Friday, 1 November 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 1,2024




Magazeti leo
       
Share:

Thursday, 31 October 2024

WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU WASAKWA, DC ATAKA RIPOTI NOVEMBA5



Na Hamida Kamchalla,  TANGA. 

VIONGOZI wote wa kata, mitaa na vijiji wametakiwa kulinda miundombinu ya aina zote iliyowekwa na serikali kwa matumizi ya wananchi iliyowekwa barabarani na kuufichua mtandao wa wizi ambao inahujumu miundombinu hiyo na kuiuza kwenye vyuma chakavu.

Wito huo umetolewa na Meya wa jiji la Tanga, Abdulrahman Shiloow katika kikao cha baraza la madiwani ambapo alisema sambamba na hilo pia wanapaswa kulinda na kutunza mazingira ya barabara na mifereji.

'Wakati wa zoezi la sensa,, halmashauri hiyo ilitenga kiasi cha shilingi millioni 402 kutoka fedha za mapato ya ndani kuweka vibao vya post code, lakini wametokea watu wasiokuwa wazalendo, wanaondosha nguzo na vile vibao vya alama za mitaa,

"Lakini pia kumekuwa na uharibifu wa barabara za Kitaifa,  pembezoni kuna zile kingo ambazo zina vyuma ndani, watu wanavunja na kwenda kuuza kwenye vyuma chakavu, kwahiyo mkuu wa Wilaya kwa nafasi yako tunaomba vyombo vyako vya ulinzi vitusaidie" amesisitiza.

Hata hivyo amewaomba wananchi kutunza mazingira kwa kulipendezesha jiji kwa kusimamia usafi wa nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na kata zao kwa ujumla lakini pia kwa kila mwenye nyumba afunge taa nje ya nyumba yake kwa ajili ya usalama 

Kufuatia hali hiyo, mkuu wa Wilaya ya Tanga Jafari Kubecha ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama kufuatilia maeneo ambayo vyuma chakavu vinauzwa na kufanya upekuzi wa miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na kuibiwa ili kukomesha mtandao wa wizi wilayani humo. 

"Kupitia kikao hiki nimuagize rasmi mkuu wa Polisi Wilaya, kupita na kupekua maeneo yote ambayo vibao miundombinu ya barabarani imeuzwa kwenye vyuma chakavu, na nipate taarifa hiyo ifikapo Novemba 5 ya maeneo yote ambayo taa za barabarani zimeondolea, tunataka kuuondoa huo mtandao,aamini nitapata taarifa nzuri, wezi wapo na wanafahamika, hivyo ni lazima wadhibitiwe ili kulinda miundombinu yetu" amesema.

Pia amevitaka vyama vya siasa kutumia demokrasia bila kupotosha maana yake na kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutunza amani na utulivu lakini pia kulindiana heshima baina ya vyama pamoja na wagombea wenyewe.

"Isije ikawa tumefungua uchaguzi iwe ndio chanzo cha kuvuruga amani na utulivu tulionao na kuvuruga maendeleo ambayo tumeyapata, kama serikali tunawaomba sana wanasiasa kutusaidia katika hili, kufanya kampeni safi na siyo za kuvunjiana utu na heshima" amesisitiza.

Hata hivyo Kubecha amewataka madiwani hao kutoa ushirikiano katika zoezi la uhamasishaji wananchi kujitokeza kupiga kura ifikapo siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa, kwani ndiyo msingi wa maendeleo. 

"Tusipokuwa na wenyeviti wazuri shida kubwa mnaoipata ni ninyi madiwani katika ufanisi kwakuwa wale ndiyo kiini na kiunganishi baina yenu na wananchi, kwahiyo niombe mshirikiane kwa pamoja katika kuwahamasisha wananchi wachague viongozi bora" amesema.

Kubecha pia amesisitiza kuhusu miradi ya maendeleo viporo ambayo haijakamilika kwa wakati na kuleta kero kwa wananchi hivyo halmashauri inatakiwa kuweka nguvu kuhakikisha miradi hiyo inakamilika japo kwa hatua ili kuwaondolea wananchi kero wanazopata.

"Tunakwenda kwenye uchaguzi, kuna miradi singing bado ni kero kwa wananchi, kwahiyo niombe baraza hili tujipande kuweka kuweka nguvu ya kuhakikisha kwamba tunakwenda kuikamilisha ili tuweze kuwaondolea wananchi kero zilizopo mbele yao"  ameongeza.

Sambamba na hayo, halmashauri hiyo imewakabidhi kompyuta mpakato 27 Maofisa Ustawi wa Jamii kila kata kwa lengo la kuboresha huduma na kufanya kazi zao kielektroniki.

Share:

TBS YATOA ELIMU YA UDHIBITI UBORA KATIKA MAONESHO YA WIKI YA MWANAKATAVI MPANDA


Afisa udhibiti ubora Kanda ya Magharibi (TBS) Bw. Hassan Hassan, akitoa elimu ya masuala ya udhibiti ubora kwa wananchi na wajasiriamali waliotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya tatu ya Wiki ya Mwanakatavi yanayoendelea katika viwanja vya Azimio Mpanda, Mkoani Katavi.

***************

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya masuala ya udhibiti ubora kwa wananchi na wajasiriamali katika Maonesho ya tatu ya Wiki ya Mwanakatavi yanayoendelea katika viwanja vya Azimio Mpanda Mkoani Katavi.



Share:

Wednesday, 30 October 2024

Wimbo Mpya : JUMA MARCO - MASAMVA

 

Share:

Ngoma Mpya : NELEMI MBASANDO - LEO LEO

 

Share:

RAS KATAVI AIPA HEKO TANROADS KWA MAFUNZO YA WATUMISHI WA MIZANI


Na Mwandishi Wetu,Katavi

Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Albert Msovela amewapongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kuendesha mafunzo ya sheria ya uzito wa magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 kwa watumishi wake wa Kanda ya Magharibi yenye mikoa ya Tabora, Rukwa, Kigoma na wenyeji Katavi.

Msovela amesema kuwa mafunzo haya ambayo pia yatawezweshwa na wakufunzi kutoka Wizara ya Ujenzi, yatawajengea uwezo watumishi hawa na kuwa makini katika utendaji wao wa kazi kutokana na kuwahudumia wasafirishaji wa ndani na nje ya nchi, ambao baadhi yao wanazifahamu vema sheria za uzito wa magari.

“Ninaimani baada ya mafunzo haya watumishi hawa watatoka wanaijua vyema hii sheria, na watatenda sawasawa na sheria hii bila kuipindisha wakijua wazi wanazilinda barabara zetu na uharibifu wa magari yenye kujaza mizigo aidha kwa makusudi au kutokujua,” amesema Msovela.

Hatahivyo, amewataka watumishi hao kuwa wazalendo, waandilifu na waaminifu siku zote wanavyofanya kazi kwenye mizani, itasaidia kupunguza uharibifu wa barabara na matengenezo ya mara kwa mara.

Ameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutumia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinui ya barabara kwa kiwango cha lami, ambapo ssa kila kona ya nchi inafikika vizuri na kwa muda mfupi, tofauti na miaka ya nyuma barabara nyingi ikiwemo ya Katavi ilikuwa mbovu na yenye mashimo mengi, na kusababisha usafiri na usafirishaji kuwa mgumu pia.

Halikalidhalika, amewataka baadhi ya wasafirishaji ambao sio waaminifu kuacha tabia za kuzidisha uzito kwenye magari yao kwa makusudi, bila kujali miundombinu inayojengwa kwa gharama kubwa, kwani ni kosa la kisheria na wataadhibiwa kwa kulipishwa faini, au kifungo au vyote kwa pamoja.

“Sio neno zuri kulitumia wasafirishaji wanatapisha wakishajaza wanajaza aidha mizigo au abiria na wakifika karibu na mizani wanatumia magari madogo na kupunguza mizigo na abiria na baada ya kuoita kwenye mizani wanarudisha kwenye magari na kuendelea.

Kwa upande wake Lawrence Boaz, Afisa Mizani kutoka Kigoma amesema watapata manufaa makubwa kwa kupata mafunzo haya na atakwenda kuwaelimisha wenzake ili waweze kwenda na sheria hii.

Naye Martha Soka, msimamizi wa mizani kituo kwa Kamsisi mkoa wa Katavi, amesema mafunzo haya yamemjengea uwezo kwa kwenda kuelimisha wasafirishaji wanaozidisha mizigo.








Share:

Tuesday, 29 October 2024

RAIS SAMIA AMLILIA MUSUGURI

 


Mkuu wa Majeshi wa zamani Tanzania, Jenerali David Musuguri amefariki Dunia

Mkuu wa Majeshi wa zamani Jenerali David Musuguri, amefariki Dunia, Oktoba 29, 2024, jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu.

Jenerali Musuguri, aliyezaliwa Januari 4, 1920 aliitumikia nchi katika Jeshi kuanzia Mwaka 1942 hadi 1988.

Jenerali Musuguri aliongoza majeshi ya Tanzania katika vita dhidi ya Idi Amin Dada wa Uganda Mwaka 1978, baada ya uvamizi wa eneo la Kyaka, Mkoani Kagera.

Jenerali Musuguri, pia alishiriki katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Battle of Madagascar, Vita vya Kagera, na Battle of Simba Hills


"Kwaheri, Jenerali.

Ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Makamanda, wapiganaji wastaafu, wapiganaji walio katika utumishi, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa kuondokewa na shujaa wetu, mpendwa wetu, mwalimu, mshauri na kiongozi wetu, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Musuguri. 

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha yake ya miaka 104, ambapo miaka 46 kati ya hiyo ameitumikia nchi yetu kwa weledi, umahiri, kujituma, ushujaa, nidhamu na kwa mafanikio ya hali ya juu, akiishi kiapo chake cha kuwa tayari kuutoa uhai wake ajili ya ulinzi wa Taifa letu. Ametuachia mfano bora wa utumishi wa umma utakaoendelea kuwa mwanga ndani na nje ya Majeshi yetu. 

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. 

Amina" _ RAIS SAMIA
Share:

TBS YAWAHIMIZA WAZALISHAJI WA BIDHAA NCHINI KUTHIBITISHA BIDHAA ZAO


Na Mwandishi Wetu, Manyara

WAZALISHAJI wahimizwa kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozalisha ili waweze kuuza bidhaa zao nje ya soko la Afrika Mashariki na pia kunufaika na sera ya Local Content.

Rai hiyo imetolewa Meneja wa TBS Kanda ya Kaskazini, Mhadisi Joseph Ismail, kwenye maonesho yaliyoandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) yanayofanyika mkoani Manyara kuanzia tarehe 20 hadi 30 Oktoba 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Maonesho hayo yenye kauli mbiu isemayo; "Manyara kwa Ustawi wa Biashara na Uwekezaji," Mhandisi Ismail alisema TBS wanaingiaji kwenye uwekezaji kwa sababu wanawezesha uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Aliwataka wazalisha kurasimisha biashara zao, kwani baada ya kupata nembo ya ubora wataweza kuuza bidhaa zao nje ya Afrika Mashariki .

Alitoa mfano akisema Manyara ni mkoa wa kimkakati una hoteli nyingi, lakini haziwezi kununua bidhaa zisizokuwa na nembo ya TBS.

"Kwa hiyo ili uweze kuuza kwenye hoteli hizo ni lazima uthibitishe ubora wa bidhaa zako. Wenye mahoteli kupitia Sera ya Local Content badala ya kwenda kununua bidhaa Arusha watanunua Manyara , lakini hawawezi kununua bidhaa Manyara ambazo hazijathibitishwa ubora wake na TBS," alisema Mhandisi Ismail.

Alisema TBS ni taasisi rafiki ambayo ipo karibu sana na wajasiriamali, ambapo Serikali inatenga fedha kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali.

"Kwa hiyo Serikali kupitia TBS inatoa huduma hiyo ya kuthibitisha ubora wa bidhaa za wajasiriamali pasipo kulipia gharama zozote," alisema na kuongeza;

"Kuthibitisha kuna gharama , lakini Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia TBS inatoa huduma hizo bure, kwa hiyo natoa hamasa kwa wajasiriamali waje TBS waweze kuthibitisha bidhaa zao."

Alisema wakishapata nembo ya ubora itawasaidia kuuza bidhaa zao katika masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi . Aidha, aliwataka wajasiriamali kurasimisha biashara zao ziweze kuwasaidia kupata mikopo kwenye mabenki.
Share:

RAIS SAMIA NI CHAGUO LA MUNGU - ASKOFU SHOO

Askofu Fredrick Shoo wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambaye pia ni mkuu Mstaafu wa KKKT amesema uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ni mpango wa Mungu kuithibitishia Dunia kwamba wanawake wanao uwezo wa kuongoza nchi, kuliko hata wanaume.


Dk. Shoo ameyasema hayo Jumapili Oktoba 27, 2024, wakati wa ibada maalumu ya kuaga watumishi mbalimbali wastaafu, wakiwemo maaskofu, makatibu wakuu, watunza fedha na wasaidizi wao, waliowahi kulitumikia Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, tangu wakati wa Sinodi, mwanzoni mwa miaka ya 1960, hadi wakati huu wa KKKT, Dayosisi ya Kati.

"Ndugu zangu ni dhambi kubwa, kudharau mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii, kwa maendeleo ya Kanisa, hivi sasa kuna mfumo dume ambao umejengwa kwamba wanawake hawawezi, na mfumo huu haupo tu kwa jamii na kwenye siasa, bali upo hata kanisani kuwa wanawake hawawezi, leo nasimama hapa kuzungumza kwa niaba ya wanawake hawa, tuuone mchango wao, na tuwe wa wazo kwamba wanawake wanaweza," amesisitiza Dk. Shoo.


Hivyo, kutokana na hali hiyo, mtaalamu huyo wa masuala ya imani, hasa dini ya Kikristo, ameitaka jamii na Kanisa kwa ujumla, kuzidi kuwaunga mkono wanawake kwenye uongozi, Ili waweze kusimamia maendeleo yanayokusudiwa na jamii husika, pamoja na Serikali yao.


Watanzania wanapaswa kutafakari maneno ya Warumi 13:1: "Kila mtu na atiye mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo imewekwa na Mungu." Kwa mafanikio ya uongozi wake ndani ya muda mfupi, ni dhahiri kuwa Mungu yuko pamoja naye na anamtumia kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.


Aidha juu ya uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa na ule mkuu wa mwakani (2025) Dk. Shoo amewataka Watanzania kijitokeza kushiriki zoezi hilo, na kuwachagua wanawake, pia na wanaume lakini wanyenyekevu, ambao jamii inawaona wana hofu ya Mungu, katika utumishi wao wa kuwaletea maendeleo.

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger