Saturday, 26 October 2024

GCLA YAWATAKA WAUZAJI NA WAAGIZAJI WA RANGI NCHINI KUZINGATIA MAELEKEZO KUDHIBITI SUMU ITOKANAYO NA MADINI YA RISASI


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kupitia kituo chake cha kudhibiti matukio ya sumu, kimewataka  wazalishaji na  waingizaji wa rangi nchini kuhakikisha wanazingatia maelekezo waliyopewa ili kudhibiti sumu itokanayo na madini ya risasi kwa lengo la kuzuia athari .

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 25,2024 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali Daniel Ndiyo kwenye mkutano uliowakutanisha wadau katika tasnia ya rangi ambapo umekusudia kuimarisha ushirikiano katika pande zote kwa dhumuni la kuhakikisha usalama kwa jamii.

"Rangi imekuwa ikitumika kupaka kwenye mabati ambapo watu katika kipindi cha mvua  hutumia maji hayo ikiwa uhakika wa usalama wake kwa matumizi haujulikani". Amesema 

Aidha ametoa rai kwa wadau wanaohusika kwenye tasnia ya rangi,kuondokana na dhana potofu ambayo imezoeleka,kutumia  maziwa pekee kwa ajili ya kudhibiti sumu mwilini kwani inaweza kudhibiti baadhi ya sumu chache pekee  na sio zote  Kama ilivyo zoeleka.

Kwa upande wake mdau Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaalam ya Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu Prof. Amos Mwakigonja amewaagiza watu wanaoshughulika na kazi zinazohusiana na madini ya risasi  kuunga juhudi zinazofanyika kwakuachana na shughuli ambazo zinahusiana na usambazaji wa madini hayo katika mazingira,ambapo itasaidia kuepusha madhara kwa watu.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 26,2024










Share:

Thursday, 24 October 2024

MGOGORO WA UONGOZI NDANI YA CHADEMA KANDA YA KASKAZINI?

Taarifa za hivi karibuni kutoka Chadema zinaonyesha kuwepo kwa mvutano wa madaraka kati ya Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, na Katibu wake, Amani Golugwa. Mgogoro huu umeonekana wazi wakati Mwenyekiti wa kanda alipoitisha mkutano na waandishi wa habari, huku Katibu akitoa taarifa kuhusu kuanza kwa uchaguzi wa ndani wa chama Kanda ya Kaskazini. 

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Oktoba 23, 2024, uongozi wote wa wilaya ya Longido na mkoa wa Arusha umepigwa chini kwa madai ya utovu wa nidhamu na kukiuka maadili ya chama. 

Uamuzi huu ulifanywa baada ya tukio la Oktoba 22, 2024, ambapo viongozi waliodaiwa kushindwa kusimamia uchaguzi wa ndani kwa haki walihusishwa na vitendo vya kihuni.

Kuvunjwa kwa uongozi huu kunadhihirisha mgongano wa kimkakati kati ya uongozi wa kanda chini ya Godbless Lema na maamuzi kutoka ofisi ya Katibu Amani Golugwa. Hali hii inakuja wakati ambapo mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji, na vijiji ukiendelea, na vyama vingine vikiwa katika maandalizi thabiti.




 

Share:

KITIVO CHA UONGOZI WA BIASHARA OUT CHAASWA KUTOA ELIMU YA UJASIRIAMALI


Kitivo cha Uongozi wa Biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimehimizwa kuendelea kutoa elimu ya ujasiriliamali ambayo itasaidia vijana na makundi mbali mbali katika jamii kuweza kujiajiri na kuondokana na dhana ya kusubiri kuajiriwa pale wanapomaliza masomo yao ya chuo kikuu.

Akifungua mdahalo wa kitaaluma katika kuadhimisha miaka 30 ya OUT uliokuwa na mada “Miaka 30 ya Elimu ya Biashara kupitia Mifumo Huria, Masafa na Mtandao: Kuunganisha Kisomo na Uajirikaji”, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Leonard Fweja, ambaye ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo wa Teknolojia za Kujifunzia na Huduma za Mikoa, amepongeza uwepo wa Mdahalo huu kwani ni mojawapo ya fursa ya kujadili na kubadilishana uzoefu, na utatuzi wa changamoto ambazo zinakwamisha utekelezaji wa majukumu fulani katika kitivo.

“Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inabadili mtazamo wake wa elimu kutoka katika elimu ya nadharia kwenda zaidi katika vitendo halisi ili kumwezesha mtu kuweza kufikiri kujiajiri pindi anapomaliza masomo yake. Kwa elimu ya ujasiriamali tunayoitoa itamwezesha mkulima kupata elimu ya usindikaji wa kuchakata mazao yake hivyo atayahifadhi kwa muda mrefu na hii itakuwa ni faida kwa mfanyabiashara huyo na katika sekta nzima ya uwekezaji kwenye taifa letu kwani atatumia maarifa hayo katika kuendesha biashara yake,” amesema Prof. Fweja.

Ameongeza kwa kufafanua “Tuna wahitimu wengi wameweza kutumia hiyo elimu kuweza kuanzisha miradi mbalimbali katika jamii, mfano kuna mmoja ameanzisha miradi mbalimbali katika mkoa wa Njombe, na mwingine ametoka magereza ameweza kuanzisha miradi mbalimbali kule na kuchochea elimu ya ujasiriamali katika kazi zake kwahiyo wanafunzi wetu wengi wamemaliza chuo na kufanya mambo mengi mazuri kwa kujiajiri zaidi kuliko kuajiriwa”.

Prof. Lemayon Melyoki kutoka Shule Kuu ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM) amesema, OUT imeongeza fursa za watu kuweza kupata elimu ya ujasiriamali na imetoa watu wengi sana ambao wameweza kuingia katika jamii kufanya kazi mbalimbali katika serikali pamoja na sekta binafsi. Elimu ya ujasiriamali inasaidia sana vijana kuweza kutafuta namna ya kujiajiri pale wanapohitimu elimu. Hili ni mojawapo ya suluhu kwa serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira nchini.

Naye Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, Dkt. Tumaini Katunzi akiwasilisha mada katika kongamano hilo amehimiza matumizi ya Data Kubwa “BIG DATA” kwa OUT ikiwa kama taasisi inayofundisha na kutoa wakufunzi katika biashara, hii itasaidia katika kufanikisha malengo yake makuu hasa katika data za wanafunzi, data za mitihani na data za kufundishia na kufanya maamuzi sahihi baada ya kupitia mkusanyiko wa data hizo.

Mkuu wa Kitivo cha Uongozi wa Biashara OUT, Dkt. Joseph Magari ameeleza namna OUT inajivunia kutoa wahitimu waliotumia elimu ya ujasiriamali kuweza kufanikisha mambo yanayohusiana na ajira katika maeneo yao wanayofanyia kazi.

“kwa sasa tupo katika mchakato wa kuhuisha mitaala na tunalenga kubadilisha mitaala ili kumfikirisha mtu kujiajiri kuliko kuajiriwa, kwa sasa somo la ujasiriamali tunalo na lipo katika nadharia na vitendo kwahiyo katika mchakato unaoendelea wa kuhuisha mitaala yetu tutaweka kipaumbele katika kuboresha dhana ya kujiajiri kuliko kuajiriwa.

Mdahalo huu ni muendelezo wa matukio ya Maadhimisho ya Miaka 30 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambapo kilele chake kinatarajiwa kuwa katika Mahafali ya 43 ya chuo hiki mkoani Kigoma.
Share:

BARAZA LA NCC LATAKIWA KUWA KIUNGANISHI CHA MENEJIMENTI NA WAFANYAKAZI

 

NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya,akizungumza wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lililofanyika leo Oktoba 23,2024 jijini Dodoma.

Mwakilisha wa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Bw.Mrisho Mrisho,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lililofanyika leo Oktoba 23,2024 jijini Dodoma.

Afisa Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Dkt. Matiko Mturi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lililofanyika leo Oktoba 23,2024 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Dk.Fatma Kassim Mohammed,akielezea lengo la baraza hilo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lililofanyika leo Oktoba 23,2024 jijini Dodoma.
MWAKILISHI wa Mjumbe wa Baraza Kuu Serikalini Bi.Maisha Mbilla,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lililofanyika leo Oktoba 23,2024 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (hayupo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lililofanyika leo Oktoba 23,2024 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (hayupo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lililofanyika leo Oktoba 23,2024 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Baraza la Wafanyakazi la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lililofanyika leo Oktoba 23,2024 jijini Dodoma.


Na Okuly Julius -DODOMA


NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya,amesema Baraza la Wafanyakazi la NCC ni jukwaa muhimu mahala pa kazi linalotumika kama kiunganishi kati ya Menejimenti na Wafanyakazi.

Mhandisi Kasekenya ameyasema hayo leo Oktoba 23,2024 jijini Dodoma wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC).

Amesema kupitia baraza la wafanyakazi na Menejimenti wanapata fursa ya kujadili kwa pamoja masuala ya msingi ya taasisi ikiwemo mipango, Bajeti na masuala mengine ya kiutendaji na kiutawala ili kuweza kufikia malengo na matarajio ya Watumishi wa Taasisi.

“Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu sana mahala pa kazi linalotumika kama kiunganishi kati ya Menejimenti na Wafanyakazi,”amesema

Ameongeza kuwa :”Kupitia Baraza hili, Wafanyakazi na Menejimenti mnapata fursa ya kujadili kwa pamoja masuala ya msingi ya Taasisi ikiwemo mipango, Bajeti na masuala mengine ya kiutendaji na kiutawala ili kuweza kufikia malengo na matarajio ya Watumishi wa Taasisi,”.

Hata hivyo Mhandisi Kasekenya amesema kuwa maeneo ambayo mabalaza yanafanya kazi ipasavyo migogoro kati ya Menejimenti na Watumishi haiwezi kutokea.

Kwa upande wake Mwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya UjenziBw. Mrisho Mrisho amesema baraza la wafanyakazi ni muhimu kwasababu ni kiunganishi muhimu na husaidia kuboresha mahusiano baina ya wafanyakazi mahala pa kazi.

“Balaza la wafanyakazi ni chombo muhimu kwa maslahi ya taasisi na taifa kwa ujumla,”amesema

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la NCC Dk.Fatma Kassim Mohammed ametaja kazi ya baraza hilo kuwa ni kushauri menejimenti na kuimarisha uhusiano mahala pa kazi.

Amesema baraza la wafanyakazi ni muhimu mahala pa kazi kwasababu husaidi kuboresha utendaji kazi wa taasisi wa maslahi ya taifa.

“Baraza la wafanyakazi ni muhimu kwasababu ni kiunganishi muhimu kati ya menejimenti na wafanyakazi na husaidia katika kuimarisha mahusiano ya taasisi na kuleta tija katika utendaji kazi,”amesema
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger