Saturday, 20 April 2024

NMB YAZINDUA KAMPENI YA UMEBIMA? KAHAMA - KANDA YA MAGHARIBI



Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Benki ya NMB imezindua kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga - Kanda ya Magharibi kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kukata Bima ili kulinda shughuli zao ikiwemo biashara pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto, mafuriko na ajali zinazoweza kusababisha madhara na kusababisha kuyumba kiuchumi.

Uzinduzi huo uliokwenda sanjari na utoaji elimu na ushauri kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kukata Bima umefanyika leo Jumamosi Aprili 20,2024 katika Kituo cha Mabasi cha CDT Mjini Kahama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio amesema lengo la Kampeni ya Umebima ni kutoa elimu ya masuala ya bima, kutoa ushauri pamoja na kuuza bima mbalimbali ikiwemo Bima ya Faraja inayolenga zaidi kutoa mafao ya pole kwa mwananchi anapopatwa na changamoto ya msiba au ulemavu ambapo mteja anajiunga kwa Shilingi 200/= na anapata fao kuanzia Sh.milioni 1 hadi 6.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio.

“Ndugu zangu hivi karibuni mmekuwa mkishuhudia majanga ya moto, mafuriko na ajali mbalimbali, hivyo ni vyema ukawa na bima ili unapopatwa na majanga usipate hasara na kuepuka kuyumba kiuchumi. Njoo ukate bima kwa ajili yako na mali zako. NMB inashirikiana na kampuni mbalimbali za utoaji bima”,amesema Urio.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha amesema Kampeni ya Umebima ni mwendelezo wa kampeni ya Umebima katika Kanda mbalimbali nchini na kwamba wameamua kuzindua Kampeni ya Umebima Wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika Kanda ya Magharibi kutokana na kwamba Kahama ni mji unaokua kwa kasi, una mwingiliano mkubwa wa watu lakini pia kuna wateja wengi wa NMB.

“Tunatoa elimu na ushauri kuhusu bima na kuuza bima ili kukabiliana na majanga yanapotokea., tunataka watu wote tuwafikie wapate bima ili kujikinga na hasara zitokanazo na majanga kwa kutoa fidia. Piatuna bima ya maisha, vyombo vya usafiri, bima kwa Wakulima na Wafugaji”,amesema Chacha.

Nao baadhi ya wafanyabiashara na wananchi waliofanikiwa kufikiwa na Benki ya NMB na kuwapatia elimu ya bima akiwemo Isaya Kisindo, Baningwa Charles na Moses Masasi wameishukuru Benki ya NMB kwa kupatia elimu ya bima na kuahidi kukata bima ili wao na mali zao ziwe salama na kwamba watahamasisha pia wananchi wengine wakate bima.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Aprili 20,2024 katika Stendi ya Mabasi CDT Mjini Kahama . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Said Pharseko akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Mabango wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima 
Mabango wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima  
Mabango wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima 
Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama
Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama
Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama

Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio (kushoto) akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Moses Masasi wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Mfanyabiashara Moses Masasi akihamasisha wananchi kukata bima wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Moses Masasi wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio (kushoto) akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Isaya Kisindo wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha (kushoto) akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Isaya Kisindo wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Mfanyabiashara Borondo Chacha akiishukuru na kuipongeza Benki ya NMB kutoa elimu kwa wananchi kwani wengi hawajui faida ya bima
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Baningwa Charles  wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Viongozi wa Benki ya NMB wakipita mtaa kwa mtaa Mjini Kahama kutoa elimu na ushauri kuhusu Bima wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Viongozi wa Benki ya NMB wakipita mtaa kwa mtaa Mjini Kahama kutoa elimu na ushauri kuhusu Bima wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Viongozi wa Benki ya NMB wakipita mtaa kwa mtaa Mjini Kahama kutoa elimu na ushauri kuhusu Bima wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Muonekano sehemu ya eneo la uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Muonekano sehemu ya eneo la uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Muonekano sehemu ya eneo la uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

KAMATI YA BUNGE UGANDA, YAVUTIWA NA MIUNDOMBINU YA UDOM




Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, wa Bunge la Uganda, wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, ofisini kwake Dodoma.

.......

Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, ya Bunge la Uganda imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa uwekezaji mkubwa iliyofanya katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, pamoja na kusifu Amani na Utulivu mkubwa uliopo, kwa kuzingatia idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Gilbert Olanya, wa Jimbo la Kilak Kusini, Alhamisi tarehe 18 Aprili 2024, walipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho pamoja na kufanya mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, kwenye ofisi yake iliyopo jengo la Benjamin Mkapa, Dodoma.

Aidha, wamevutiwa na aina ya masomo yanayofundishwa katika Ndaki, Shule Kuu na Taasisi za Chuo, pamoja na namna chuo kinavyoendelea kuwekeza katika kuanzisha programu mpya za masomo zinazoakisi mabadiliko makubwa ya kisekta yanayozingatia utoaji mafunzo wenye kutatua changamoto kubwa za ajira, na matumizi ya teknolojia katika ufundishaji.

Akiukaribisha ujumbe huo, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Kusiluka amelishukuru Bunge la Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuwaleta wabunge hao kuja kujifunza UDOM, na kueleza ni kwa namna gani wabunge hao wana mchango mkubwa katika kuongeza hamasa ya ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kutunga Sera zenye kusaidia nchi hizo kuendana na mabadiliko makubwa ya kisanyansi na teknolojia katika Sekta ya Elimu.

Aidha, amewahamasisha waganda kuja kusoma Tanzania kutokana na uwepo wa mitaala mizuri na masomo yenye kukidhi mahitaji katika soko la Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

“Tunayo fursa ya wananchi wa Uganda na nchi nyinginezo za Afrika Mashariki kuja kusoma UDOM. Niwahakikishie tunayo mazingira mazuri na thabiti ya kujifunzia kwa wana Afrika Mashariki kuja kusoma Tanzania. Mazingira yetu, tamaduni na mahitaji yetu yanafanana, kwangu mimi hii ni fursa kwetu sote” alisisitiza

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo waliofika kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma ni pamoja na Mhe. Betty Ethel Naluyima, Mhe. Dkt. Isingoma Patrick Mwesigwa, Mhe. Rwemulikya Ibanda Gerald, Mhe. Patrick Ocan na Mhe. Lillian Obiale Paparu.


Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, wa Bunge la Uganda, wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, ofisini kwake Dodoma.


Wakiwa kwenye picha ya pamoja ni ujumbe kutoka Uganda, wakiwemo wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, wa Bunge la Uganda. Katikati ni Mhe. Gilbert Olanya, wa Jimbo la Kilak Kusini, Mwenyekiti wa Kamati; na kushoto kwakwe ni Prof. Lughano Kusiluka, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, (aliyevaa Kaunda).


Prof. Lughano Kusiluka akikamkabidhi zawadi ya ukumbusho Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Uganda, Mhe. Gilbert Olanya. Wabunge hao walifika kutembelea chuo na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu utoaji wa Elimu ya Juu nchiniTanzania.


Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiagana na waheshimiwa wabunge wa Uganda, baada ya kuhitimisha ziara yao chuoni hapo.
Share:

Friday, 19 April 2024

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 20, 2024



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger