Tuesday, 23 January 2024

BENKI YA CRDB KANDA YA MAGHARIBI YAZINDUA KAMPENI YA AMKA NA CRDB MTAANI KWAKO


Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imezindua Kampeni yake mpya iitwayo Amka na CRDB Mtaani Kwako inayolenga kuwafikia wateja wengi zaidi ambao walikuwa hawana elimu kuhusu benki ya CRDB na hawajajiunga na benki hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo ya Amka na CRDB Mtaani Kwak oleo Jumanne Januari 23,2024 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana amesema Kampeni hiyo itafanyika kwa siku 22 ndani ya mikoa minne ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora.

Amesema Kampeni hiyo imelenga kuamsha (Amka na CRDB) wateja wote wa Kanda ya Magharibi wakiwemo wafanyabiashara, wakulima, Watumishi, Wastaafu, Wachimbaji wa madini, Wanafunzi na hata watoto wadogo ambao walikuwa hawajajiunga na huduma za CRDB.

“Kampeni hii imelenga kuwafikia wateja wa Benki ya CRDB popote walipo mtaani, wale ambao bado hawajajiunga na familia ya CRDB wajiunge na huduma za CRDB, tunaenda kuwaamsha na kuwaleta wajiunge na CRDB kwa sababu bado kuna watu wengi hawajajiunga na huduma za CRDB inawezekana hawana elimu kwa hiyo tutapita mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba, barabara kwa barabara , mahali pote penye watu wengi kanda yote ya Magharibi”,ameeleza Wagana.
“Kupitia kampeni hii tutapita mtaa kwa mtaa wilaya kwa wilaya ndani ya mikoa minne ya Kanda ya Magharibi kutoa elimu ya bidhaa za CRDB ambapo wateja wengi wataweza kufungua akaunti kwa masharti nafuu kabisa ikiwemo kuwa na namba NIDA pekee inatosha kufungua akaunti na kama hauna basi kitambulisho chochote kinachotambulika kama Kitambulisho cha Mpiga kura, Leseni ya Udereva , Pasipoti ya kusafiria n.k.”,ameeleza Wagana.


Amesema pia watatoa huduma zingine kama Mikopo, Huduma za Bima, Huduma kuunganishwa Kidigitali ikiwemo Sim Banking, kusimika Mawakala wapya na vituo vya Malipo na huduma zingine nyingi.


“Tuna Matawi 25 Kanda ya Magharibi, na tunayo timu yetu ya Freelancers ambao wapo kila tawi ndiyo wanahusika kupeleka ujumbe wa Benki ya CRDB na kutuletea wateja wengi zaidi kuweza kufikia mafanikio yetu ya Benki. West is The Best, Ulipo Tupo”,amefafanua.


“Tunataka kupeleka ujumbe na bidhaa zetu kwa wateja kule kule walipo lakini na kuwaambia kuwa CRDB Wakala ipo kule mtaani wanaweza kupata huduma za Kibenki ikiwemo kufungua Akaunti, kuweka fedha, kutoa fedha, kulipa Bili za serikali n.k”,ameongeza Wagana.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako leo Jumanne Januari 23,2024 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na mabango yaliyoandikwa West is the Best wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na mabango yaliyoandikwa West is the Best wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na mabango yaliyoandikwa West is the Best wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na mabango yaliyoandikwa West is the Best wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako

Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako.




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 23,2024

 

Magazeti
 

Share:

Monday, 22 January 2024

MIGODI YA BARRICK TANZANIA KATIKA MWELEKEO WA DARAJA LA KWANZA,IKIWA NA UWEZO WA KUONGEZA UHAI, KUKUZA ZAIDI UZALISHAJI


Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa akiongea katika mkutano huo

                                                 ****

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, ameipongeza kampuni ya Dhahabu ya Barrick, ambayo inaendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals Corporation kwa kufanya uwekezaji wenye tija na ufanisi ambao umeanza kuleta mabadiliko chanya kwa kuchangia pato la Taifa sambamba na kufanikisha miradi mbalimbali ya kijamii na kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania.

Dkt. Kiruswa alitoa pongezi hizo kwa niaba ya Serikali wakati wa mkutano ulioandaliwa na Barrick kwa ajili ya kutoa taarifa za utendaji wa kampuni katika kipindi cha robo mwaka uliopita kwa waandishi wa habari na wadau mbalimbali uliofanyika katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu ambao pia ulijumuisha viongozi wa Serikali.

Alisema ubia wa Serikali na kampuni ya Barrick umekuwa ukiendelea kupata mafanikio siku hadi siku na mchango wa faida inayotokana na ubia huu kuingia katika mfuko wa Serikali na huduma za kijamii kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka migodi ya Barrick kupata huduma bora kupitia miradi inayotekelezwa kwa fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR).

"Serikali tunajivunia uwekezaji huu ambao ni mfano wa kuigwa pia natoa wito kwa makampuni ya wawekezaji kuwa na programu za kukutana na viongozi wa Serikali katika maeneo yao na kutoa ripoti za utendaji,hii mbali na kudumisha uwazi inachangia kupata maoni ya wadau kutoka pande zote mbili", alisisitiza, Dkt. Kiruswa.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akiongea katika mkutano huo, kushoto kwake ni Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido.

Kwa upande wake, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, alisema kuwa migodi ya Dhahabu ya Barrick ya North Mara na Bulyanhulu imeendelea kudumisha rekodi yake ya utendaji mzuri na kufikia mwongozo wa uzalishaji kwa mwaka 2023.

Alisema mageuzi ya migodi miwili iliyokuwa imetelekezwa kuwa mkusanyiko wa maeneo ya uchimbaji wenye hadhi ya kimataifa ambayo kwa pamoja inazalisha dhahabu katika kiwango cha daraja la kwanza,yanaonesha mafanikio yanayoweza kufikiwa pale kampuni za uchimbaji madini na Serikali wenyeji zinaposhirikiana katika kuwapatia wadau wao thamani halisi.

“Ubia wa Twiga sio tu kwamba umeleta mageuzi katika tasnia ya uchimbaji wa dhahabu nchini Tanzania bali pia umeiweka nchi, inayojulikana kama kivutio cha utalii barani Afrika,katika nafasi ya kivutio kikuu cha uwekezaji ambacho kina utajiri mkubwa wa raslimali za chuma na madini,” alisema Bristow.

Uchimbaji wa kupekecha katika migodi yote miwili unaonyesha mafanikio katika hifadhi zake za dhahabu zilizokuwa zimeishiwa au kupungukiwa dhahabu. Katika mgodi wa North Mara, uwezekano wa kuwa na shughuli nyingine za uchimbaji chini ya ardhi unachunguzwa huku uboreshaji wa mpango wake wa mgodi wa wazi unatarajiwa kuongeza miaka zaidi katika uhai wake, katika mgodi wa Bulyanhulu, kuna fursa karibu na uso wa ardhi na uwezekano wa kuongeza uzalishaji na kunyumbuka kwa uchimbaji.

Bristow, alisema tangu Barrick ichukue migodi ya Tanzania mwaka 2019 imekua na kuwa mchangiaji mkubwa wa mapato ya Serikali, kupitia kodi, ajira, malipo kwa wazabuni wa ndani, miradi ya jamii na gawio kwa wanahisa.

Uwekezaji wake katika uchumi hadi sasa una jumla ya zaidi ya dola bilioni 3.4 (kwa msingi wa 100%), ambapo kutokana na mafanikio haya migodi yake katika kipindi cha mwaka jana imetunukiwa tuzo mbalimbali za utendaji kazi kwa ufanisi mkubwa.

Awamu ya kwanza ya mpango wa Twiga wa kusongesha Mbele mustakabali wa Elimu ( Twiga Future Forward Education Initiative) wenye thamani ya Dola milioni 30 inakaribia ukingoni. Mpango huu utaboresha kwa kiasi kikubwa miundombinu ya elimu ya Tanzania kwa kutoa vyumba vya madarasa,mabweni na vyoo kwa wanafunzi zaidi wapatao 49.000.

Kwa upande wao Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme na Mkuu wa mkoa Geita, Martin Shigella, wakiongea kwa nyakati tofauti katika mkutano huo walipongeza kampuni ya Barrick kwa kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika mikoa yao hususani kupitia miradi inayotekelezwa na fedha za uwajibikaji kwa jamii ambayo imeboreha sekta mbalimbali hususani afya ,elimu ,maji safi na miundombinu ya barabara.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigella akiongea katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mndeme akiongea katika mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akitambulisha viongozi wa mkoa katika mkutano huo
Viongozi wa Barrick na Serikali katika meza kuu
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa akishirikiana na Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigella na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na Christina Mndeme kukikabidhi mfano wa hundi zenye thamani ya dola 10,000 kwa viongozi wa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusiha na kupambana na changamoto mbalimbali katika jamii. Fedha hizo zimetolewa na taasisi ya NVeP inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow (pichani mwenye kofia). Mashirika 5 yasiyo ya kiserikali yamefanikiwa kupata msaada huo katika awamu hii ya robo ya mwaka.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, akishirikiana na Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigella na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na Christina Mndeme kukikabidhi mfano wa hundi zenye thamani ya dola 10,000 kwa viongozi wa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusiha na kupambana na changamoto mbalimbali katika jamii. 
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, akishirikiana na Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigella na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na Christina Mndeme kukikabidhi mfano wa hundi zenye thamani ya dola 10,000 kwa viongozi wa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusiha na kupambana na changamoto mbalimbali katika jamii. 
Share:

MWANAJESHI MATATANI KWA KUJIPANDISHA CHEO NA KUWA MEJA


Mwanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) yuko matatani kwa madai ya kujipandisha cheo na kuwa Meja na kujifanya hivyo.

Kyambadde, ambaye kwa sasa ana cheo cha Binafsi, yuko kizuizini kwa kosa la uigaji. 

UPDF ilishiriki habari hiyo kwenye Twitter, na kuongeza kuwa askari huyo atakuwa akijibu mashtaka ya uigaji na shughuli nyingine zinazoathiri utaratibu mzuri na nidhamu ya UPDF. 

Msemaji wa Jeshi hilo, Brig. Jenerali Felix Kulayigye, aliliambia gazeti la The Monitor kwamba ilikuwa vigumu kueleza alianza lini.

"Jambo la msingi ni kwamba tunaye chini ya ulinzi kwa sababu hiyo. Nimeambiwa amekuwa akijihusisha na uhalifu, lakini bado tunaendelea na uchunguzi," Brig Jenerali Kulayigye alisema.

 Maelezo yanaonyesha kuwa Pte Kyambandde sio mwanajeshi wa kwanza kuiga mwandamizi, kwani visa kama hivyo vimetokea katika Jeshi. 

Mnamo Februari 2023, mwanamke aliyejulikana kama Eunice Keinembabazi alikamatwa kwa madai ya kujifanya kama Kanali.

Wakati wa kukamatwa kwake, Keinembabazi alisemekana kuwalaghai waathiriwa wasioshukiwa wa takriban USh 15 milioni (KSh 627,000). 

Uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa kila kulipokuwa na operesheni dhidi ya uvuvi haramu, mshukiwa alikuwa akiwaita makamanda wa Kitengo cha Ulinzi wa Uvuvi akijitambulisha kama Kanali Mbabazi.

 Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi la Uganda, Keinembabazi ataamuru kuachiliwa kwa washukiwa. 

Bahati yake ilitoweka alipompigia simu mmoja wa maafisa hao akimtaka aachilie boti haramu iliyokuwa imezuiliwa, na kutakiwa kuonekana kimwili.

Alipofika, aliombwa atoe kitambulisho chake, lakini alivunjika na kukiri kwamba alikuwa raia.
Share:

BIBI NA MJUKUU WAKE WATAKA KUTOA UHAI WANGU

Naitwa Amani kutokea Moshi, Tanzania, kila siku nilikuwa naletewa chakula na msichana wa jirani ambaye alikuwa anaishi na Bibi yake alikuwa anafanya kazi mgahawani kwa Mama yangu.

Alikuwa anamsaidia kazi, kwa kuwa Mama yangu alikuwa anachelewa kufunga mgahawa, alikuwa anamkabidhi binti chakula aniletee nyumbani ili niwahi kula.

Siku moja aliniletea chakula kama kawaida, ila ilikuwa tofauti na siku zote, alinisisitiza sana nile kile chakula, alitania kuwa Mama yangu amesema silagi chakula anachoniletea.

Tulicheka halafu nikamwambia asijali, nitakula, akaondoka zake, sijui hata kile chakula kiliwekwa nini kwani baada ya kula usiku tumbo liliniuma sana, ni kama mtu alikuwa anasugua visu tumboni, nilihisi kufa.

Kesho yake asubuhi mapema kabla Mama hajaamka, nilitoka kwenda kwa Mama yangu mdogo, nilikuwa natapika na kuharisha, choo kinatoka cheusi kama cha mnyama, hayakuwa maumivu ya kawaida.

Nilimueleza Mama yangu mdogo kila kitu, aligundua kuna jambo hali sawa, mara moja alinichukua na kunipeleka kwa Kiwanga Doctors, huko nilifanyiwa tiba na kuelezwa chakula kile kilikuwa na mambo ya kishirikina.

Baada ya dawa ya Kiwanga Doctors, nililala usingizi mzito sana, sikujua hata nini kiliendelea, ile naamka nipo sawa kabisa, maumivu yote yameisha, ilikuwa ni kama nimerudishiwa uhai wangu upya.

Yule bibi ambaye mjukuu wake ndiye aliyeniwekea vitu, alikuja kuniulizia nyumbani asubuhi, Mama alimwambia hajui nilipo, maana hakunikuta chumbani kwangu asubuhi ile.

Baadaye tulivyomsimulia Mama nini kimetokea, aliniambia yule Bibi alimuuliza maswali ya kidadisi ili kujua nipo wapi, kwa bahati nzuri mama mwenyewe alikuwa hajui nipo wapi na nini kinaendelea.

Ilikuwa bado hajapewa taarifa, ila alikuwa na wasiwasi maana ingekuwa sio rahisi kwa mimi kuondoka asubuhi ile bila taarifa wala kuaga.

Baada ya maswali mengi, yule bibi alimwambia Mama kuwa mjukuu wake hataweza kufika mgahawani kwa siku ile, sababu wamepatwa na matatizo. Akaondoka.

Kesho yake tulisikia wote wamesafiri, bibi na mjukuu wake, ila hatukufuatilia sana wameenda wapi, sasa hivi nipo chuo, naogopa kwenda hata nyumbani, maana hapa ndio wivu ulipoanzia.

 Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.

Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.

Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.

Mwisho.

 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger