Saturday, 19 October 2024

SHYDC WAFANYA BONANZA LA MICHEZO KUHAMASISHA WANANCHI WAJITOKEZE KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAKAZI

 




Na Marco Maduhu,SHINYANGA
HALMASHAURI ya wilaya ya Shinyanga,imefanya bonanza la michezo, kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi.

Bonanza hilo la michezo limefanyika leo Oktoba 17,2024 katika Stendi ya Mabasi Salawe,ambalo limeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga.
Dk.Kasanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo la michezo, amewasihi wananchi wa wilaya ya Shinyanga, kwamba waendelee kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi, ili wapate fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu.

"Siku za kujiandikisha kwenye daftari la wakazi zimebaki 3 ambalo lilianza Oktoba 11 na litatamatika tarehe 20, na waombeni wananchi mjitokeze kujiandikisha ili mtumie haki yenu ya kikatiba kupiga kura na kuchagua viongozi wazuri watakao waletea maendeleo," amesema Dk.Kalekwa.
Diwani wa Salawe Joseph Buyugu,naye amewasisitiza wananchi kwa wale ambao bado hawajajiandikisha, kwamba wajiandikishe kwani siku siyo rafiki,ili wasije wakashindwa kupiga kura.

Uchaguzi huo wa serikali za mitaa ambao utafanyika Novemba 27 mwaka huu, ni kuchagua wenyeviti wa vijiji,vitongoji,mitaa pamoja na wajumbe.
Katika Bonanza hilo imefanyika michezo mbalimbali ikiwamo ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia na magunia na ngoma za kitamaduni.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga akizungumza kwenye bonanza hilo.
Diwani wa Salawe Joseph Buyugu akizungumza kwenye bonanza hilo.
Wananchi wakiendelea kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wakazi kwenye bonanza hilo.
Michezo mbalimbali ikiendelea kwenye bonanza hilo.
Share:

BIASHARA YANGU IMEPAMBA MOTO BAADA YA KUFANYIWA DAWA HII!

 


Naitwa Steve, baada ya miaka mingi za kukusanya fedha zangu kwenye akiba, niliamua kuingia katika biashara ili kuweza kupata kipato cha kila siku.

Hivyo niliamua kufungua duka la kuuza vipodozi na nilihakikisha duka hilo lina vipodozi vya kutosha kwa wateja wangu ambao wengi wao walikua ni wanawake, inavyojulikana wanawake hutumia asilimia kubwa ya fedha zao kwa kujipodoa. 

Kulikuwa na biashara kama yangu pale lakini nilikua na imani kuwa biashara hiyo ingefanya vizuri, kile nilichotilia maanani katika biashara hiyo ni njia ya kuweza kuvutia na kuwamiliki wateja wangu.

Chuoni nilikuwa nimesomea mambo yanayohusiana na biashara, kwa hivyo nilikua na akili za kutosha.

Baada ya miezi mitatu katika biashara hiyo nilipigwa na butwaa kwa kuwa mauzo yalikuwa chini sana, kwa muda huo ilinibidi kutumia fedha zangu nyingine kulipa kodi ya fremu ya biashara.

Maji yalizidi unga kwa kuwa nilikuwa napata hasara kila uchao, wenzangu waliokuwa na biashara kama yangu walianza kunicheka na kusema sikuwa na akili yoyote ya kufanya biashara.

Mwaka moja baadaye niliweza kumuarifu ndugu yangu yakuwa ninaiacha biashara hiyo na kurejea katika kazi yangu ya kuajiriwa.

Kaka yangu aliniambia nisikate tamaa kwani biashara hiyo itakuja kufanikiwa siku moja, aliweza kunipeleka kwa Dr Bokko, wataalam wa tiba asilia ambao waliweza kunisaidia kuinua biashara yangu.

Nilirejea katika biashara hiyo nikiwa na matumaini kiasi, siku tatu baada ya kukutana na Dr Bokko, biashara yangu ilianza kuchangamka sana, nilianza kumpokea mteja wengi sana.

Ikanibidi niongeze vipodozi katika duka hilo kuweza kumudu idadi kubwa ya wateja wanaokuja dukani.

Kwa sasa biashara yangu inaendelea vizuri sana, pia Dr Bokko wanatibu magonjwa kama kifafa, kifua kikuu na mengine mengi. Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Dr Bokko kwa namba; +255618536050.

Mwisho.


Share:

KAMPENI YA "TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA" , YAZINDULIWA RASMI SHINYANGA ,WADAU WAELEZA NAMNA ITAKAVYO ZUIA UKATILI WA KIJINSIA



Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga leo Oktoba 18, 2024 limezindua kampeni ya "Tuwaambie kabla hawajaharibiwa" yenye lengo la kufikisha ujumbe kwa wanafunzi wote wa Shule za msingi, Sekondari na vyuo vya kati mkoani humo.

Kampeni hiyo imezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude ambaye amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha  ambapo amelipongeza Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha dawati la Jinsia na watoto kwa kubuni na kuzindua kampeni hiyo yenye lengo la kuwajengea uwezo watoto na vijana kuweza kutambua hatari na kuchukua tahadhari ili wasijiunge katika makundi ambayo yanaweza kupelekea kutofikia ndoto zao.

Aidha Mhe. Mkude amewakumbusha wazazi na walezi kuwa mtoto hajawahi kukua kwa mzazi wake hivyo wasichoke kuwafundisha na kuwakemea pale ambapo wanaenda kinyume na maadili ya nchi yetu.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Polisi Jamii mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha amesema kuwa kampeni hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwajengea uelewa watoto pamoja na vijana wa Shule za msingi, Sekondari na vyuo vya kati.
  
  "Napenda kumshukuru Afande Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuruhusu kampeni hii kutekelezwa nchi mzima ambayo kitaifa ilizinduliwa rasmi Agosti 29, 2024 mkoani Njombe hii itasaidia kuwatayarisha vijana wetu ili kujenga Taifa la kizazi chenye maadili mema" alisema ACP - Tesha.

Naye afisa ustawi wa Jamii Halmashauri ya Kishapu ndugu Paul Palaso amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kampeni hiyo ambayo itaokoa jamii kutokana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto,  "tumewahi kuona madhara mengi sana ya ukatili wa kimwili ambao unapelekea vifo na ulemavu wa kudumu kwa watoto wetu pia ukatili unadumaza Taifa hivyo tutumie vyema kampeni hii kuongea na watoto wetu kuwaelimisha na kuwafuatilia kwa ukaribu mienendo yao ili wasije wakaharibiwa.
Msanii Nyumbu Mjanja akiwa nabango lenye ujumbe kwenye maandamano ya uzinduzi wa kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Polisi Jamii mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiwa na mwakilishi wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa Kishapu.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kishapu (OCD) Esther Zephania Gesogwe akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa Kishapu.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiwa na mwakilishi wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa Kishapu.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiwa na mwakilishi wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga akiwa na Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Fraterine Tesha pamoja na OCD Wiliaya ya Kishapu Esther Zephania Gesogwe
Askari Polisi na wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.


Meneja wa Benki ya NMB Tawi wilaya ya Kishapu akiwasalimia wageni wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari polisi pamoja na Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari Polisi na wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari Polisi na wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari Polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari Polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari Polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari Polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Msanii Nyumbu Mjanja akitoa burudani ya wimbo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Msanii Nyumbu Mjanja akitoa burudani ya wimbo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Wadau pamoja na Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari polisi pamoja na Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari polisi pamoja na Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.

Askari polisi pamoja na Wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari polisi pamoja na Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.
Askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.







Mabango mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambiea kabla hawajaharibiwa.








Share:

Friday, 18 October 2024

MPASUKO NDANI YA CHADEMA, IKUNGI., MBINU ZA UPINZANI ZAFICHUKA

 

 SINGIDA-Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameanza kutibuana wenyewe wilayani Ikungi Mkoa wa Singida huku chanzo kikuu kikitajwa kuwa ni siasa za uadui na chuki zinazoenezwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA- Bara, Tundu Lissu.


Kwa nyakati tofauti mwandishi wa habari hizi ameshuhudia mmoja wa wanachama hicho wilayani hapa akizua taharuki ikiashiria wazi kuwa, tayari siasa hizo za chuki zinazoanzia ngazi ya taifa, sasa zimefika mpaka kwa wanachama wa ngazi za chini.

"Lissu amechochea mgawanyiko kila kona anapopita, na kuacha uhasama mkubwa kutokana na ugomvi wake na Mbowe.

"Lissu, ambaye siasa zake zinalenga kulipiza kisasi na kueneza chuki bila kujali maslahi ya Watanzania, amechagua kutumia mgawanyiko kujinufaisha kisiasa,"amedai mmoja wa wanachama wa chama hicho wilayani Ikungi.

"Hapa Ikungi, ameacha machafuko, akiwaacha wana CHADEMA katika hali ya kuchanganyikiwa baada ya kuwasha moto wa fitina. Hii ni kawaida kwa upinzani kueneza chuki na kugawa jamii bila kutoa suluhisho lolote,"ameongeza mwanachama mwingine huku akionesha kukerwa na tabia hiyo.

Wakati Lissu na wenzake wanadaiwa kuzidi kueneza chuki, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan anaendelea kujenga amani na kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

Miongoni mwa wanachama wa chama hicho na mkazi wa Ikungi anasema kuwa, "Uongozi wake (Rais Dkt.Samia) unalenga kutatua migogoro na kujenga mazungumzo ya kidemokrasia, tofauti kabisa na uharibifu unaosababishwa na siasa za Lissu.

"Mbinu hizi za upinzani kuchochea mgawanyiko ni ishara ya wazi kuwa hawako tayari kuongoza jamii pana ya Watanzania. Lengo lao ni kudhoofisha maendeleo ambayo Tanzania imefikia, na Ikungi ni mfano hai wa jinsi siasa zao za chuki na fitina zinavyoweza kuharibu jamii.

"Ni wazi kabisa kwamba ajenda ya upinzani sio kujenga bali ni kubomoa. Ni lazima tuungane na viongozi kama Rais Samia ambaye anafanya kazi usiku na mchana kuwaunganisha na kuwawezesha Watanzania wote,"ameongeza mwanachama hicho.

Hata hivyo, jitihada za kutaka kupata ufafanuzi kuhusu hali hii ya mtifuano kutoka kwa uongozi wa CHADEMA ngazi ya wilaya na Kitaifa inaendelea. Tazama video fupi hapa chini;
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger