Thursday, 23 May 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 24, 2024

Share:

TANROADS LINDI YAREJESHA MAWASILIANO BARABARA YA KILWA MASOKO-NANGURUKURU-LIWALE

Na Mwandishi Wetu. 

Wakala ya barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Lindi umefanikiwa kurejesha mawasiliano yaliyokuwa yamekatika kati ya Kilwa Masoko-Nangurukulu wilaya ya Kilwa na wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Mawasiliano hayo yamereshwa ndani ya saa 24 kupitia kazi iliyofanyika usiku na mchana hadi kuhakikisha daraja la muda katika mto Zinga ambao unatenganisha kijiji cha Zinga na Miguruwe linatengamaa ili shughuli za usafirishaji wa abiria na mazao ya chakula na biashara ziweze kuendelea.

Daraja hilo lilisombwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo uliosababishwa na kimbunga Hidaya kilichotokea Mei 3 na 4, 2024 katika mkoa wa Lindi na Mtwara.

Kurejea kwa mawasiliano hayo ni kama kurudisha matumaini ambayo watu walikuwa wameyapoteza kwani hiyo ndiyo njia pekee waliyokuwa wakiitegemea kufikisha mazao yao sokoni na hata bidhaa za kutumia majumbani.

Meneja wa Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Emil Zengo amesema kimbunga hidaya kilipopita maji yaliongezeka wingi na kasi kiasi cha kupita juu ya daraja hilo.

“Daraja hili liliweza kusukumwa kabisa, kusogea pembeni na kuta zake kubomolewa, kimbunga hiki ndiyo pia kilisababisha athari katika maeneo mengine pia ya barabara zetu ambayo ni barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kuja Lindi hadi Mtwara,” amekaririwa Mhandisi Zengo

Kwa sasa eneo hilo limekamilika na barabara ya kutoka Liwale hadi Nangurukulu inapitika huku matengenezo madogo madogo katika baadhi ya maeneo yakiendelea kufanyika ili wananchi waweze kupita na kufurahia uongozi wa Serikali ya awamu ya Sita.

Mbali na daraja hilo, kimbunga Hidaya kilipopita nchini, pia kilisababisha zaidi

ya madaraja manne kukatika yakiwamo ya Somanga, Songas, Mikereng'ende, na la Mto Matandu, huku baadhi ya vijiji vikizingirwa na maji.

Baadhi ya wananchi wameeleza furaha yao juu ya kurejea kwa mawasiliano huku wakielezea adha waliyokuwa wakiipata awali ikiwemo kukosa mahitaji muhimu.

Kwa nyakati tofauti walipotoa maoni yao waliishurukuru Serikali kwa kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida.

Mary Mwela mkazi wa Miguruwe, Mwajuma Kassim Kibweku mkazi wa Miguruwe na Mjumbe wa Serikali ya kijiji, Fadhil Hemed Ngulile mkazi wa Miguruwe, Nurdin Maiki diwani wa kata ya Njinjo, Abdul Sadick dereva wa basi, Hemed Kingwande mwenyekiti kijiji cha Miguruwe wametoa shukrani zao kwa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za dharula kwa ajili ya kurejesha mawasiliano ya barabara.

Kwa upande wake Msimamizi wa barabara ya Kilwa Masoko-Nangurukuru-Liwale Mhandisi Anna Nnko amesema Mbali na daraja hilo pia ipo sehemu ya barabara hiyo ilimegwa na maji yaliyosababishwa na mvua kubwa za El-Nino zilizokuwa zikinyesha jambo ambalo lilifanya TANROADS kulazimika kuihamishia upande mwingine ili shughuli za kiuchumi ziweze kuendelea.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 23,2024

Share:

Wednesday, 22 May 2024

TANROADS LINDI YAREJESHA MAWASILIANO BARABARA YA KILWA MASOKO-NANGURUKURU-LIWALE

Wakala ya barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Lindi umefanikiwa kurejesha mawasiliano yaliyokuwa yamekatika kati ya Kilwa Masoko-Nangurukulu wilaya ya Kilwa na wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Mawasiliano hayo yamereshwa ndani ya saa 24 kupitia kazi iliyofanyika usiku na mchana hadi kuhakikisha daraja la muda katika mto Zinga ambao unatenganisha kijiji cha Zinga na Miguruwe linatengamaa ili shughuli za usafirishaji wa abiria na mazao ya chakula na biashara ziweze kuendelea.

Daraja hilo lilisombwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo uliosababishwa na kimbunga Hidaya kilichotokea Mei 3 na 4, 2024 katika mkoa wa Lindi na Mtwara.

Kurejea kwa mawasiliano hayo ni kama kurudisha matumaini ambayo watu walikuwa wameyapoteza kwani hiyo ndiyo njia pekee waliyokuwa wakiitegemea kufikisha mazao yao sokoni na hata bidhaa za kutumia majumbani.

Meneja wa Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Emil Zengo amesema kimbunga hidaya kilipopita maji yaliongezeka wingi na kasi kiasi cha kupita juu ya daraja hilo.

“Daraja hili liliweza kusukumwa kabisa, kusogea pembeni na kuta zake kubomolewa, kimbunga hiki ndiyo pia kilisababisha athari katika maeneo mengine pia ya barabara zetu ambayo ni barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kuja Lindi hadi Mtwara,” amekaririwa Mhandisi Zengo

Kwa sasa eneo hilo limekamilika na barabara ya kutoka Liwale hadi Nangurukulu inapitika huku matengenezo madogo madogo katika baadhi ya maeneo yakiendelea kufanyika ili wananchi waweze kupita na kufurahia uongozi wa Serikali ya awamu ya Sita.

Mbali na daraja hilo, kimbunga Hidaya kilipopita nchini, pia kilisababisha zaidi ya madaraja manne kukatika yakiwamo ya Somanga, Songas, Mikereng'ende, na la Mto Matandu, huku baadhi ya vijiji vikizingirwa na maji.

Baadhi ya wananchi wameeleza furaha yao juu ya kurejea kwa mawasiliano huku wakielezea adha waliyokuwa wakiipata awali ikiwemo kukosa mahitaji muhimu.

Kwa nyakati tofauti walipotoa maoni yao waliishurukuru Serikali kwa kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida.

Mary Mwela mkazi wa Miguruwe, Mwajuma Kassim Kibweku mkazi wa Miguruwe na Mjumbe wa Serikali ya kijiji, Fadhil Hemed Ngulile mkazi wa Miguruwe, Nurdin Maiki diwani wa kata ya Njinjo, Abdul Sadick dereva wa basi, Hemed Kingwande mwenyekiti kijiji cha Miguruwe wametoa shukrani zao kwa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za dharula kwa ajili ya kurejesha mawasiliano ya barabara.

Kwa upande wake Msimamizi wa barabara ya Kilwa Masoko-Nangurukuru-Liwale Mhandisi Anna Nnko amesema Mbali na daraja hilo pia ipo sehemu ya barabara hiyo ilimegwa na maji yaliyosababishwa na mvua kubwa za El-Nino zilizokuwa zikinyesha jambo ambalo lilifanya TANROADS kulazimika kuihamishia upande mwingine ili shughuli za kiuchumi ziweze kuendelea.
Share:

Tuesday, 21 May 2024

MBASHA: MR. MANGURUWE APEWE USHIRIKIANO NA BODI YA NYAMA

Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara mkubwa nchini Emmanuel Mbasha amesema amesikitishwa na taarifa iliyotolewa na Bodi ya Nyama juu ya Mfugaji wa Nguruwe kutoka Bahi Mkoani Dodoma Maarufu kama Mr. Manguruwe.

Mbasha amesema aliona Mitandaoni taarifa ya Bodi ya Nyama wakisema kuwa Mfungaji huyo amekiuka sheria kwani alipewa kibali cha kufuga Nguruwe 49 tu, na sasa ana Nguruwe zaidi ya 1, 000, amesema kwanza Mfungaji huyo anapaswa kupongezwa na ni kitu ambacho haiwezekani kubakia na idadi hiyo kwani Nguruwe hao wanazaliana kila siku.

Aidha, amesema haoni sababu ya Bodi hiyo kuongea mambo hayo Mitandaoni bali wangemuita mdau wao/muwekezaji huyo na kuongea naye kiofisi na kumshauri cha kufanya ili wasimvunje moyo bali wampe ushirikiano ili kukuza sekta ya Uwekezaji na Ufugaji kwa ujumla.

Mbasha amefunga safari kutoka Jijini Dar es Salaam hadi Dodoma kwa ajili ya kujionea mradi huo wa Nguruwe, na kukiri kuwa iwapo muwekezaji huyo atapewa ushirikiano basi ataikuza sekta ya Uwekezaji, Mifugo na Biashara kwa ujumla ambayo ndio maono ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mifugo Mhe. Abdallah Ulega.
Share:

MAADHIMISHO YA SIKU YA VIPIMO DUNIANI, TBS YANENA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeungana na mataifa mengine duniani kufanya maadhimisho ya siku ya Vipimo ambayo hufanyika Mei 20 kila mwaka ambapo TBS imeitumia maadhimisho hayo kutoa elimu na hamasa kwa wadau wa vipimo kuhakiki vipimo kwa lengo la kumlinda mtumiaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 20,2024 Jijini Dar es Salaam Afisa Metrolojia Mwandamizi TBS, Joseph Kadenge amesema kupitia Kauli Mbiu ya maadhimisho kwa Mwaka huu ni "Tunapima leo kwa kesho endelevu", amewataka wenye viwanda na wadau mbalimbali kutumia huduma za TBS kwa kuhakiki vipimo kwenye sekta mbalimbali ili kupata usahihi wa vipimo hivyo hatimaye kuweza kumlinda mtumiaji.

Kadenge amesema kuwa ni vyema wadau katika sekta mbalimbali wakaendelea kuhakiki vipimo vyao ikiwemo mahospitalini, viwandani, kwenye sekta ya mafuta na gesi na wengineo ili kuwa na vipimo sahihi.

Ameeleza kuwa TBS imeandaa semina kuhusu Siku ya Vipimo Duniani kwa Tanzania ambapo kwa mwaka huu imepangwa kufanyikia mkoani Mbeya ili kutoa uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya Umuhimu wa vipimo.

Kwa upande wake Afisa Vipimo Mkuu Maabara ya Vipimo ya Taifa Metrolojia, Joseph Mahilla amesema maadhimisho hayo yanafanyika kila mwaka na TBS huhakikisha elimu ya vipimo inawafikia wadau wote wa vipimo nchini

Amesema Shirika la Viwango linashughulika na Vipimo viwili vya metrolojia ambayo ya kwanza ni Sayansi ya Vipimo msingi ambayo inajihusisha zaidi na tafiti na sehemu ya pili ni Sayansi ya Vipimo viwandani .

Pamoja na hayo amebainisha kwamba TBS ina maabara ya kisasa ya vipimo na yenye umahiri hivyo ni vyema wadau kuendelea kuitumia kwa manufaa na maendeleo ya viwanda
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger