Sunday, 14 January 2024

MFUKO WA JIMBO WAWEKA ALAMA - MTATURU




MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amewaongoza wajumbe wa mfuko wa jimbo kukagua miradi iliyotengewa na kutekelezwa kwa fedha za mfuko huo kiasi cha Sh 67,498,970 kwa mwaka 2022/2023.

Ziara hiyo ameifanya baada ya kumaliza kikao cha kupokea na kujadili maombi ya fedha za mfuko huo.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Mbunge Mtaturu amesema Kamati ya mfuko wa Jimbo baada ya kutembelea miradi hiyo imeridhishwa na hatua ya utekelezaji.

"Kamati hii iligawa miradi katika Kata 13 na tumepata nafasi ya kuitembelea baadhi ya miradi hiyo na tumeridhika na hatua ya utekelezaji iliyofikiwa,na tukiendelea na kasi hii tutakuwa tumeunga mkono kwa kiasi kikubwa dhamira ya Rais wetu mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo,tunafahamu Rais wetu halali kwa ajili ya watanzania,hivyo na sisi tulio chini yake tunawajibu wa kumuunga mkono kwenye jukumu hilo,".amesema.

Mtaturu ameainisha miradi waliyotembelea kuwa ni pamoja na ujenzi wa M Matundu ya vyoo katika shule ya Msingi Ulyampiti ambayo utekelezaji wake imetengewa Sh 2,000,000.

"Tumetembelea na kujionea ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Ighuka iliyotengewa Sh 2,000,000 ambayo kwa sasa wamekamilisha ufungaji wa renta na Serikali Kuu imetenga Sh Milioni 50 kwa ajili ya umaliziaji ili huduma zianze kutolewa,Kamati pis imetembelea ujenzi wa vyumba viwili vya maabara ambapo walitengewa Sh Milioni 5,katika ujenzi huu tayari wameshajenga msingi na kufunga mkanda wa renta chini na sasa wanatarajia kuanza kunyanyua ukuta,"amebainisha.

Mbali na miradi hiyo amesema wametembelea pia ujenzi wa nyumba ya Mganga Zahanati ya Ujaire ambayo ilitengewa Sh Milioni 1.5 na wameshajenga boma na kufunga renta.

Aidha,wametembelea na kujionea ujenzi na ukarabati wa madarasa ya Shule ya Msingi Ujaire ambayo ilitengewa Sh Milioni 2 na kwa sasa ukarabati na ujenzi wa maboma ya madarasa umekamilika ambapo pia serikali kuu ilipeleka Sh Milioni 41 kumalizia madarasa mawili na ofisi.

Mtaturu amewapongeza wananchi wakiongozwa na viongozi kwa kujitolea kwenye miradi hiyo na kuishawishi serikali kupeleka fedha za umaliziaji.

"Ndugu zangu niwatie moyo na kuwahimiza kuwa tuendeleze juhudi hizi tulizozianza na jitihada tulizozionyesha katika kiradi hii tuziendeleze katika miradi mingine tunayoisimamia,"amesema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Madiwani wa Kata za Ikungi na Lighwa wamempongeza Mbunge na Kamati yake kwa kuwatengea fedha za kusaidia miradi kwenye sekta ya elimu na afya ambayo sasa matunda yake yanaonekana kwa kuwa baadhi ya miradi imeanza kufanya kazi.

Share:

WMA NA ZAWEMA ZAKUBALIANA KUSHIRIKIANA KUSIMAMIA MATUMIZI SAHIHI YA VIPIMO


Taasisi za Wakala wa vipimo za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (WMA) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (ZAWEMA) zimetiliana saini hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) ili kuimarisha utendaji kazi wao katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubadilishana utaalamu na vitendea kazi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi wanao hudumiwa kwa upande wa Bara na Visiwani Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini huo katika Ukumbi wa Dokt Mwinyi kituo cha maonesho ya biashara Nyamanzi Fumba Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Hashil Abdallah amesema ni vyema kuimarisha mashirikiano kati ya taasisi hizo ili kuhakikisha vipimo vyote vinakuwa sahihi na mnunuzi wa bidhaa anapata kulingana na thamani ya fedha anayotoa.

Dkt. Hashil amesema, kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Wakala wa Vipimo ndio taasisi pekee inayopaswa kusimamia matumizi sahihi ya vipimo kwa kuhakikisha kuwa vipimo vinavyotumika katika biashara viko sahihi, na kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo ili kuepusha madhara yatokanayo na vipimo batili na kulinda walaji na watumiaji.

Aidha, amesema makubaliano hayo yatasaidia kuimarisha utendaji wa kazi na kuongeza ufanisi utakaopelekea kufikia malengo ya Taasisi hizo kwakuwa taasisi ya Wakala wa Vipimo Bara (WMA) ilianzishwa muda mrefu na inauzoefu wa muda mrefu na vifaa vingi vya kisasa kwa mashirikiano haya itaiwezesha zaidi taasisi ya ZAWEMA kutumia pia vifaa hivyo na wataalamu ili kusimamia matumizi sahihi ya vipimo katika sekta nyingi zaidi.

Kadhalika, Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Ndugu. Ali Khamis Juma ameeleza kuwa mashirikiano baina ya taasisi za WMA na ZAWEMA ni mashirikiano ya kudumu kwa muda mrefu sio ya kipindi cha muda mfupi kwani hivyo itaiwezesha taasisi ya ZAWEMA kukua zaidi na kuingia katika maeneo mengi ya kiutendaji kama ilivyo upande wa WMA Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Bara (WMA) Bi. Stella Kahwa ameeleza kuwa mashirikiano baina ya WMA na ZAWEMA yamekuwepo kwa muda japo hayakuwa rasmi kimaandishi na sasa yamekuwa rasmi taasisi hizi zitazidi kuimarisha zaidi mashirikiano hayo na mara nyingi WMA na ZAWEMA hushirikiana hata katika kuendesha kaguzi mbalimbali visiwani Zanzibar kwa wauzaji wa vito na madini, mafuta na hata katika sekta ya gesi ili kuhakikisha vipimo vinakuwa sahihi wateja hawapunjiki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa wakala wa Vipimo Zanzibar (ZAWEMA) Bw. Mohammed Simai Mwalim ameeleza kuwa endapo vipimo vitasimamiwa kwa usahihi katika bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini na bidhaa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi itasaidia Serikali kukusanya kodi kwa usahihi.

Hata hivyo alisema endapo vipimo hivyo havitasimamiwa vyema itasababisha wananchi kupata huduma au bidhaa ambazo haziendani na thamani ya fedha wanayotumia.

Mkurugenzi Mohammed ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara wote wa Tanzania bara na Zanzibar kuhakikisha wanatumia vipimo sahihi na endapo watakutana na changamoto yoyote inayohusu vipimo wafike kwenye ofisi za Wakala wa Vipimo kwa ajili ya kupata msaada wa kitaalamu.

Hata hivyo aliwaonya Wamiliki wa vipimo kutochezea vipimo kwa lengo la kuwaibia wananchi, kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kufanya vitendo hivyo ambavyo vinakatazwa hata kwenye maandiko matakatifu.

Nao Washiriki walioshuhudia utiaji wa saini huo walisema kuwa makubaliano hayo yametiwa saini katika kipindi muafaka cha kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi na yataongeza mashirikiano zaidi ili kuyaenzi na kuyalinda Mapinduzi hayo.

Hati hiyo ya makubaliano ya kiutendaji yalisainiwa na Mtendaji Mkuu wakala wa vipimo Bara (WMA) Stela Kahwa na kwa upande wa Zanzibar Mkurugenzi wakala wa vipimo Zanzibar (ZAWEMA) Mohammed Mwalim Simai.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 14,2024




Magazeti ya leo Jumapili

















Share:

Saturday, 13 January 2024

MLANDEGE FC YAINYUKA SIMBA SC 1-0, YANYAKUA KOMBE LA MAPINDUZI CUP


NA EMMANUEL MBATILO,

KLABU ya Mlandege Fc imefanikiwa kuutetea ubingwa wake mara baada ya kuichapa Simba Sc bao 1-0 kwenye fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup ambayo ilikuwa inaendelea visiwani Zanzibar.

Katika mchezo huo ambao Simba Sc ilifanikiwa kuutawala mchezo kwenye vipindi vyote licha ya kutofanikiwa kupata bao huku wakiruhusu kufungwa bao moja na kushindwa kunyakua taji hilo.

Bao pekee ambalo limewafanya Mlandege Fc kuibuka washindi limefungwa na Joseph Akandwanao mnamo dakika ya 54 ya mchezo baada ya kuwatoka mabeki wa Simba Sc na kupiga shuti kali lililomshinda kipa na kuingia nyavuni.

Ikumbukwe Mlandege Fc kabla ya fainali haijawahi kushinda ndani ya dakika 90 kwenye michuano hiyo ya kipindi hiki.
Share:

TGNP YAPENDEKEZA JESHI LA POLISI KUTOJIHUSISHA NA UCHAGUZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi

Na Deogratius Temba, Dodoma

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umependekeza jeshi la Polisi Tanzania kutojihusisha na shughuli za kusimamia masuala ya ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi badala yake kuundwe kikosi maalum cha cha uchaguzi chini ya Tume ya taifa ya Uchaguzi kitakachohudumu wakati wa mchakato wa uchaguzi pekee.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha maoni na mapendekezo ya maboresho ya miswaa mitatu (3), ambayo ni Mswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa mwaka 2023, Mswada wa sheria ya Uchaguzi wa Madiwani, wabunge na Rais wa mwaka 2023 na mswada wa marekebisho ya sheria ya mambo ya Vyama vya siasa ya mwaka 2019, ambao umewasilishwa Bungeni Oktoba 10,2023.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, amesema kwama, ni vizuri Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC), ikaunda kikosi maalum cha kusimamia masuala ya usalama na ulinzi wakati wa uchaguzi, ambapo wahusika watajengewa uwezo namna ya kulinda usalama wa raia wote bila kusababisha changamto za uvunjivu wa Amani.

“.. Masuala ya ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi ni lazima yajitokeze bayana katika sheria hii ili kudhibiti vitendo vya uvunjivu wa Amani, Tunapendekeza kifungu kipya cha 69 (1) kutakuwa na kikosi maalum cha Polisi watakaofanya kazi ya kulinda Amani na Utulivu wakati wote wa uchaguzi, kifungu cha 169 (2) Tume iwapatie mafunzo polisi wote wa kikosi cha Uchaguzi kuhusu masuala ya mchakato wa uchaguzi ikiwepo unyanyasanji na udhalilishaji wa kijinsia”, alisema Lilian

Pia, TGNP imependekeza kwamba, kuwepo kwa kifungu kipya cha 169 (3) kitakachosomeka kwamba, Polisi wa kikosi cha uchaguzi watakula kiapo cha uaminifu, na uadilifu mbele ya Hakimu wa mahakama ya mwanzo kabla ya kuanza majukumu ya kulinda usalama kwenye uchaguzi,

Pendekezo lingine ni kwamba kuwepo na kifungu cha 169 (4) ambapo Kikosi cha Polisi cha Uchaguzi kitaundwa kwa misingi ya uwiano wa Kijinsi yaani wanawake na wanaume hasa vijana wa kike na kiume.
Share:

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA




Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza na wadau wa uvuvi kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Kasanga Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, akibainisha juu ya utekelezaji wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba katika Ziwa Tanganyika baada ya mpango huko kufanya vizuri Ziwa Victoria. Serikali imetenga Shilingi Bilioni 20 kwa ajili uwekaji vizimba katika Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika.

Na, Edward Kondela

Serikali imeanza utekelezaji wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba katika Ziwa Tanganyika baada ya mpango huo kuonesha mafanikio makubwa katika Ziwa Victoria.

Akizungumza katika Mwalo wa Kasanga uliopo Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amesema tayari wizara imeanza kutoa elimu kwa wavuvi wa ukanda wa Ziwa Tanganyika kabla ya kufikisha vizimba hivyo na mbegu bora za samaki.

Mhe.Mnyeti ameongeza kuwa kwa sasa serikali imetenga Shilingi Bilioni 20 kwa ajili uwekaji vizimba katika Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa sababu ufugaji wa samaki unakua kwa kasi maeneo mbalimbali duniani kutokana na upungufu wa samaki waliopo kwenye maji ya asili yakiwemo mabonde, maziwa, mito na bahari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya uharibifu wa mazingira, ongezeko la watu na uharibifu wa mazalia ya samaki.

Ameongeza kuwa ili kunusuru upungufu wa samaki katika masoko ya ndani na nje ya nchi serikali imeamua kuanza kusambaza vizimba kwa wavuvi wa Ziwa Tanganyika ambavyo vitatolewa kwa mkopo nafuu usio na riba.

Awali akiwa katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alipokutana na mkuu wa mkoa huo Mhe. Charles Makongoro Nyerere alimueleza azma ya serikali ya kulipumzisha Ziwa Tanganyika katika shughuli zozote za uvuvi kwa kipindi cha miezi mitatu kila mwaka kwa miaka mitatu mfululizo ambapo kwa mwaka huu litafungwa kuanzia tarahe 15 mwezi Mei hadi 15 mwezi Agosti 2024 ili kupisha samaki waweze kuzaliana.

Amesema kupumzishwa kwa shughuli za uvuvi katika ziwa hilo ni utekelezaji wa Mkataba wa Kikanda wa Usimamizi wa Uvuvi endelevu katika ziwa hilo na bonde lake ambapo nchi wanachama wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika kwa maana ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokeasia ya Kongo, Tanzania na Zambia zilitia saini mkataba huo Tarehe 9 Mwezi Desemba Mwaka 2021 kwenye mkutano wa 9 wa mawaziri wa nchi hizo.

Amebainisha kuwa kupumzishwa kwa ziwa hilo kutatoa fursa kwa wavuvi kujifunza namna bora ya kufuga samaki pamoja na kuwa na njia nyingine za kujipatia kipato zikiwemo za kufuga mifugo na kilimo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Charles Makongoro amesema mpango wa serikali kuhamasisha kufuga samaki kwa njia ya vizimba ni mzuri kwa kuwa wavuvi watapata fursa ya kujifunza namna nyingine ya kuendeleza biashara ya samaki na kwamba mkoa utasimamia utekelezaji huo ili wananchi waendelee kunufaika na mazao ya uvuvi.

Baadhi wananchi wanaofanya shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti katika Kata ya Kasanga, wamepongeza juhudi za serikali kwa kuwatafutia njia mbadala ya kuendeleza Sekta ya Uvuvi na kuiomba serikali kuzidi kutoa elimu zaidi juu ya ufugaji kwa njia ya vizimba.

Aidha, wamekiri kwamba kwa sasa mazao ya samaki yamepungua kwa kiasi kikubwa katika ziwa hilo na samaki wanaopatikana ni wadogo ambao wanahitaji kubakia ziwani ili kukua.

Naibu Waziri Mnyeti amepata pia fursa ya kushuhudia maendeleo ya ujenzi wa soko la samaki katika Kata ya Kasanga linalogharimu Shilingi Bilioni 1.4 na kuwataka wananchi hao mara soko litakapokamilika ni vyema wakaliendesha wao wenyewe na kulifanya la kisasa zaidi.
Share:

Friday, 12 January 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 13, 2024


Share:

TAASISI ZA KIFEDHA ZASHAURIWA KUJA NA PRODUCTS ZITAKAZOSAIDIA WAFANYABIASHARA WADOGO HANANG’





Mkurugenzi wa Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Condrad Millinga akizungumza wakati wa kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Tarehe 11 Januari 2024. Aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe. Janeth Mayanja.


Ikionesha baadhi ya wafanyabiashara Wilayani Hanang’ katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara Tarehe 11 Januari 2024.
Mwenyekiti wa Soko la Hanang’ Bw. Mathia Jonisi akizungumza katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Mnyara Tarehe 11 Januari 2024.



Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Tarehe 11 Januari 2024.




Bw. Godfrey Chacha Afisa Vijana Mwandamzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Tarehe 11 Januari 2024.



NA; MWANDISHI WETU HANANG’

Taasisi za kifedha Hususani Mabenki, yameshauriwa kuja na Dirisha maalum na Products zitakazosaidia wafanyabiasha wadogo walioathiriwa na maafa ya maporomoko ya tope, miti na mawe yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana Wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara.

Hayo yamesemwa tarehe 11 Januari 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Bi Janeth Mayanja alipokutana na Wafanyabiashara wilaya hiyo na wawakilishi wa mabenki na Taasisi za kifedha katika Mkutano wa Mafunzo Ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC).

Bi. Mayanja alisema ni wakati sasa kwa mabenki kuwafikiria wafanyabiashara wadogo wasiyo na mali ya kuweka rehani katika kupata mikopo yenye unafuu kuja na Products zitakazowawezesha wafanyabiasha hao kukopesheka kwa riba nafuu kwani wafanyabiashara hao wanakopa kwenye taasisi nyigine za kifedha zenye masharti magumu na kwa watu binafsi na wanaweza kulipa.

“Inawezekana mikopo hivyo kwa mabenki ikaonekana ni midogo midogo kwa sababu wafanyabiahara hao ni wengi lakini bado mabenki yanaweza kupata faida, tukiendelea kijikita kwa wafanyabiashara wakubwa wenye mali za kuweka rehani maendeleo ya watanzania wanaojikita kwenye biashara ndogondogo yatachelewa.” Alisema Mhe. Mayanja

Kwa wakati huo huo Banki ya NMB imekabidhi hundi ya fedha ya Tsh 269,000,000 (Milioni Mia Mbili sitini na tisa) kwa Waathirika kumi na nane wa maporomoko ya Mlima Hanang , ambapo fedha hizo ni sehemu ya fidia kwa wateja wa Benki hiyo waliokata Bima kwenye Biashara na Bima za Mikopo Kupitia Bank ya NMB, na imeelezwa kuwa Benki hiyo itaendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa Bima.



Awali Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo Wilayani Hanang’ kuchangamkia fursa zitakazotolewa na mabenki hayo na kuachana na mikopo yenye masharti kandamizi ili kuwainua kiuchumi.
Share:

BUNGE LAPITISHA SHERIA KUKOMESHA ULAJI NYAMA YA MBWA


Bunge la Korea kusini limepitisha sheria mpya ambayo imeonekana kuwa mtihani kwa walaji na watumiaji wa nyama ya mbwa.

Sheria hiyo ambayo imelenga kukomesha uchinjaji na uuzaji wa nyama ya mbwa, Desturi ambayo imekuwa ikitumika kwa wananchi wa Korea kusini kwa zaidi ya karne hivi sasa.

Na kwa ambaye atapatikana kujihusisha na biashara ya kuuza na kununua mbwa kwa lengo la kitoweo, basi adhabu kali ikiwemo kifungo itaambatana naye.

Chanzo: BBC
Share:

TPA YAPONGEZWA KWA UFANISI WA HUDUMA ZAKE


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA imepongezwa kwa utendaji wenye ufanisi mkubwa na kutakiwa kuongeza juhudi ili kupata mafanikio zaidi na kuongeza mchango wa Sekta ya Bandari katika Uchumi wa Taifa.

Pongezi hizo zimetolewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali waliotembelea Banda la TPA katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Zanzibar yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya maonesho vya Fumba, Zanzibar.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema, Sekta za Viwanda na Biashara zinaitegemea sana Sekta ya Uchukuzi katika kufanikisha mipango yake ya kuhudumia Wananchi na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Bidhaa zinazozalishwa na Wajasiriamali na Viwanda vyetu vya ngazi zote, vinahitaji sana uhakika wa kupata malighafi na uhakika wa kuyafikia masoko ya ndani na nje ya Nchi. Tunaipongeza TPA na Taasisi nyingine za Uchukuzi kwa kazi kubwa ya kuwezesha Wananchi kupata tija katika shughuli zao za uzalishaji na Biashara ya mazao na bidhaa zinazozalishwa katika Sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara ameipongeza TPA kwa kushiriki maonesho yanayoendelea na kwa mafanikio makubwa ya kuhudumia Meli na Shehena katika nusu ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/2024.

‘Nimefurahi kwanza kwa kushiriki kwenu katika maonesho haya ambapo tunaungana na Watanzania wenzetu wa upande wa Visiwani kutafakari kwa pamoja namna bora ya kuongeza ufanisi wa huduma zetu kwa Wananchi na Wanufaika wengine. TPA na ZPC mnafanya kazi nzuri katika Sekta ya Bandari lakini bado zipo fursa za kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na ndio maana Serikali zote mbili zinafanya jitihada kubwa za kuwezesha ufanisi huo kupatikana.

Natoa wito kwa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TPA kusimamia kikamilifu mipango yenu mliyojiwekea ambayo ikitekelezwa vyema, shughuli za Bandari zitakuwa na mchango mkubwa zaidi katika Pato la Taifa na Maendeleo ya Nchi yetu kwa ujumla’

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ally Possi amesema, ushiriki wa TPA katika maonesho haya ya Zanzibar ni fursa muhimu ya kukuza ushirikiano kati ya TPA, ZPC na Taasisi nyingine ili kubadilisha uzoefu na kukutana na Wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa Huduma zinazotolewa na Taasisi hizi.

“TPA mnafanya kazi kubwa sana, mnastahili pongezi, lakini haitoshi sisi viongozi kujua kuwa mnafanya vyema, Wananchi nao wanastahili kujua hivyo. Tumieni wasaa huu kuwaelimisha, toeni ufafanuzi wa kina kuhusu maswali yao na pokeeni hoja na ushauri wao, kwa kufanya hivyo mtakuwa mmetimiza vyema wajibu wenu wa kushiriki katika tukio hili muhimu ambalo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Akizungumza katika mapokezi ya Viongozi hao kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TPA Bw. Nicodemus Mushi amesema, tumefurahi kupata wasaa wa kukutana na Wananchi wa Tanzania Visiwani na tunaendelea kuwapa Elimu kuhusu utendaji wa Sekta ya Bandari upande wa Bara pamoja na mipango ya kuboresha Huduma katika eneo la Majahazi katika Bandari ya Dar es Salaam ambalo linahudumia Abiria na Mizigo inayosafiri kati ya Tanzania Bara na Visiwani.

Bw. Mushi ameongeza kuwa, TPA tumejipanga vyema kuboresha Miundombinu yake katika eneo hilo pamoja na kufanya marejeo ya Kanuni zinazosimamia utoaji huduma za Bandari ili kuondoa kero zinazolalamikiwa na Wateja na Wadau wake.

‘Katika kipindi kifupi kijacho, TPA itafanya uchimbaji wa kuongeza kina katika eneo la majahazi ili Vyombo vinavyotumia eneo hilo viweze kutoa huduma kwa ufanisi wakati wote, tumejipanga pia kuimarisha gati la Abiria na Miundombinu ya ukaguzi wa bidhaa bandarini ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma katika eneo hilo, Amesema Bw Mushi.

Katika kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 (Julai- Desemba, 2023) Bandari za TPA zimehudumia jumla ya tani 13.945 Milioni sawa na asilimia 109.4 ya lengo la kipindi husika la kuhudumia tani 12.752 Milioni ambapo bandari ya DSM imehudumia jumla ya tani 12.052 milioni.

Katika kipindi husika bandari za TPA pia zimehudumia jumla ya makasha 536,683 TEUs sawa na asilimia 105.8 ya kuhudumia makasha (TEUs) 507,212 ambapo bandari kuu ya DSM imehudumia makasha (TEUs) 509,594.

Aidha, TPA ilijiwekea lengo la kuhudumia magari 102,500 katika bandari ya Dar es Salaam ambapo hadi kufikia mwezi Desemba, 2023 TPA ilikuwa imehudumia 106,823 sawa na asilimia 104.2 ya lengo la kipindi husika.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger