Saturday, 27 May 2023

Picha : HAFLA YA KUPONGEZANA MISA TANZANIA YAFANA

Zoezi la kukata Keki likiendelea wakati wa hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.
Wanachama na wadau wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara,Tawi la Tanzania MISA Tanzania  wamefanya hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.

Hafla hiyo iliyofanyika Ijumaa Mei 26,2023 Jijini Dodoma imeenda sambamba na kutoa vyeti kwa taasisi za nje,ndani, wanachama wakongwe walioitumikia taasisi kwa muda mrefu na mwanachama chipukizi Kadama Malunde aliyetoa mchango mkubwa kwa taasisi hiyo ndani ya kipindi kifupi.

Aidha, Bodi ya Uongozi na Mkurugenzi wameongoza wanachama kukata keki ya kuadhimisha miaka 30 na uzinduzi kwa jukwaa la tafakuri ya uhuru wa vyombo vha habari, kujieleza na upatikanaji wa taarifa ambalo limesajiliwa kisheria kwa MISA-TANZANIA kutekeleza kila mwaka.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Elizabeth Riziki na  Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari (kulia) wakiwa kwenye hafla hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Elizabeth Riziki akizungumza kwenye hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania. Katikati ni Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Misa Tanzania, Wakili James Marenga
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Elizabeth Riziki akizungumza kwenye hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.
Mkurugenzi wa UTPC, Kenneth Simbaya akizungumza kwenye hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.
 Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari (kushoto) akimpa cheti cha pongezi Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Elizabeth Riziki
Keki Maalumu wakati wa hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.
Keki Maalumu wakati wa hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.
Furaha ikitawala wakati wa hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.
Zoezi la kukata Keki likiendelea wakati wa hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.
Zoezi la kukata Keki likiendelea wakati wa hafla ya kupongezana kwa miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MISA Tanzania.
Wanachama wa MISA Tanzania wakimpa zawadi ya kitenge Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Elizabeth Riziki






Share:

Friday, 26 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 27,2023

















Share:

APONA KIFAFA ABAKI KUSHANGILIA AFYA YAKE

 

Ni mama yangu mzazi hatujuwi shida hii ilimuanza vipi na kwanini amekuwa hivyo ghafla kwa kuwa hatukuwahi kupewa malalamiko kokote alikoenda na wala hatukuwahi kushuhudia sisi wenyewe kwa yale tuliyoambiwa mpaka shida hii ilipoanza kujitokeza nyumbani siku ambayo dada yangu wa damu alipokuwa ameleta mwanaume nyumbani kumposa.

Ghafla tu bila ya dalili zozote zile tena baada ya chakula cha pamoja cha mchana na kufanya utambulisho wa haraka tulikaa pamoja na kuanza kumzungumiza hiyo mkamwana wa mama ambaye hakuwa amekaa na sisi kwa wakati huwo alikuwa yupo nje na huyo dada – mke wake mtarajiwa. Wakati tukianza kusimuliana na kuulizana juu ya mpenzi wa dada ghafla tu mama alipiga uyowe na kuanza kadondoka chini na kuanza kutowa mapovu mdomoni akiwa anatetemeka sana kwa kung’ata ulimi.


Kwetu wote ni wasomi ndio urithi tuliopewa na baba yetu marehemu japokuwa hatukuwa waajiriwa tayari lakini sote tulijizuwa ni dalili za ugonjwa gani huwo, haraka haraka tukachukuwa kimti na kukiweka mdomoni mwake kisha kumgeuzia upande asiendelee na shida hiyo na kutafuta usafiri kumfikisha hospitali mapema kwa kuwa huduma yetu ya kwanza haikuzidi pale tulipoishia, tulipofika hospitali ya mwananyamala , tukapokelewa kisha akapewa vipimo na majibu yakaja yakinesha mama ana kifafa cha ukubwani sote tulishangaa kwa kuwa hali kama ile haikuwahi kumtokea katika kipindi chochote kile.


Shida ndio zinatukuza akapewa dawa za uangalizi huku madaktari wakisema kuwa hakuna dawa ya kumtibu mmoja kwa mmoja japokuwa ni kumpa uangalizi na kumjali kwa karibu tu. Tukarudi nyumbani na zoezi la kumuoza dada likasimama kwa muda na kwa kuwa dada ndiye mwanamke pekee nyumbani zaidi ya mama ikambidi asitishe zoezi lote kwanza na kuuguza hali ya mama --- uposaji ukakoma hapo kwa muda.


Baada ya muda kama miezi sita mama akaanza kupata afadhali kwani mara ya mwisho alidondokea kwenye chini kwenye mkeka akapiga kichwa kwa hivyo hakuwa saw asana, nafuu akaiona lakini cha ajabu tena jioni hiyohiyo alipokuwa anaandaa chakula cha usiku alishiikwa na hali ileile tena na akadondokea miguu kwenye jiko la mkaa hii ikawa mbaya zaidi kwetu.


Kumuuguza mama ndio ikawa kazi sasa na ajira yetu kwanza ana kifafa na pili ameunguwa miguu kwakweli hatukuwa na ahuweni hapo.Mamam akawa sio mtokaji wala mtembeaji nin wakitandani tu usiku na mchana.Siku mmoja kikundi chake cha mchezo wa kila jumanne kilipokuja kumtembelea ndipo rafiki yake kumpasha habari za daktari BAKONGWA mwenye tovuti zake https://bakongwadoctors.com .


Mama akaelewa lakini kwa kukata tama akaniagizia mimi ndiye ni shughulikie swala hilo nikalifanyia kazi kuzunguka kwenye tovuti zake nikapata namba za whatsapp za daktari +243990627777 na kumueleza shida zinazotusumbuwa sisi, yeye hakuoneshwa kusita aknisikiliza na kutupa dawa ya mama ambaye ilimtaka atumie kwa muda wa siku mbili tu.


Maajabu yalianza kuonekana ndani ya siku moja kabla hata ya mama kumaliza dawa tulizopewa na daktari , mama alianza kutembea makovu yakaanza kufutika miguuni na siku hiyo tulikula pamoja hakukaa chumbani mwenyewe tena, taarifa zakiaanza kusambaa za mama kupona na hali ya kifafa haikuonekana tena asante daktari na dawa zako zimerejesha faraja kwenye familia yetu sasa zoezi la daad kuozwa limerudi mezani tunalikamilisha.


Share:

MWENGE WA UHURU WASISITIZA UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Ndugu Abdalla Shaibu Kaim amewaonya wananchi kutokufanya shughuli yoyote ikiwemo kilimo na ufungaji karibu na vyanzo vya maji kwani ni kinyume cha sheria na ni uharibifu wa Mazingira.

Ameongeza kwa kusema kuwa hairuhusiwi kwa mtu yeyote kufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa ya kukagua utekelezaji wa mradi wa utunzaji Mazingira unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwenye mradi wa maji Kigamboni.

“Hatua hii ni muhimu kwa ajili ya kulinda na kuviendeleza vyanzo vya maji pamoja na uoto wa asili ikizingatiwa kuwa maji ni uhai. Sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali za upandaji miti rafiki yenye kutunza mazingira katika vyanzo vyetu vya maji." amesisitiza Ndugu Kaim.

"Sheria, miongozo na kanuni zipo wazi kwani tunafanya hivyo kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji kwa kuwa maji ni uhai," ameeleza.

"Niwapongeze DAWASA kwa jitihada kubwa mnazozifanya za kulinda na kuendeleza Mazingira kwa kutunza vyanzo vya maji, mnafanya kazi nzuri, niwapongeze sana." ameeleza Ndugu Kaim.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Ndugu Kiula Kingu amesema kuwa katika jitihada za kutunza na kuendelea vyanzo vya maji katika mradi wa maji Kigamboni, Mamlaka imefanikisha kupanda miti ya matunda na kivuli takribani miti 3,300.

"Huu ni mpango endelevu ambapo katika awamu ya kwanza tumeanza kupanda miti 1,800 kwenye eneo la tenki kubwa la maji." amesema.

Amebainisha kuwa mpango wa upandaji miti Kigamboni ulitekelezwa kwa kushirikisha wananchi wa maeneo jirani kwa kuwapa elimu ya umuhimu wa utunzaji wa Mazingira ili waweze kutunza na kunufaika na mazao ya miti hii.

"Utunzaji wa Mazingira ni mojawapo ya kipaumbele cha Mamlaka kwa kuwa tunaelewa uendelevu wa huduma ya maji unategemea usalama wa vyanzo vya maji, hivyo DAWASA imeweka nguvu kubwa katika kuhakikisha vyanzo vya maji ikiwemo vya Mto Ruvu na visima virefu vinalindwa ipasavyo." ameeleza Ndugu Kingu.

Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zimeongozwa na kauli mbiu Tunza Mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa uchumi wa Taifa.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 26,2023



















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger