Friday, 22 December 2023

RC MNDEME AKABIDHI MISAADA YA WANA SHINYANGA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WILAYA YA HANANG


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha misaada ya kibinadamu iliyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amekabidhi misaada hiyo leo tarehe 22 Desemba, 22,2023 kwa Mkuu wa wilaya ya Hanang Mhe. Janeth Mayanja.

Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Mhe. Mndeme amesema WanaShinyanga wanaungana na  Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa pole kutokana na janga lililotokea Hanang lililosababishwa mvua kubwa iliyoambana na tope, mawe na miti hivyo kupelekea vifo, mali kupotea, mifugo kufa, mashamba kuharibika, nyumba kuharibika.
"Sisi wana Shinyanga tukiwa sehemu ya Watanzania tulipoguswa na janga hili tulipokea kwa masikitiko makubwa, baada ya kupokea taarifa hii ya kusikitisha, wanashinyanga kwa mapenzi mema wakaona nao wamuunge mkono Mhe.  Rais Samia Suluhu Hassan lakini vile vile wawaunge mkono wananchi wengine kutoa pole kwa wananchi wa Hanang hivyo tumefika hapa katika mji huu wa Katesh kuwasilisha kwako mhe. DC pole zetu ili kuonesha mshimamano, umoja na kwamba tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu ambapo kwa wenzetu wa Hanang wanapitia",amesema Mhe. Mndeme.

"Kwa niaba ya wananchi wa Shinyanga ambao wamejitolea kutoa pole zao kwa ndugu zao wa Hanang, naomba nikakibidhi mifuko 1000 ya saruji, mchele kilo 700, unga wa mahindi kilo 355, unga lishe kilo 250,juisi katoni 500, chumvi pakti 90,sukari kilo 25,sabuni katoni 13,mafuta ya kula lita 5, viatu pea 43, nguo balo 30 kati ya balo hizo 27 zina nguo za wanaume na tatu nguo mchanganyiko”, amesema
“Misaada hii inatoka kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga ambao wamejitolea kwa mapenzi yao mema, wameguswa kwa namna moja au nyingine. Poleni sana wan Hanang, pole sana Mhe. Rais Samia, tuendelee kumuomba Mungu atuepushe na majanga haya, mvua tunaihitaji, tunaumuomba Mungu atuletee mvua yenye neema. Msaada tuliotoa ni mdogo ukilinganisha na madhara yaliyotokea tunaomba hiki kilichotolewa na wana Shinyanga mkipokee”,ameongeza Mhe. Mndeme.

Akipokea misaada hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Janeth Mayanja amewashukuru Wana Shinyanga kwa upendo,huruma, utu, ubinadamu na undugu wa kweli waliouonesha kwa wan Hanang akisisitiza pia wamemuunga mkono kwa vitendo mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Tunawashukuru sana Wana Shinyanga kwa misaada ya kibinadamu mliyotupatia, mmeongeza nguvu Hanang na vifaa hivi vya ujenzi mlivyotoa vitasaidia katika ujenzi wa makazi ya waathirika wa janga lililotokea”,amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara  Mhe. Janeth Mayanja kufuatia janga la mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang'. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha misaada ya kibinadamu iliyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikabidhi sehemu ya nguo zilizotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikabidhi sehemu ya nguo zilizotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara  Mhe. Janeth Mayanja akitoa neno la shukrani kwa wananchi wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara  Mhe. Janeth Mayanja akitoa neno la shukrani kwa wananchi wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara  Mhe. Janeth Mayanja akitoa neno la shukrani kwa wananchi wa Shinyanga
 Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakikagua mzigo walioleta Hanang'
Muonekano wa magari yaliyobeba misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Muonekano wa magari yaliyobeba misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Muonekano wa magari yaliyobeba misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakitembelea moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'
Katibu Tawala Wilaya ya Hanang' Mwl. Athuman Likeyekeye akiwaonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakitembelea moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme( katikati) Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakiwa katika eneo la Jorodom moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiangalia miongoni mwa mawe yaliyosukumwa na maji kutoka Mlima Hanang' hadi katika eneo la Jorodom moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiangalia miongoni mwa miti iliyosukumwa na maji kutoka Mlima Hanang' hadi katika eneo la Jorodom moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'

Share:

NCC : UWEPO WA SHERIA YA MAJENGO KUWEZESHA MFUMO WA PAMOJA USIMAMIZI WA UJENZI

 

Mhandisi Ujenzi katika Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Geofrey Mwakasenga ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 21,2023 Jijini Dodoma, wakati akielezea masuala muhimu kuhusu sheria ya majengo nchini ambapo NCC inaratibu uandaaji wake.
Mhandisi Ujenzi katika Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Geofrey Mwakasenga (kulia),akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 21,2023 Jijini Dodoma, wakati akielezea masuala muhimu kuhusu sheria ya majengo nchini ambapo NCC inaratibu uandaaji wake.

Na Okuly Julius-Dodoma

Mhandisi Ujenzi katika Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Geofrey Mwakasenga amesema uwepo wa sheria ya majengo nchini utawezesha kuwepo kwa mfumo wa pamoja wa usimamizi wa ujenzi wa majengo wenye uwezo wa kudhibiti uharibifu wa mazingira, ubora, usalama na afya.


Mhandisi Mwakasenga ameyasema hayo leo Desemba 21,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea masuala muhimu kuhusu sheria ya majengo nchini ambapo NCC inaratibu uandaaji wake.

"Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,iliamua uandaliwe mfumo Bora wa kisheria wenye kanuni na miongozo inayojitosheleza utakaotumika katika usimamizi wa Ujenzi wa majengo nchini, kwani kwa sasa Ujenzi wa majengo unasimamiwa na sheria nyingi mbalimbali, kwa kukosekana kwa Sheria Moja Maalum,hivyo kusababisha usumbufu katika uendelezaji wa majengo na gharama zisizo za lazima kwa waendelezaji Majengo," amesema Mwakasenge


Amesema baadhi ya sheria zinazosimamia ujenzi wa majengo nchini ni pamoja na sheria za mipango miji, afya na usalama mahali pa kazi, zimamoto na uokoaji, mazingira, ukandarasi na usajili pamoja na sheria zinazosimamia taaluma na wanataaluma katika fani ya za uhandisi, ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi.


“Sheria hizi zinatoa mwongozo katika baadhi ya maeneno na kuyaacha mengine bila usimamizi, jambo linaloifanya sekta ndogo ya ujenzi wa majengo inayohusiana pia na ubomoaji wa majengo kutosimamiwa ipasavyo,”amesema.


Ameongeza kuwa mbali na jukumu ambalo baraza hilo limepewa la kuratibu uandaaji wa sheria ya majengo pia wana majukumu mengine ya kisheria inayotekeleza ikiwemo kuhamasisha na kuweka Mikakati ya kukuza,kuendeleza na kupanua sekta ya Ujenzi nchini na kushauri Serikali juu ya Maendeleo ya Sekta ya Ujenzi nchini na kuandaa mapendekezo ya utekelezaji wake.


Jukumu lingine la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ni kutoa ushauri na msaada wa Kitaalamu kwa wadau wa Sekta ya Ujenzi kuhusu mambo yanayohusiana na sekta ya Ujenzi pamoja na kuratibu na kuwezesha utatuzi wa migogoro inayotokea katika miradi ya Ujenzi Kwa ufanisi.


Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ni Chombo kinachohusika na Uratibu wa Sekta ya Ujenzi nchini,pamoja na uchagizaji wa Maendeleo ya Sekta hiyo kwa ujumla,Baraza hili lipo kwa mujibu wa Sheria na lilianzishwa Mwaka 1979 kwa sheria ya Bunge Na 20,ambapo Baraza hilo likaanza kutekeleza majukumu yake rasmi mwaka 1981.
Share:

Thursday, 21 December 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 22,2023




Share:

NSSF, CMA WAINGIA MKATABA WA USHIRIKIANO UTAKAOCHOCHEA UTENDAJI WA TAASISI HIZO KATIKA KUWAHUDUMIA WANANCHI


Na MWANDISHI WETU, MOROGORO
Mfuko wa Taifa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umeingia mkataba wa ushirikiano na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), wenye lengo la kuongeza ufanisi baina ya taasisi hizo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo katika Ofisi za NSSF Mkoani Morogoro, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema ushirikiano huo ni nzuri na utachochea ukuaji wa taasisi hizo pamoja na kuboresha huduma.

"Sisi wote wanaNSSF na CMA tupo chini ya Waziri Mkuu ambapo zote tunasimamia sheria mbili ile ya NSSF na ya CMA, lakini mwisho wa siku sheria zote zina mahusiano kwani zinalenga waajiri na waajiriwa ambao wote tunahusika nao, na ndio maana lazima tushirikiane," amesema Mshomba.

Ametaja faida za uhusiano huo kuwa utachochea ukuaji wa usajili wa waajiri na waajiriwa na pia wataendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo uwezeshaji hususan CMA kufahamu vizuri masuala ya hifadhi ya jamii.

Naye, Mkurugenzi wa CMA, Usekelege Mpulla amesema majukumu makuu ya tume hiyo ni kusuluhisha na kuamua migogoro ya kazi Tanzania Bara, huku akibainisha kuwa miongoni mwa madai yanayowasilishwa katika tume hiyo ni pamoja na mwajiri kutowasajili wafanyakazi wake NSSF au kutowasilisha michango yao.

"Pamoja na migogoro mengine tunayoipokea, watu wanapokuja kuleta migogoro ya kikazi mojawapo wadau wetu yaani waajiri na waajiriwa wanakuja kuibua madai ya michango ya NSSF," amesema Mpulla.

Amesema makubaliano waliyosaini yamegusa maeneo matano. Miongoni mwa hayo ni kushirikishana taarifa, kuwa na mkakati wa pamoja wa kufikisha huduma za tume na kukusanya taarifa zitakazoenda NSSF na eneo la tatu ni uwezeshaji wa vikao vya tathimini pamoja na mafunzo ili kuwa na uelewa wa pamoja.

Mpulla amesema kuungana huko kutaleta tija kwa pande zote mbili, kutaleta ufanisi na kustawisha taasisi zote mbili kwa sababu zote zinawahudumia wadau wanaofanana.

Share:

VIONGOZI MAMLAKA YA MASOKO YA MITAJI BURUNDI WAFANYA ZIARA YA KIMAFUNZO TANZANIA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA CPA. Nicodemus Mkama akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kupokea ujumbe kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya nchini Burundi (CMA – Burundi) unaojumuisha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Timu ya Wataalamu kwa ajili ya kufanya ziara ya mafunzo ya siku tano.
******************

Na Mwandishi Wetu, 

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Tanzania imepokea ujumbe kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya nchini Burundi (CMA – Burundi) unaojumuisha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Timu ya Wataalamu kwa ajili ya kufanya ziara ya mafunzo ya siku tano.

Ujumbe huo utafanya ziara katika Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Kampuni za Usimamizi wa uwekezaji na watendaji wengine katika masoko ya mitaji huku ikielezwa ziara hiyo imelenga kujenga uelewa wa namna masoko ya mitaji yanavyoendeshwa.

Pia kuainisha masuala muhimu yatakayoiwezesha nchi ya Burundi kuwa na masoko ya mitaji imara, himilivu, yenye ufanisi na yatayowezesha kuwa na matokeo chanya katika kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi nchini Burundi kama ilivyo nchini Tanzania.

Akizungumza leo Desemba 20, 2023 jijini Dar es Salaam Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA CPA. Nicodemus Mkama amesema ujio wa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi, menejimenti na timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya nchini Burundi umetokana na mafanikio yaliyopatikana katika masoko ya mitaji hivi karibuni nchini Tanzania.

Ameongeza ambapo bidhaa mpya na bunifu zinazowezesha kupata fedha za kutekeleza shughuli za biashara na miradi ya maendeleo katika sekta ya umma na binafsi zimeidhinishwa na kuorodheshwa katika soko la hisa kwa mafanikio makubwa.

Amesema bidhaa hizo ni pamoja na hatifungani za kijani yaani green bond, hatifungani zenye mguso kwa jamii yaani social bonds, na hatifungani zenye kukidhi misingi ya Shariah yaani Sukuk bonds.

"Matokeo hayo yameiweka Tanzania katika ramani ya masoko ya mitaji ulimwenguni yanayotoa bidhaa mpya na bunifu, zinazovutia wawekezaji wa ndani ya nchi na kimataifa, " amesema CPA. Mkama.

Ameeleza Masoko ya Mitaji Tanzania ni miongoni mwa masoko yaliyopata mafanikio makubwa kiutendaji barani Afrika, katika kipindi cha hivi karibuni. "CMSA, ambayo ni Mamlaka yenye jukumu la kusimamia na kuendeleza masoko ya mitaji hapa nchini ...

" Imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza será na mikakati mbalimbali ya serikali ambayo imewezesha kufikia mafanikio hayo.Mamlaka imetekeleza mikakati ambayo imewezesha kuongeza thamani ya uwekezaji katika masoko ya mitaji.

"Ambapo thamani ya uwekezaji katika masoko ya mitaji imeongezeka kwa asilimia 7.6 na kufikia shilingi trilioni 36.13 katika kipindi kilichoishia Novemba 2023, ikilinganishwa na shilingi trilioni 33.59 katika kipindi kilichoishia Novemba 2022."

Akielezea mafanikio yaliyopatikana, CPA. Nicodemus Mkama amesema yametokana na mazingira wezeshi, shirikishi na endelevu ya kisera, kisheria na kiutendaji yanayotolewa na kuwezeshwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, sera za uchumi wa kidiplomasia na uhusiano wa kimataifa zinazotekelezwa chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia, zimekuwa chachu yenye matokeo chanya katika kukuza ushiriki wa wawekezaji wa ndani na wakimataifa na hivyo kuleta mafanikio makubwa zaidi katika masoko ya mitaji nchini Tanzania.

Hivyo kuvutia Mamlaka za masoko ya mitaji kutoka nchni nyingine kuja kupata mafunzo kwa lengo la kuimarisha na kuongeza ufanisi wa Taasisi katika nchi zao, kama ambavyo CMA Burundi wamekuja kujifunza CMSA Tanzania .

CPA. Mkama pia amesema, kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya Dunia kuhusu tathmini ya Utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani East African Common Market, Tanzania imepanda viwango vya alama za tathmini kwa asilimia 157 kutoka alama 7 hadi alama 18 kati ya 20 na kuwa miongoni mwa nchi zinazotekelezaji vizuri itifaki ya soko la pamoja kwenye masoko ya mitaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki .

Kwa sasa, Tanzania hakuna vikwazo vya ushiriki wa wawekezaji wa kigeni katika soko la hisa, hatifungani za kampuni na mifuko ya uwekezaji wa pamoja.

CPA. Mkama ameeleza katika kutumia fursa ya masoko ya mitaji ya ndani na ya kimataifa yanayowezesha kupatikana kwa fedha za kugharamia miradi na shughuli zinazochangia Utunzaji wa Mazingira, Maendeleo ya jamii na Utawala Bora CMSA imeidhinisha Kanuni za Soko la Hisa la Dar es Salaam yaani Stock Exchange Rules, ili kuwezesha uorodheshwaji na mauzo ya bidhaa hizo.

Maboresho hayo yameongeza mauzo na kuweka mazingira wezeshi kwa kampuni na taasisi kupata fedha za kugharamia shughuli za biashara na maendeleo.Aidha maboresho hayo yameongeza matumizi ya bidhaa na huduma, hivyo kuongeza ukwasi kwenye masoko ya mitaji.

CPA. Mkama pia alieleza CMSA imetekeleza mkakati wa kuwezesha utoaji wa Hatifungani za Serikali za Mitaa na Taasisi za Umma ili kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa (Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya) na Taasisi za Umma, ikiwa ni pamoja na Mamlaka za Maji na Mazingira kugharamia miradi ya kimkakati yenye uwezo wa kujiendesha kibiashara.

"Jitihada hizi ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Serikali wa njia mbadala za kugharamia miradi ya maendeleo katika sekta ya umma na binafsi uliozinduliwa na Waziri wa.Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu.

"Jitihada hizo zimeiwezesha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Tanga Tanga-UWASA kuwa Taasisi ya kwanza nchini kukidhi vigezo vya awali vitakavyoiwezesha kutoa hatifungani kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji na utunzaji wa mazingira.

Aidha, CPA. Mkama pia alieleza kuwa, Katika kuwezesha matumizi ya teknolojia, CMSA imeidhinisha mifumo ya Sim Invest na Hisa Kiganjani ambayo inawezesha kutoa huduma katika masoko ya mitaji kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuuza na kununua dhamana.

Hatua hiyo imewezesha kuongeza ushiriki wa wananchi mijini na vijijini katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja na soko la hisa.

Aidha, CMSA imeshirikiana na wadau kuandaa miongozo ya kuendesha na kusimamia bidhaa za mitaji halaiki yaani crowdfunding. Bidhaa hizi zitawezesha upatikanaji wa fedha kwa kampuni changa, ndogo na za kati.

Pamoja na hayo amesema CMSA itaendelea kujenga mazingira wezeshi na shirikishi ili kuwezesha taasisi katika sekta ya umma na binafsi kutumia masoko ya mitaji kupata fedha za kutekeleza miradi na shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuuza hisa kwa umma, hatifungani za miundombinu, hatifungani Rafiki wa mazingira, hatifungani za bluu na hatifungani za taasisi za Serikali.

Pia CMSA itaendelea kushirikiana na CMA – Burundi ili kufanikisha azma ya kuwa na masoko ya mitaji imara, yenye ufanisi na yanayochochea ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla katika jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya nchini Burundi (CMA – Burundi) Bwa.Allisen Mgenzi ameishukuru Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Tanzania kwa kuwapokea vizuri .

Bwa. Mgenzi amesema amekuja nchini Tanzania akiwa ameongozana na Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya CMA-Burundi,Menejiment na timu ya Wataalamu kwa ajili ya kufanya ziara ya Mafunzo ya siku tano katika Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) nchini Tanzania,Soko la Hisa la Dare es Salaam (DSE),kampuni ya Usimamizi wa Uwekezaji na Watendaji wengine katika masoko ya mitaji.

"ziara yetu imelenga kujenga uelewa wa namna masoko ya mitaji yanavyoendeshwa na kuainisha masuala muhimu yatakayoiwezesha nchi ya Burundi kuwa na masoko ya mitaji imara,himilivu,yenye ufanisi na itakayozesha kuwa na matokeo chanya katika kuchochochea ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi nchini Burundi kama ilivyo nchini Tanzani'',amesema Mgenzi.

Mgenzi ameushukuru Uongozi wa CMSA Tanzania kwa kuwapokea vizuri na kuwaonesha namna ambavyo CMSA ilivyofanikiwa katika suala zima la kukuza soko la mitaji nchini Tanzania,lakini pia ameishukuru Serikali ya Tanzania kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri na nchi ya Burundi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA CPA. Nicodemus Mkama akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kupokea ujumbe kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya nchini Burundi (CMA – Burundi) unaojumuisha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Timu ya Wataalamu kwa ajili ya kufanya ziara ya mafunzo ya siku tano.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya nchini Burundi (CMA – Burundi) Bwa.Allisen Mgenzi kuhusu ujio wao kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya nchini Burundi (CMA – Burundi) unaojumuisha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Timu ya Wataalamu kwa ajili ya kufanya ziara ya mafunzo ya siku tano nchini Tanzania.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger