Sunday, 3 March 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 4, 2024


Share:

BARRICK BULYANHULU YAFANIKISHA KUWAJENGEA UWEZO WALIMU WA SEKONDARI HALMASHAURI YA MSALALA


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Khamis Katimba akifunga mafunzo hayo.
Afisa Elimu Halmashauri ya Msalala, Seleko Ntobi
Mmoja wa wakufunzi waliondesha mafunzo hayo akongea wakati wa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, William Chungu, akiongea katika hafla ya kufunga mafunzo hayo.
Walimu walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali
Walimu walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali
Walimu walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali
**

Katika jitihada za kuinua kiwango cha elimu ya sekondari kwa kuinua ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya taifa kidato cha pili na nne, Halmashauri ya wilaya ya Msalala iliyopo mkoani Shinyanga kwa ufadhili wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu, imeendesha mafunzo kwa walimu 336 wa masomo ya sanaa na Lugha, kuhusu namna ya kufundisha kwa kuwajengea umahiri wanafunzi.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku mbili , Afisa Elimu Halmashauri ya Msalala, Seleko Ntobi, amesema mafunzo waliyopatiwa walimu yatakuwa na manufaa makubwa katika sekta ya elimu na kuleta tija na matokeo mazuri .


"Kwa muda wa siku mbili tumepata mafunzo kutoka kwa timu ya wakufunzi wabobezi kutoka chuo cha ualimu SHYCOM, ambao wamekuwa msaada mkubwa sana kwa walimu wetu, kwani kabla ya mafunzo haya walikuwa hawana uelewa unaofanana katika kufundisha na kupima kwa kuzingatia umahili wa wanafunzi", alisema Ntobi.


Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo hayo, Khamis Katimba, alisema baada ya Mafunzo hayo Halmashauri inatarajia kuona utofauti mkubwa wa ongezeko la ufaulu katika shule zote za Halmashauri hiyo.


"Nichukue nafasi hii kuwapongeza ndugu zetu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kazi kubwa mnayoifanya hasa kwa kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo lakini niwaombe walimu wote mliopata mafunzo haya yakalete tija kwa wanafunzi wetu lakini mkawe wazazi pia huko shuleni Unyanyasaji wa kijinsia hautakiwi", Katimba alisema.


Naye Mwakilishi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika hafla hiyo, William Chungu alisema, Barrick itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kuboresha maisha ya wananchi hususani katika sekta za elimu na afya.

"Tunafurahi kuona jinsi Serikali inavyofanya jitihada za kuboresha maisha ya wananchi, nasi kama wawekezaji tutaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali husuani katika suala la elimu ikiwemo kufanikisha miradi ya ujenzi wa miundo mbinu ya shule ili kuwawezesha wanafunzi kusomea katika mazingira rafiki", alisema.

Nao baadhi ya walimu waliohudhuria na kushiriki mafunzo wamesema wamenufaika na wameahidi kwenda kuleta mabadiliko chanya katika ufundishaji na upimaji wa wanafunzi wanaowafundisha.

Barrick Bulyanhulu pia imekuwa ikitekeleza Mpango wa kuinua ufaulu shuleni wa wanafunzi wa sekondari (Performance Improvement Program (PIP) kwa kushirikiana na Halmashauri za Nyang’hwale na Msalala kwa lengo la kufanikisha kupata matokeo mazuri kwa kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi wilayani kwenye wilaya hizo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zinazotolewa na mgodi huo.
Share:

DKT. NCHIMBI AKUTANA NA MSANII DIAMOND KWENYE MAZISHI YA HAYATI ALHAJ ALI HASSAN MWINYI


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana, kuzungumza na kufurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media Group Ndg. Nasib Abdul Isack (Diamond platinumz), ambaye pia ni mmoja wa wasanii nyota na maarufu wa Mziki wa Bongo Fleva na mfanyabiashara, walipokutana baada ya mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, huko Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.
Share:

Saturday, 2 March 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 3, 2024


Share:

Wimbo Mpya : NG'WANA KALANGA - WIVU DOO

 

Share:

TACAIDS YAKUTANISHA WADAU KUJADILI VYANZO ENDELEVU VYA MWITIKIO WA UKIMWI

 
Mwakilishi kutoka Wizara ya Fedha Dkt Muhajir Kachwamba akichangia umuhimu wa upatikanaji wa vyanzo endelevu vya Mwitikio wa UKIMWI nchini wakati wa kikao cha wadau kilichofanyika jijini Arusha tarehe27 hadi 29 Februari,2024

Mkurugenzi wa fedha na Utawala wa TACAIDS CPA(T) Yasin Abas akiwasilisha mapendekezo ya kamati ya fedha wakati wa kikao cha Wadau cha Kujadili vyanzo Endelevu vya Mwitikio wa UKIMWI nchini.

MKurugenzi wa Sera na Utafiti Bw.Godfrey Godwin akiwasilisha malengo ya kikao na mapendekezo ya kamati ya uongozi na utawala wakati wa kikao cha kujadili vyanzo endelevu vya mwitikio wa UKIMWI nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa wadau namna ambavyo nchi imepiga hatua katika Mwitikio wa UKIMWI na namna inavyojipanga kuelekea kumaliza UKIMWI ifikapo 2030.

Wadau walioshiriki kikao cha Kujadili vyanzo Endelevu vya Mwitikio wa UKIMWI nchini kilichofanyika tarehe 27 hadi 29, Februari,2024 jijini Arusha anayezungumza ni Mratibu wa Mpango wa dharura wa Rais wa Marekeni wa Kudhibiti UKIMWI (PEPFAR) nchini Dkt Hiltruda Temba akichangia namna ambavyo nchi inaweza kuweka mikakati mizuri na kuweza kujitegemea katika Mwitikio wa UKIMWI.

Dkt.Bonaveture Mpondo kutoka UNAIDS akiwasilisha mapendekezo ya kamati ya programe wakati wa kikao cha Wadau cha Kujadili vyanzo Endelevu vya Mwitikio wa UKIMWI nchini kilichofanyika tarehe 27 hadi 29, Februari,2024

Na Mwandishi wetu, ARUSHA

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania - TACAIDS kwa kushirikiana na wadau wamefanya Kikao cha Siku tatu Jijini Arusha kwa lengo la kufanya mafunzo, kujadili na kuweka mikakati endelevu kwa ajili ya  mwitikio wa UKIMWI nchini.

Akizungumza katika Kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Jerome Kamwela amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika mwitikio wa UKIMWI, ambapo suala la uendelevu la raslimali za mwitikio wa UKIMWI limetajwa katika Sera ya UKIMWI ya mwaka 2001.

Dkt. Kamwela amefafanua kuwa Tanzania imekuwa moja ya nchi ambayo imepiga hatua  kwa kuanzisha Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI, pia tayari imeanzisha Kamati ya Uendelevu wa Mwitikio wa UKIMWI, Tanzania imepokea Mwongozo wa Kimataifa wa Uendeshaji wa mpango huu, na kuwa na kamati ndogo za Fedha, Uongozi na Utawala, Programu na Jamii. Aidha, Dkt. Kamwela amesisitiza kuwa  katika mwitikio wa UKIMWI ni suala mtambuka hivyo ni wajibu wa kila mdau kutekeleza wajibu wake, ili kufikia malengo ya Dunia ya kumaliza UKIMWI ifikapo 2030.

Naye, Mwakilishi wa UNAIDS Bw. Koech Rotich ametoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kazi kubwa iliyofanyika na kuleta mafanikio makubwa katika Mwitikio wa UKIMWI.

“Kazi inayofanyika hapa ni kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa mkoani Lindi mwaka 2022, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani. Suala la uendelevu la Mwitikio sio fedha pekee, bali ni kuangalia ni kwa namna gani tunapambana kumaliza UKIMWI ifikapo 2030 na mipango baada ya 2030. Ifikapo Disemba Mwaka huu tutawasilisha taarifa ya utekelezaji wa agizo hili, ambapo tutakuwa na mpango wa utekelezaji (road map), alisisitiza Koech”

Kwa upande mwingine Mratibu wa Mpango wa dharura wa Rais wa Marekeni wa Kudhibiti UKIMWI (PEPFAR) nchini, Bi. Jessica Greene ameipongeza TACAIDS na UNAIDS kwa hatua iliyofikia katika maandalizi ya mpango wa utekelezaji wa Uendelevu wa Mwitikio wa UKIMWI. Aidha, Bi Greene amesema kuwa matokeo ya Tanzania HIV Impact Survey (THIS) yanaleta matumaini makubwa na kutakiwa kujipanga kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa katika kutekeleza afua za UKIMWI na kujipanga kwa mipango ya baadaye. PEPFAR itaendelea kufanya kazi na Serikali, ili kuandaa na kutekeleza Uendelevu wa Mwitikio wa UKIMWI.

Aidha, washiriki wa kikao hicho wameeleza kuwa miongozo na mikakati ya nchi inayolenga kumaliza au kupunguza tatizo la UKIMWI, itaendelea kutoa kipaumbele kwenye suala la kuwa na chanzo endelevu cha rasilimali za UKIMWI, ili kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kupata chanzo cha kudumu cha rasilimali za Mwitikio wa UKIMWI.

Wadau wa maendeleo waliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali katika kuhakikisha Mpango wa kuimarisha upatikanaji wa chanzo endelevu cha rasilimali za UKIMWI na kusisitiza kuwa chanzo endelevu sio tu raslimali fedha, bali ni pamoja na njia nyingine zitakazo wezesha kumaliza UKIMWI ifikapo 2030.

 Katika kikao hicho kuliwasilishwa hali ya UKIMWI, ambapo ilielezwa kuwa Tanzania bado haijafikia hatua nzuri katika malengo ya asilimia 95 ya kwanza ya kuhakikisha wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wanafahamu hali zao, hivyo bado kuna haja ya kuhamasisha au kuweka mipango ya uhamasishaji jamii kupima na kujua afya zao. Hii ni pamoja na kuanza kutumia dawa.

Kikao hicho cha mafunzo na mjadala, kwa ajili ya Uendelevu wa Mwitikio wa  UKIMWI, kimewashirikisha pia wadau na sekta zote zinazojumuisha shughuli zinazoweza  kuchangia ongezeko la maambukizi ya VVU. Sekta hizo ni pamoja na madini, Sekta Binafsi, Kilimo, Ujenzi, Utalii na Sekta ya Usafirishaji. Aidha, Washiriki wameishukuru Serikali kwa jitihada zinazofanyika kuandaa mpango wa Uendelevu wa Mwitikio wa UKIMWI.

Kaimu Mkurugenzi wa TACAIDS Dkt Jerome Kamwela, amewashukuru washiriki wote kwa michango yao na ushirikiano walioutoa tangu mwanzo wa kikao hadi kumalizika kutokana na ushirikiano waliutoa.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 2, 2024



Share:

Friday, 1 March 2024

CCM YAJAZA NAFASI ZILIZO WAZI MOROGORO


Na Christina Cosmas, Morogoro

HALMASHAURI kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro 
imemteua na kumpitisha Gervas Mbaruku Zugumbwa kugombea nafasi ya udiwani kwenye uchaguzi mdogo ndani ya kata ya Kamwene wilayani Kilombero.

Akizungumza kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari Katibu wa siasa, Uenezi na mafunzo mkoani hapa Zangina Shanang Zangina alisema CCM kupitia kikao cha kawaida cha Mkoa wa Morogoro chini ya mwenyekiti Mhandisi Joseph Masunga kimefanya uteuzi na kuwapitisha wagombea mbalimbali wa kujaza nafasi mbalimbali zilizokuwa wazi katika chama.

Zangina alisema katika nafasi ya mwenyekiti wa CCM kata ya Konde Wilaya ya Morogoro Vijijini waliopitishwa ni wagombea watatu ambao ni pamoja na Augustina Lucas Makonde, Salum Shaban na Nestory P. Mbena.

Alisema nafasi ya ukatibu wa CCM kata ya Bungu Wilayani Morogoro Vijijini waliopitishwa pia ni wagombea watatu ambao ni Abdalah A. Lubegete, Athumani Shomari Hega na Hashimu Omari Shabani.

Zangina alisema pia nafasi ya ukatibu wa CCM kata ya Kalengakelu Wilayani Kilombero waliopitishwa ni Anthony Mwangwela, Frank Lyanzile na Vicent Mkanyipelele.

Alitaja nafasi nyingine iliyopata wagombea kupitishwa kuwa ni ya uenyekiti wa CCM kata ya Mkula Wilayani Kilombero ambapo aliwataja wagombea waliopitishwa kuwa ni Athuman J. Molem, JunisiaP. Mtangire na Robert V. Njogope.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger