Saturday, 9 December 2023

MIAKA 62 YA UHURU: ETE, HUDEFO WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI


Taasisi isiyo ya Kiserikali ya World Sustainable initiatives kwa kushirikiana, MBRC Tanzania, HUDEFO, Mazingira Plus, taasisi mbalimbali pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wamefanya usafi katika ufukwe wa bahari eneo la Geza Ulole ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru ambapo Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alielekeza katika maadhimisho haya kila Mkoa ufanye shughuli mbalimbali za kimaendeleo hii ikiwa ni moja wapo.

ETE pamoja na kushiriki kufanya usafi katika eneo hilo wanatumia Dijitali kuyasemea mazingira ambayo hayawezi kujisemea yenyewe, kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya mtandaoni kwa lengo la kufikisha ujumbe wa kukumbusha jamii kuendelea kutunza mazingira na kuyapenda ili yaendelee kuwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.


Picha na Fredy Njeje wa ETE insta @official.ete







Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 9, 2023

 

Magazeti ya leo Jumamosi
 
Share:

Friday, 8 December 2023

BYABATO ASHIRIKI MKUTANO WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI





Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Wakili Stephen Byabato(Mb) anashiriki Mkutano wa Pili, Kikao cha Pili cha Bunge la Tano la Afrika Mashariki, Kigali, Rwanda Bunge hilo linaendelea tangu Tarehe 23 Novemba,  2023 Mpaka 07 Disemba, 2023.

Katika Bunge hili miswaada mitatu itajadiliwa, hoja mbalimbali kwa maslahi ya Jumuiya zitajadiliwa pamoja na taarifa kutoka Kamati 6 zitajadiliwa na kutolewa maamuzi.
Share:

Picha : RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA HANANG... ATOA MAAGIZO JANGA LA MAFURUKO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Hanang kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Katesh Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023. Rais Samia alifika Katesh kwa ajili ya kuwapa pole wananchi wa maeneo hayo ambao wameathirika na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni.
Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Katesh Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.





Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye akiwa pamoja na viongozi wengine wakati wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Katesh Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger