Monday 22 July 2024

MIUNDOMBINU YA USAFI WA MAZINGIRA YABORESHWA SINZA "A"






Kazi ya ujenzi wa mifuniko ya chemba za Majitaka ikiendelea katika maeneo mbalimbali ya mtaa wa Sinza A chini ya usimamizi wa mafundi wa DAWASA.

Utekelezaji wa kazi hii maalum inalenga kudhibiti taka ngumu kuingia katika miundombinu ya majitaka na kupelekea uzibaji wa mara kwa mara unaosababisha uchafuzi wa Mazingira kwa majitaka kutiririka mtaani.

DAWASA inasisitiza matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka na kuwaasa wananchi kutotupa taka ngumu kama vile mifuko, mawe, neti, nguo na matairi katika chemba za majit aka.
Share:

KADI ZA MPIGA KURA ZENYE JINA LA ZAMANI LA TUME NI HALALI

 


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan (kulia) akizungumza na Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kasulu Vijini, Bw. Emmanuel Ladislaus alipofika kwenye ofisi za afisa mwandikishaji huyo kwa ajili ya kufanya ziara ya kukagua vituo vya kuandikisha wapiga kura. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan (kulia) akizungumza na Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kasulu Vijini, Bw. Emmanuel Ladislaus alipofika kwenye ofisi za afisa mwandikishaji huyo kwa ajili ya kufanya ziara ya kukagua vituo vya kuandikisha wapiga kura. 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan akiwa kwenye ziara ya kukagua vituo ambapo kwenye baadhi ya maeneo aliagiza kuongezwa kwa BVR Kit kutokana na hamasa kubwa ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha na wapiga kura waliojitokeza kuboresha taarifa zao.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan akiwa kwenye ziara ya kukagua vituo ambapo kwenye baadhi ya maeneo aliagiza kuongezwa kwa BVR Kit kutokana na hamasa kubwa ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha na wapiga kura waliojitokeza kuboresha taarifa zao.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan akiwa kwenye ziara ya kukagua vituo ambapo kwenye baadhi ya maeneo aliagiza kuongezwa kwa BVR Kit kutokana na hamasa kubwa ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha na wapiga kura waliojitokeza kuboresha taarifa zao.
***********
Na. Mwandishi Wetu, Kasulu
Kadi za mpiga kura zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 ni halali na zitaendelea kutumika kwenye chaguzi kuu zijazo bila kujali mabadiliko ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Akizungumza wakati wa ziara aliyoifanya ya kukagua vituo vya kuandikishia wapiga kura leo tarehe 22 Julai, 2024 katika Halmashuari ya Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan amesema wapiga kura wenye kadi hizo hawahusiki na zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

“Naomba nitoe wito kwa wale ambao kadi zao ni zile zenye jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wanadhania kuwa kubadilika kwa jina la Tume kunasababisha kubadili kadi watambue kuwa kadi zao ni halali kwa mujibu wa kifungu cha 168 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024,” amesema. 

Mkurugenzi huyo wa uchaguzi ambaye kwenye ziara yake aliambatana na Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kasulu Vijini, Bw. Emmanuel Ladislaus na maafisa wengine waandamizi, alieleza kwamba wenye kadi hizo ambazo zimeharibika, zimepotea au wamehama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo lingine wanahusika kwenye zoezi hilo.  

“Nimebaini kuwa wapo wapiga kura wenye kadi  za zamani zilizotolewa kabla ya mwaka 2015 (zile za karatasi) hao waje vituoni ili waandikishwe upya kwa kuwa mfumo uliotumika wakati huo ni tofauti na mfumo wa sasa,”  amesema.

Bw.  Kailima amewakumbusha wananchi wa mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi kuwa zimebaki siku tatu kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kukamilika kwenye mikoa yao, hivyo, ni muhimu kujitokeza kwa wingi na kutumia vizuri siku hizo.

Uboreshaji wa Daftari kwenye mikoa hiyo umeanza tarehe 20 Julai, 2024 na utafanyika kwa siku saba hadi tarehe 26 Julai, 2024 ambapo vituo vinafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni. 
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 22, 2024




Share:

Sunday 21 July 2024

MITA ZA LUKU ZA MAJI ZITUMIKE KUMALIZA MALALAMIKO YA WANANCHI - WAZIRI AWESO


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema mfumo wa matumizi ya luku kwenye ulipaji wa bili za maji utakuwa mwarobaini wa kumaliza malalamiko ya wananchi waliokuwa wakidai kubambikiwa bili.

Waziri Aweso ameyasema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi ya uboreshaji wa huduma za maji kwa fedha za hatifungani jijini Tanga na kwamba tekinolojia hiyo umekuwa ikifanya vizuri kwa Taasisi ambazo wameshaanza kuitumia.

"Lazima tukubali sasa kama Wizara ya Maji, tekinolojia zitumike kwenye kufanya mageuzi kwenye sekta ya maji, hatuwezi kukubali kila kukicha mwananchi analalamika amebambikiwa bili ya maji,

"Luku za maji zitumike kwani ndiyo uelekeo sahihi, hatutamvulia Mkurugenzi au Mtendaji ambao hatachukulia uzito wa huduma hii kwa kuona siyo muelekeo sahihi" amesema Aweso.

Mbali na hilo Waziri huyo ameutaka uongozi wa Tanga UWASA kushirikisha jamii pamoja na viongozi wa maeneo ambayo wanakwenda kuweka miradi kwani itasaidia wao kufanya kazi zao kwa uhakika na kufanikiwa katika kukamilisha miradi hiyo.

"Jamii ipo na viongozi wapo ukiwashirikisha utafanikiwa na usiwashirikisha utakwama, wakati mwengine Taasisi zinakwama kutowashirikisha viongozi, utakuta mnaenda kwenye ukaguzi wa mradi lakini hata Mtendaji wa eneo husika hayupo, hii siyo sawa,

"Hawana tatizo ni kiasi cha kuwaambia na kuwaweka wazi hata kama kuna tatizo ni vema kuwapa taarifa na utakapowapa ahadi ukifika siku mliyoahidiana basi liwe limepata ufumbuzi, mnapofanya bila taarifa mnatengeneza malalamiko yasiyo ya lazima" amesema.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga UWASA), Geoffrey Hill amesema mradi huo una lenga kuboresha huduma ya maji katika maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na Tanga UWASA ya maji safi, maji taka pamoja na utunzaji wa mazingira katika vyanzo vya maji.

"Mradi huu pia upo kwenye kutekeleza agizo la Rais kwani umelenga kupunguza malalamiko ya wateja wetu kwa kufunga dira janja za malipo ya kabla ambapo mteja atapata maji kulingana na malipo yake, hakuna kudaiana wala kubambikiana bili" amesema.

Hata hivyo amebainisha kwamba awali walilenga kufunga mita za maji za luku zipatazo elfu kumi lakini tkupitia mradi huo wamepata mita nyingine elfu nne na kufanya kuwa na jumla ya mita elfu 14 ambazo zitaanza kufungwa kwa wateja mwezi huu

Sambamba na hayo, Hill amebainisha kwamba mradi pia umelenga kuongeza uzalishaji wa maji ambao utawanufaisha wakazi ndani ya Wilaya nne za Mkoa ambazo ni Tanga, Muheza, Pangani na Korogwe.

"Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kugarimu kiasi cha shilingi bilioni 53.12  na unatazamiwa kumalizika ndani ya kipindi cha miezi 15 mpaka kufikia Octoba 2025 na pia utakuwa unatekelezwa kwa awamu kwa miezi mitatu kila awamu" amesema.

Vilevile amesema mkataba huo uliosainiwa umegawanyika katika makundi matatu, ambapo kundi la kwanza utatekeleza eneo la Mabayani kwa kuboresha zile pampu za kudukumia maji za zamani ambazo ni ndogo na kuweka kubwa, lkini pia utafanya ukarabati mkubwa wa kituo cha kusukumia maji na kujenga bomba kubwa ili kufika kwenye mtambo wa Moe.

Amesema kundi la pili, "utafanya kazi kwenye mtambo wa Moe, kukarabati na kutatua mtambo pamoja na kujenga tanki kubwa la kuhifadhia maji linalotarajiwa kuwa na lita milioni 35 ambapo hata tukiwa na shida ya maji tunaweza kukaa na maji masaa takribani 20,

"Na kundi la tatu, utafanya kazi ya kusambaza mabomba mitaani hasa kwa maeneo yaliyopo pembezoni, lakini pia kazi kubwa ya kufanya ukarabati mkubwa wa eneo la Ngamiani ambalo lina mabomba ya tangu enzi za mkoloni" ameongeza.




Share:

Saturday 20 July 2024

WATOTO YATIMA WAPATIWA HUDUMA ZA ELIMU BORA NA SHIRIKA LA MASISTER




Mwandishi wetu,Moshi,

Watoto yatima na waishio katika mazingira magumu kutoka maeneo mbalimbali wamepatiwa huduma za elimu bora na shirika la masister wa shirika damu takatifu ya Yesu,ikiwa ni moja sehemu ya huduma yako.

 
Akizungumza na wandishi wa habari msimamizi wa kituo cha watoto yatima Upendo-OKAT iliyopo Njia Panda wilaya Moshi mkoani Kilimanjaro,Sister Deodora Mtagona kutoka shirika la damu takatifu ya Yesu,ameeleza namna ambavyo waliweza kuwasaidia watoto hao.


Sister Mtagona amesema watoto yatima na waishio katika mazingira magumu wameweza kupatia elimu pamoja na huduma za kiroho na kimwili,huko wakifanyiwa ushauri nasa ili waweze kufikia ndoto zao za maisha.


Amesema kuwa chimbuko la kituo hicho ni kutokana na watoto yatima na wale wamazingira magumu kukosa huduma muhimu ikiwemo elimu,afya na malazi.

Amesema kituo hicho kinajiendesha kwa nguvu za wadau mbalimbali ikiwemo mama Rioba Mosha mhadhiri chuo kikuu cha marekani baada ya kuja Tanzania na wanafunzi wake kuguswa na adha na maisha magumu ya watoto yatima.

Aidha amesema mama Rioba Mosha aliona na kuguswa kuwasaida vijana wakitanzania ili waweze kufikia ndoto zao.


"Mwaka 2020 mama Rioba Mosha mhadhiri chuo kikuu cha marekani alikua Tanzania na kutembelea kituo cha watoto yatima cha Upendo children home iliyopo shanty na kupewa historia ya kituo ambapo kinalea watoto wachanga na baada ya  kufikia umri wa miaka ya mitano nakuhamishwa kwenda maeneo mbalimbali,ndiyo alianzisha bodi Tanzania na marekeni ndipo kikajengwa hiki kituo,"amesema.


Amesema kuwa kituo hicho kwa sasa kinawatoto wa 26,kati ya hao wakiume 11 wakike 15 na kwamba watoto wote wanasoma.

"Baadhi yao wako shule ya sekondari na msingi ambapo wanasoma katika shule mbalimbali za binafsi,asubuhi wanapelekwa shule na jioni wanarudishwa kulala kituoni,".

Katika hatua nyingine sister Mtagona ametoa wito kwa jamii kuonyesha upendo kwa watoto na kuwalea katika mazingira bora bila kuwatelekeza.

Amesema watoto ni baraka kutoka kwa Mungu hivyo hatua budi kuwapenda na kuna kuwajali.

 Kwa upande wake mjumbe wa Bodi ya kituo hicho Antony Semagi amesema kuwa bodi hiyo imeona umuhimu wakuwaendeleza watoto hao ili waweze kujitegemea.

Share:

IJUE MBINU YA KUWA NA BAHATI NZURI MAISHANI MWAKO



Kwenye kufanikiwa kimaisha kuna tegemea na mambo mengi sana, kufanya kazi kwa bidii au kujuana na watu wengi wenye uwezo katika eneo fulani hakutoshi kukuhakikishia kufanikiwa kimaisha.

Na ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye hataki bahati nzuri katika maisha yake, kila mtu anataka bahati katika eneo ambalo analifanyia kazi au ambalo yupo na pengine upande wa jambo fulani.

Wapo ambao wanataka kuwa bahati katika biashara, wengine katka mapenzi, wengine katika kazi, wengine katika masomo, wengine katika ndoa na mambo mbalimbali ya kufanana na hayo.

Hata hivyo, ikumbukwe hakuna mtu ambaye anaweza kulazimisha kwamba bahati nzuri itokee maishani mwake, hii ni hali ambayo humtokea mtu pasipo yeye mwenyewe kutambua hilo.

Jina langu ni James toka Morogoro, nimekuwa nikifanya kazi kama wakala wa kutoa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi, ni kazi ambayo ni rahisi kuibiwa kutokana na kuongeza kwa visa vya wizi wa mtandaoni, pia yenye ushindani mkubwa maana vijana wengi wanaifanya kwa sasa.

Kabla sijaanza kazi hii niliweza kuwasiliana na Kiwanga Kiwanga kwa namba hizi +255763926750 au +254769404965 na kumueleza kuwa anahitaji kuwa mtu mwenye bahati maishani mwangu.

Kipindi nawasiliana naye, sikuwa nafanya kazi yoyote, nilikuwa nimechoka kwa kutafuta kazi sehemu mbalimbali na nikagundua sina bahati.

Baada ya kufanyiwa dawa na Kiwanga Doctors, nilishangaa naamka na kukuta Sh2 Milioni imetumwa katika simu yangu bila kujua ni mtu gani kaituma.

Niligojea kwa muda wa wiki moja kuona labda kuna mtu amekosea namba atanipigia simu na kuniuliza lakini sijapokea simu ya namna hiyo.

Basi zile fedha ndizo zilizitumia kama mtaji wa kuanzisha biashara yangu ya kutoa na tuma fedha kwenye mitandao ya simu kama wakala, na uzuri kwenye biashara yangu wateja ni wengi kiasi cha kufanya mtaji wangu kuongezeka hadi kufikia zaidi ya Sh10 Milioni kwa sasa.

Mtaji huo ndio upo kwenye biashara lakini faida nishapata ya kutosha kiasi kwamba nimeweza kununua Bodaboda mbili ambazo nimewakabidhi vijana ambao kila jioni wananiletea hesabu. Hata kununua bodaboda hizi nako nilikumbana na bahati kwani nilikutana na mfanyabiashara anayeziingiza nchini, hivyo akaniuzia kwa bei nafuhu kidogo.

Kumbuka Kiwanga Doctors ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda katika michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger