Friday, 1 November 2024

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI ATEMBELEA UJENZI WA KITUO MAMA CHA GESI ASILIA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa Kituo mama cha Kushindilia na Kujaza gesi asilia kwenye magari (CNG) ambacho kijapatikana Ubungo Jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 01,2024 Ubungo Jijini Dar es salaam Naibu Katibu wizara ya Nishati Dkt.Mataragio amesema,Kituo hicho kinalenga kuhudumia magari yote ambayo yanatumia gesi asilia ambayo ni chanzo Cha nishati safi ukilinganisha na Petroli na dizeli.

Aidha Maragio amesema Kituo hicho kinatarajiwa kutoa huduma kwa wafanyabiashara wadogo ambao nao watawasogezea watu huduma hiyo kwa ukaribu, kwasababu watakuwa na sehemu ya kuchukuliwa nishati hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Biashara ya Gesi na Mafuta,TPDC,Mhandisi Emmanuel Gilbert amesema kituo hicho kitatoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo ambao watahitaji kuwekeza katika biashara ya Gesi kwa ajili ya kujaza kwenye magari.

Amesema kutokana na ukubwa wa kituo hicho kinahimili kuhudumia magari nane kwa wakati mmoja ambapo kwasiku kinaweza kuhudumia magari zaidi ya Elfu moja.

Aidha Mhandisi Gilbert. amesema Gesi itakayo patikana katika kituo hicho itatumika kwa matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya shule,hospitali,pamoja na viwandani.

Aidha amebainisha kuwa hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH)pamoja na kiwanda cha Kairuki tayari wameishaingia makubaliano na TPDC kwa ajili ya kuwapelekea gesi kwa aili ya matumizi yao.

Kituo hicho chakushindilia na kujaza gesi kinatarajiwa kuwa mbadala wa petroli na disel kwani kitatumika kuzalisha nishati ya Gesi kwa ajili ya magari,nishati ya viwandani ambapo katika hospitali ya Muhimbili watatumia nishati hiyo kwa ajili ya kuzalisha mvuke wa kufanyia usafi
Share:

MAANA YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUIFUNGUA NCHI


Tangu aingie madarakani Machi 2021 hadi Agosti 2024, Rais Samia Suluhu Hassan ameufungua  uchumi wa Tanzania kwa dunia na kujenga mazingira bora ya biashara za kimataifa. 

Matokeo ya juhudi hizi yanaonekana wazi katika ukuaji wa biashara yetu kimataifa, kutoka USD 17.4 bilioni (Mauzo nje - $8.4bn, Uingizaji bidhaa - $9bn) hadi kufikia USD 31.4 bilioni (Mauzo nje - $15bn, Uingizaji bidhaa - $16.4bn). Hii ni sawa na ongezeko kubwa la 84%! 📈 

Huku tukishuhudia ongezeko hili la kibiashara, deni la nje limeongezeka kwa asilimia 33%, kutoka $24.4 bilioni hadi $32.6 bilioni, ambalo ni jambo la kawaida kwa nchi zinazopiga hatua za kimaendeleo kupitia uwekezaji wa kimkakati. 

Kwa kufanya hivyo, Rais Samia amefungua milango ya fursa mpya kwa Watanzania na kukuza uchumi kwa kuhakikisha Tanzania inakuwa sehemu ya ushindani wa kibiashara duniani. 

Twende pamoja na Mama kwa maendeleo zaidi!

Chanzo benki kuu ya Tanzania monthly Economic Review May2021 and Monthly Economic Review for October 2024
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 1,2024




Magazeti leo
       
Share:

Thursday, 31 October 2024

WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU WASAKWA, DC ATAKA RIPOTI NOVEMBA5



Na Hamida Kamchalla,  TANGA. 

VIONGOZI wote wa kata, mitaa na vijiji wametakiwa kulinda miundombinu ya aina zote iliyowekwa na serikali kwa matumizi ya wananchi iliyowekwa barabarani na kuufichua mtandao wa wizi ambao inahujumu miundombinu hiyo na kuiuza kwenye vyuma chakavu.

Wito huo umetolewa na Meya wa jiji la Tanga, Abdulrahman Shiloow katika kikao cha baraza la madiwani ambapo alisema sambamba na hilo pia wanapaswa kulinda na kutunza mazingira ya barabara na mifereji.

'Wakati wa zoezi la sensa,, halmashauri hiyo ilitenga kiasi cha shilingi millioni 402 kutoka fedha za mapato ya ndani kuweka vibao vya post code, lakini wametokea watu wasiokuwa wazalendo, wanaondosha nguzo na vile vibao vya alama za mitaa,

"Lakini pia kumekuwa na uharibifu wa barabara za Kitaifa,  pembezoni kuna zile kingo ambazo zina vyuma ndani, watu wanavunja na kwenda kuuza kwenye vyuma chakavu, kwahiyo mkuu wa Wilaya kwa nafasi yako tunaomba vyombo vyako vya ulinzi vitusaidie" amesisitiza.

Hata hivyo amewaomba wananchi kutunza mazingira kwa kulipendezesha jiji kwa kusimamia usafi wa nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na kata zao kwa ujumla lakini pia kwa kila mwenye nyumba afunge taa nje ya nyumba yake kwa ajili ya usalama 

Kufuatia hali hiyo, mkuu wa Wilaya ya Tanga Jafari Kubecha ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama kufuatilia maeneo ambayo vyuma chakavu vinauzwa na kufanya upekuzi wa miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na kuibiwa ili kukomesha mtandao wa wizi wilayani humo. 

"Kupitia kikao hiki nimuagize rasmi mkuu wa Polisi Wilaya, kupita na kupekua maeneo yote ambayo vibao miundombinu ya barabarani imeuzwa kwenye vyuma chakavu, na nipate taarifa hiyo ifikapo Novemba 5 ya maeneo yote ambayo taa za barabarani zimeondolea, tunataka kuuondoa huo mtandao,aamini nitapata taarifa nzuri, wezi wapo na wanafahamika, hivyo ni lazima wadhibitiwe ili kulinda miundombinu yetu" amesema.

Pia amevitaka vyama vya siasa kutumia demokrasia bila kupotosha maana yake na kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutunza amani na utulivu lakini pia kulindiana heshima baina ya vyama pamoja na wagombea wenyewe.

"Isije ikawa tumefungua uchaguzi iwe ndio chanzo cha kuvuruga amani na utulivu tulionao na kuvuruga maendeleo ambayo tumeyapata, kama serikali tunawaomba sana wanasiasa kutusaidia katika hili, kufanya kampeni safi na siyo za kuvunjiana utu na heshima" amesisitiza.

Hata hivyo Kubecha amewataka madiwani hao kutoa ushirikiano katika zoezi la uhamasishaji wananchi kujitokeza kupiga kura ifikapo siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa, kwani ndiyo msingi wa maendeleo. 

"Tusipokuwa na wenyeviti wazuri shida kubwa mnaoipata ni ninyi madiwani katika ufanisi kwakuwa wale ndiyo kiini na kiunganishi baina yenu na wananchi, kwahiyo niombe mshirikiane kwa pamoja katika kuwahamasisha wananchi wachague viongozi bora" amesema.

Kubecha pia amesisitiza kuhusu miradi ya maendeleo viporo ambayo haijakamilika kwa wakati na kuleta kero kwa wananchi hivyo halmashauri inatakiwa kuweka nguvu kuhakikisha miradi hiyo inakamilika japo kwa hatua ili kuwaondolea wananchi kero wanazopata.

"Tunakwenda kwenye uchaguzi, kuna miradi singing bado ni kero kwa wananchi, kwahiyo niombe baraza hili tujipande kuweka kuweka nguvu ya kuhakikisha kwamba tunakwenda kuikamilisha ili tuweze kuwaondolea wananchi kero zilizopo mbele yao"  ameongeza.

Sambamba na hayo, halmashauri hiyo imewakabidhi kompyuta mpakato 27 Maofisa Ustawi wa Jamii kila kata kwa lengo la kuboresha huduma na kufanya kazi zao kielektroniki.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger