Wednesday, 2 August 2023

DCEA YAENDESHA OPERESHENI YA SIKU 8 MFULULIZO MOROGORO KUKABILIANA NA BANGI, YAKAMATA NA KUTEKETEZA MASHAMBA


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama wakiwemo JKT Ruvu imefanya operesheni ya siku nane (8) mfululizo mkoani Morogoro katika wilaya za Morogoro, Morogoro vijijini na Mvomero na kukamata jumla ya gunia 131 za bangi kavu iliyo tayari kusafirishwa, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketeza jumla ya hekari 489 ya mashamba ya bangi ambapo jumla ya watuhumiwa 18 wanashikiliwa kuhusika na dawa hizo.

Katika wilaya ya Morogoro vijijini kata ya Kisaki, kijiji cha Rumba zimekamatwa gunia 70 za bangi, Kijiji cha Mbakana zimekamatwa gunia 59 za bangi, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketezwa hekari 350 za mashamba ya bangi. 

Aidha, wilayani Mvomero Mamlaka imeteketeza hekari 139 na wilaya ya Morogoro zimekamatwa gunia mbili (2) za bangi.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo, kamishna jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, wakulima wa bangi mkoani Morogoro wanalima pembezoni mwa mto, na kukata miti ili wawezekupata maeneo ya kulima bangi.

“Wakulima wa bangi wa mkoa huu wanachepusha maji na kuyazuia yasiende kwenye maeneo mengine yakahudumie wananchi ili kumwagilia mashamba yao. Pia wanafanya uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti katikati ya msitu ili waweze kulima bangi. Hivyo, wanafanya uharibifu mkubwa wa mazingira na kuharibu vyanzo vya maji katika maeneo haya” ,amesema kamishna jenerali Lyimo.

Pia, amesema kwamba, wakulima wa bangi wanalima mashamba yao katika maeneo ya mbali, yaliyojificha na yasiyoweza kufikika kirahisi lakini Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeweza kuyafikia maeneo hayo kuwakamata wanaojihusisha na bangi, pamoja na kuteketeza bangi iliyovunwa na mashamba yao.

“Kwa mfano katika maeneo haya ya Morogoro ambayo tumefanya hii operesheni, eneo ambalo wamelima bangi ni mbali kutoka mjini. Kutoka unapoachia gari mpaka kufika huku unatembea masaa sita mwendo wa kijeshi. Kwa hiyo wanaamini hakuna mtu anayeweza kufika” ,ameongeza kamishna jenerali Lyimo.

Aidha, amewaasa waanchi kutoa taarifa juu ya watu wanaolima bangi na mirungi ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Niwaase wananchi wote Tanzania watusaidie kutoa taarifa za wakulima wa bangi na mirungi katika maeneo mbalimbali ili tuwakamate na kuharibu mashamba yao. Kwani mbali na madhara mengine yanayotokana na zao la bangi, wakulima hawa wanaharibu misitu, vyanzo vya maji, na wanaweza kutengeneza jangwa kwani wanakata miti sana ili wapate maeneo ya kulima bangi”,amesema.

Kulingana na Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2022, mkoa wa Morogoro ni kati ya mikoa mitano iliyokithiri kwa kilimo cha bangi Nchini Tanzania.
Share:

WATATU WAFARIKI AJALI YA NOAH



Watu watatu wakazi wa Lugala, Kata ya Manzase mkoani Dodoma, wamefariki dunia jana Jumanne usiku baada ya gari aina ya Noah walilokuwa wamepanda kutumbukia kwenye korongo.

Imeelezwa kuwa dereva wa gari hilo alishindwa kupandisha mwinuko uliopo kwenye barabara kuu katika eneo hilo hali iliyosababisha kupoteza mwelekeo na kuingia kwenye korongo.

Akizungumza kuhusu ajali hiyo leo Agosti 2, 2023 Diwani wa Kata ya Manzase, John Mika amesema majira ya saa 2 usiku gari hiyo ilichukua abiria kutoka mnada wa Fufu na kuwarudisha kwenye maeneo yao.

“Ilikuwa usiku wakati gari hiyo inatoka mnadani na kabla ya kupanda mlima ikawa imemshinda dereva na kupelekea gari kuangukia kwenye korongo na watu wawili walikufa hapohapo na mmoja alifariki wakati anapelekwa hospitali,” amesema.

John amesema waliofariki ni Amos Matereka, John Nghambi na Nhoya Mashamba ambao familia zao zinatarajia kufanya mazishi leo na majeruhi wawili wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Aidha amesema watu wanane waliotolewa kwenye gari hilo walipatiwa matibabu kwenye zahanati ya kata na kufanya idadi ya watu waliokuwepo kwenye gari hiyo kuwa 13.

Mkazi wa kijiji hicho Anna Chihicha ameiomba Serikali kuwasaidia kusawazisha eneo hilo ambalo lina mwinuko hivyo kuhatarisha usalama wa watumiaji wa eneo hilo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Martin Otieno amethibitisha kutokea ajali hiyo na kuahidi kutoa taarifa kamili baadaye.
CHANZO-MWANANCHI.
Share:

NEC YASHIRIKI MAONESHO YA KILIMO NANE NANE KANDA YA KATI


TUME ya Taifa ya Uchaguzi ni miongoni mwa taasisi mbalimbali za binafsi na serikali zinazoshiriki katika Maonesho ya Wakulima maarufu kama Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma na kuwapa fursa wananchi hasa wakazi wa mikoa ya Kanda ya Kati kupata elimu ya Mpiga Kura ambayo hutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Katika banda la NEC wananchi mbalimbali wameweza kutembelea leo Agosti 1,2023 ikiwa ni siku ya kwanza ya maonesho hayo ya siku 10.

Wananchi hao waliweza kuuliza maswali mbalimbali ambayo yalipatiwa majibu kutoka kwa maofisa wa Tume.
Wananchi waliotembelea banda la Tume, wakiangalia Album iliyo na picha za uteuzi wa wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Afisa wa NEC, Nuru Riwa akitoa amelezo kw mgeni aliyefika katika Banda la Tume.
Afisa wa NEC, Loshilu Saning'o akitoa amelezo juu ya matumizi ya BVR inavyo fanya kazi wakati wa uboreshaji.
Maofisa wa Tume wakitoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wageni waliofika Bandani.
Maofisa wa Tume wakitoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wageni waliofika Bandani.
Share:

Tuesday, 1 August 2023

DIWANI AWAKUMBUSHIA WALIMU UTUMISHI BORA

Diwani wa kata ya Bwilingu halmashauri ya Chalinze Mh. Nassar Karama(suti nyeusi) akizungumza na walimu


NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE

DIWANI wa kata ya Bwilingu ,katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani, Mh. Nassar Karama amesisitiza walimu kufanya kazi kwa bidii na kufuata kanuni za Utumishi wa umma ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Mh. Nassar ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na walimu  wa shule ya msingi Kibiki katika kata ya Bwilingu, alipowatembelea leo shuleni hapo.

Mh. Nassar amesema Jambo pekee linalomjengea mwalimu heshima ni pamoja uadilifu na ufanisi katika kazi yake ya ualimu vitakavyomfanya kuepuka migogoro na mwajiri wake.

Aidha Mh.Nassar amesema kuwa kata yake bado inauhitaji mkubwa wa shule shikizi kutokana na wanafunzi wengi kusafiri umbali mrefu kufuata shule Kongwe mahali  zilipo.

" Mfano maeneo ya Kibiki Maziwa  na  Kitoho Kuna wimbi kubwa la wanafunzi kutembea umbali mrefu kuja kusoma hapa. Lazima tuone namna ya kuanzisha miradi ya Ujenzi wa shule kwenye maeneo yenye changamoto", alisema Diwani huyo.

 Mh. Diwani aliuelekeza uongozi wa shule hiyo kuitisha vikao vya wazazi na wadau wa maendeleo ya elimu kwa ajili ya  uhamasishaji wa kuwapatia watoto chakula shuleni, kuhimiza maadili pamoja na masuala ya kitaaluma.

Katika ziara hiyo walimu walitoa changamoto mbalimbali za kikazi zinazowakabili ikiwamo uhaba wa nyumba za walimu, uzio na kuwepo barabara inayopita pembezoni mwa  eneo la shule ambayo jamii itakuwa ikiitumia badala ya barabara ya Sasa ambayo inapita katikati ya viwanja vya shule hiyo.

Share:

MKAZI WA DAR-ES-SALAAM AJISHINDIA MILIONI 14 NA MERIDIANBET

Kama ilivyo kauli mbiu “CHAGUA TUKUPE” sasa watu wamechagua na wamepewa kwani Mkazi mmoja kutoka jijini Dar-es-salaam ameweza kujishisdia kiasi cha milioni 14 baada ya kubashiri na kampuni ya kibabe na inayotoa ODDS KUBWA na bomba kabisa nchini Tanzania.

Mteja huyo alifanikiwa kuchagua timu saba kutoka nchi mbalimbali na kuweka kiasi cha shilingi 25000 za kitanzania na kupata jumla ya ODDS 626 na kupelekea kushinda kiasi hicho cha pesa kutoka kwa wataalamu wa michezo ya kubashiri.

Ligi mbalimbali zinakaribia kurejea barani ulaya ni wakati wako sasa wewe mteja wa Meridianbet kujiandaa na msimu mpya wa ligi ambapo Tumekuandalia huduma bomba zaidi na ODDS za kibabe kabisa ambapo unaweza kubashiri kupitia tovuti zetu za mitandanoni na kwenye simu za kitochi kwa kupiga *149*10#

Wataalamu hao wa michezo ya kubashiri wanaendelea kutoa washindi kila siku kupitia michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, lakini vilevile Kasino mitandaoni ambapo watu wanajishidia mikwanja tu kwakua wanatoa ODDS nzuri kuliko sehemu yeyote.

Hii inaendelea kuonesha namna gani kampuni ya Meridianbet inaendelea kuonesha sio wababaishaji kwani inaendelea kutoa washindi kila kukicha na leo hii Mkazi wa Dar-es-salaam ameweza kujishindia kitita cha milioni 14 baada ya kubashiri na wataalamu wa michezo ya kubashiri nchini Tanzania.


Pata mizunguko 50 ya bure kucheza sloti na michezo ya kasino ya mtandaoni ukijisajili na Meridianbet. Jisajili kupitia link hii

 

Unataka kucheza kasino ya mtandaoni? Basi nenda Meridianbet wana michezo mingi sana ambayo ni rahisi kwako kushinda kama Aviator kwa dau la shilingi 200/= tu basi unaweza kuwa Milionea, Poker, Roullete, Piggy Party na mingine ambayo ni rahisi sana na pesa yake ni ya chap chap hakuna kusema unasubiri wiki au siku iishe.

Pia Meridianbet imeleta mchongo wa  hela kila siku. Kuna hii bonasi ya ukaribisho kwa wateja wapya wote wanapata Tsh 25,000/= ya kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Ingia mchezoni www.meridianbet.co.tz

Unachelewa wapi kujiunga na Meridianbet upate bonasi kubwa kama hiyo uitumie kucheza michezo ya kasino ambayo inayotolewa na Meridianbet na uipendayo wewe mteja wao. Jiunge sasa na Mabingwa ujiweke kwenye nafasi ya ushindi.

 

 

Usikose kucheza Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette, Piggy Party, Pia Premium ambayo hiyo yote itakuwa karibu nawe wakati ligi zikiwa zimeisha na wewe utaweza kujipigia pesa huko.


Share:

VUNA ZAIDI NA AIRTEL MONEY YA MERIDIANBET YAZINDULIWA LEO

Habari mteja wa Meridianbet, zikiwa zimebaki siku chache Ligi mbalimbali barani Ulaya kurejea, wababe wa ODDS KUBWA Tanzania Meridianbet wamekuletea promosheni mpya ijulikanayo kwa jina la “Vuna Zaidi na Airtel Money” ambayo imeanza leo hii.

Uzinduzi huo ulifanyika leo hii majira ya saa 4:30 pale Posta katika Four Points by Sheraton Hotel huku waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakijumuika pia kuona nini Meridianbet wamekuja nacho msimu huu amvao ligi zinaelekea kuanza.

Aliyefungua uzinduzi huo alikuwa ni Meneja wa Malipo wa Meridianbet Dora Kinyaiya ambaye alizungumza mengi akisema kuwa promosheni hiyo ni kwa wale ambao wanatumia mtandao wa Airtel kufanya miamala kwenda Meridianbet, au pia unaweza ukajisajili na mtandao huo ili ushiriki promosheni hiyo huku awamu hii kushiriki lazima uweke dau la shilingi elfu kumi.

Pata mizunguko 50 ya bure kucheza sloti na michezo ya kasino ya mtandaoni ukijisajili na Meridianbet. Jisajili kupitia link hii

Baada ya kuweka pesa yako unatakiwa kucheza michezo ya kasino sasa kama vile Roullette, Poker, Aviator, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao, pia ubashiri mechi kibao ili sasa uweze kujiweka kwenye nafasi ya washindi siku ya droo kuchezeshwa.

Dora aliendelea kuzungumza akisema kuwa zawadi zilizopo ni Simu Janja aina ya Samsung zaidi ya 20 zitatolewa, bonasi ya kasino na michezo pia hela ambayo utakuwa umeliwa utapata 10% na vilevile kuna bodaboda mbili kutolewa katikati ya promosheni na mwisho wa promosheni hiyo.

Piga *149*10# kwa USSD pia uweza kubashiri bila bando au ukiwa hata na kitochi, yani kila kitu ni rahisi ukiwa na mabingwa wa ubashiri Tanzania nzima Meridianbet.

 Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.

Ndugu mteja endelea kubeti na Meridianbet huku ukisubiri mechi za ligi zote kurejea wiki ijayo na kwasasa odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.

Hivyo usisubiri kupitwa na zawadi hizi mbalimbali ambazo zitatolewa na Meridianbet ukiwa kama mteja unaetumia Airtel Money fursa ndio kama hizi usikubali zikupite kirahisi. Kama hujajisajili pia na Airtel fanya hivyo uweze kushiriki kwenye promosheni hii sasa.

Kujiweka kwenye nfasi kubwa ya kushinda zawadi kibao kama simu aina ya Samsung ambazo zitatolewa kwa washindi, bonasi mbalimbali za kasino na michezo, pamoja na bodaboda unachotakiwa kufanya ni kufanya miamala zaidi na Airtel kwenda Meridianbet ili uwe bingwa mwisho wa promosheni hii.

NB: Habari njema kwako, Meridianbet imesikia ombi la wengi imekuja na Jackpot kubwa ya mechi 13 kwa dau dogo la kuanzia 1,000/=TZS mshindi atajinyakulia donge nono la Tsh 85,000,000/= PIGA *149*10#

#MERIDIANBET CHAGUA TUKUPE


Share:

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUUJUA MFUMO WA NeST.


Na Mwandshi Wetu-DODOMA.

Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma PPRA imezitaka Taasisi zote za Umma nchini kuhakikisha zimepatiwa mafunzo elekezi kwa ajili ya utumiaji wa Mfumo mpya wa Ununizi wa Umma kwa njia ya mtandao (NeST).

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Bw. Eliakim Maswi wakati akiendesha mafunzo kwa wafundishaji (ToT) juu ya matumizi ya mfumo wa NeST jijini Dodoma hivi karibuni.


Bw. Maswi amesema kuwa katika kukamilisha mpango wa Serikali wa kupata thamani ya fedha katika ununuzi wa umma Taasisi zote za umma zinatakiwa kuhakikisha watendaji wake wote waliopo kwenye mnyororo wa ununuzi wanapatiwa mafunzo elekezi juu ya utumiaji wa mfumo wa NeST.

“Niwaombe Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Taasisi nyingine za Umma kuhakikisha wanaleta watu wao kwenye mafunzo ya matumizi ya mfumo, na isitoshe tu kuwa watu bali ni watu wenye upeo mpana wa kuelewa, kwa sababu kupitia wao tunataka wakawe msaada kuwafundisha wengine namna ya kutumia mfumo huu”


Aidha Bw. Maswi ameweka bayana juu ya hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya taasisi ambazo zitakwepa kutumia mfumo katika michakato ya kufanya ununuzi kuwa Sheria itatoa adhabu ya faini ya kiasi kisichopungua Shilingi milioni kumi. Kwani kufanya hivyo ni kuzorotesha juhudi za Serikali katika mpango wa kuleta maendeleo hususan katika Sekta ya ununuzi.


“ Sheria itatoa adhabu ya kutozwa kiasi cha fedha kisichopungua milioni kumi kwa Taasisi yoyote ambayo itaendesha shughuli za ununzi nje ya mfumo” Alisema Bw, Maswi.


Mafunzo hayo yanayotarajiwa kuendeshwa ndani ya siku tano yamehusisha jumla ya washiriki zaidi ya 160 kutoka katika Mikoa 26 na Halmashauri ikiwa kila Halmashauri zilizoshiriki zikitoa wawakilishi 6 wanaopatiwa mafunzo kwaajili ya Kwenda kuwafundisha watendaji wengine.


Kwa upande wake Mgeni rasmi wa mafunzo hayo Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru naye amesisitiza kuwa Taasisi za umma zinatakaiwa kuendelea kuwataka wazabuni wao kujisajili kwenye mfumo wa NeST kwani bila kufanya hivyo malengo ya kutolewa mafunzo hayo hayatafikiwa kwani bila ya wazabuni kujisajili lengo la kuendesha mchakato wa ugawaji wa zabuni za umma halitafikiwa.


“Nitoe wito kwenu nyinyi na Taasisi nyingine za umma kuendelea kuwasisitiza wazabuni kujisajili katika mfumo, kwani bila ya wao hiki tunachokifanya hapa ni bure”


Muendelezo wa utoaji wa mafunzo Hayo elekezi ni maandalizi ya kuwajengea uwezo watumiaji wa mfumo huo mpya wa NeST ambao ni Taasisi zote za umma na wazabuni, ambapo mpaka ifikapo Septemba 30 hakuna taasisi yoyote ambayo itaruhusiwa kutangaza zabuni nje ya mfumo wa NeST.




Share:

FEDHA ZA UJENZI WA ZAHANATI ZASHTUKIWA KUPIGWA NA VIONGOZI WA KITONGOJI, MBUNGE AFICHUA MADUDU


Wananchi wa Kitongoji cha Kinyika, Kata ya Mkwese, Wilayani Manyoni wamelalamikia Viongozi wa Serikali kitongoji hapo kwa ucheleweshwaji wa ujenzi wa Zahanati ikiwa walishachangishwa na kutoa michango yao.

Wananchi hao wametoa malalamiko yao mbele ya Mbunge wa Manyoni Mashariki Mhe. Dkt. Pius Chaya alipofika kufanya Ziara.

Wananchi hao wamekiri kuumizwa na kuwa na wasiwasi wa Upotevu wa Fedha ambazo zilikusanywa ikiwa ni takribani Milioni 2 katika nyakati tofauti huku Mfuko wa Jimbo ukiwa ulishatoa Milioni 6.5 ambapo mpaka sasa ujenzi upo kwenye hatua za msingi na umeshapita muda mrefu.

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wakitoa kero mbele ya Mbunge wao kwa niaba ya Wananchi hao akiwemo Bwn. Christopher Shauri na Mrosha Juma , wamesema
“Baadhi ya viongozi wanajibeba, walitangaza kwamba wanahitaji kutengeneza zahanati tukaambiwa tuchange mchango tukatoa lakini mpaka Leo ujenzi upo katika hatua ya Msingi, ukuta umeanza kuchanika siku jengo likimalizika si litamwangukia mgonjwa kweli?, Unaposema sisi tutoe michango ya Zahanati Hawa viongozi ukitoka hiyo imeisha ni mpaka mwakani, viongozi wetu hawana ushirikiano na sisi”.


Kutokana na malalamiko hayo Mhe, Dkt. Chaya amewapa Siku Saba wasimamizi wa Mradi huo ambao ni Viongozi wa eneo hilo kuhakikisha jengo hilo linasimama na ikiwa vinginevyo atapendekeza wafanyiwe uchunguzi na TAKUKURU.

"Natoa maagizo kwa viongozi wanaohusika anzeni kufanya mchakato wa kutafuta mafundi wazuri na huyo fundi ambaye amelipwa laki nne na kazi hajafanya azirejeshe ndani ya siku 3 na nawapa siku saba muwe mmeshakamilisha ujenzi mpaka kufikia hatua ya lenta na kama ikibidi uchunguzi uje kufanywa na TAKUKURU utafanywa juu ya haya malalamiko yenu” ,alisema Dkt. Chaya

Hata hivyo Ziara ya Mbunge huyo inaelekea ukingoni ambayo dhima kuu ikiwa ni kusikiliza na kutatua kero za wananchi ikiambatana na mikutano ya hadhara juu ya miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita inayoendelea kutekekezwa katika Jimbo la Manyoni Mashariki.

Share:

Monday, 31 July 2023

NEMC YAPIGA KAMBI MBEYA KUWAWAPA SOMO WANANCHI


Na Mwandishi Wetu,MBEYA

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) limeanzisha mfumo wa kielektroniki wa usajili wa miradi ili kuwarahisishia wawekezaji kufanyiwa tathmini ya athari ya mazingira(TAM).

Kutokana na hatua hiyo, limewataka wawekezaji wa miradi kutekeleza sheria ya mazingira inayotaka miradi kupata cheti cha TAM kabla ya kuanza utekelezaji wake.

Ofisa Elimu ya Jamii wa NEMC, Suzan Chawe akizungumza kwenye banda la Baraza hilo katika maonesho ya nanenane viwanja vya John Mwakangale jijini hapa, alisema baraza limerahisisha mchakato wa TAM kwa kuanzisha usajili wa miradi

kwa mfumo wa kielektroniki na kusogeza huduma katika ofisi za Kanda zinazopatikana nchini.

"Tunawakaribisha wenye sifa za kuwa washauri elekezi wa Mazingira kujisajili na kupata cheti cha utendaji kwa ajili ya kufanya TAM na ukaguzi wa mazingira,"alisema.

Meneja wa NEMC Kanda ya nyanda za juu kusini, Josia Mlunya, alisema katika banda hilo shughuli zinazofanyika ni kusajili wataalamu elekezi wa mazingira, usajili wa miradi kwa ajili ya cheti cha TAM.


"Pia tunatoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira, pamoja na kupokea malalamiko na maoni yanayohusu mazingira na kuyashughulikia,"alisema.
Share:

COSTECH YAAGIZWA KUWEKA MFUMO KURATIBU TAFITI




Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa Kikao kazi cha kujadili usimamizi ya utafiti na maendeleo nchini kilichofanyika leo Julai 31,2023 Mjini Morogoro.

Na.Mwandishi Wetu-MOROGORO

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameitaka Tume ya ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuwa na mfumo mathubuti wa kuratibu tafiti utakaosomana na Taasisi nyingine zinazofanya tafiti.

Agizo hilo Julai 31, 2023 mjini Morogoro katika Kikao kazi cha kujadili usimamizi ya utafiti na maendeleo nchini ambapoa amesema ili kutekeleza hilo kwa ufanisi wizara itaunda kamati ndogo shirikishi ambayo itapitia maoni ya kikao kazi na kuangalia sheria mbalimbali za taasisi zinazohusu masuala ya tafiti ili kutoa mapendekezo.

"Utafiti ni muhimu kwa maendeleo ni vyema ukaratibiwa vizuri ili kupunguza milolongo ya kupatika kwa vibali vya kufanya utafiti na kuwezesha upatikanaji wa matokeo kwa urahisi" amesisitiza Prof. Nombo.

Katibu Mkuu huyo ameongezea kuwa no muhimu kwa taasisi mabimbli kujikita katika kufanya tafiti za pamoja ilinkuleta tija, lakini pia kuhakikisha zinatenga fedha kwa ajili ya tafiti

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Prof. Maulilo Kipanyulu amesema kuwa kikao kazi hicho kinafanyika kwa kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ina jukumu la kutunga na kusimamia utekelezaji wa Sheria na Miongozi ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Utafiti

Naye Mshiriki wa Kikao hicho Makumu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka ameiponeza wizara kwa kikao hicho na kutaka kifanyike mara kwa mara ili kujadili vipaumbele, utekelezaji na matokeo ya tafiti katika maendeleo
Share:

AUAWA KWA KUKATWA KICHWA AKICHUMA MBOGA



MKAZI wa Kijiji cha Mgongola A Kata ya Kwamgwe wilayani Handeni mkoani Tanga, ameuawa kwa kukatwa kichwa na watu wasiojulikana wakati akichuma mboga shambani.

Akizungumzia tukio hilo lililotokea juzi Julai 29, 2023 kijijini hapo Diwani wa Kwamgwe, Sharifa Abebe amesema mwanamke huyo wa kabila la Kimang’ati alikuwa akichuma mboga ndipo alipouawa kwa kukatwa shingo huku akiwa na mtoto mdogo wa mwezi mmoja na nusu mgongoni.

“Kichwa mpaka sasa hakijajulikana kilipo lakini juhudi za polisi zinaendelea. Ukweli ni kwamba hatujajua nini kilisababisha mauaji haya kwa kweli,” ameeleza Abebe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya, Albert Msando aliyefika eneo la tukio kwa pikipiki, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kueleza kuwa hadi sasa watu watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi huku juhudi ya kutafuta kichwa cha marehemu zikiendelea.

“Mpaka sasa hivi chanzo cha mauaji hayo hatujajua ni nini na Jeshi la Polisi tangu juzi linaendelea na upelelezi,” amesema.

Alisema kwa ujumla hali ya usalama katika kijiji hicho ni nzuri japokuwa juzi wanakijiji hao walikusanyika wakiwa na silaha za jadi na kufanya vurugu hali ambayo hata hivyo ilitulizwa.

Msando alisema pia watuhumiwa hao watano wanaendelea kuhojiwa na polisi ili kuona kama kuna lolote linaloweza kubainika kuhusu mauaji hayo.

Baba mkwe wa marehemu, Dingo Shauri amesema hata wao hawafahamu chanzo cha tukio hilo.

“Taratibu za mazishi bado tunasubiria askari waseme na tumepanga wakituruhusu tutamzika hapa hapa Kwamgwe hata kama hatujapata kichwa, mwili tunao tutazika tu tutafanyaje sasa,” ameeleza.

Mkazi wa eneo hilo Malick Mohamed aliomba serikali kuingilia kati na kushughulikia mauaji hayo kutokana na wakazi wa eneo hilo kuingiwa na hofu.

“Hali ya amani ni tete. Tumeishi na hawa wafugaji Wamang’ati kwa takribani miaka 10 sasa, pametokea matukio mbalimbali na inapotokea tukio lolote hata kama ni mtu kakwazwa shamba lake limelishiwa akamchapa viboko hawa wenzetu wana tabia ya kulipiza visasi,” amesema Mohamed.
Amesema kutokana na hali hiyo eneo hilo limekuwa na matukio ya mauaji zaidi ya moja.


Share:

13 WAHOFIWA KUFARIKI BAADA YA MITUMBWI MIWILI KUZAMA ZIWA VIKTORIA


Watu 13 wanahofiwa kufariki dunia huku wengine 14 wakiokolewa baada ya mitumbwi miwili kuzama ndani ya Ziwa Victoria wakati wakitoka kusali ibada ya Jumapili Kijiji cha Ichigondo Wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Jumatatu Julai 31, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema tukio hilo lilitokea jana saa 12:30 jioni na tayari mwili wa mtoto anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja umeopolewa.

“Hapa Kijiji cha Igundu kuna kama ras sasa watu walikuwa wakitoka kusali katika kanisa la KTMK ndipo mtumbwi mmoja ukapigwa na dhoruba na kuanza kuzama, ukaja mtumbwi wa pili kwaajili ya kuokoa nao ukapigwa na dhoruba mitumbwi yote miwili ikazama,"amesema Dk Naano.

CHANZO-MWANANCHI.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger