mpango kazi wa uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili.

Kikao cha Pamoja cha Wataalamu (JTC) kimeanza siku ya jumatatu tarehe 18 Novemba 2024 na kinatarajia kumalizika siku ya ijumaa tarehe 22 Novemba 2024.

Zoezi la uimarishaji mipaka ya kimataifa ni utekelezaji wa makubaliano ya umoja wa Afrika kuwa ifikapo mwaka 2027 mipaka baina ya nchi za afrika iwe imeimarishwa.

Gavana wa jimbo la Rutana nchini Burundi Nibitanga Olivier (kulia) akitoa maelekezo kwa wataalamu waliokuwa wakivuka moja ya mito kwenye eneo la mto Malagarasi wakati Kamati ya Pamoja ya Wataalamu wa Uimarishaji mpaka wa Tanzania na Burundi (JTC) ilipotembelea eneo hilo tarehe 20 Novemba 2024.
Kiongozi wa wa timu ya Tanzania Bw. Samwel Katambi (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa Kamati ya Pamoja ya Wataalamu wa Uimarishaji mpaka wa Tanzania na Burundi (JTC) ilipotembelea eneo la mto Malagarasi uliopo wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma. kushoto ni kiongozi wa timu ya wataalamu kutoka Burundi Mhe. Meja Jenerali Mbonimpa Maurice. 
Kiongozi wa wa timu ya wataalamu kutoka Burundi Mhe. Meja Jenerali Mbonimpa Maurice (kushoto) pamoja na kiongozi wa timu ya Tanzania Bw. Samwel Katambi (kulia) wakiwaongoza wataalamu wakati wa kutembelea sehemu ya eneo la mto malagarasi wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma wakati Kamati ya Pamoja ya Wataalamu wa Uimarishaji mpaka wa Tanzania na Burundi (JTC) ilipotembelea eneo hilo.
Wataalamu wakitembelea eneo la mto Malagarasi wakati Kamati ya Pamoja ya Wataalamu wa Uimarishaji mpaka wa Tanzania na Burundi (JTC) ilipotembelea eneo hilo tarehe 20 Novemba 2024.
Wataalamu wakitoka katika moja ya eneo walipotembelea eneo la mto Malagarasi wakati Kamati ya Pamoja ya Wataalamu wa Uimarishaji mpaka wa Tanzania na Burundi (JTC) ilipotembelea eneo hilo tarehe 20 Novemba 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Share:

BoT YASISITIZA MATUMIZI YA SHILINGI KATIKA KUPANGA BEI NA KUFANYA MALIPO TANZANIA



Share:

Wednesday, 20 November 2024

IAA YAJIKITA KUIMARISHA HUDUMA ZAKE KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA


Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) ukiongozwa na Mkuu wa Chuo,  Prof. Eliamani Sedoyeka wamefanya ziara nchini Uingereza kwa ajili ya kujifunza na kuangalia njia mbalimbali za kuboresha huduma za ujifunzaji na ufundishaji. 

Katika ziara hiyo Uongozi wa IAA umetembelea ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na kukutana na Mheshimiwa Balozi Mbelwa Brighton Kairuki.

Mhe. Balozi amekipongeza Chuo kwa juhudi zake katika kuboresha elimu na pia amejadiliana na viongozi juu ya fursa mbalimbali zilizopo nchini uingereza katika sekta ya elimu na nyinginezo.

Aidha , Novemba 19, 2024 Mkuu wa Chuo Prof. Eliamani Sedoyeka na timu yake wametembelea ARU university (Anglia Ruskin University) mjini Cambrigde ambapo pamoja na mambo mengine mengi wamejadili masuala mbalimbali ya kitaaluma, tafiti na ushauri. Lengo ikiwa ni kujifunza na kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuendelea kuboresha ufundishaji, ujifunzaji na huduma mbalimbali zinazotolewa na Chuo. 

Prof. Sedoyeka ameeleza kuwa, ajenda ya serikali ni kuhakikisha Taasisi za Elimu ya Juu zinatoa huduma kwa hadhi ya Kimataifa na IAA kama Taasisi ya Umma tumejipanga kuhakikisha kuwa tunatoa huduma katika ubora wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa na mitaala inayokidhi viwango vya kimataifa, kuongeza udahili wa wanafunzi wa kimataifa na kuhakikisha wahitimu wetu wanakidhi soko la ajira la ndani na lile la kimataifa.

Katika ziara hiyo Chuo kinatarajia kutembelea vyuo vingine ikiwemo Oxford university, Nottingham University, commonwealth AI academy pamoja na kukutana na Watanzania (Diaspora) waishio Uingereza ambao ni wataalam katika sekta za fedha, uhasibu, uchumi, tehama na nyingine nyingi.











Share:

SIMBA SC YAZINDUA JEZI MPYA!!


Na Isri Mohamed

Klabu ya Simba leo Novemba 20, 2024 imezindua rasmi jezi mpya watakazotumia kwenye mashindano ya kimataifa wanayoshiriki ambayo ni kombe la shirikisho barani Afrika ( CAFCC)

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jezi hizo iliyofanyika Katika duka la Sandaland kinondoni, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amewataka mashabiki kuzichangamkia jezi hizo mapema.

“Kipekee tunamshukuru Sandaland kwa utekelezaji wa haya mambo, jezi ni nzuri  naamini Wanasimba watajitokeza kununua kwa wingi”

Nae Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ametoa taarifa ya kikosi baada ya kumalizika kwa Mechi za kimataifa ambapo wachezaji wao kadhaa walikwenda kushiriki.

“Kikosi kwa sasa kinaendelea na programu ya mazoezi kikijiandaa na mchezo dhidi ya Pamba, leo usiku tutaondoka kwenda Mwanza, na wachezaji wanne waliokuwa Taifa Stars na Camara aliyekuwa timu ya Taifa ya Guinea ameshajiunga na kambi, Steven Mukwala atawasili Dar kesho asubuhi na kuunganisha kuja Mwanza”

Simba watazitumia jezi hizo mpya kwa mara ya kwanza kwenye mechi yao ya Kombe la shirikisho hatua ya makundi dhidi ya FC Bravos itakayochezwa Novemba 27, katika dimba la Benjamin Mkapa.
Share:

News Alert! MUDA WA KUPIGA KURA SAMIA KALAMU AWARDS UMEONGEZWA MPAKA NOVEMBA 25! Kura yako ni Muhimu


 

JINSI YA KUPIGA KURA... Tazama Video hapa au soma maelezo hapo chini .. Gusa Hapa

Zoezi hili linawahusisha wananchi ambao ndio walaji wa maudhui ya habari na ambao watakuwa na nafasi ya kuchangia asilimia 60 ya matokeo. Asilimia 40 ya alama zitakuwa zimetolewa na jopo la majaji kulingana na vigezo vya kitaaluma. 

Huu ni wakati muhimu ambapo wananchi wanapata nafasi ya kutoa maoni yao kwa kupiga kura na kutoa maamuzi ya mwisho.

Nani anapigiwa kura?

Wanahabari na vyombo vya habari vilivyokidhi vigezo vya kitaaluma vya uandishi wa habari za maendeleo ndivyo vitakavyoshiriki katika tuzo hizi. Makala 1,131 zilizowasilishwa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kuwania Tuzo hizi, zimepitia mchakato wa uchambuzi wa kitaaluma na kazi 85 zilizokidhi vigezo zimewekwa kwenye tovuti ya www.samiaawards.tz na kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram (@samiakalamuawards), YouTube, na Facebook (Samia Kalamu Awards).

Mchakato wa Upigaji Kura

  1. Kupiga Kura Kupitia Tovuti

    • Tembelea tovuti ya www.samiaawards.tz
    • Fungua sehemu iliyoandikwa "Piga Kura"
    • Chagua makundi ya Tuzo na namba ya mshiriki kwa kuangalia picha na kazi aliyochapisha
    • Bofya Piga Kura ili kumchagua mshindi unayemtaka.
  2. Kupiga Kura Kupitia Simu ya Kiganjani

    • Nenda kwenye sehemu ya kutuma ujumbe wa kawaida (SMS)
    • Andika neno “Kura”, acha nafasi, kisha weka namba ya mshiriki
    • Tuma ujumbe kwenda namba 15200
    • Utapokea ujumbe wa kuthibitisha kuwa kura yako imepokelewa.

Kaulimbiu ya Tuzo: "Uzalendo Ndio Ujanja"

Tuzo za Samia Kalamu Awards zimegawanywa katika makundi matatu makuu:

  1. Tuzo Maalumu za Kitaifa
  2. Tuzo za Vyombo vya Habari
  3. Tuzo za Kisekta

Lengo kuu la tuzo hizi ni kuhamasisha, kukuza na kupanua wigo wa uandishi wa habari za ndani kupitia vyombo vya habari vya asili na mitandaoni, ili kuchochea maendeleo, uwajibikaji, na kujenga taswira nzuri ya taifa letu.

Tunaomba Ushiriki Wenu!

Karibuni wananchi na wadau wa habari kushiriki kwa wingi katika mchakato huu wa upigaji kura ili kuhakikisha tunapata washindi wanaostahili. 

Kwa maelezo zaidi, tembelea www.samiaawards.tz au wasiliana nasi kupitia namba +255716622200 na 0800008272

Kura Yako Ni Muhimu!
Jiunge na zoezi hili la kihistoria na changia kwenye ujenzi wa taifa letu kupitia uandishi wa habari bora.

Share:

Tuesday, 19 November 2024

RAIS SAMIA AMUAGIZA WAZIRI MKUU KUHARAKISHA UOKOAJI KARIAKOO


Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na ajali ya kuporomoka kwa ghorofa, Kariakoo Mtaa wa Mchikichi na Kongo jijini Dar es Salaam, ambapo amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kushirikiana na timu za uokoaji kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa haraka na ufanisi.

Kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo 'Instagram' na 'WhatsApp channel' Rais Samia ameandika: " Hivi punde nimezungumza kwa kirefu na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge) kuhusiana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, na kazi ya uokoaji inayoendelea. 

Nimempa maelekezo kuhakikisha kazi hii inafanyika kwa haraka na ufanisi, na niendelee kupata taarifa ya kila hatua ya maendeleo yake"

Akionesha masikitiko yake Rais Samia amesema: Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam. 

Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi. 

Wakati hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii.

Share:

Monday, 18 November 2024

WAZIRI MKUU AONGOZA WANANCHI KUAGA MIILI YA WALIOFARIKI KWA AJALI YA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA KARIAKOO


Matukio katika Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu..

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Dar es Salaam kuaga miili ya waliofariki kutokana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la Ghorofa eneo la mtaa wa Congo na Mchikichi kata ya Agrey Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam lililoanguka tarehe 16 Novemba, 2023.













Share:

SERIKALI YATOA ANGALIZO KUHUSU MISAADA YA WAHANGA KARIAKOO


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akizungumza na wanahabari Kariakoo. 


Na Mwandishi WETU, Dar

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia walioathirika na kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam unatolewa kwa akaunti maalum ya maafa ya 9921159801 ambayo ipo Benki Kuu ya Tanzania na kushughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Dkt. Yonazi ameyasema hayo leo Novemba 18, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali inayoendelea katika zoezi la uokoaji.

Amesema akaunti hiyo ni pekee nchini ambayo inakusanya misaada ya kifedha kwa ajili ya maafa.

"Kuna watu wana nia njema kabisa ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii". Amesema Dkt. Yonazi.

Aidha amesema akaunti hiyo ni maalumu imethibitishwa na serikali ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo.

Amesema kwa sasa operesheni inaendelea mpaka pale watakapokamilisha zoezi la kuokoa baadhi ya watu ambao bado hawajaokolewa.











Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger