Thursday, 1 February 2024

DK. MWIGULU: GGML KAMPUNI KINARA INAYOKUZA MAHUSIANO MAZURI KATIKA SEKTA YA MADINI


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba (kulia), akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya AngloGold Ashanti (AGA), Gillian Doran (kushoto) aliyemtebelea ofisini kwake wiki iliyopita. Anayefuata kushoto ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti -GGML anayeshughulikia miradi endelevu na masuala ya ubia/ushirika (Afrika), Simon Shayo pamoja na viongozi wengine wa GGML. Wakati wanaofuata kulia ni baadhi ya maofisa wa wizara ya fedha.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya AngloGold Ashanti (AGA), Gillian Doran aliyemtebelea ofisini kwake wiki iliyopita. Anayefuata kushoto ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti -GGML anayeshughulikia miradi endelevu na masuala ya ubia/ushirika (Afrika), Simon Shayo pamoja na viongozi wengine wa GGML. Wakati wanaofuata kulia ni baadhi ya maofisa wa wizara ya fedha.
NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amesema mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Serikali na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) yamechangia kukuza uchumi wa Taifa hususan kwenye makusanyo mazuri ya kodi, ajira na manunuzi ya bidhaa na huduma kutoka ndani ya nchi.

Pia amesema GGML ambao wamekuwa wadau wazuri kwenye sekta ya madini pamoja na ushirikiano mzuri unaotolewa kwa wizara ya madini umeendelea kukuza sekta hiyo ya madini na kutoa mchango mkubwa kwa jamii na Taifa.

Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dodoma alipokuwa anazungumza na Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Anglo Gold Ashanti, inayomiliki mgodi huo wa Geita Gold Mine-GGM), Gillian Doran.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Mwigulu alisema; “Tumekuwa na mahusiano mazuri sana na GGML kama wizara ya fedha hususani katika masuala ya kikodi na kiuchumi.

“GGML wamekuwa wadau muhimu sana wa masuala ya kodi na masuala ya kukuza uchumi wa nchi yetu pia wamekuwa mahusiano mazuri na wizara ya kisekta (madini) kwa kuwa moja ya mgodi wa mfano ambao una ushirikiano mkubwa na wizara ya kisekta na wizara nyingine kama sisi,” alisema Dk. Mwigulu.

Aidha, alisema GGML umekuwa moja ya mgodi wa mfano wenye mahusiano mazuri na jamii mgodi ulipo kwa kutekeleza ipasavyo mpango wa uwajibika wa kampuni kwa jamii (CSR).

Pamoja na mambo mambo mengine alitoa wito kwa kampuni hiyo kutumia viwanda vya kuchenjua dhahabu kwa njia ya kusafisha iliyopo nchini ili kuendelea kukuza uchumi wa Taifa.

Aidha, katika majadiliano hayo Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya AngloGold Ashanti (AGA), Gillian Doran aliyemtembelea Dk. Mwigulu akiwa na timu ya uongozi wa kampuni hiyo, alimweleza waziri huyo kuhusu mipango ya muda mrefu ya AngloGold Ashanti kwa Tanzania.

Alimshukuru Dk. Mwigulu kwa kutambua mchango wa GGML ambayo imeendelea kusalia kuwa mlipakodi bora zaidi katika tasnia ya uziduaji nchini.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 1,2024

 

Magazeti ya leo
 
Share:

Wednesday, 31 January 2024

WALIOPATA ELIMU YA USALAMA BARABARANI DODOMA WATOA SHUKRANI KWA AMEND, USWIS


NA MWANDISHI WETU, DODOMA

SHIRIKA la AMEND Tanzania ambalo linajihusisha na utoaji wa elimu ya usalama barabarani limepongezwa na maofisa usarishaji maarufu bodaboda katika Jiji la Dodoma kwa kuwapatia elimu ya usalama barabarani masuala ya kutoa elimu ya usalama barabarani.

Elimu hiyo ya usalama barabarani kwa madereva bodaboda iliyotolewa shirika hilo imetolewa kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania ambapo lengo ni kuliwezesha kundi hilo kuepushwa na ajali za barabarani kwa kupatiwa elimu ya usalama barabarani ikiwemo kutambua alama za barabarani na kufuata sheria zilizopo.

Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa mahojiano maalumu , madereva hao wa bodaboda waliokuwa wakitoa elimu ya usalama barabarani kwa wenzao ambao walikuwa hawajafikiwa na mafunzo hayo wamesema wanaishukuru Amend Tanzania na Ubalozi wa Uswisi nchini kwa kuwapatia mafunzo hayo.


Nuhu Toyi ambaye ni balozi wa mafunzo ya usalama barabarani na Ofisa Usafirishaji katika Jiji la Dodoma ambaye kituo chake ni UDOM amesema alibahatika kupata mafunzo na yamemsaidia kuendesha chombo chake kwa kujiamini bila kusababisha ajari.

“Pongezi za dhati ziende kwa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania hususan kitengo cha afya kinachofadhiliwa na miss Vivian kwa kutambua umuhimu wa kundi hili la vijana wa bodaboda wengi ni vijana ambao tupo kati ya umri wa miaka 25.


"Kazi hii wengi tumekuwa tukiifanya kwa mazoea na hatuna elimu kwahiyo wengi tumekuwa ni waathirika wa kusababisha au kusababishiwa ajali kwasababu ya kukosa elimu barabarani lakini ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania umeona itakuwa ni vyema kama vijana hawa ambao ni taifa la kesho na nguvu kazi ya taifa wasiweze kudhuulika na ajali," amesema Toyi.
Kwa upande wake Ofisa Usafirishaji, Laurenti Mayowa amesema alikuwa haelewi alama za barabarani lakini kupitia mafunzo hayo wamepokea kutoka shirika la Amend Tanzania kwani limekuja kitofauti katika kutoa mafunzo yao kwani wamefundishwa kwa nadharia pamoja na vitendo.

“Tulipata mafunzo mazuri sana kwenye swala la uendeshaji wa pikipiki lakini pia tumeweza kufundishwa namna ya kutumia barabara lakini pia namba ya kutumi vyombo vyetu, kwa kweli mafunzo yalikuwa mazuri.

"Nimejifunza mambo mengi na mazuri na kabla ya mafunzo nilikuwa sielewi kwamba barabarani nilikuwa naendesha hovyo hovyo tu na baada ya mafunzo nashukuru mpaka sasaivi nime elewa na tulikuwa wengi sana tukifundishwa awamu kwa awamu nafikiri bodaboda takriban 230 au 250 kwa Dodoma hapa na sasahivi wame elimika”, amesema Mayowa.

Ameongeza alama za barabarani ilikuwa ni changamoto kwa madereva wengi , walikuwa wanaziona lakini wanashindwa kuzitumia kama ipasavyo na walidhani ni michoro tu lakini baada ya mafunzo waliweza kuelewa aina za michoro na alama zinazotumiwa barabarani.

“Tulifundishwa kuna alama za onyo, alama za amri, kuna alama za maelekezo kwahiyo yote haya tumefundishwa pia nimefundishwa alama nyengine ambazo nilikuwa sizielewi vizuri kama alama za michoro juu ya sakafu ya barabara hizo nazo nilikuwa sizielewi nilikuwa naona tu michoro na sielewi maana yake na baada ya elimu nimeelewa vizuri”, amesema Mayowa.


Aidha amesisitiza kwa maafisa usafirishaji kubadilika na kuwa na mahudhurio mazuri ya mafunzo yanayotolewa na shirika la AMEND Tanzania kwasababu yanafundishwa kwa vitendo pamoja na kutii sheria za barabarani.


“Tumefundishwa dereva kujihami kwahiyo wale ambao hawajapata mafunzo hawawezi kuelewa na kutii sheria akiwepo barabarani na anaweza kusababisha ajari kwasababu anakuwa hana uelewa wowote lakini vigumu kujilinda anapotumia chombo chake”,Mayowa.
Naye afisa usafirishaji kutoka kituo cha Ndasha,Ally Rashid Ally amesema kuwa bodaboda ni ajira kama zilivyo ajira nyengine na imeteka soko kubwa la ajira kwa vijana kwenye upataji wa kipato na awali haikupewa thamani kama zilivyo biashara nyingine.

Amesema wamekuwa na madereva usafirishaji wengi lakini baadhi yao kwenye kundi hilo hawana elimu ya kutosha ya barabarani na kutambua alama zilizomo.

Ally amesema elimu iliyotewa ni msaada mkubwa kwa maafisa usafirishaji mkoani Dodoma kwani wengi wao wamekuwa na nidhamu iwapo wanatumia vyombo vyao barabarani na changamoto za ajari na vifo vimeweza kuepukika kutokana na maarifa waliopokea kutoka kwa wakufunzi kupitia shirika la AMEND Tanzania.
Share:

WANANCHI WAFUNGA BARBARA YA MWANZAA - SHINYANGA KUKITHIRI MATUKIO YA AJALI UGWETO , WATU WAWILI WAMEGONGWA LEO

Wakazi wa kata ya Bugweto manispaa ya Shinyanga wamelazimika kufunga barabara kuu ya Shinyanga - Mwanza baada ya leo watu wawili kugongwa na gari na kusababisha kifo cha mtu mmoja na mwingine kujeruhiwa wakidai ajali nyingi zinazotokea kwenye barabara hiyo zikisababishwa na mwendokasi unaosababishwa na baadhi ya madereva wa magari.

Baadhi ya wananchi wamedai kuwa ukosefu wa kizuia mwendo (matuta) kwenye barabara hiyo na baadhi ya madereva kutofuata sheria za usalama barabarani  imekuwa chanzo cha kusababisha vifo vitokanavyo na ajali.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi amefika eneo la tukio na kuzungumza na wananchi hao ambapo amesema wataendelea kuimarisha doria za usalama barabarani katika eneo huku katibu tawala wilaya ya Shinyanga Said Kitinga amefika na kuchukuwa hatua kwa kuzielekeza mamlaka husika.

Msafara wa magari yakiwa yamezuiwa.









Share:

SERA ZA UCHUMI ZA RAIS SAMIA ZALETA NEEMA KWA MABENKI



* Benki kubwa za biashara zavunja rekodi ya mapato na faida

* Zamwaga ajira kwa Watanzania na kulipa kodi zaidi kwa Serikali

* Benki za CRDB na NMB zaendelea kuwa vinara

Januari 31, 2024

Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam

Sera nzuri za uchumi za serikali tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani zimeleta neema kubwa kwenye sekta ya benki nchini, huku benki za biashara zikivunja rekodi ya mapato na faida mwaka jana.

Faida kubwa ambazo benki zimepata nchini kutokana na uchumi tulivu na unaokuwa kwa kasi tangu Rais Samia aingie madarakani Machi 2021, zimeziwezesha kufungua matawi mengi zaidi nchini na kumwaga ajira kwa Watanzania.

Benki hizo pia zimeongeza idadi na ukubwa wa mikopo zinazotoa kwa sekta binafsi na kuchochea zaidi ukuaji wa uchumi.

Ongezeko kubwa la faida kwa benki hizo limezifanya zilipe kodi kubwa zaidi kwa serikali na gawio kubwa zaidi kwa zile benki ambazo serikali inamiliki hisa.

Taarifa za robo ya nne ya mwaka (Oktoba-Desemba 2023) za mabenki ambazo zimechapishwa jana zinaonesha kuwa benki mbili kubwa nchini - CRDB na NMB - zinaendelea kuwa vinara wa sekta ya fedha nchini.

Benki ya NMB imevunja rekodi nchini kwa kupata faida ghafi (gross profit) ya Shilingi bilioni 775 kwenye kipindi cha mwaka mmoja kinachoishia Desemba 31, 2023.

Benki hiyo pia ilifungua matawi mapya manne na kuajiri wafanyakazi wapya 98 mwaka jana.

Hii imeongeza jumla ya wafanyakazi wa NMB kufikia 3,642 na jumla ya matawi yake kuwa 231.

Kutokana na mazingira mazuri ya uchumi nchini tangu Samia awe Rais, NMB iliongeza kiasi cha mikopo inayotoa kwa asilimia 28, hadi kufikia Shilingi trilioni 7.7 mwaka jana.

Kwa upande wa CRDB, benki hiyo ilipata faida ghafi ya Shilingi bilioni 599 mwaka jana.

CRDB pia iliongeza jumla ya mali (total assets) zake hadi kufikia Shilingi trilioni 13.2, wakati amana za wateja (customer deposits) ziliongezeka hadi kufikia Shilingi trilioni 8.8.

Kutokana na uchumi wa Tanzania kukuwa kwa kasi chini ya Rais Samia, Benki ya CRDB mwaka jana iliongeza kiasi cha mikopo inayotoa hadi kufikia Shilingi trilioni 8.8.

Ukuaji wa kasi wa uchumi nchini umeiwezesha CRDB kufungua mawawi 10 mapya nchini mwaka jana na kuajiri wafanyakazi wapya 232.

Benki za biashara zinatarajiwa kuweka rekodi mpya ya faida mwaka huu mpya wa 2024 na kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi kutokana na mazingira mazuri ya uchumi na uwekezaji chini ya serikali ya Awamu ya 6 ya Rais Samia.
Share:

EWURA YAENDESHA SEMINA KWA KAMATI YA BUNGE YA SHERIA NDOGO


Mkurugenzi wa Petroli EWURA, Bw. Gerald Maganga, akijibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Sheria Ndogo, wakati wa semina iliyoandaliwa na EWURA, bungeni jijini Dodoma.
Ofisa Mkuu wa Uhusiano EWURA, Bw. Wilfred Mwakalosi, akiwasilisha mada kuhusu Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, wakati wa semina iliyoandaliwa na EWURA kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Sheria Ndogo,iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Sheria ya Ndogo, Mhe. Jasson Rweikiza, akitoa hoja, wakati wa semina ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, iliyoandaliwa na EWURA, iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo wakifatilia semina iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.

..........

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeendesha semina ya siku moja kuhusu Udhibiti kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Jasson Rweikiza.

Akiwasilisha mada kuhusu kazi na majukumu ya EWURA, Ofisa Mkuu wa Uhusiano, Bw. Wilfred Mwakalosi, alisema EWURA ina jukumu kuu la kuhakikisha huduma zinazodhibitiwa zinapatikana kwa wakati na kwa gharama sahihi.

Akijibu hoja kuhusu masuala ya petroli kwenye semina hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Petroli Bw. Gerald Maganga alisema EWURA iko mbioni kuanza kuwianisha gharama za mafuta kwa bandari zote zinazopokea mafuta nchini ili kuongeza tija.

Semina hiyo pia imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga na viongozi wengine kutoka Wizara ya Nishati na EWURA.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger