Thursday, 17 October 2024

KAWAIDA AMJIBU LEMA, HIZI HAPA SABABU ZILIZOWAFANYA VIONGOZI WA CHADEMA KUTIMKIA CCM

Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida akihutubia wananchi wa Jimbo la Ngara Mkoani Kagera Oktoba 17, 2024.

Na, Mwandishi wetu - Fichuzi Blog.

Kufuatia Kauli za kiongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godless Lema zilizozua taharuki katika mitandao ya kijamii kuwakashfu baadhi ya viongozi na wasimamizi wa uandikishaji daftari la mkazi akilalamikia kutokufuata taratibu rasmi Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida ameonyesha kustaajabishwa na jambo hilo.

Hayo yamejiri leo Oktoba 16, 2024 Wilayani Ngara Mkoani Kagera wakati alipokuwa kwenye ziara ya kawaida ya kukijenga Chama ambapo pamoja na mambo mengine ametolea ufafanuzi wa mada hiyo na kwamba haina uhalisia bali analenga kuvuruga uchaguzi kwa kupotosha umma.

"Leo Asubuhi wakati naangalia mitandaobya kijamii nikamuona kiongozi mmoja wa upinzani Godless Lema akilalamika na kuaminisha umma eti Kuna mambo ya ovyo yanafanyika, kuwa wakurugenzi wa uchaguzi na mawakala wanaosajili watubkwenye madaftari ya makazi kwamba wanawasajili wanafunzi wa shule katika lile Daftari". Amesema Kawaida

“Tunalaani kitendo hichi, wanataka tuwapore watu haki zao za msingi?, tunawataka waendelee kusajili muhimu wawe wametimiza umri wa kupiga kura hata kama bado anasoma, wangetumia muda mwingi wa malalamiko kuwahamasisha watu waende kujiandikisha na waweze kupigiwa kura” Kawaida.

Ikumbukwe kuwa kauli hiyo imekuja mara baada ya Godbless Lema kudai kuwa baadhi ya vituo vya uandikishaji havifanyi kazi kwa uadilifu na kwamba baadhi ya maafisa wa uandikishaji wanakwepa taratibu rasmi hivyo haridhishwi na mwenendo wa zoezi hilo linaloendelea Nchini.

Aidha katika Mkutano huo Kawaida akiambatana na viongozi wengine wamepokea wanachama wapya waliokuwa viongozi watatu kutoka Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA na kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM huku chanzo wakieleza ni kuridhishwa na maendeleo wanayoyapata nchini yatokanayo na Utekelezaji wa Ilani ya Chama tawala CCM.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida amempongeza Mbunge wa jimbo hilo kwa jitihada anazozifanya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kuanzia ngazi ya jamii ikiwa ni pamoja na kuwainua kiuchumi.

Mamia ya Wananchi wakifurahia jambo katika Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Sehemu ya wananchi walioshiriki katika Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro akihutubia mamia ya wananchi walioshiriki kwenye Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Wananchi wakifurahia jambo katika Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Picha za Matukio Mbalimbali wakati wa Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Picha ya pamoja: Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida, Viongozi wa Chama, Mbunge wa Jimbo La Ngara Ndaisaba Ruhoro katika picha ya pamoja na wanachama wapya waliokuwa Viongozi wa CHADEMA ambao wamekaribishwa rasmi kwasasa ni wanachama wa CCM  Oktoba 17, 2024  Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida akimkaribisha mwanachama mpya kutoka CHADEMA Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Share:

Tuesday, 15 October 2024

WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA KUJIUNGA NA VETA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewahamasisha vijana kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vya VETA, ili waweze kuajiriwa au kujiajiri kwa urahisi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo juzi, tarehe 11 Oktoba 2024 alipokuwa akizindua Wiki ya Vijana Kitaifa katika uwanja wa Furahisha, jijini Mwanza.

Amesema Serikali imewekeza nguvu kubwa kwa vijana kupitia ujenzi wa vyuo vya VETA ambapo vyuo vipya 25 vimekamilika na vingine 65 vinajengwa katika kila wilaya na kwamba jukumu lililobaki ni la vijana kujiunga na mafunzo katika vyuo hivyo ili kujipatia ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri.

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas P. Katambi (MB) ameipongeza VETA kwa juhudi za kusaidia kukuza na kuendeleza ubunifu wa vijana.

Katambi ameyasema hayo alipotembelea banda la VETA kwenye maonesho hayo, tarehe 10 Oktoba 2024 na kujionea ubunifu mbalimbali wa wahitimu kutoka vyuo vya VETA nchini.

Kipekee, Mhe. Katambi amevutiwa zaidi na ubunifu wa mhitimu wa chuo cha VETA Mwanza, Benjamin Samweli ambaye ametengeneza gari linalotumia injini ya pikipiki lenye uwezo wa kubeba nusu tani, kutembea Kilometa 80 kwa saa, kutumia lita moja kwa Kilometa zaidi ya 20.

“Serikali katika Sera yake ya maendeleo ya vijana imeongelea kuwezesha vijana wenye uwezo na vipaji kuhusiana na ubunifu na uvumbuzi. VETA fuatilieni COSTECH kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kumsaidia mhitimu huyu kukuza na kuendeleza kipaji chake kwa kupatiwa mkopo nafuu ili aweze kuendeleza kipaji chake,” amesema.

Aidha ametoa wito kwa vijana kujiunga na Mafunzo na Elimu ya Ufundi Stadi ili kukuza uchumi wao kupitia ajira rasmi na zisizo rasmi.
Share:

SERIKALI KUANZA MAHOJIANO RASMI NA WAKIMBIZI

Serikali ya Tanzania inatarajia kuanza mahojiano ya kina na wakimbizi wa Burundi wanaoishi nchini ifikapo 2025. Mahojiano haya yatashirikisha wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR). Lengo kuu ni kubaini changamoto wanazokabiliana nazo wakimbizi na kutafuta suluhisho la kudumu kulingana na maoni yatakayokusanywa katika mahojiano.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo, alipowasilisha ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 75 wa Kamati Tendaji ya UNHCR nchini Uswisi, tarehe 15 Oktoba 2024.

Mhe. Sillo alibainisha kwamba Tanzania inahifadhi wakimbizi zaidi ya 240,000, wengi wao wakiwa kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alisema serikali imefanikiwa kutafuta suluhisho la kudumu kwa wakimbizi 17,283 kwa mwaka huu, ambapo wakimbizi 12,717 walirudi kwa hiari katika nchi zao za asili, na 4,566 walipatiwa makazi mapya katika mataifa mengine.
Aidha Mhe. Sillo katika Ujumbe wake alieleza kuwa licha ya Mafanikio hayo, Operesheni za Kuhudumia Wakimbizi nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa za kifedha, hasa katika sekta za afya na elimu katika kutoa huduma bora kwa Wakimbizi

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake katika kuhifadhi wakimbizi kwa miaka mingi na sasa kujikitika katika kutafuta suluhisho la kudumu kwa Wakimbizi hao. Aidha alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuungana ili kusaidia wahanga wa migogoro na kuhakikisha wanapata misaada inayohitajika.

Share:

MKATABA WA BILIONI 13.5 WASAINIWA KWA UJENZI WA JENGO LA TIA SINGIDA

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo (kulia) pamoja na Mwakilishi wa Salem Construction, Charles Casmir (kushoto) wakionesha mkataba waliosaini kwaajili ya ujenzi wa jengo la TIA kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.

************************

TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA), imesaini mkataba na kampuni ya Salem Construction kwaajili ujenzi wa jengo la kampasi yake mkoani Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5.

Mkataba huo utachukua miezi 24 hadi kukamilika kwa ujenzi jengo hilo mkoani Singida.

Akizungumza leo Oktoba 15,2024 katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo amesema fedha za ujenzi wa kampasi hiyo zimetolewa chini ya Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kwa Vyuo Vikuu nchini (HEET) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).

Aidha amemtaka mkandarasi kuhakikisha anajenga jengo lenye ubora na kufanyakazi kwa karibu na wananchi wa Singida ili wawe walinzi wa mradi huo mpaka utakapokamilika kwa muda ambao umewekwa.

“Tumemtaka mkandarasi azingatie kanuni za ujenzi ili kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa salama wakati wote tunataka mpaka mradi unapokamilika watu wawe salama kusitokee kifo hata kimoja wala majeruhi,” amesema Prof. Pallangyo.

Amesema watajitahidi kufanyakazi kwa karibu na benki ya dunia ambayo ndiyo inayofadhili mradi huo kuhakikisha kila mkandarasi anapoomba malipo analipwa kwa wakati ili mradi usisimame.

Kwa upande wake Mratibu wa HEET Kitaifa, Dkt. Kenedy Hossea, ameipongeza TIA na menejimenti yake kwa kupata mkandarasi mapema kwaajili ya ujenzi wa jengo katika Kampasi ya Singida

“Nawapongeza Mtendaji Mkuu wa TIA kwasababu kuna watu walianza muda mrefu hawajapata mkandarasi mpaka sasa wanalumbana tu zabuni inatangazwa inafutwa wanashindwa kufikia muafaka,” amesema

Pamoja na hayo, Dkt. Hossea amemtaka mkandarasi wa jengo hilo kuzingatia ubora na kuahidi kuwa wataalamu wanaosimamia mradi huo kutoka wizarani watakuwa wakipita mara kwa mara kuhakikisha ubora unazingatiwa.

Nae Mwakilishi wa Salem Construction, Charles Casmir, amesema mkataba huo ni wa miezi 24 lakini kwa namna walivyojipanga watakamilisha mradi huo ndani ya miezi 18.

Amesema wanatarajia kuwa jengo hilo litakuwa la mfano na kwamba watahakikisha wanazingatia usalama wa wafanyakazi na jamii inayozunguka mradi huo katika Mkoa wa Singida.

Mratibu wa mradi wa huo TIA , Oyombe Simba, aliishukuru serikali kwa kukubali fedha hizo kupelekwa kwenye taasisi hiyo kwaajili ya kuboresha mazingira ya wanafunzi kujisomea.

Amesema TIA imepokea jumla ya shilingi bilioni 27.6 ambazo zinakwenda kuboresha kampasi za taasisi hiyo ambapo mbali na ujenzi wa jengo la Singida pia watajenga majengo kwenye kampasi ya Mwanza.

Hata hivyo amesema jengo la bweni litakalojengwa Mwanza litagharimu shilingi bilioni 7.2 na litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 306 kwa wakati mmoja.

“Mbali na ujenzi wa majengo mradi huu umelenga kuboresha mitaala na kuwajengea uwezo wakufunzi kwenye taasisi yetu kwa hiyo tunapoanza kutekeleza mradi huu ni fahari kubwa sana kwetu,” amesema
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo (kulia) pamoja na Mwakilishi wa Salem Construction, Charles Casmir (kushoto) wakisaini mkataba wa ujenzi wa jengo la TIA kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo (kulia) pamoja na Mwakilishi wa Salem Construction, Charles Casmir (kushoto) wakisaini mkataba wa ujenzi wa jengo la TIA kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo (kulia) pamoja na Mwakilishi wa Salem Construction, Charles Casmir (kushoto) wakisaini mkataba wa ujenzi wa jengo la TIA kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo (kulia) pamoja na Mwakilishi wa Salem Construction, Charles Casmir (kushoto) wakionesha mkataba waliosaini kwaajili ya ujenzi wa jengo la TIA kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo (kulia) pamoja na Mwakilishi wa Salem Construction, Charles Casmir (kushoto) wakipongezana huku wakionesha mkataba waliosaini kwaajili ya ujenzi wa jengo la TIA kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa HEET Kitaifa, Dkt. Kenedy Hossea akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa jengo la TIA kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo- Taaluma, Utafiti na Ushauri wa kitaalamu TIA, Dkt. Momole Kasambala akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa jengo la TIA kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakiwa katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa  jengo la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo, Mratibu wa HEET Kitaifa, Dkt. Kenedy Hossea, Mratibu wa mradi wa HEET katika taasisi ya (TIA), Oyombe Simba pamoja na wadau wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa  jengo la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kampasi ya Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 15,2024 kwenye Ofisi za TIA Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger