Saturday, 17 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 17,2024













Share:

Friday, 16 August 2024

KANISA KATOLIKI LATOA MUONGOZO IBADA NA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MISA YA MAZIKO


Kanisa Katoliki la Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Makongo Juu Jimbo Kuu la Dar es Salaam.


DAR ES SALAAM – Kanisa Katoliki Tanzania limetoa muongozo mpya kuhusu shughuli za ki imani zikihusisha utaratibu wa ibada na salamu za rambirambi katika misa ya miziko.

Taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Liturujia Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Stefano Kaombe likirejea kikao kilichoongozwa na Askofu Mkuu Jude Thadeus Ruwa’ichi imesema utaratibu wa salamu hizo kwa sasa utahusu wawakilishi watano pekee.

Wawakilishi hao ni mmoja kutoka parokia, Jumuiya, Chama chake cha Kitume, Ajira na Kiongozi wa jamii (mtendaji, diwani).

Pd. Kaombe amesema katika mkutano wa Waklero wote uliofanyika Juni 25, 2024, katika Kituo cha Msimbazi, mkutano ulielekeza kuwa kabla ya komunyo katika tukio la msiba maelekezo yatolewe kwa kuzingatia kuwa wanajumuika waamini wa madhehebu na imani mbali mbali.

“Sasa tunaingia hatua ya kupokea Ekaristi Takatifu. Hili ni tendo la pekee la kiimani. Wanaalikwa kushiriki Wakristo Wakatoliki waliojiandaa kiroho ipasavyo,” ilisema taarifa ya Pd. Kaombe.

Amefafanua kuwa salamu za rambirambi katika Misa ya maziko zitolewe na wawakilishi tu zikifuatiwa na neno la shukrani toka katika familia.

“Rambirambi zingine zaweza kutolewa nyumbani na makaburini baada ya ibada,” imesema taarifa hiyo.

Vile vile Kanisa limesema Ibada ya marehemu katika Misa ina sehemu nne: nyumbani, mlangoni, Misa inaendelea bila ibada ya toba, sala ya buriani. Misa inahitimishwa bila baraka kanisani, kwani makaburini kuna maziko na Baraka ya mwisho.

Kuhusu jeneza, taarifa hiyo imesema litengenezwe kwa namna nzuri, liweze kufunuliwa kutoka kushoto kuelekea kulia kwa marehemu, kama kuna sababu za msingi si lazima kufungua jeneza wakati wa sala ya buriani.

Aidha wakati wa kunyunyizia maji ya Baraka na kufukiza ubani, ni kipindi cha ukimya na maombolezi ya moyoni, hakuna sala ya hadhara katika maombezi kwa marehemu wetu.

Chanzo - Habarileo 


Share:

Thursday, 15 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 16, 2024






Share:

DK. BITEKO ASHIRIKI KIKAO CHA MAWAZIRI WA NISHATI NCHINI UGANDA




Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto BIteko leo tarehe 15 Agosti, 2024 ameshiriki kikao cha 19 cha pamoja cha Mawaziri wa Nishati ambao ni Wanachama wa Umoja wa soko la pamoja la kuuziana umeme na kuimarisha mifumo ya Gridi ya EAPP (Eastern Africa Power Pool) unaofanyika nchini Uganda.

Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo kupitisha mabadiliko ya mikataba ya uongozi wa EAPP, kuridhia kanuni za uanzishwaji wa kitengo kinachojitegemea cha kusimamia soko la biashara ya umeme kwa nchi wanachama (Marketing and Trading unit) na kuridhia kanuni na taratibu za uendeshaji wa vikao vya Baraza la Mawaziri, Makatibu wakuu, na kamati ya uongozi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (TANESCO) Mha. Gissima Nyamo-Hanga, Naibu Mkurugenzi Mipango, utafiti na uwekezaji CPA Renatha Ndege, na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na taasisi zake.
Share:

Video Mpya : KUSEKWA LUKUBHA - BHUHABE

 

Share:

WATENDAJI VILABU VYA LIGI KUU WANUFAIKA NA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII KUTOKA NSSF

 


*Karia avitaka vilabu vyote ligi kuu kuchangamkia fursa ya kujiwekea akiba

*NSSF waeleza namna  watakavyonufaika kupata mafao, matibabu

Na MWANDISHI WETU,
Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Wallace Karia amevitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara kuwaandikisha wachezaji, makocha na wafanyakazi wao katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili waweze kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa na Mfuko huo ikiwemo matibabu.

Bw. Karia amesema hayo tarehe 14 Agosti 2024 wakati akifungua semina kwa watendaji wakuu wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu, ambayo imeandaliwa na TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPBL) pamoja na NSSF, iliyofanyika katika ukumbi wa Mafao House Ilala, Dar es Salaam.

Amesema zipo faida nyingi za wachezaji na wadau wengine wa mpira kujiunga na kuchangia NSSF ikiwemo kupata mafao pamoja na huduma za matibabu na wategemezi wao na kuwa jambo hilo litawasaidia kipindi ambacho hawana nguvu za kucheza mpira.

Bw. Karia amevitaka vilabu vyote kuchangamkia fursa hiyo yenye manufaa kwa wachezaji, na kuwa vielekeze nguvu zaidi ya kuandikisha NSSF wachezaji vijana walio chini ya umri wa miaka 20 ili wanapostaafu mpira wanufaike na pensheni ya uzeeni inayotolewa na NSSF.

“Tunawashukuru wenzetu wa NSSF kwa kuja na jambo hili kwetu sisi litatuepusha na zile lawama tulizokuwa tunatupiwa ambazo hazituhusu za wachezaji wa zamani kuishi maisha magumu kwa kukosa kukidhi gharama za matibabu na gharama za maisha, angalau sisi tunaosimamia mpira tutahakikisha wachezaji wanaocheza kipindi hiki wasipate changamoto ambazo wanazipata wenzao,” amesema Bw. Karia.

Naye, Bw. Cosmasi Sasi, Meneja Uandikishaji, Ukaguzi na Michango wa NSSF, amesema kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya jamii sura ya 50 ya mwaka 2018, NSSF ndio Mfuko pekee uliopewa jukumu la kuandikisha wanachama waliopo katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi wakiwemo wachezaji wa mpira pamoja na wajasiriamali wengine wote.

“Lengo la NSSF ni kuwafikia wafanyakazi waliopo katika sekta binafsi na tayari kazi hiyo tunaifanya kwa njia mbalimbali, lakini ili tuweze kumfikia kila mmoja tuna jukumu la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, mafao tunayotoa na faida zake. Tunashukuru kupata fursa hii ya kujumuika na wenzetu TFF, TPBL pamoja na watendaji wakuu wa vilabu vinavyoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa lengo la kutoa elimu hii ili waweze kujiunga na kuchangia,” amesema Bw. Sasi.

Amesema wachezaji na watendaji wa vilabu vya mpira ni wadau muhimu ambao wanatakiwa wapate kinga ya hifadhi ya jamii ili waweze kunufaika moja kwa moja kipindi ambacho hawana uwezo wa kucheza mpira kwa kupata mafao yatakayowasaidia kuishi maisha bora uzeeni.

Bw. Sasi amesema sheria ya NSSF imezungumzia mahususi wanaopaswa kujiunga na Mfuko kuwa ni wafanyakazi wote walioajiriwa katika sekta binafsi, raia wa kigeni wanaofanya kazi Tanzania bara, watumishi wa taasisi za kimataifa zinazofanya kazi Tanzania bara na watu waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi.

“Tutahakikisha elimu ya hifadhi ya jamii inawafikia wana michezo wote hata waliopo vilabu vya chini, lengo waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa ajili ya kesho yao iliyokuwa njema,” amesema Bw. Sasi.

Naye, Meneja wa NSSF Mkoa wa Temeke, Bw. Ferouz Mtika ameishukuru Bodi ya Ligi, TFF na vilabu vya mpira wa miguu kwa kushiriki semina hiyo yenye lengo la kupata elimu ya hifadhi ya jamii.



Share:

Wednesday, 14 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 15, 2024

Share:

MISA TAN YALAANI WAANDISHI WA HABARI KUKAMATWA MBEYA

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger