Sunday, 5 November 2023
KEWANJA FC BINGWA LIGI YA BARRICK NORTH MARA MAHUSIANO CUP 2023... TIMU YA NORTH MARA FC YAANZISHWA
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele, akisaidiana na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kukabidhi kombe kwa kapteni wa timu ya Kewanja FC, Geofrey Emmanuel, baada ya kuibuka washindi wa Barrick North Mara Mahusiano Cup 2023,baada ya kuichapa timu ya Kerende FC bao 1-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime .
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele (wa pili kulia) akikabidhi kombe kwa Kapteni wa timu ya Kewanja FC, Geofrey Emmanuel baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa Barrick North Mara Mahusiano Cup 2023, baada ya kuichapa timu ya Kerende FC bao 1-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime .Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini,Mwita Waitara na kushoto ni Meneja Mahusiano wa Barrick North Mara, Francis Uhadi.
Wachezaji wa timu za Kewanja FC na Kerende FC, wakionyeshana ubabe uwanjani wakati wa mechi ya fainali ya ligi ya Barrick North Mara Mahusiano Cup iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime
Mashabiki na wachezaji wa timu ya Kewanja FC wakisherehekea ushindi baada ya kuibuka kidedea katika ligi ya Barrick North Mara Mahusiano Cup iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime .
Mashabiki na wachezaji wa timu ya Kewanja FC wakisherehekea ushindi baada ya kuibuka kidedea katika ligi ya Barrick North Mara Mahusiano Cup iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime.
Mashabiki wa soka wakifuatilia mechi hiyo ya fainali
Mashabiki wa soka wakifuatilia mechi hiyo ya fainali
Mashabiki wa soka wakifuatilia mechi hiyo ya fainali
Baadhi ya wachezaji walioshiriki ligi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Rais na Afisa Mtendaji wa Barrick, Mark Bristow (nyuma aliyevaa kofia) wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo mwezi Septemba mwaka huu
***
Mechi ya fainali ya soka ya ligi ya soka ya Barrick North Mara Mahusiano Cup, ilichezwa mwishoni mwa wiki katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe iliyopo katika kitongoji cha Nyamongo wilayani Tarime, ambapo timu ya Kewanja FC iliichapa Kerende FC bao 1-0 na kutetea ubingwa wa mashindano hayo kwa mara ya tatu mfululizo.
Mashindano ya Mahusiano Cup 2023, yalizinduliwa kwenye uwanja huo huo Septemba 29, mwaka huu na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow. Yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Mahusiano Bora kwa Uwekezaji Endelevu”.
Mgeni rasmi katika fainali hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mtenjele, ambaye alikabidhi zawadi ya kombe na fedha taslimu kwa timu ya Kewanja FC, na zawadi ya fedha taslimu kwa mshindi wa pili (Kerende FC) na wa tatu (Mrito FC).
Wengine waliopata zawadi ya fedha taslimu ni mwamuzi bora, Jacob Odongo, kocha bora, mchezaji bora, kipa bora, timu iliyoonesha nidhamu na mtangazaji bora wa mashindano hayo, Frank Jackson Chacha.
Mechi ya fainali ya mashindano hayo ilifana na kuwa kivutio kikubwa kutokana na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi kutoka vijiji na kata zinazozunguka mgodi wa Barrick North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime, Mara.
Viongozi wengine waliohudhuria fainali hiyo ni Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Baarick North Mara, Francis Uhadi aliyemwakilisha Meneja Mkuu wa mgodi huo, Apolinary Lyambiko, na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ulipo mgodi wa North Mara, Solomon Shati na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Gimbana Ntavyo.
Wakati huo huo mashindano hayo yamewezesha upatikanaji wa wachezaji 37 watakaounda timu mpya itakayoitwa North Mara FC
Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano Mahusiano Cup, Mwita Marwa Magige, alisema wachezaji 37 walioteuliwa kuunda timu ya North Mara FC ni wale ambao wameonesha ubora na vipaji mahiri katika mashindano hayo.
Mwita, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyamwaga alisema wachezaji hao wakiwemo magolikipa watatu wameteuliwa kutoka timu mbalimbali zilizoshiriki mashindano hayo.
GGML ILIVYONG’ARA USIKU WA MADINI, YATWAA TUZO 2
Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang'anamuno (kushoto) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika kipengele cha uhifadhi mazingira, afya na usalama mahala pa kazi, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Hafla hiyo iliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang'anamuno (kushoto) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR), Makamu Rais wa AngloGold Ashati- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Hafla hiyo iliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam
Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang'anamuno (mwenye nguo nyekundu katikati) akiwa amebeba tuzo yake ya heshima ya ushiriki wa kongamano la Kimataifa la Madini na Uwekezaji Tanzania 2023. Wengine ni viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) walioshiriki katika hafla ya usikun wa madini.
Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wakifurahia ushindi wa kampuni hiyo iliyonyaku tuzo mbili katika hafla ya usiku wa madini iliyofanyikawiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Mchango wa Kampuni ya AngloGold Ashanti - Geita Gold Mining Limited (GGML) umeendelea kutambuliwa na wadau mbalimbali wa sekta ya madini kupitia Kongamano la Kimafaifa la Uwekezaji na Madini Tanzania 2023 kutokana na jitihada zake katika uwajibikaji kwa jamii pamoja na kuzingatia afya na usalama mahala pa kazi.
Hatua hiyo inatokana na Kampuni hiyo kushinda tuzo mbili ambazo ni mshindi wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) pamoja na uhifadhi wa mazingira, afya na usalama kazini. Tuzo hizo zilizotolewa na Wizara ya Madini zimeendelea kudhihirisha hadhi ya GGML kuwa mfano wa kuigwa katika masuala hayo ya afya na usalama kazini pamoja na kukuza uchumi wa Taifa.
Waziri wa Madini wa Serikali ya Malawi, Monica Chang'anamuno akiongozana na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alikabidhi tuzo hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong pamoja na Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo.
Hafla hiyo iliyopewa jina la Usiku wa Madini, ilifanyika tarehe 25 Oktoba 2023 jijini Dar es salaam.
WALIMU WAIOMBA SERIKALI KUZUIA SHEREHE ZA SIKU YA MWALIMU
Rais wa Chama cha walimu Tanzania (CWT)Leah Ulaya
Na Dotto Kwilasa,DodomaWakati Uongozi wa Chama cha walimu Tanzania (CWT)ukiwa kwenye maandalizi ya Sherehe ya Siku ya Mwalimu inayotarajiwa kufanyika Desemba 13,2023 Jijini Mwanza,baadhi ya wanachama wake wametilia Shaka Sherehe hizo na kueleza kuwa ni batili .Wakizungumza na malunde Blog jijini Dodoma,Wamesema jumla ya Bilioni Tano zinatarajiwa kutumika kukamilisha mkutano huo kwa mgawanyo wa posho ,vinywaji na chakula na kuwaacha walimu ambao kimsingi ndiyo wenye fedha wakifa maskini jambo linalotafsiriwa kuwa ni upigaji.Mwalimu wa Shule ya Sekondari Iyumbu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma Maxson Maboje ameeleza kuwa Sherehe hizo hazipaswi kuwepo kulingana na kanuni za chama hicho na kwamba zinafanyika kwa ajili ya viongozi kujinufaisha na kufuja fedha za wanachama.Mwalimu Maboje ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kuingilia kati kumaliza mgogoro ndani ya Chama hicho kwa maslahi ya walimu nchini kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi kuzungumzia migogoro ya Chama kuliko kufanya kazi.Amesema kikanuni CWT kilipaswa kufanya Sherehe hizo kitaifa Oktoba 5,2023 lakini cha ajabu haikufanyika japo kuna baadhi ya maeneo walifanya ikiwemo wilaya ya Bukombe na kutaja sababu ya kutofanya hivyo ni kuandaa mazingira ya upigaji wa fedha za walimu."Hii ni kutudharau sisi walimu, Madame Leah na Maganga wametudharau kwa kutosha, kama Sherehe zilitakiwa kufanyika Oktoba 5 mwaka huu iweje ifanyike Desemba, huu ni mwanya wa upigaji, kinachoniuma ni kuwa pesa hiyo inatokana na mishahara yetu, tunakuwa tunamhudumia Leah na Maganga badala ya kuhudumia Chama, " AmesemaWakati haya yakiendelea ikumbukweSeptemba 25,2023 wakati wa mkutano wa dharula Rais wa Chama hicho Leah Ulaya aliionya Serikali kutoingilia Mambo yaona kwamba Serikali inapaswa kujua kuna uhuru wa vyama vya wafanyakazi, hivyo wana uhuru wa kukutana popote na kufanya kazi bila ya kuzuiliwa .Kitendo hicho kilitafsiriwa na baadhi ya walimu kama ni ukosefu wa nidhami na kuwa na Uhuru uliopitiliza hasa ikizingatiwa viongozi hao wa ngazi ya juu wa CWT walipaswa kuendelea na majukumu waliyopangiwa na Rais.Athman Kihinga ameeleza kuwa ifike wakati Serikali ione haja ya kuingilia matatizo yaliyopo ndani ya CWT kwani yakiendelea yanaweza kusababisha walimu kutokuwa na ari ya kufanya kazi kwa bidii na kushusha hadhi yao."Nashindwa kuamini kwamba kelele zote tunazopiga kuomba msaada hazisikiki,tunatambua kuwa usajili wa CWT upo chini ya Serikali kwanini mamlaka husika inaogopa kutushughulikia au kutoa tamko lolote ili tujue tupo upande gani, " Anaeleza Kihingana kuongeza;"Viongizi hawa wamekuwa wanatudharau walimu pamoja na Serikaki,nakumbuka Mnamo Januari 25, mwaka huu, Makamu wa Rais wa CWT, Dinna Mathaman,Katibu Mkuu wa CWT Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Wakuu wa Wilaya lakini Maganga na Ulaya hawakufika kuapa, hii ni dharau, "amesemaAmesema,"uhuru ukizidi unakuwa mwenda wazimu,Viongozi hao wakati wenzao wakiapishwa, wao walionekana kuendelea na majukumu ya Chama jambo linalotufanya tukitafsiri kitendo hicho kuwa wamegomea uteuzi wa Rais Samia, ni dharau," amesema
Amefafanua kuwa licha ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kufanya mchakato wa kufungua shauri la nidhamu dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japhet Maganga baada ya kutorejea katika kituo chake cha kazi tangu alipotakiwa kufanya hivyo Oktoba Mosi mwaka huu hakuna mabadiliko yoyote."Maganga ni Mwalimu Mwandamizi katika Manispaa ya Temeke, aliomba kibali cha kuazimwa kuitumikia CWT Agosti 2017 hadi Septemba 30, 2020, akaomba tena Juni 1, 2020 na kumalizika Septemba 30, 2023, na baadaye aliomba kibali hicho kwa mara ya tatu, tunaomba aachie madaraka kwa hiari aache kujidharirisha, " amesisitizaMaganga alichaguliwa Desemba 2022 na Mkutano Mkuu wa CWT kuwa Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Deus Seifambapo awali alikwa akitumikia nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.