Thursday 18 July 2024

VISWASWADU KUTUMIKA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

 

Wapiga kura waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wataweza kutumia simu zao ndogo za mkononi (vitochi au viswaswadu) kuanzisha mchakato wa kuboresha au kuhamisha taarifa zao. 
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Tume na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani leo tarehe 18 Julai, 2024, uamuzi huo wa Tume umetokana na maoni ya wadau wa uchaguzi. 

“Tume imefanyia kazi maoni na ushauri huo (wa wadau) na kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 watu wote wenye simu za kawaida (maarufu kama kitochi au kiswaswadu) na watahitaji kuboresha au kuhamisha taarifa zao, watapata huduma hiyo kwa kupiga USSD Code *152*00# na kubonyeza namba 9 kisha kuendelea na hatua zingine kama itakavyokuwa inaelekezwa kwenye simu husika,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mpiga kura anayetumia njia hii atapokea namba maalum (token) kupitia simu yake kisha atalazimika kwenda na namba hizo kwenye kituo anachotarajia kutumia kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ili kukamilisha mchakato na kupewa kadi mpya.

Katika hatua nyingine, Tume imetoa taarifa kwa umma kuhusu kuanza rasmi kwa kituo cha huduma kwa mpiga kura (Call Centre) kinachoanza kutoa huduma kuanzia leo Alhamis tarehe 18 Julai, 2024. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Bw. Kailima, huduma hiyo ni ya bure na itatolewa kwa saa 14 kila siku kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku.

“Kupitia kituo hiki wananchi watapata fursa ya kupiga simu bila malipo kupitia namba 0800112100 na kupata majibu au ufafanuzi wa maswali au jambo lolote linalohusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hivyo, wananchi wote mnakaribishwa kutumia huduma hii kwa kipindi chote cha uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo. 
Share:

KUELEKEA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUBORESHA MIFUMO YA CHAKULA NCHINI, MWENDAMTITU MBARALI KUIMARISHA ULINZI NA KUKOMESHA MIFUGO KWENYE SKIMU

 
Mwenyekiti wa skimu ya umwagiliaji Mwendamtitu iliyopo Mbarali mkoani Mbeya Evaristo Mgiya

Na Christina Cosmas, Morogoro

WAKULIMA wa mpunga kwenye skimu ya Mwendamtitu iliyopo Wilayani Mbarali mkoani Mbeya wamejipanga kuimarisha ulinzi na kuhakikisha mifugo haiingii mashambani na kuharibu utaratibu wa mradi wa kuboresha mifumo ya chakula na kuleta tija ya kilimo unaotarajiwa kuanza mwakani hapa nchini.

Mwenyekiti wa skimu ya umwagiliaji ya Mwendamtitu iliyopo Wilayani Mbarali Evaristo Mgiye alisema hayo kwenye Kongamano la wadau wa Wizara ya kilimo na FAO wakijadili mbinu za kuanza kutekeleza mradi huo mara baada ya mwaka mmoja kuanzia sasa ambao utatekelezwa kwenye nchi 35 duniani ikiwemo Tanzania unaofadhiliwa na mfuko wa mazingira (GEF).

Mgiye alisema watahakikisha watakaoingiza mifugo na kuharibu miundombinu ikiwemo barabara wanachukulia hatua kali za kisheria ili kuiweka skimu kwenye mazingira bora na kuleta tija ya mradi huo.

Aidha aliiomba Serikali kuwaongezea nguvu ya kuboresha miundombinu kwenye skimu hiyo ambayo ina uwezo wa kuiingizia Halmashauri pato la shilingi Bilioni 1.5 kwa mwaka itakayotokana na kila gunia la mpunga kukatwa kwa shilingi 1,000 na kuwezesha suala la chakula nchini.

 “serikali itujengee miundombinu kwa maana mifereji ina changamoto kubwa ya kujaa mchanga, pamoja na kujenga, suala la mchanga linapaswa kuchukuliwa hatua kwa utaalamu kwa kuangaliwa zaidi sababu maji yakipita kipindi cha mvua mchanga unaletwa mwingi, ambao unafanya maji yanasambaa na kupotea sababu ya kupoteza mwelekeo na ujenzi huo utasaidia kuondoa upotevu wa maji pia” alisema Mgiye.

Mgiye alisema kwa kila hekari huzalisha gunia 30-35 kwa sasa ambapo wakulima bado wanakosa mazao baada ya mifereji kujaa mchanga na ikiwa changamoto hiyo itatatuliwa wataweza kuzalisha gunia 35-40 kutokana na eneo lenye ukubwa wa hekta 15,000 walilopo.

Alisema wameshatumia zaidi ya shilingi Milioni 100 katika kufanya tathmini ya uharibifu na kupata ramani halisi ya eneo kwenye skimu hiyo kama walivyoelekezwa ambapo wanaiomba Serikali kuona namna ya kurejea kuwasaidia ili kukamilisha ujenzi kwenye eneo hilo.

Naye Afisa Umwagiliaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wilayani Mbarali mkoani Mbeya Titus Osano alisema Tume imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wakulima na kuhakikisha miundombinu na mazingira yanayowazunguka yanakuwa katika hali ya usawa kulingana na matakwa ya mradi huo.

Alisema uharibifu wa mazingira unachangiwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo kama vile wa bonde la Usangu ambapo wao wanatoa elimu itakayowahakikishia kupata uzalishaji mkubwa kwenye mazao wanayolima huku wakitunza mazingira.

Osano alisema kwa kutumia katiba na sheria zilizopo kwenye kila skimu watahakikisha miti inazidi kupandwa kuzunguka vyanzo vya maji na kuhakikisha makopo ya viuatilifu yanachomwa au yanatunzwa kwenye mazingira mazuri zaidi ili kuepusha athari zozote za kijamii na mimea.

Akizungumzia bonde la Usangu alisema zipo zaidi ya skimu 70 katika bonde hilo huku kukiwa na vyama vya wakulima vingine vilivyopata kibali kuendeleza kilimo katika maeneo hayo ambazo zinapaswa kufuata kanuni bora za kilimo huku zikizingatia utunzaji wa mazingira.

Hivyo Osano aliwashauri wakulima kuhakikisha wanafuata miongozo ya skimu za umwagiliaji zilizopo chini ya serikali na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kutunza miundombinu ambayo ni mifereji na vyanzo vya maji na kufuata taratibu zilizopangwa katika kuhakikisha skimu hizo zinaratibiwa vizuri kwa kufuata miongozo iliyopo.

Mradi wa kuboresha mifumo ya chakula (food systems integrated program) unatarajia kutekelezwa baada yam waka mmoja kuanzia sasa katika maeneo ya Usangu jijini Mbeya na Zanzibar kwa kutumia zaidi ya Dola za kimarekani Milioni 9 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 20 za kitanzania.

Share:

DC KILAKALA ASISITIZA MIRADI KUKAMILIKA KWA WAKATI ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA


Na Hadija Bagasha Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mussa Kilakala amewataka wasimamizi wa miradi yote ya maendeleo kwenye eneo lake kuhakikisha miradi hiyo inasimamiwa kwa viwango vinavyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi. 

Kilakala amesema miradi hiyo inapaswa kusimamiwa vizuri ili kuhakikisha inakamilika na kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi 
ili iendane na mpango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuleta fedha kwenye Wilaya hiyo kwajili ya maendeleo ya wananchi. 

Kilakala ametoa maelekezo hayo wakati alipofanya ziara katika Kata ya Masaika Wilayani Pangani yenye lengo la kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali sambamba na kufanya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi. 

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu ya usafi chini ya program ya uendelevu wa usambazaji wa maji na usafi wa mazingira vijijini (SRWSSP) katika zahanati ya Masaika ambao umepokea kiasi cha shilingi 49,000,000.00.

 Miradi iliyokaguliwa ikiwa katika hatua za utekelezaji inahusisha ujenzi wa choo cha mashimo 03 kwa ajili ya wagonjwa, ukarabati wa choo cha mashimo 02 kwa ajili ya watumishi, ujenzi wa kichomea taka, shimo la kutupia kondo la nyuma, shimo la kutupia majivu, ujenzi wa kinawia mikono, ujenzi wa mnara wa tanki la maji na uingizaji wa maji katika jengo la zahanati. 

Aidha Kilakala amepongeza maendeleo ya kazi ya ujenzi na kusisitiza mradi huo kusimamiwa vizuri ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi.

Sambamba na mradi huo katika zahanati ya Masaika Mkuu wa Wilaya alifika katika Kijiji cha Kigurusimba na kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Masaika ambayo ilipatiwa fedha za ujenzi kiasi cha shilingi 584,280,028.28 kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari (SEQUIP).

 Miundombinu iliyojengwa katika shule hii ilihusisha; ujenzi wa nyumba 08 vyumba vya madarasa, jengo la Utawala, vyumba 03 vya maabara za sayansi, jengo la maktaba, jengo la TEHAMA na vyoo matundi 11 (wavulana matundu 05 na wasichana matundu 06) kwa ajili ya wanafunzi.

 "Pamoja na fedha hizo shule hii pia imepokea fedha kiasi cha shilingi 98,000,000.00 kupitia mradi huo wa kuboresha elimu ya sekondari kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu mbili kwa moja ikiwa na vyumba 03 kila moja ambapo taratibu kumpata fundi zinakamilishwa, "amesisitiza DC Kilakala.  

Hata hivyo Kilakala amewapongeza wananchi kwa kushiriki katika ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni ishara ya kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha elimu katika Wilaya ya Pangani.

Share:

Wednesday 17 July 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULAI 18, 2024

Share:

KAMPUNI YA SHERIA YA KIGENI YADAIWA KUJINUFAISHA KUPITIA MADAI YA KUWATETEA WAHANGA WA UKIUKWAJI WA HAKI ZA KIBINADAMU MGODI WA NORTH MARA

Kampuni ya sheria ya kigeni imedaiwa kujinufaisha kupitia madai ya kuwawetea wahanga wa ukiukwaji wa haki za kibinadamu Mgodi wa North Mara


The law firm successfully sought compensation for alleged human rights abuses from North Mara Gold Mine on behalf of 13 villagers.
Leigh Day is accused of doing injustice the London-based law firm claims to be against. PHOTO | LEIGH DAY
Leigh Day spokesperson Caroline Ivison says the intensity at which African Barrick Gold defended itself in the litigation as well as the duration of the case led to significant legal case costs, denying the law firm benefiting from claimants. PHOTO | LEIGH DAY

By The Tranquility News Reporters, Tanzania

A London-based law firm is accused of shortchanging Tanzanian villagers a gold mine compensated for purpoted human rights abuses; The Tranquility Newshas learnt.

Leigh Day, which deals in employment law, human rights, clinical negligence and personal injury, sought the compensation on behalf of 13 villagers at North Mara Gold Mine.

The litigation against Acacia Mining Plc. owning the mine was settled out of court in 2015, compelling the gold mine to pay staggering Sterling Pounds 143,501.

Leigh Day though refutes taking a lion’s share of the compensation paid, available evidence shows the firm pocketed over 61 per cent, leaving one of the victims with the remaining 38 per cent.

One of the represented villagers Charles Marwa (not his real name) admits signing the Leigh Day’s letter on January 16, 2015, detailing his payment after the case was settled.

Marwa was finally paid Sterling Pounds 55,500 while the firm took home Sterling Pounds 88,001.

Leigh Day spokesperson Caroline Ivison, nonetheless, denied the firm benefiting from claimants as was the case with Marwa saying the allegations were false.

“We strongly refute the allegations on inappropriate and excessive fees,” said Ivison, explaining that significant legal costs were compounded by the intensity at which African Barrick Gold defended itself in the litigation as well as the duration of the case.

“No money allocated to claimants’ compensation was deducted for legal costs, we explained everything clearly to every client,” said Ivison as she declined to divulge details of their clients’ payments saying they were confidential.

Marwa was shot and injured in 2008 when invading the mine. A politician and activists linked him up with Leigh Day which filed a law suit in the UK before it was settled out of court.

Intruders invade North Mara Gold Mine in Tanzania. PHOTOS | FILE

Marwa, who is only one of the victims Leigh Day filed law suits against the gold mine on their behalf, said the politicians and activists told him the firm raised funds in support of claimants like him.

“So, all what we needed was giving full cooperation and following their instructions, assuring us that we would be compensated handsomely,” said Marwa as he recalled:

“I was happy when I received the Sterling Pounds 55,500 before my visiting cousin, who is a teacher at a neighboring village, clarified to me what exactly was in the agreement letter I signed.

His cousin wondered the firm, which pledged to assist the claimant free of charge, walked away with more than Sterling Pounds 88,001.

“It pained me a lot, I felt and still feel they used my problem for their own benefit,” Marwa lamented.

A CCTV footage shows invaders confronting police officers inside Tanzania’s North Mara Gold Mine.

In its agreement letter, Leigh Day states: “Given the difficulties and risks of litigation, including extremely substantial risk of not being successful in the litigation, we consider that the total sum constitutes very good settlement of the claim.

“If you accept the settlement, the compensation paid in respect of the claim will be significantly more than you would have achieved if you had sought to resolve the claim without Leigh Day through the North Mara Gold Limited Grievance Mechanism.

“The amount that is proposed to be paid in settlement of a claim has been calculated by using the maximum total amount that could potentially have been awarded if your claim was successful.”

Marwa mulled resorting to court to seek assistance only to be discouraged by the politician he considered supporting him not picking calls after the payment was done.

Litigations and lawsuits on allegations on human rights abuse at North Mara Gold Mine is a climax of a well calculated syndicate.

Barrick president and Chief Executive Officer Mark Bristow says he is proud of North Mara Gold Mine’s strong working relations with its host community. PHOTO | MINING GMX

A cartel comprising business persons, politicians and local and international human rights activists have for quite a long time been spoiling ties between the gold mine and the hosting community.

On the frontage, intrusions into North Mara appear as grievances against the mine, but a deep dive into the deadlock debunks the ugly organised criminal invasions.

Marwa admits some sponsors had organised the incident that led to his injuries, assuring him and his accomplices of their safety, as police officers on duty had agreed to cooperate with the intruders.

The intruders never noticed the law enforcers agreed with were not on guard at the area, they kept on moving forward even after several warnings.

“The police officers were resolute, making us angry, thinking they were betraying the deal into which they entered with our boss

A police officer guards waste dump at North Mara Gold Mine.

We decided to fight and I got injured as we confronted the police officers, several law enforcers were injured as well,” Marwa explained.

A several months’ investigation by The Tranquility News reportersteam revealed that the so-called mining invasions are actually an organised crime.

Wealthier and influential business persons, politicians and civil servants run the cartel assisted by several unfaithful mine’s staffs.

The cartel has all along been enjoying the cover of human rights abuses once its invading squads clash with police officers guarding the mine.

The invasions are categorised in four classes, with the first one involving youth, women, and the elderly having little or no harm at all.

Allegations on human rights violation against North Mara Gold Mine in Tanzania often call into question the credibility of activists.

All what the first unarmed category does is collecting few stones around the mine without intruding into the mine or causing any violence.

The second and notorious category comprises hired youth from different parts of the Lake Zone. The third category, which consists of direct beneficiaries of gold ores stolen from the mine includes influential and wealthier people who recruit the youth in the second category.

This is the violent category armed with machetes, daggers and other tradition weapons that invades the mine in a broad daylight, as they dare police officers in their large numbers.

“On the façade they look like just youths aggrieved by the presence of the mine, fooling some human rights outfits to regard them as victims.

“They are very good at playing the victims’ role, but in reality, they are the assaulters,” says Timasi Peter, the chairman of Mujata, an NGO that deals with welfare of the society.

Mara Regional Commissioner Col Evans Mtambi says a lot of disinformation surround regular invasions of North Mara Gold Mine and that the matter has been politicised for both political and financial gains.

The third category facilitates all activities, including bribing officials when the need arises, and hiring, paying and protecting the youth invading the mine to fetch them gold ores ready for processing and selling at gold markets within Tarime District.

“The invasionsare well focused and calculated to make them appear as just expressions of grievances against the mine,” former village leader said on condition of anonymity.

“The litigations and lawsuits are not against the mine, they are actually against Tanzanians owning the mine through Twiga Minerals Corporation,” Timasi said.

Barrick and the Tanzania Government had jointly set a model for the natural-resource rich country to benefit from the godsend and avert resource curse, Timasi, who resides at Nyakunguru Village situated a stone’s throw away from the mine, explainedΩ

Share:

UCHECHEMUZI MAPUNGUFU SHERIA ZA HABARI KUSAIDIA UPATIKANAJI SHERIA MPYA


IMEELEZWA juhudi za Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na wadau na waandishi wa habari Zanzibar kufanya ushawishi na utetezi wa mabadiliko ya sheria zenye vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari zimesaidia kuweka matumaini ya baadhi ya sheria hizo kufanyiwa marekebisho.

Hayo yameelezwa na wadau katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa programu ya uchechemuzi wa sheria za habari Zanzibar kilichowashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kisiwani Pemba.

Zaina Mzee ambaye ni afisa programu hiyo kutoka TAMWA ZNZ,   amesema program ya uchechemuzi wa mabadiliko ya sheria za habari zinazokwaza uhuru wa habari Zanzibar imeonyesha kuleta mabadiliko ya maboresho kwenye baadhi ya vifungu vya sheria za habari ambazo ni kandamizi.

Alieleza, kupitia programu hiyo tayari TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar ZAMECO  wamefanya vikao na taasisi za serikali ambazo zinahusika na utungaji wa Sheria kwaajili ya maboresho ya vifungu vya Sheria husika.

Alieleza, "kupitia mradi huu tumefanya  vikao vingi na wadau wa Sheria ikiwemo tume ya kurekebisha Sheria, wajumbe wa Baraza la wawakilishi, NGOs pamoja na wandishi wa habari unguja na Pemba.”

Akitoa maelezo ya tathimini ya vipindi, makaka na habari, Mohamed Khatib ambaye ni mtaalam wa tathimini na ufuatiliaji alisema shabari, makala na vipindi ambavyo vimetolewa vimeonyesha ni jinsi gani wandishi wamekuwa na uwelewa wa kutosha juu vifungu vya sheria ambavyo ni kikwazo kwao.

"Tumepokea makala nyingi kutoka kwenye social media, magazeti, na vipindi vya redio. Kwa kweli zimechambua Sheria na mapungufu pamoja na mapendekezo ya nini kifanyike ili kusiwe na vikwazo Kwa wandishi wa habari," alifafanua Mohammed.

Baadhi ya wandishi wakichangia  wameushauri kuwa na mwendelezo wa uchechemuzi wa vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari ili sheria hizo ziwee kufanyiwa marekebisho na kuwawezesha waandishi kutekeleza majukumu yao kwa uhuru.

Mwanddishi wa habari Masanja Mabula alieleza, “waandishi wa habari tunatakiwa tutumie fursa hii ya elimu tuliyopata ya kuzijua sheria na mapungufu yake kwa kuidi kuyaandikia mapungufu yaliyopo ili yafanyiwe marekebisho.”

TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau wa habari ilifanya  mapitio ya sheria nane (8) za habari zenye vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari Zanzibar ikiwemo Sheria ya usajili wa wakala wa habari, magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria no.8 ya 1997, Sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar namba 7 ya mwaka 1997 iliyorekebishwa na sheria namba 1 ya mwaka 2010.

Share:

TIC YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WAZAWA KAGERA, YAHAMASISHA UWEKEZAJI



Na Mbuke Shilagi Kagera.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeendesha semina kwa wawekezaji wazawa Mkoani Kagera ambapo kimeeleza umuhimu na faida za kuwekeza ndani ya Tanzania hasa Mkoa wa Kagera.

Akizungumza katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera uliopo Manispaa ya Bukoba, Ambapo kimehudhuriwa na wafanyabiashara, wawekezaji wazawa wa Mkoa wa Kagera Kutoka wilaya mbalimbali pamoja na kiongozi Kutoka chuo Kikuu Cha Dar es salaam, Mkuu wa idara ya uhandisi, Kilimo chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dk. Arnold Towo amesema kuwa kupitia uwekezaji kutatengeneza ajira kwa vijana lakini pia kuwajengea uwezo, ujuzi na ufahamu mkubwa wa kutengeneza miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii.

''Kupitia uwekezaji tunajenga na kukuza walipa kodi wadogo wakati na wakubwa ambao baada ya miradi yao kukamilika na kusimama wataanza kulipa kodi na kunufaika lakini pia kupitia uwekezaji tunalenga kutengeneza bidhaa bora na bidhaa hizo  zitauzwa ndani na nje ya nchi'', amesema.

Aidha amesema kuwa sio miradi yote inasajiliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania na kusema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha B kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya uwekezaji Tanzania sura namba 38 iko miradi minne isiyosajiliwa na kituo ambayo ni miradi ya madini, utafutaji wa mafuta na gesi {utafiti}  na miradi ya ujenzi wa viwanda vya kemikali hatarishi , silaha na vilipuzi.

Pia amesema kuwa jukumu hilo la kuhamasisha na kusimamia uwekezaji katika nchi ya Tanzania halisimamiwi na kituo cha uwekezaji Tanzania TIC pekee ila zipo tasisi zingine ambazo zimeundwa na serikali ambazo zinashiriki pia kuifanikisha  lakini pia kuitengeneza ambapo ni IPZA,Tume ya madini,ZIPA, TIC na PPP.

'' Tunapoongelea nchi yetu ni nchi ya uwekezaji hoja ya kwanza nchi yetu ni ya amani na utulivu kwanini amani na utulivu? sisi ni nchi ya kidemokrasia na ni nchi ambayo tayari imeshuhudia mabadiliko sita ya uongozi na tuko awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini pia tangu tupate uhuru katika nchi yetu hatukuwahi kupata machafuko wala kuingia katika matatizo makubwa ya vita na mwekezaji wa nje na hata wa ndani kikubwa anachoangalia ili kufanya maamuzi ya kuwekeza ni uwepo wa amani'',amesema.

Sambamba na hayo amesema kuwa mchakato na utaratibu wa kusajili mradi ni pamoja na cheti cha usajili wa kampuni ambazo zote zinasajiliwa na BRELA ambao ni sehemu ya kituo cha huduma kwa wawekezaji mahala pamoja lakini pia katiba ya kampuni na fomu ambayo inatakiwa kujaza na inawezekena kujazwa kwa mfumo wa kidijitali kupitia simu pia kuwa na andiko fupi la nini unaenda kufanya pia na ushahidi wa mtaji wa kuwekeza na muhimu zaidi ni bodi na unasajili.

''Kama ni mwekezaji raia wa nje au ni mtanzania anayeingia ubia na wawekezaji kutoka nje katika kutekeleza mradi kiwango cha chini kabisa cha mtaji ni fedha za Tanzania zisizopungua dola laki tano lakini kama mwekezaji ni mtanzania kiwango cha chini cha mtaji ni fedha za Tanzania zisizopungua dora elfu 50 takribani Tsh. 125 milioni'' amesema.

''Ikiwa ni mwekezaji mahiri {strategic inversters} kutoka nje kiwango cha chini cha mtaji ni fedha za Tanzania zenye thamani ya dola milioni 50 na ikiwa ni mtanzania ni kiwango kisichopungua fedha za Tanzania zenye thamani ya dola milioni 20''

''Wawekezaji mahiri maalum {special strategic inversters} ambao wao ni wenye mtaji usiopungua fedha za Tanzania zenye thamani ya dola milioni 300'', amesema Dk. Arnold Towo.

Kwa upande wake Alhaji Shakiru Yahaya Kyetema maarufu Dangote wa Muleba amewashukuru TIC kwa elimu na semina waliyoitoa huku akiomba semina nyingine waje na watu wengine ambao ni TRA, Idara ya uhamiaji na mabenki ili wajue changamoto zilizopo na ziweze kutatuliwa.

''Serikali inabidi kwenye mkutano mwingine nimewashauri wakija watu wa TIC waambatane na watu wote wahusika wa mabenki, Idara ya uhamiaji, TRA ili kusudi sisi wafanyabiashara tunaojitoa muhanga wa kuwekeza na wale watu tuzungumze mambo ambayo yanaweza  lkutusaidia ili serikali au TIC iweze kushirikiana na kutupa nguvu ya kutupunguzia mzigo'' amesema Dangote wa Muleba.


Kaimu katibu tawala Mkoa wa Kagera Bw. Isaya Tendega akizungumza katika semina ya TIC na wawekezaji wazawa Mkoani Kagera 
Prof. Nelson Boniface Naibu Makamu wa Mkuu wa chuo - utafiti akiwa katika semina ya TIC na wawekezaji wazawa Mkoani Kagera 
Mkuu wa idara ya uhandisi, Kilimo chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dr. Arnold Towo 
Alhaji Shakiru Yahaya Kyetema maarufu Dangote wa Muleba Mwekezaji mzawa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera 

Share:

Tuesday 16 July 2024

AKIRI KUMUUA MKEWE, WATOTO ILI AFAIDI ZAIDI PENZI LA MCHEPUKO

Hyderabad, India - Mwanafiziotherapia mwenye umri wa miaka 32, aliyekuwa ameajiriwa katika hospitali moja huko Hyderabad amekamatwa kwa madai ya kumuua mkewe na binti zake wawili wachanga.

Uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa mshukiwa huyo alihusika katika uhusiano wa nje ya ndoa na muuguzi kutoka hospitali moja.

Akiwa amechochewa na nia yake ya kuendelea na uhusiano huo, inadaiwa aliamua kuiondoa familia yake.

Kulingana na mamlaka, mwanamume huyo alimchukua mkewe na binti zake hadi Raghunadhapalem mandal katika wilaya hiyo, ambapo kwanza alitoa dozi yenye sumu ya kufisha ganzi kwa mke wake wa miaka 26.

Baadaye, alidaiwa kuwanyonga binti zake wa miaka minne na wa miaka miwili na nusu, kama NDTV ilivyoripoti.

Mwanamume huyo wa Hyderabad alifanya nini baada ya kudaiwa kuua familia?

Katika kujaribu kufanya vifo hivyo vionekane vilitokana na ajali, mshukiwa aliuweka mwili wa mkewe kwenye kiti cha nyuma cha gari lao, na kuwaweka watoto wake kwenye viti vya mbele na kuligongesha gari hilo kwenye mti makusudi.

Hata hivyo, uchunguzi wa kisayansi ulibaini kutoendana na hali inayodhaniwa ya ajali.

Aidha polisi walieleza kuwa mshtakiwa alijaribu kuficha ushahidi wa kitaalamu unaomhusisha na mauaji hayo baada ya kutekeleza kitendo hicho.
Share:

KIMEI AANZA ZIARA JIMBONI


Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mheshimiwa Dkt Charles Stephen Kimei akizungumza na wananchi wa vijiji vya Kisangesangeni na Miwaleni kata ya Kahe, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro hii leo.

Kimei yupo jimboni kuzungumza na wananchi wa Jimbo hilo kusikiliza na kutolea ufafanuzi wa masuala na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Katika ziara yake hiyo aliambatana na diwani wa kata ya Kahe Mhe Aloyce Momburi, wajumbe wa kamati ya siasa ya kata wakiongozwa na katibu wa CCM Kata Ndg Melau Laizer, maafisa watendaji kata na vijiji wakiongozwa na Ndg Happy Msuya pamoja na wataalam toka bonde la Mto Pangani.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger