Sunday, 14 April 2024
MBUNGE BYABATO : MIRADI MINGI IMETEKELEZWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 3 YA RAIS SAMIA
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Stephen Byabato akizungumza na wananchi .
Na Mariam Kagenda - Kagera
Katika kipindi cha miaka 3 ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Manispaa ya Bukoba imepokea kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 15 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa hiyo .
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhe. Adv Stephen Byabato amesema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Jimbo la Bukoba mjini ambao umefanyika maeneo ya Soko kuu lililopo katika Manispaa hiyo.
Mhe.Byabato amesema kuwa katika miaka 3 ambayo imefikiwa mwaka huu ya serikali ya awamu ya 6 ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan zaidi ya shilingi Bilioni 15 zimeletwa kutoka serikali Kuu na nyingine zimekusanywa na Manispaa ambapo fedha hizo zimetumika katika shughuli mbalimbali.
Amesema kuwa kupitia fedha hiyo mambo mengi yamefanyika katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali katika elimu msingi na Sekondari,Afya,Barabara,Viwanda,Biashara na uwekezaji pamoja na maendeleo mengine kama hayo ambayo yamefanyika katika kila kata na wananchi wameyaona hivyo amewahimiza viongozi walioko katika maeneo hayo kuendelea kuyazungumzia na kuyaeleza kwa wananchi ili kwa ambao hawayafahamu waweze kufahamu kilichofanyika katika miaka 3 ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ametaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa kipindi hicho kwa uchache kuwa ni pamoja na uwekaji wa yaa za barabarani, marekebisho katika Soko kuu,usafishaji wa mto Kanoni,ujenzi wa shule mpya za Msingi na Sekondari , uboreshaji wa miundombinu ya Madarasa,Hospitali ya wilaya iliyopo Nshambya ,Ujenzi wa Zahanati ,ufunguaji wa Barabara kila eneo pamoja na ufungaji wa huduma ya umeme kwa wananchi na kuongeza kuwa yapo mambo mengine mengi mazuri yanayotarajiwa kutekelezwa katika manispaa hiyo.
Ameongeza kwa kuwahimiza wafanyabiashara wa soko kuu kuwa watulivu kwani taratibu zitakapokamilika watapewa taarifa na kuwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa .
TAASISI MBILI ZA KIJAMII ZAPATA MSAADA WA DOLA 20,000 KUTOKA SHIRIKA LA NVEP KWA UFADHILI WA BARRICK
Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido (kulia) akimkabidhi mwanzilishi wa Maktaba ya Jamii ya Martha Onesmo iliyopo Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa mwazilishi wake,Jennifer Dickson (katikati) hundi yenye thamani ya dola 10,000, katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam .Msaada huo umetolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP) inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow (kushoto) ni Mjumbe wa kamati ya maktaba hiyo Gloria Munthali.
Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa taasisi ya Mwangaza ( OMCW), Marshalo Chikoleka, (kushoto) hundi yenye thamani ya dola 10,000, katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam .Msaada huo umetolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP) inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow (katikati) ni Mtaalamu wa Afya na lishe kwa watoto wenye utapia mlo kutoka shirika hilo Loyce Njilla.
Wanufaika wa msaada wa fedha za msaada wa NVeP wakipatiwa maelezo ya sera za Barrick kusaidia miradi ya kijamii katika hafla hiyo.
Mtaalamu wa Afya na lishe kwa watoto wenye utapiamlo kutoka shirika Mwangaza Loyce Njilla, akionyesha hundi ambayo taasisi yao imepatiwa kwa ajili ya kusaidia kuboresha lishe ya watoto wakati wa hafla hiyo.
Mwanzilishi wa Maktaba ya Jamii ya Martha Onesmo iliyopo Mwanga mkoani Kilimanjaro, Jennifer Dickson akifurahia hundi ya msaada wa kuboresha maktaba hiyo kutoka NVep na Barrick.
Viongozi wa Barrick nchini katika picha ya pamoja na wanufaika wa msaada wa fedha za NVep wakati wa hafla hiyo.
**
Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, imetoa msaada wa dola za Kimarekani 20,000 kwa taasisi zisizo za Serikali za Mwangaza OMCW na Maktaba Jamii ya Martha Onesmo kwa ajili ya kukabilliana na changamoto za elimu na afya katika jamii zenye mazingira magumu.
Martha Onesmo ni maktaba ya kijamii iliyoanzishwa wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwezesha jamii kupata huduma za kupata elimu kupitia maktaba hiyo na taasisi ya Mwangaza OMCW iliyopo jijini Dar es Salaam inajishughulisha na kuwezesha wanawake kiuchumi,elimu na afya ya motto (Mother&Child in Health).
Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa Barrick Nchini Tanzania, Melkiory Ngido, amesema kila robo ya mwaka,taasisi imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji.
“Hadi sasa tumeweza kutoa msaada kwa zaidi ya mashirika 15 nchini Tanzania kupitia taasisi ya NVeP ,lakini huu ni mwanzo,leo tuko hapa kuleta mabadiliko katika taasisi mbili kwa kuzipatia msaada wa dola za Kimarekani 10,000 kila moja kwa ajili ya kuboresha elimu na afya na lishe kwa watoto katika jamii ’’, amesema Ngido.
Akiongea baada ya kupokea hundi ya fedha za msaada huo, Mwanzilishi wa maktaba ya Jamii ya Martha Onesmo, Jennifer Dickson, ameshukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kuboresha huduma za maktaba hiyo kuwa za kisasa zaidi kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea duniani kote.
Naye Mwenyekiti wa taasisi ya Mwangaza(OMCW),Marshalo Chikoleka, ambaye alipokea hundi kwa niaba ya taasisi hiyo , ameshukuru kupatiwa msaada huo na amesema kuwa utasaidia kuboresha huduma kwa makundi mbalimbali yenye mahitaji ambayo taasisi hiyo inahudumia,fedha hizi zinatasaidia kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto kupitia lishe bora ,elimu na kuwezesha wanawake kiuchumi.
Ngoma Mpya Kalii ! MALIGANYA MADIRISHA - SHULE
Hii hapa ngoma nyingine ya Msanii Maarufu Maliganya Madirisha 'Shikomba Bhulolo' inaitwa Shule.. Video nzuri hakika utafurahia
Saturday, 13 April 2024
WIZARA YA AFYA KUWAKINGA WASICHANA DHIDI YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Na Dotto Kwilasa, DODOMA..
Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo imeandaa kampeni ya kitaifa ya kutoa,Chanjo ya Kukinga saratani ya mlango wa Kizazi kwa wasichana wote
walio na umri wa miaka 9 hadi 14 ili kukinga saratani ya shingo ya mlango wa kizazi .
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma , Dkt.Tumaini Haonga ameeleza hayo jijini Dodoma wakati wa
Mafunzo ya chanjo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa kuwawezesha kůwa na uelewa sahihi kuhusu Kampeni hii.
Akizungumzia ufanisi wa chanjo hiyo ameeleza kuwa ni dhabiti hata kama ikitolewa kwa dozi moja na kumfabya mhusika kuwa imara kwa vigezo vya shirika la afya duniani na kwamba Ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kama ilivyo kwa saratani nyingine sio rahisi kuona hatua za mwanzo licha ya kwamba una maambukizi.
Naye Afisa Mpango wa Taifa wa chanjo Lotalis Norbert Gadau ameeleza kuwa asilimia 70 ya wanaofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya huwa wamechekewa huku wakiwa kwenye hatua mbaya hadi kupelekea vifo.
Kutokana na hayo amewahimiza wasichana na wanawake kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara ili kukabiliana na saratani hiyo hali itakayisaidia kupunguza na kuzuia viwango vya vifo vya wanawake, na kuleta matokeo Bora ya matibabu.
BALOZI DKT. NCHIMBI NA WAJUMBE WAKE WAMEWASILI MKOANI KATAVI KUANZA ZIARA YA MIKOA SITA NCHINI
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk, Emmanuel John Nchimbi na ujumbe wake amewasili asubuhi hii mkoani Katavi kuanza ziara ya mikoa sita nchini. Katika ziara hii anaongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makala na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Issa Ussi Haji Gavu