Friday, 29 December 2023

VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA VYATOA MREJESHO WA UCHAMBUZI WA BAJETI KIJINSIA HALMASHAURI YA KISHAPU… VYAPONGEZA SEKTA YA ELIMU NA AFYA, MAJI BADO




Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Kishapu vimefanya Kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo vimepongeza hatua kubwa zilizofanywa na Halmashauri hiyo katika utengaji wa bajeti ya mrengo wa kijinsia katika sekta ya elimu, kilimo na afya huku vikionesha kutoridhishwa na bajeti katika sekta ya maji iliyopangiwa bajeti ndogo katika mwaka wa fedha 2023/2024 wakati uhitaji wa maji bado ni mkubwa.

Kikao hicho kilichokutanisha pamoja Viongozi wa Vituo 9 vya taarifa na maarifa  wilaya ya Kishapu na Maafisa na Wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kimefanyika leo Ijumaa Desemba 29,2023 Wilayani humo.

Akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo vya taarifa na maarifa, Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila amesema malengo ya uchambuzi huo ni pamoja na kupongeza juhudi za serikali katika kutatua kero za wananchi kupitia utekelezaji wa bajeti za shughuli za maendeleo.


“Lengo la uchambuzi huu wa bajeti kijinsia pia ni kuishauri serikali kuhusu vipaumbele vya kibajeti vyenye manufaa kwa jinsia zote (mwanamke na mwanaume), kubainisha changamoto za utekelezaji wa bajeti na kushauri serikali kuhusu sera na Program mbalimbali zenye manufaa kwa jinsia zote ndani ya nchi pamoja na kujua ni kundi gani ndani ya jamii linaguswa moja kwa moja na utekelezaji wa bajeti na kushauri serikali kuhusu jinsi ya kuyafikia makundi yaliyoachwa nje”,amesema Abila.
Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila.

Abila amesema katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, jumla ya shilingi Bilioni 12 (12,997,010,000/=) zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwa ni ongezeko la asilimia 3 kutoka bajeti yam waka 2022/2023 (Shilingi 12,651,769,415.98/=) ambapo 7.3% ya pesa zilizotengwa zimepokelewa hadi Septemba 2023 na 49% ya fedha zilizopokelewa zimetumika hadi Septemba 2023.

“Tunaipongeza sana Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kuongeza bajeti kwenye Sekta za vipaumbele ikiwemo afya imetengewa 22.43%, elimu 56.08%, Kilimo/mifugo 3.69%. Lakini Maji bajeti ni kidogo sana 0.23%”,ameongeza.

Akielezea kuhusu Sekta ya Afya licha ya kwamba bajeti imezingatia mrengo wa kijinsia inayotoa kipaumbele kwa afya za akina mama na watoto wachanga,dawa,vifaa tiba,zahanati,mama na mtoto, watumishi wa afya na miundombinu ya afya kwa kuidhinishiwa shilingi 3,478,048,389.92/=, bado ni ndogo ukilinganisha na mahitaji ya huduma za afya wilayani Kishapu.


“Kwa upande wa vipaumbele vya elimu ikiwemo matundu ya vyoo mashuleni,mabweni na miundombinu Rafiki kwa watoto wenye uhitaji maalumu vipaumbele vya bajeti vinashabihiana na vya TGNP na wadau wa vituo vya taarifa na maarifa. Hapa tunaipongeza serikali kutekeleza bajeti yenye mrengo wa kijinsia jumuishi”,amesema Abila.
Viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakiwa kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia.

Hata hivyo amesema mabweni bado ni changamoto katika shule nyingi wilayani Kishapu hali inayohatarisha usalama wa watoto wa kike wanaotembelea umbali mrefu kwenda shuleni, pia baadhi ya wazazi kushindwa gharama za bweni na ukosefu wa madaraja, vivuko vya mito hasa sehemu za Mwadui Luhumbo hali inayosababisha watoto kuacha kwenda shule wakati wa mvua kubwa.


Akielezea kuhusu sekta ya kilimo/ufugaji amesema vipaumbele vimeegemea zaidi kwenye ufugaji badala ya kilimo cha mazao na kwamba ushuru wa mazao unaokatwa haunufaishi wakulima hasa wanawake na mikopo ya zana za kilimo zina gharama kubwa na siyo rafiki kwa mkulima mdogo.

Katika hatua nyingine ameipongeza serikali kwa kuwapa kipaumbele wanawake kumiliki ardhi.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ibrahim Sakulia.

Aidha amesema katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu changamoto ya maji bado ni kubwa kwani yanapatikana kwa umbaili mrefu kwa baadhi ya maeneo mfano kata ya Kiloleli wanatembea umbali wa kilomita 15 kupata maji, Mwadui Luhumbo maji yamepita kwenda Kishapu Mjini wananchi hawana maji na bei kubwa za maji.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ibrahim Sakulia amesema wamezipokea changamoto zilizojitokeza katika mrejesho wa uchambuzi wa bajeti ya kijinsia na kwamba watazifanyia kazi.

Sakulia ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kushiriki katika michakato ya bajeti kwa kushiriki vikao na mikutano mbalimbali inayofanywa katika ngazi ya vijiji ili watoe maoni yao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Kishapu, Fredina Said.

Kwa upande wake, Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Kishapu, Fredina Said amesema wananchi wanataka bajeti inapotengwa iwe na mrengo wa kijinsia ili kuhakikisha hakuna mtu anaachwa nyuma katika jamii.

“Tunatamani kuona bajeti inatengwa ili ikatatue changamoto za jamii. Bajeti inapotengwa ije kwenye jamii, tunaamini mabadiliko yatatokea. Na sisi wana jamii tusisubiri kila kitu kifanywe na serikali mfano tuhamasishane watoto wapate chakula shuleni ili wasome kwa furaha”,amesema Fredina.

“Kishapu ni Halmashauri ambayo imekuwa mfano mzuri katika utengaji wa bajeti ya mrengo wa kijamii kwa ajili ya kutatua changamoto za kijamii. Tunaipongeza sana kwa kuwa na vipaumbele vya mrengo wa kijinsia”,ameongeza.

Aidha ameshauri kuanzishwa kwa jukwaa la wakulima wadogo ili kuwa na sauti ya pamoja ili kilimo kiwe na tija huku akihamasisha matumizi ya mbolea za asili katika kilimo kwani ni salama na upatikanaji wake ni rahisi.

Naye Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, John Mchele amesema wanaendelea kukazia mafunzo kwa wakulima na maafisa ugavi kuhusu matumizi ya mbolea za asili huku akiwahamasisha wakulima kuchangamkia fursa ya kupimiwa udongo ili kujua lishe ya udongo ili wajue wanapozalisha, wanazalisha kwa kiwango gani na zao gani linafaa kwa udongo huo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo 9 vya taarifa na maarifa Wilaya  ya Kishapu leo Ijumaa Desemba 29,2023 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo 9 vya taarifa na maarifa Wilaya  ya Kishapu
Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo 9 vya taarifa na maarifa Wilaya  ya Kishapu
Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo 9 vya taarifa na maarifa Wilaya  ya Kishapu
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Kishapu, Fredina Said akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Kishapu, Fredina Said akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Kishapu, Fredina Said akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ibrahim Sakulia akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ibrahim Sakulia akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakiwa kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu 
 Kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kikiendelea
Maafisa na Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu 
Maafisa na Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu 
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, John Mchele akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu  
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, John Mchele akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu 
 
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joyce Mathias akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu  
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Shoma Richard Sitta akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu 
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mtwangi Mwipola akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu 
Washiriki wa kikao cha mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakipiga picha ya kumbukumbu
Washiriki wa kikao cha mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

ADC YAJIWEKA MGUU SAWA UCHAGUZI WA 2024/2025


Na Oscar Assenga,TANGA

CHAMA cha Alliance For Democratic Change (ADC-Dira ya Mabadiliko ) kimeanza kujiweka sawa kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na ule Mkuu mwaka 2025 baada ya kutangaza kufanyika kwa uchaguzi wa ndani wa chama hicho kwa mwaka 2024.

Akizungumza leo Katibu Mkuu wa ADC Taifa Doyo Hassan Doyo (Pichani kulia) alisema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho toleo la tatu la mwaka 2019,Uchaguzi wa viongozi ndani ya chama hufanyika kila baada ya miakaa mitano.

Alisema kwamba tamko hilo linaonyeshwa katika katiba yao kwenye sura ya nane ibara ya 53(i) “Ukomo wa uongozi ni miaka mitano” na sasa ni wakati wa kufanyika chaguzi ambazo zitawapa fursa ya kupatikana viongozi wapya katika ngazi mbalimbali.

Katibu huyo alisema kutokana na chama kufanya uchaguzi ndani ya chama mnamo mwaka 2019 ambapo ulifanyika Mkutano mkuu mwezi Aprili katika ukumbi wa Hotel ya Madinat Bahri iliyopo Zanzibar.

Aidha alisema kwamba mwaka 2024 viongozi waliopo madarakani wanatimiza miaka mitano tangu kufanyika uchaguzi na mkutano mkuu husika kwa madhumuni ya kuchagua viongozi ambao wako madarakani hadi muda huu.

“Kwa kuzingatia utekelezaji wa miongozo kutoka katika katiba yetu Ofisi ya chama makao makuu inatoa ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho kwa mwaka 2024”Alisema Katibu huyo.

Katibu huyo alisema kwamba uchaguzi huo ngazi ya Tawi utaanza Januari Mosi hadi Januari 31 mwakani wakati ule wa kata utafanyika kati ya Februari Mosi hadi February 29 mwaka 2024 utakaokwenda sambamba na ule wa majimbo.

Alisema baada ya hapo kutafanyika chaguzi ngazi ya wilaya utaanza Machi 1 mpaka Machi 31 mwakani utakaoambatana na ule ngazi ya Kanda huku akiwataka wanachama kuchangamkoa fursa za kuwania nafasi mbalimbali.

Katibu huyo alisema baada ya hapo kutafanyika uchaguzi Mkuu wa chama chicho ambao unatarajiwa kwisha mwezi Mei mwakani na hatimaye kuweza kupata safu mpya za uongozi.

Hata hivyo Katibu huyo alitoa agizo kwa viongozi wote wa chama hicho nchi nzima kusimamia zoezi hilo kwa ufanisi na kushirikisha wanachama wote wa ADC ili kukamilisha chaguzi hizo kwa mafanikio.
Share:

WASHINDI WA TCAA FUN RUN WAAGWA UWANJA WA NDEGE WA JNIA WAKIELEKEA DUBAI


Mamlaka ya USafiri wa Anga nchini imeratibu zoezi la kuwaaga washindi watano wa mbio za kujifurahisha (FUN RUN) zilizofanyika Oktoba 29 jijini Dar es salaam zikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuundwa kwa TCAA.

Washindi hao walipata zawadi za tikteki kutoka kwa wadau wa Usafiri wa Anga ambao ni mashirika ya ndege ya Ethiopian Airlines, Kenya Airways na Fly Dubai ambapo wataelekea Dubai kwa mapumziko ya siku tano.

Akizungumza wakati wa kuwaaga, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA ambaye pia ni Meneja Mipango wa Mamlaka hiyo Bi. Mellania Kasese aliwapongeza washindi hao na kuyashukuru Mashirika yaliyotoa tiketi hizo kwa kutimiza ahadi hiyo na kuishukuru TCAA kwa kugharamia fedha za kujikimu kwa washindi hao wawapo katika mapumziko hayo.


"Ni siku ya sote kufurahia utimilifu wa zoezi hili kwa washindi wetu hawa watano ambao walipatikana miongoni mwa zaidi ya washiriki 300. Nawatakia safari njema na hii iendelee kuwa chachu ya kujali afya zenu lakini ikawe hamasa kwa wengine ili wajikite katika kuimarisha afya zao kwa mazoezi," amesema Mellania.


Meneja wa Shirika la Ndege la Ethiopia Bi. Seble Woldemariam amewapongeza washindi na kuwataka kutumia fursa hii kufanya utalii na kujifunza mengi mema na mazuri watakayojionea huko waendako.
Meneja Mipango TCAA Melania Kasese akizungumza na wanahabari wakati wa tukio la kuwaaga washindi wa TCAA FUN RUN waliojishindia tiketi za kuelekea Dubai ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Bw. Samuel Makalla mtumishi wa TCAA akielezea maandalizi aliyofanya kuelekea safari ya Dubai mara baada kuibuka mshindi wa TCAA FUN RUN kwenye Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Mtumishi wa TCAA Bw. Aidan Adrian ambaye ni miongoni mwa washindi akitoa shukrani kwa wote waliofanikisha zoezi hilo wakati TCAA FUN RUN iliyofanyika katika maadhimisho ya Miaka 20 ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) iliyopelekea kutangazwa mshindi wa mashindano hayo.
Mtumishi wa LATRA Bw. Lugano Mwasomola ambaye ni miongoni mwa washindi akitoa shukrani kwa wote waliofanikisha zoezi hilo pamoja nasafari hiyo ya kwenda Dubai wakati wa hafla ya kuondoka hapa nchini kuelekea Dubai.




Meneja wa Shirika la Ndege la Ethiopia Bi. Seble Woldemariam (katikati) akizungumza wakati wa kuwaaga washindi wa tiketi ya kuelekea Dubai ambapo Shirika hilo ni miongoni mwa wadau waliotoa tiketi moja wapo kwa mshindi.


Meneja Mipango kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Melania Kasese akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa tiketi ya kuelekea Dubai pamoja na viongozi wa Shirika la Ndege la Ethiopia pamoja na Emirate wakati wa kuondoka nchini kwa ajili ya kwenda kutembea Dubai.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 29,2023

Share:

Thursday, 28 December 2023

SERIKALI KUWANYANYUA VIJANA KIUCHUMI NA KIMITAJI - KATAMBI




Na: Mwandishi wetu - Mwanza

SERIKALI imeendelea kubuni Mikakati ya kuhakikisha Vijana wanapata ujuzi na fursa za kuwainua kiuchumi ili waweze kujiajiri na kuajiri wenzao.


Hayo yamebainishwa Desemba 27, 2023 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 15 la Umoja wa Vijana Wakatoliki wa Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu Tanzania (TMCS) Taifa, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.

Aidha, Mhe. Katambi amesema kuwa Serikali kwa kutambua mchango wa vijana katika ujenzi wa taifa vijana nchini wameendelea kunufaika kwa kupatiwa mafunzo ya kuendeleza ujuzi wao, kuboresha Mwongozo wa Utoaji Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) na kutenga maeneo katika Halmashauri kwa ajili ya shughuli za vijana.

Mhe. Katambi pia amewataka Vijana nchini kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zinazotolewa na Serikali.

Vilevile, amewasisitiza vijana wanaokidhi vigezo kuchangamkia nafasi za kazi 500, Kada ya Uuguzi kwa kutuma Maombi yao kupitia tovuti ya www.jobs.kazi.go.tz ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeingia makubaliano na Serikali ya Saudi Arabia pamoja na nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusu ajira za watanzania katika nchi hizo, mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31 Disemba, 2023.

Share:

Video Mpya : SHITUNGULU - UTANIKUMBUKA

Msanii Shitungulu anakualika kutazama Video ya wimbo wake mpya unaitwa Utanikumbuka
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger