Friday, 11 August 2023

VANILLA INTERNATIONAL LTD YAANZISHA MRADI WA 'VANILLA VILLAGE KENYA'


Kampuni ya Vanilla International Limited imeanzisha mradi wa VANILLA VILLAGE KENYA ,Mombasa nchini Kenya katika mji mdogo wa Mariakani.


Mkurugenzi wa Vanilla International Limited Duniani Simon Mnkondya amechukua uamuzi huo baada ya kuona Wakenya wengi wanachangamkia katika kilimo cha Vanilla kuliko hata watanzania licha ya kwamba tumekuwa tukifanyia mradi wa VANILLA ARUSHA,ZANZIBAR na VANILLA VILLAGE DODOMA.

Mnkondya amesema ni wakati sahihi kwa Kenya kuanza kilimo cha VANILLA kwa mfumo wa mashamba Shufwaa yaani Block Farming ili kupunguza gharama za uwekezaji, kwa ajili ya usalama na kwa ajili ya kuhakikisha Uwepo wa Soko la Vanilla.


WASHIRIKA

Vanilla International Limited itafanya mradi ikishirikiana Na Taasisi ya MRM Foundation na Karibuni Foundation zote za Kenya na Taasisi ya Society Watch ya Tanzania.

Lengo la mradi wa VANILLA VILLAGE KENYA ni kukuza uchumi wa Wakenya na Waafrika kwa ujumla kwa sababu bei ya vanilla imewahi kufikia mpaka Dola za Kimarekani 500$ takribani 1,000,000/= ya kitanzania.
Mkurugenzi wa Nyali Cinemax ,Dipan Shah amesema Vanilla India imewafanya wakulima wawe matajiri sana kwa maana ni zao la pili kwa bei duniani.

Naye Rais wa Upendo Foundation , bw. Bruno Cern'o mwenye Asili ya Italia amesema kwa vile vanilla ni zao la bei kubwa ni vyema sasa Waafrika kulima Vanilla ili kupata utajiri endelevu na kuwa na unafuu wa maisha.

Kwa upande wake Gianfranco Ranieri ambaye ni Rais wa KARIBUNI ASSOGIOCATTOLI ya Milano Italia amesema atalima heka zaidi ya 100 hapa Kenya na anaenda kulima Vanilla kama Kichaa na atakuwa Kichaa wa Vanilla Kenya.

Naye Mama Siprosa Rabach Meneja mkazi wa MRM Foundation amesema lazima vanilla ilimwe Kenya watu wapate kazi na utajiri Kenya.


Pia kampuni ya Vanilla International imetangaza namba ya +255629300200 , Kenya +254 759604040
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akizungumza na wadau wa kilimo cha Vanilla
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya (kushoto) akipiga picha na wadau
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akizungumza na wadau wa kilimo cha Vanilla
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya







Share:

WAZIRI MABULA ATAKA WAMILIKI WA ARDHI KUMILIKI MAENEO KWA HATI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi hati milki ya ardhi mmoja wa wananchi wa wilaya ya Makete wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Njombe tarehe 10 Agosti 2023. Wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Njombe Athony Mtaka na wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga.

********************

Na Munir Shemweta, WANMM MAKETE

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wamiliki wa ardhi nchini kuhakikisha wanamilikishwa maeneo yao kwa kupatiwa hatimiliki za ardhi ili kuwa na salama ya miliki zao.

Dkt Mabula alisema hayo tarehe 10 Agosti 2023 wilayani Makete mkoani Njombe wakati wa kukabidhi hatimiliki za ardhi kwa wananchi wa wilaya hiyo akiwa katika ziara yake ya siku tatu katika mkoa huo.

Alisema, wananchi wa Makete waliojitokeza kuchukua hati mara baada ya kukamilisha taratibu za umilikishwaji wamechukua uamuzi sahihi unaoenda kuwahakikishia usalama wa milki zao.

Alibainisha kuwa, mmiliki wa ardhi mwenye hati mbali na kuwa na salama ya miliki yake lakini hati hiyo inampa fursa nyingi ikiwemo kuhukua mikopo benki pamoja na kuitumia kama dhamana.

Hata hivyo, Dkt Mabula alishangazwa na idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza kuchukua hati ambapo alisema kati ya wamiliki 88 wa wilaya ya Makete waliothibitisha kwenda kuchukua hati katika tukio la kukabidhi hati ni wamiliki 25 tu waliojitokeza na kukabidhiwa hati zao.

‘’Hii mara nyingi inatokea wanaothibitisha kwenda kuchukua hati ni wengi lakini wanaokwenda kuchukua ni wachache sasa mimi naomba ninyi mkawe mabalozi pengine wasiokuja wameona wamekuwa wakidanganywa na leo wangedanganywa ‘’ alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Serikali ya Awamu ya Sita imeamua kuwawezesha wananchi kupitia ardhi zao na uwezeshwaji huo ni kuwa na umiliki halali wa ardhi unaowapa salama ya maeneo yao sambamba na kuwawezesha kutumia hati katika kujiwezesha kiuchumi.

Alisema, wamiliki wa ardhi wanaojua alama za mipaka katika maeneo wanayomiliki ni tofauti na wale wanaomiliki maeneo wakiwa na hati zao na kueleza kuwa wanaopatiwa hati wana shughuli nyingi za kimaendeleo wanazoweza kuzifanya kupitia hati.

Kwa upande wao Wananchi wa Makete waliokabidhiwa hati milki za ardhi waliishukuru Wizara ya ardhi kupitia waziri mwenye dhamana kwa kuwapatia hati milki za ardhi amabpo walisema huko nyuma ilikuwa vigumu kuzipata.

Faidon Kyando mkazi wa Makete aliyekabidhiwa jumla ya hati sita na Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula alisema hakuamini alipopigiwa simu akitakiwa kwenda kuchukua hati za maeneo yake hasa akiwa na kumbukumbu za huko nyuma kusikia kwamba kuna mtu alichukua hati kwa kiasi cha milioni mbili.

‘’Baada ya kukuona mama umefika hapa na kutushika mkono kwa kutukabidhi hati ambapo kama mimi nilisikia mwaka 1998 kuna mtu alichukua hati mkoani mbeya kwa milioni 2 na ndiyo maana niliposikia tunakuja kukabidhiwa hati sikuamini’’ alisema Kyando.

Jumla ya wamiliki 25 kati ya 88 wa ardhi katika wilaya ya makete mkoani Njombe walikabidhiwa hati milki za ardhi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula katika tukio lililohudhuriwa pia na Mkuu wa mkoa wa Njombe Athony Mtaka pamoja na mbunge wa jimbo la Makete Festo Sanga.



Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimuonesha Faidon Kyando mkazi wa Makete namna anavyoweza kujua kiasi anachotakiwa kulipa kodi ya pango la ardhI wakati alipokabidhi hati kwa wananchi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe tarehe 10 Agosti 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na viongozi, watendaji wa sekta ya ardhi na wananchi wa Makete aliowakabidhi hati wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Njombe tarehe 10 Agosti 2023. Wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Njombe Athony Mtaka na wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga.
Mbunge wa jimbo la Makete Festo Sanga akizungumza katika zoezi la utoaji hati kwa wananchi wa wilaya ya Makete wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula wilayani humo mkoa wa Njombe Agosti 10, 2023. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Sheushi Mbuli na wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Athony Mtaka akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula katika wilaya ya Makete mkoani Njombe Agosti 10, 2023. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Sheushi Mbuli na wa pili kushoto ni Mbunge wa jimbo la Makete Festo Sanga.


Sehemu ya wananchi waliokabidhiwa hati miliki za ardhi wakimskiliza Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Njombe tarehe 10 Agosti 2023.

(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)


Share:

BENKI YA CRDB YAWAPA PUNGUZO LA BEI WATEJA SIMU ZA SAMSUNG GALAXY Z


Dar es Salaam. Tarehe 10 Agosti 2023: Benki ya CRDB imeingia ushirikiano na kampuni ya Samsung Tanzania ili kuwapa punguzo la bei wateja watakaonunua simu mpya aina ya Samsung Galaxy Z Fold5 na Galaxy Z Flip5.


Ushirikiano huo umetangazwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Huduma za Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif aliyeambatana na Mkuu wa Kitengo cha Simu cha Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga mbele ya waandishi wa Habari.


Akizungumzia ushirikiano huo, Seif amesema kuanzia sasa, wateja wanaopenda kuzinunua simu hizo mpya wanaweza kuweka oda zao ili kuanza kufurahia huduma katika simu hizo zenye ubora wa kimataifa.
“Katika kipindi hiki, wateja wetu wataweka kuokoa kati ya shilingi 308,000 hadi shilingi 565,000 iwapo watanunua simu hizi kipindi hiki cha promosheni. Ukienda kwenye maduka ya Samsung yaliyoenea kote nchini au kwenye matawi yetu ya wateja wakubwa, utatakiwa kulipia asilimia 20 ya bei ya simu unayoitaka na ukiletewa utarudishiwa asilimia 10 ya bei uliyolipa,” amesema Seif.


Kwa aliye mbali na duka, Seif amesema anaweza kuweka oda yake kwa kuingia kwenye akaunti za mitandao ya kijamii za Benki ya CRDB katika majukwaa ya Instagram, Twitter na Facebook ambako kuna ‘link’ itakayowaunganisha na kitengo cha huduma kwa wateja cha Samsung Tanzania ambako wanaweza kuweka oda ya simu waitakayo.


“Kwa njia yoyote kati ya hizi, mteja atakayelipa kwa kutumia kadi ya Benki ya CRDB au kupitia Simbanking atarudishiwa asilimia 10 ya malipo aliyoyafanya,” amesisitiza Seif.
Kwa miaka mingi, Benki ya CRDB imekuwa ikongoza kwa ubunifu katika kuwahudumia wateja wake. Ilikuwa ya kwanza kuanzisha matumizi ya kadi zinazofahamika zaidi kama CRDB Tembocard na ikawa ya kwanza kuzindua programu ya huduma kupitia simu za mkononi almaarufu kama Simbanking ambayo inaongoza kwa kutumiwa nchini miongoni mwa programu za benki zilizopo.


Kwa Watanzania ambao hawajajiunga na huduma za Benki ya CRDB hivyo kutokidhivigezo vya kunufaika na punguzo hili, Seifa amesema wanawakaribishwa kufanya hivyo na kuwa sehemu ya mtandao mkubwa wa matawi yaliyopo kwenye halmashauri zote nchini pamoja na huduma za mawakala wengi wanaopatikana mitaani.


“Kwa sasa utaratibu umerahisishwa, mteja anaweza kujifungulia akaunti yeye mwenyewe au akaenda kufungulia kwa wakala yaani CRDB Bank Wakala au akaenda kwenye tawi letu lolote na kuanza kufuarahia huduma likiwamo punguzo la bei la simu bora za Samsung,” amesema Seif.
Kuhusu unafuu uliopo, Kiwanga amesema mteja atakayenunua simu zinazoingizwa sokoni sasa hivi atanufaika na punguzo hilo la bei, na atapata saa ya mkononi yenye thamani ya shilingi 900,000 au ‘earpods’ zinazouzwa shilingi 450,000 kutegemeana na aina ya simu atakayoinunua.


“Simu aina ya Galaxy Z Fold5 tunaiuza kwa shilingi milioni 5.65 na ile ya Galaxy Z Flip5 ni shilingi milioni 3.08. Ukiweka punguzo la asilimia 10 ambalo mteja atalipata akilipa kupitia mifumo ya Benki ya CRDB pamoja na zawadi hizi anazopewa, utaona kuwa anaipata simu hii kwa bei ndogo kuliko uhalisia wake. Nawakaribisha Watanzania kuchangamkia fursa hii kwenye maduka yetu ndani ya kipindi cha promosheni kitakachodumu mpaka mwishoni mwa mwezi huu,” amesema Kiwanga.


Simu hizi mbili, Kiwanga amesema ni mwanzo tu ushirikiano wao na Benki ya CRDB ila huko mbeleni wanatarajia kuzijumuisha bidhaa nyingine zote za kampuni ya Samsung ili kuwapa unafuu Watanzania wanaopenda kutumia bidhaa bora za kielektroniki.
Kwa sasa, kampuni ya Samsung Electronics inanadi toleo lake la tano la simu aina ya Galaxy Z ambazo zinakunjika huku zikiwa na urahisi mwingi katika matumizi yake. Zikitamblishwa kwa tarehe tofauti duniani, uzinduzi wakee nchini ulifanyika tarehe 26 mwezi uliopita katika maduka ya Sansung yaliyopo Mlimani City, Palm Village na Royal Communications jijini Dar es Salaam.


Ili kunufaika na ofa iliyopo, Kiwanga amesema maduka yao yote yapo wazi kupokea oda za wateja na akawakaribisha kwenye maduka ya F&S Electronics Mlimani City, SES Mlimani City, Gadget Masaki, SES JMall na Brandshop Palm Village ya jijini Dar es Salaam Pamoja na Samsung Brandshop na Dodoma Express ya jijini Dodoma bila kusahau duka la Benson & Company jijini Arusha.
Mkuu wa Huduma za Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Simu cha Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga wakitangaza punguzo la asilimia 10 kwa wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy Z Fold5 na Galaxy Z Flip5 wakilipa kupitia mifumo ya Benkiya CRDB.
Mkuu wa Huduma za Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Simu cha Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari waliojishindia zawadi wakati wa kutangaza punguzo la asilimia 10 kwa wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy Z Fold5 na Galaxy Z Flip5 wakilipa kupitia mifumo ya Benki ya CRDB.
Mkuu wa Huduma za Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Simu cha Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hizo mbili baada ya kutangaza punguzo la asilimia 10 kwa wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy Z Fold5 na Galaxy Z Flip5 wakilipa kupitia mifumo ya Benki ya CRDB.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger