Friday, 5 January 2024

RUWASA KISHAPU YAKUTANA NA WADAU WA MAJI, DC MKUDE AMSHUKURU RAIS SAMIA KUPELEKA FEDHA NYINGI MIRADI YA MAJI

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kishapu umeendesha Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maji na usafi wa mazingira.

Mkutano huo umefanyika leo Ijumaa Januari 5,2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maji wilayani Kishapu ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo, Mhe. Mkude ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi wa Kishapu.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kutuletea miradi ya maji yenye pesa nyingi. Tunaipongeza sana serikali kwa kutuletea maji Kishapu, hivi sasa hali ya upatikanaji wa maji inaridhisha tofauti na miaka ya nyuma”,amesema Mkuu huyo wa wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude.

Aidha Mkude amewataka wananchi kulinda na kutunza miradi akisisitiza kuwa ni jukumu la kila mwananchi kutunza miradi ya maji.

“Ni jukumu letu kuhakikisha miradi hii inatunzwa. Mtu yeyote anayehujumu miundombinu ya maji achukuliwe hatua, tusimuonee huruma mtu yeyote anayeharibu miradi ya maji. Tuendelee kutunza miradi hii kwani ni rasilimali muhimu sana duniani inayozidi hata mafuta”,ameongeza.

Katika hatua nyingine amewakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia huduma za maji na kuachana na mtazamo hasi kwamba huduma ya maji inatolewa bure.

Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima amesema lengo la mkutano huo ni kuwaleta pamoja wadau wa maji katika Wilaya ya Kishapu ili kuweza kutathmini, kubadilishana uzoefu na kujadili mafanikio na changamoto katika hutoaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

“Matumizi ya maji hayana mbadala hivyo sisi sote tunalo jukumu la kutunza mazingira ili vyanzo vya maji visiharibiwe, laikini pia tunalo jukumu la kutunza miundombinu ya maji kwenye maeneo yetu ambapo miradi ya maji inajengwa ili iweze kuwa endelevu na kutoa huduma ya maji kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na tunalo jukumu la kuchangia gharama za uendeshaji na matengenezo ya skimu za maji kwenye maeneo yetu, ili huduma ya maji endelee kupatikana muda wote”,amesema Mhandisi Kamazima.

Aidha amewaomba wadau wa maji wote wakawe mabalozi wazuri kwa wananchi hasa kwa suala ya kuchangia gharama za uendeshaji na matengenezo ya skimu za maji.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima 
“Ukweli ni kwamba hakuna maji ya bure kama ilivyozoeleka kwa wananchi wetu, kwa sababu uzalishaji wa maji unahitaji gharama kama vile gharama za umeme na madawa, kwa hiyo lazima kuchangia gharama hizi ili miradi yetu iweze kuwa endelevu na kutoa huduma kwa wananchi wetu”,amesema Mhandisi Kamazima.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akishauri kuwe na ushirikiano wa karibu kati ya viongozi katika kutunza miradi ya maji

Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela ametahadharisha wanaotoboa mabomba ya maji kwamba yana Presha kubwa waijaribu kufanya michezo hiyo ili kuepusha majanga

“Naomba viongozi tuchukue hatua kwa wananchi wanaoharibu miundombinu ya maji ili kuepusha majanga yanayoweza kujitokeza mfano watu kupoteza maisha”,amesema Mhandisi Payovela.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela
 
Mhandisi Payovela pia amehamasisha watumiaji wa huduma za maji kulipia ankara za maji kwa wakati huku akiwashauri wananchi watumie maji safi na salama kupitia miradi ya maji.

"Naomba tuhamize wananchi kutumia maji safi na salama yaliyotengenezwa kupitia miradi ya maji",amesema Payovela.

Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kishapu (OCD), Esther Gesongwe ameitaka RUWASA na wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa pindi zinapojitokeza changamoto ikiwemo uharibifu wa miundombinu.

“Pia acheni kuchanganya siasa kwenye mambo ya maji, mtu aharibu miundombinu ya maji anakamatwa halafu anakuja mtu anasema huyu ni mpiga kura wangu muachie, hii hapana”,amesema Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Joel Ndettoson  ametaka viongozi wa vijiji na kata kuwa na ushirikiano katika kuwabaini watu wanaoharibu miundombinu ya maji na kuwachukulia hatua za kisheria.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala ameagiza watendaji kushughulikia wote wanaoharibu miundombinu ya maji kwani ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha miundombinu inalindwa na kutunzwa huku akiziomba taasisi zenye madeni kulipia huduma ya maji.

Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Neema Mwaifuge amesema suala la kutunza na kulinda miundombinu ni wajibu wa kila mwananchi.

Nao washiriki wa mkutano huo wameomba mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua kali wale wanaoharibu miundombinu hususani katika eneo la Ng'wang’holo na Busongo ambapo mabomba yamekuwa yakiharibiwa na wananchi.

Pia wameshauri kuwa wananchi wanapaswa watambue kuwa miradi ya maji siyo ya serikali bali inatokana na wananchi wenyewe waitunze ili iwe endelevu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza leo Ijumaa Januari 5,2024 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kishapu kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maji na usafi wa mazingira. Picha na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Neema Mwaifuge akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Wadau wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Meza kuu wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Meza kuu wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Wadau wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Kishapu, Godfrey Mbussa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Joel Ndettoson akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Kishapu, Gven Noah akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kishapu (OCD), Esther Gesongwe akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Share:

TBS YAINGIA MAKUBALIANO NA JESHI LA POLISI KUKAGUA MAGARI YANAYOTUMIKA NCHINI

Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji wakisaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.

*************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Jeshi la Polisi ili kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kutekeleza azma ya kuendelea kulinda Maisha ya watanzania kwa kuhakikisha kuwa ukaguzi wa magari wakati yanapotumika hapa nchini unaofanyika kwa mujibu wa Sheria ya Trafiki (yaani Road Traffic Act, Cap 168), unafanyika kwa kutumia mitambo ya kisasa ili kuthibitisha usalama wake.

"Kwa kuzingatia uwezo uliopo,TBS itatumia wataalam wake, viwango pamoja na mitambo ya kisasa katika kukagua na kupima magari yote yatakayoletwa na Jeshi la Polisi, Kitengo cha  Trafiki kwa ukaguzi kwa mujibu wa Sheria Usalama Barabarani Sura 168 ambayo inalazimu kufanyika ukaguzi wa vyombo vya moto ili kuhakikisha vinakidhi matakwa ya vigezo vya usalama kwa lengo la kulinda usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara". Amesema 

Aidha amelihakikishia jeshi la polisi  kwamba TBS ni mshirika sahihi wa Jeshi la Polisi Tanzania, kwani ndiyo inayodhibiti ubora na usalama wa vyombo vya moto vinavyoingia nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji amesema kupitia makubaliano hayo wanatarajia usalama barabarani kuimarika zaidi kwa watumiaji wa barabara.

"Tukiwa na Vyombo vya Moto salama tutakuwa na watumiaji salama wa barabara, tutakuwa na barabara salama na pia shughuli za uokozi zinaweza kuimarishwa na mwisho tutakuwa na tumeimarisha uongozi katika usalama barabarani". Amesema 

Amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa Maelekezo ya Tume ya Haki Jinai inayosisitiza kushirikiana na wadau mbalimbali katika usimamizi wa sheria za usalama barabarani ili kuzuia uhalifu barabarani.

Pamoja na hayo amewataka wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha wanatimiza wajibu wa kisheria wa kukagua vyombo vyao kama inavyoelekezwa katika sheria kwani jeshi la polisi litakuwa na muhari kwa watakaoshindwa kutii sheria bila shuruti.

Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akibadilishana mikataba na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji mara baada ya kusaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji wakionesha mikataba mara baada ya kusaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Makamishna wa Polisi wakifuatilia hafla ya utiaji saini Makubaliano (MoU) kati ya Jeshi la Polisi na Shirika la Viwango Tanzania katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wakurugenzi na watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakifuatilia hafla ya utiaji saini Makubaliano (MoU) kati ya Jeshi la Polisi na TBS katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi wakipata picha ya pamoja na Wakurugenzi na watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Makamishna wa Polisi katika hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi wakipata picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani katika hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi wakipata picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna wa Jeshi la Polisi katika hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TBS na Jeshi la Polisi katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Share:

PROF. NDALICHAKO ASISITIZA CMA KUJA NA MFUMO KIDIGITALI WA KURAHISISHA USULUHISHI NA UAMUZI

Na; Mwandishi Wetu - Morogoro

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kuja na mfumo wa kidigitali ambao utarahisisha usuluhishi na utatuzi wa migogoro.

Prof. Ndalichako amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha tathimini ya utendaji kazi wa tume hiyo na mafunzo kilichofanyika leo tarehe 4 Januari, 2024 mkoani Morogoro.

Ameeleza kuwa, mfumo huo utasaidia kufanya utatuzi wenye haki na kwa wakati na pia kupunguza mrundikano wa kesi.

Kwa upande mwengine amewataka watumishi wa ofisi hiyo kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidii na waledi ili kuimarisha uchumi wa wananchi pamoja na taifa kwa ujumla.

Pia, amewasisitiza kila mtumishi katika ofisi hiyo kushiriki katika mafunzo hayo kwa kuwa yanalenga kuleta maendeleo na mahusiano mazuri katika utendaji kazi wao.

Naye, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose Mlyambina amesema Tume inatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na mahakama ili kuweza kupunguza mlundikano wa mashauri, kwani Uchumi utakua kwa kasi na uwekezaji utaongezeka ukichochewa na huduma bora za utoaji haki hususani haki kazi.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekerege Mpulla amesema kuwa CMA itahakikisha ina anzisha mfumo wa kidijitali ambao utawawezesha watumishi kufuatilia taarifa na kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger