Tuesday, 8 October 2024

DAWASA YAGONGA HODI KWA WANANCHI KINONDONI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Wiki ya huduma kwa mteja ikiwa inaendelea, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetembelea wateja wake katika maeneo ya Msasani, Masaki, Mwananyamala wilayani Kinondoni kwa lengo la kubadilishana nao mawazo juu ya uboreshaji huduma za maji.


Akizungumza na wateja mbalimbali, Meneja wa DAWASA Kinondoni, Ndugu Tumain Muhondwa ameahidi kuendeleza mashirikiano mazuri yaliyopo baina ya Mamlaka na wateja ili kuhakikisha huduma bora inawafikia wote kwa wakati.

"Leo tumetembelea wateja mbalimbali ambao ni Slipway Hotel, Seacliff Hotel, Ada estate na Ubalozi wa Marekani na pia wateja wa kawaida katika kata ya Mwananyamala na Kinondoni. Tumeahidi kuboresha huduma ya maji katika maeneo yao," ameeleza ndugu Muhondwa.

Muhondwa ameongeza kuwa Mamlaka imejipanga kuongeza maunganisho ya huduma ya maji na kufikia asilimia 95 ya upatikanaji wa huduma ifikapo mwaka 2025.

"Tumeadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kutembelea wateja wakubwa na wadogo, tunafahamu kuna maeneo ambayo huduma haijafika, nipende kuwahakikishia wananchi kuwa Mamlaka inafanya kazi kubwa kusogeza huduma maeneo yote kwa kuongeza vyanzo vya maji na kufanya miradi ili kila mwananchi apate huduma ya maji," ameeleza ndugu Muhondwa.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mwananyamala na Meya wa manispaa Wilaya ya Kinondoni, ndugu Songoro Mnyonge ameishukuru DAWASA kwa huduma bora zinazotolewa na kuahidi ushirikiano wa kutosha kwa Mamlaka ili huduma izidi kuimarika.

"Nikiri kwamba DAWASA wanatoa huduma hapa kwetu, huduma ya maji tunaipata kama inavyostahiki na imechangia utulivu mkubwa kwa wananchi, tutaendelea kutoa ushirikiano kwao ili huduma iwe bora na endelevu," ameeleza ndugu Mnyonge.

Josephine Wange mkazi wa Kinondoni ameishukuru DAWASA kwa kuwafikia katika wiki ya huduma kwa mteja na kueleza kuridhishwa na huduma.

Wiki ya huduma kwa wateja inaakisi usimamizi bora na wa viwango wa huduma zitolewazo na Mamlaka kwa wateja na kaulimbiu ya mwaka huu inasema "Ni zaidi ya Matarajio."
Share:

DAWASA YANOGESHA WIKI YA HUDUMA KISARAWE

 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imeanza kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja katika Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kisarawe kwa zoezi la kutembelea wateja mtaa kwa mtaa katika Kata ya Kisarawe hususan maeneo ya Bomani na Matumbini.


Zoezi hilo la kutembelea wateja Mtaa kwa Mtaa limelenga kuwafikia wateja kwenye maeneo yao na kuwahudumia kwa kusikiliza changamoto walizonazo na kuzitatua.

Maadhisho ya wiki ya huduma kwa wateja hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 7 hadi 11 Oktoba ambapo mwaka huu kauli mbiu inasema "Ni Zaidi ya Matarajio".
Share:

NSSF KUFIKISHA HUDUMA KWA WATEJA KIDIJITALI ZAIDI



*Mkurugenzi Mkuu asema kila mwanachama atafungua madai ‘online’

*Aahidi kuifikia sekta isiyo rasmi ili Watanzania wengi waweze kunufaika na huduma za NSSF 

Na MWANDISHI WETU
MBEYA. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) amesema Mfuko unaendelea kuboresha na kutoa huduma bora kwa wateja kwa kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA, ambapo kwa sasa wanachama wanaweza kufungua madai kidijitali ‘online’ bila ya kulazimika kufika katika Ofisi za NSSF.

Amesema hatua hiyo ni njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuwaondolea kero wananchi, ambapo kwa upande wa NSSF wanachama wanapata taarifa zao mbalimbali huko huko waliko jambo ambalo linawaondolea usumbufu wa kufuata huduma umbali mrefu.  

Bw. Mshomba amesema hayo tarehe 7 Oktoba 2024 jijini Mbeya wakati akifungua Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyobeba kauli mbiu isemayo ‘Huduma Bora Popote Ulipo’.

Aidha, amesema NSSF inaendelea kufikisha elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi ambayo imebeba kundi kubwa la Watanzania kama wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wa madini na wajasiriamali wengine ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha bora ya sasa na ya baadaye.

Bw. Mshomba amewahakikishia wateja kuwa NSSF iko imara na endelevu katika kutoa huduma za hifadhi ya jamii hususan kupitia majukumu ya msingi ambayo ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao. Hivi sasa thamani ya Mfuko imefikia trilioni 8.5.

“Natumia fursa hii kuwashukuru wateja, watumishi wenzangu, Bodi ya Wadhamini, Benki Kuu ya Tanzania, Ofisi ya Waziri Mkuu hawa wote wamekuwa wadau muhimu katika kufanikisha utoaji wa huduma zetu,” amesema Bw. Mshomba.

Amesema mafanikio makubwa ambayo NSSF imeyapata yamechangiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye katika uongozi wake amefungua nchi na kumekuwa na ongezeko kubwa la waajiri kutokana na mazingira mazuri aliyoweka.
Naye, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bw. Omary Mziya, amesema wanaendelea kuboresha huduma za wateja siku hadi siku kwa kuwa umuhimu wa wateja ni mkubwa na ndio sababu za kuwepo kwa NSSF.

Amesema wanachama wachangiaji wa NSSF wameongezeka kutoka 1,189,000 mwezi Juni 2023 na kufikia 1,342,654 mwezi Juni 2024. Idadi ya wanufaika wa Pensheni nao wameongezeka ambapo mpaka kufikia mwezi Juni 2024 wamefikia wastaafu 31,914.

Bw. Mziya amesema wanufaika wa mafao mengine wakiwemo wa Matibabu wamefikia 207,229 mpaka kufikia Juni 2024 na kuwa idadi ya waajiri imeongezeka na kufikia 41,616.

Amesema wanufaika wa Mafao ya Uzazi mpaka kufikia Juni 2024 walikuwa 10,809, wanufaika wa Mafao ya Kupoteza Ajira mpaka kufikia Juni 2024 walikuwa ni 109,286. “Hivyo utaona idadi ya wateja wetu imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na sisi kipaumbele chetu ni kuendelea kutoa huduma bora na kuongeza idadi ya wanachama wengi zaidi,” amesema Bw. Mziya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Ekwabi Mujungu ameahidi kuwa wafanyakazi wataendelea kusikiliza wateja, kutoa huduma za kipekee, kuwasiliana kwa uwazi, kujitolea kwa wateja kwa maana ya kuvaa viatu vyao, kujifunza na kuboresha huduma kila siku, lengo ni kupunguza malalamiko.

Naye Robert Kadege, Meneja wa Huduma kwa Wateja, amesema Wiki ya Huduma kwa Wateja ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1987 kwa lengo la kutambua umuhimu wa huduma bora kwa wateja pamoja na wafanyakazi wanaotoa huduma bora kwa wanachama.

Amesema NSSF inatumia wiki hii kwa ajili ya kukumbushana umuhimu wa huduma bora kwa wateja na kuwashukuru kwa namna ambavyo wanaunga mkono juhudi mbalimbali za NSSF ambapo kwa sasa imejikita katika kuboresha huduma zake kupitia mifumo ya kidijitali.

Awali, Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya, Bw. Deus Jandwa amewahakikishia wateja kuwa wanaendelea kutoa huduma bora za hifadhi ya jamii, kutatua kero mbalimbali pamoja na kufikisha elimu ya hifadhi kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.












 
Share:

Monday, 7 October 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 7,2024


Share:

NSSF YATUMIA FURSA YA MAONESHO YA MADINI GEITA KUTOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII


Na MWANDISHI WETU GEITA.

Maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini yamefunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambapo Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unatumia Maonesho hayo kuendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ikiwemo Sekta ya Madini.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa maonesho hayo, Mhe. Dkt. Biteko amesema maonesho yametoa fursa ya wananchi kupata elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Aidha, amewataka wafanyabiashara wa madini kutumia mazingira rafiki yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha mazingira ya uwekezaji ili wafanye biashara zao kwa uhuru na kukuza uchumi.

Naye, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema mchango wa sekta ya madini unaendelea kukua siku hadi siku na kuwa wanatarajia hadi kufikia mwakani, sekta ya madini iwe inachangia katika pato la Taifa kwa asilimia kumi.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela amesema maonesho ya mwaka huu yameshirikisha zaidi ya washiriki 800 na yamechangia mafanikio ya mkoa huo.


Awali, akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mkuu, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Bi. Lulu Mengele amesema NSSF inashiriki maonesho hayo kwa malengo ambapo katika mwaka wa fedha 2023/24, Mfuko kupitia Ofisi ya Mkoa wa Geita iliweza kukusanya shilingi bilioni 64 na kuwa asilimia 80 ya fedha hizo zilikusanywa kwenye makampuni mbalimbali ya madini.

Bi. Mengele amesema sekta ya madini ni wadau muhimu wa NSSF wakiwemo wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa ambao wote ni wanachama wa Mfuko na kuwa wamekuwa wakikusanya kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwenye sekta ya madini.

Aidha, amesema NSSF imeendelea kuboresha huduma kupitia mifumo ya TEHAMA, ambapo kwa sasa wanachama wa NSSF wanaweza kufungua madai yao kidijitali huko huko waliko lengo ni kuondoa kero za wanachama na kusogeza huduma hukohuko waliko. Pia waajiri wanalipia michango ya wanachama wao wakiwa Ofisini bila ya kufika katika ofisi za NSSF.


Bi. Lulu amesema kupitia mifumo imechagiza mafanikio ya NSSF ambapo thamani imekua na kufikia trilioni 8.6. "Tunakushukuru sana mgeni rasmi hii ni kazi kubwa ya nyie viongozi mnayoifanya kutuongoza," amesema Bi.Lulu Mengele

Share:

MERIDIANBET PROMO CODE |PROMO CODE YA MERIDIANBET TANZANIA

 

Promo code Ni msimbo maalumu wa kujisajili na meridianbet ambapo utatakiwa kujaza namba 1109 Kama promo code yako wakati wakujisajili na Meridianbet Tanzania.

Historia ya meridianbet

Meridianbet Ni kampuni ya kubashiri nchini Tanzania iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria   iliyosajiliwa mwaka 2017 kwa Mujibu wa Wikipedia (https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Meridian_Bet_Tanzania)

Tangu wakati huo imekuwa na mafanikio makubwa katika tasnia ya michezo ya bahati nasibu Tanzania.

YALIYOMO

1. JINSI YA KUJISAJILI MERIDIANBET

2. PROMO CODE YA MERIDIANBET (MERIDIANBET PROMO CODE)

3. MICHEZO INAYOPATIKANA MERIDIANBET

4. HITIMISHO


JINSI YA KUJISAJILI MERIDIANBET TANZANIA 

Hapa tutaeleza Hatua kwa Hatua jinsi ya kuweza kufungua account yako ya meridianbet mtandaoni

a) Tembelea tovuti ya meridianbet tz au Bofya >HAPA> https://a.meridianbet.co.tz/c/AertQt


b) Jaza namba yako ya simu bila kuanza na 0

c) Tengeneza password yako yenye mchanganyiko wa namba na neno

d) Jaza Tena password yako Kama ulivyojaza hapo juu

e) Bonyeza kiduara kilichoandikwa promo code na ujaze namba hizi 1109 Kama promo code ya Pmbet

f) Kubali vigezo na masharti kwa kubofya kiduara cha terms and conditions

g) jisajili, utapokea ujumbe kwenye simu yako kwenye namba uliyojaza, deposit na uendele kufurahia huduma


MERIDIANBET PROMO CODE (PROMO CODE YA MERIDIANBET)

Kama tulivyokwisha kuona hapo juu kuwa promo code ni msimbo maalumu ambao hutumika wakati wa kujisajili au kufungua account . Namba hiyo ni 1109 , mteja hutakiwa kujaza kwa usahihi code hiyo ili kupokea bonasi pale atakapoweka pesa kwa Mara ya kwanza kulingana na promosheni zilizopo.


MICHEZO INAYOPATIKANA MERIDIANBET

Kampuni ya kubashiri ya meridianbet inazo huduma mbalimbali kwa wateja wake ikiwemo kubashiri mpira wa miguu, michezo ya casino na slots za mitandaoni, michezo ya virtual, tennis, boxing, aviator miongoni mwa michezo mingine. Aidha kampuni ya kubashiri ya meridianbet hutoa huduma nzuri kwa wateja 24/7, malipo ya haraka, odds nzuri , na masoko mengi.


HITIMISHO

Je una changamoto yoyote na ungependa kuwasiliana na meridianbet? Unaweza kuwasiliana na meridianbet kupitia njia ya simu ya mkononi pamoja na barua pepe kama ifuatavyo, simu namba 0768988200

Barua pepe, info@meridianbet.co.tz

Beti kistaarabu

Soma zaidi https://www.mashelle.co.tz

Share:

BONANZA LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WILAYANI MKALAMA LAFANA

 

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewataka wananachi wilayani Mkalama kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Mpiga Kura ili wawe na sifa za kuchagua viongozi katika Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa utakaofanyika tarehe 27/11/2024.


Wito huo ameutoa tarehe 6/10/2024 wakati wa Bonanza la Hamasa ya Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa lililofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Nduguti inayopatikana katika kata ya Nduguti wilayani Mkalama.

“Ili uweze kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 unapaswa kuwa umejiandikisha katika Daftari la orodha ya Wapiga Kura. Hivyo wenye Umri kuanzia miaka 18, nawasihii mjitokeze kujiandikisha ili muwe na sifa ya kuchagua viongozi mnaowataka” Mhe. Machali amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amesema kuwa zoezi la uandikishaji Orodha ya Wapiga Kura litaanza tarehe 11-20, Oktoba 2024 na zoezi hilo litachukua muda wa siku 10 hivyo wananchi watumie fursa hiyo kujitokeza kwa wingi “Kama unataka kumchagua kiongozi umpendae hakikisha unajiandikisha”, amesema Mhe. Machali.

Kwa upande wake, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Wilaya, Mohamed Atiki ametoa rai kwa vijana na wanawake  wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

“Vijana wenye umri kuanzia miaka 21 na kuendelea, pamoja na kina mama nawasihi mjitokeze kwa wingi mgombee nafasi za uongozi ili kwa pamoja muwe sehemu ya mabadiliko katika jamii zetu lakini pia wananchi wenye sifa wakati wenu ni huu wa kuchagua viongozi mnaowataka” amesema Atiki.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger