Wednesday, 24 May 2023

MTOTO WA TEMBO ALIYETUMBUKIA KISIMANI MANYONI AOKOLEWA

Maafisa Wahifadhi wa TAWA kutoka Pori la Akiba Muhesi wamefanikiwa kumuokoa mtoto wa tembo anaekadiriwa  kuwa na umri wa kati ya  wiki 2 au 3 aliyetumbukia katika kisima cha maji kitongoji cha Ipunguli, Kijiji cha Doroto Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Mtoto huyo wa tembo aliyekuwa amepoteana na kundi la wazazi wake alitumbukia kisimani katika harakati za kuwatafuta wazazi wake.

Baada ya zoezi la kumuokoa mtoto huyo wa tembo Mei 23, 2023,  Maafisa Wahifadhi wa TAWA walimpatia huduma ya kwanza, Kwa kumpa maziwa na  kulitafuta kundi la wazazi wake na hatimaye kumuunganisha pamoja nalo.

Hii ni mojawapo ya kazi za Maafisa na askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuhakikisha wanalinda na kuokoa maisha ya Wanyamapori Kwa faida ya kizazi kilichopo na vizazi vijavyo Ili waweze kufaidi urithi wa Nchi yao na kutekeleza Kwa vitendo Kauli Mbiu ya Wizara ya Maliasili na Utalii isemayo "Tumerithishwa...Tuwarithishe"

Share:

LIPANGILE ARUDISHA MTAANI KWAKE AKISHIRIKIANA NA MERIDIANBET


Mchezaji wa KMC Sadala Lipangile amefanikiwa kutimiza ahadi yake ya kurudisha kwenye jamii yake baada ya kushinda challenge ya penati iliyosimamiwa na Meridianbet baada ya kujikusanyia kiasi cha shilimgi Laki tano na leo amefika mtaani kwake Salasala na Kilongawima na kutoa msaada.

Mchezaji Sadala Lipangile aliungana na Meridianbet ambao ndio waratibu wa shindano hilo na kuweza kutoa msaada katika mitaa ya Salasala na Kilongawima kwa familia zenye uhitaji msaada uliotelewa leo ulijumuisha Mafuta ya kupikia, Sukari, Sabuni, Mchele, pamoja na vifaa vya kufanyia usafi.

Akiongea na wanahabari Sadala Lipangile alisema “Kwanza ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufika hapa leo, Lakini kubwa zaidi nawashukuru wadhamini wa timu ninayoitumiikia kwani imekua faraja kuifikia siku hii na kuweza kutoa msaada kwa jamii yangu iliyonikuza na kunilea nawashukuru sana Meridianbet kwa namna wanavyohakikisha wanarudisha kwa jamii hata kile kidogo wanachopata”

Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko kutoka Meridianbet Matina Nkurlu pia alipata nafasi ya kuzungumza “Hiki kilichofanywa na Lipangile ni uungwana kwa maana ya tafsiri ya Uungwana ni pamoja na kujali njia ulizopita na kuzipa faraja.

Jisajili Meridianbet upate mizunguko 50 ya bure kucheza kasino ya mtandaoni, jisajili leo ushinde mtonyo mrefu, twende kazi.

“Leo Meridianbet tukishirikiana na Sadala Lipangile kuzipa faraja familia na wakazi wa Salasala na Kilongawima alipoishi Lipangile hadi kufikia ndoto zake, Na kesho huenda akawa mtu mwingine mkubwa akafikia jamii yake kupitia sisi, Hivo basi tunaahidi huu utakua mwendelezo kutoka Meridianbet kwa kshirikiana na klabu ya KMC FC kurudisha kwenye jamii” Alisema Matina Nkurlu

Lakini pia waliopokea msaada hawakua nyuma katika kushukuru kile kilichofanywa na Sadala Lipangile kwa kushirikiana na Meridianbet na kusema wamefurahishwa sana na kilichofanywa na kijana wao kuweza kuwakumbuka na kuwapa msaada, Vilevile wakitoa shukrani kwa Meridianbet na kusema wao ni mfano wa kuigwa kwani wamekua wakirudisha kwenye jamii kila inapowezekana.

Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.

NB: Habari njema kwako, Meridianbet imesikia ombi la wengi imekuja na Jackpot kubwa ya mechi 13 kwa dau dogo la kuanzia 1,000/=TZS mshindi atajinyakulia donge nono la Tsh 85,000,000/= PIGA *149*10#

#MERIDIANBET CHAGUA TUKUPE

Share:

TBS KUADHIMISHA SIKU YA VIPIMO MEI 30,2023 JIJINI ARUSHA

Afisa Metrolojia TBS, Bi.Angela Charles akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 24,2023 katika Ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewakaribisha wadau mbalimbali kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Vipimo ambayo TBS inatarajia kusherekea Mei 30,2023 mkoani Arusha yenye kauli mbiu "VIPIMO VINAVYOUNGA MKONO MFUMO WA CHAKULA DUNIANI".

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 24,2023 Jijini Dar es Salaam, Afisa Metrolojia TBS, Bi.Angela Charles amesema kwa mwaka huu katika kusheherekea Siku ya Vipimo Duniani, wanaangalia dhana nzima ya upatikanaji wa chakula kutokana na ongezeko la watu Duniani.

Amesema mabadiliko ya hali ya hewa yameleta changamoto katika upatikanaji wa chakula hivyo basi kupitia kauli mbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku ya vipimo duniani, wanaangalia upatikanaji wa chakula pamoja na umuhimu wa vipimo katika mnyororo mzima wa thamani kwenye chakula kuanzia shambani hadi kumfikia mlaji.

Aidha amesema katika maadhimisho hayo wanategemea kuwa na Mada mbalimbali pamoja na kuwatembelea wadau wao walipo mkoani Arusha kwaajili ya kuendelea kutoa elimu ya namna ya kufanya vipimo sahihi na namna ya kupata na kutumia huduma zinazotolewa na TBS.

Kwa upande wake Mmetrolojia Mkuu, Kitengo cha Maabara ya Metrolojia TBS, Bw.Joseph Mahilla amewataka wananchi kuzingatia vipimo ambavyo ni sahihi katika hatua za uzalishaji wa chakula kuanzia shambani hadi kumfikia mlaji.

Hata hivyo amewataka wananchi kuhakikisha mbegu ambazo wanazitumia katika uzalishaji ni zile ambazo zimethibitishwa ubora.

"Kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu, tuaanza kuangalia vipimo kuanzia mwanzo wa mfumo wote wa chakula, utaanzia kwenye maabara ya utafiti ambao unaangalia ni aina gani wa udongo unafaa kwaajili ya zao fulani". Amesema Bw.Mahilla.

Mmetrolojia Mkuu, Kitengo cha Maabara ya Metrolojia TBS, Bw.Joseph Mahilla akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 24,2023 katika Ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam
Share:

LIFT YA MILLENIUM TOWER YAPOROMOKA...YAJERUHI SABA


Katika hali isiyotarajiwa lifti iliyopo katika jengo la ghorofa la Millenium Tower Makumbusho jijini Dar es salaam imeporomoka na kujeruhi watu saba.


 Inaelezwa kuwa chanzo ni kushindwa kuhimili uzito mkubwa kinyume na kiwango chake ambapo ilibeba watu zaidi ya 10.
Share:

Tuesday, 23 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 24,2023





















Share:

JISHINDIE TV UKICHEZA KASINO



 Hii hapa nyingine kutoka kasino ya mtandaoni ya Meridianbet ni promosheni kubwa kwa wateja watakaocheza mchezo wa kasino 3 dancing Monkey, mshindi atapewa TV mpya Inch 55.

 

Promosheni hii ya kijanja ambayo ni maalum kwaajili ya kufunga mwezi May na kuukaribisha mwezi wa mavuno Juni, imeanza tarehe 22 May, 2023 mpaka 31 May 2023, mshindi atatangazwa Juni 1, 2023.

 

Mshindi wa promosheni ya mchezo wa 3 dancing monkey atapatikana kwa kuangalia idadi kubwa Zaidi ya michezo na dau alilotumia kucheza mchezo wa kasino ya mtandaoni. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.

 

Njia za Kucheza na Kushinda 3 dancing Monkey

 

“3 dancing Monkey” ni mchezo wa karata kutoka kasino ya mtandaoni ya Meridianbet, mchezo huu hautumii kadi badala yake unatumia herufi mfan A, J, Q na K kila herufi ina kiwango chake cha malipo.

 

Ili kushinda mchezo huu unapaswa kuanza kwa kuweka dau lako unalotaka huku dau la chini ni kuanzia 750 na la juu Zaidi ni Tsh 350,000/=, malipo yanatokana na mstari wa kulia na kushoto endapo karata itadondokea kwenye herufi kati ya A, J, Q, na K.

 

Mbali na hayo mchezo huu unakupatia mizunguko kuanzia 1 mpaka 5000x ya bure kadri uchezavyo na mizunguko hii ipo ya aina tatu ikitokea alama ya Wild inakupa machaguo yenye rangi ya kijani, buluu na nyekundu kila moja inakulipa kulingana na ushindi wako ambapo ushindi wa juu kabisa ni 12,077x odds

 

Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye sloti na michezo ya kasino kama Poker, Aviator, Roulette.

 

N.B: Jambo kubwa jingine ni kwamba, Meridianbet wanakupa mizunguko ya bure kucheza kwenye kasino ya mtandaoni kwa mteja mpya baada ya kujisajili. Unasubiri nini ingia mchezoni kufurahia ofa hizi.


Share:

SERIKALI YARIDHIA KUONGEZWA MUDA WA TATHMINI YA HALI YA VYOMBO VYA HABARI NCHINI



Na Dotto Kwilasa,Dodoma.

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na teknolojia ya Habari,imeridhia kuiongezea muda wa miezi sita  Kamati ya Tathmini ya hali ya uchumi kwa Vyombo vya Habari na Wanahabari nchini  ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi.

Waziri wa Habari,Mawasiliano na teknolojia ya Habari,Nape Nauye ametoa kauli hiyo leo Mei 23,2023 Jijini Dodoma mara baada ya Kukutana na Kamati hiyo huku ikiomba kuongezewa muda huo kutokana na kazi waliyopewa  kuhitaji utafiti wa kina na waki taalam  na muda wa miezi mitatu ambao walipewa awali kutotosha.

Katika hatua nyingine Waziri Nape ametoa wito kwa wadaiwa wote   ambao wanadaiwa na Vyombo mbalimbali vya Habari  hapa nchini kulipa madeni hayo.

Amesema tathimini ya hali ya uchumi wa vyombo vya habari nchini inatarajiwa kutolewa mwezi Novemba mwaka huu, huku serikali ikiwata waandishi wa habari pamoja na wadau wa tasnia hiyo kutoa ushirikiano kwa kamati husika ili kunuru vyombo vya habari nchini.

“Nimekutaka na Kamati hii awali tulikuwa tumeipa miezi mitatu lakini kutokana na umuhimu wa tasnia hii na maagizo ya Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa jambo hili lisifanywe kwa kuhalakishwa bali lifanywe kwa umakini wa hali ya juu ili kuleta mabadiliko katika tasnia hii”amesema Nape

Waziri huyo, amesema kamati hiyo badala ya kuharakisha jambo hilo inapaswa kufanya tafiti za kina kwa kuhusisha wadau wengi ili kupata maoni ambayo yatakuwa na manufaa na vyombo vya habari nchini.

“Jambo hili linasubiriwa sana na dunia watu wanataka kuona nini Tanzania inakwenda kufanya katika kuleta mageuzi kwenye tasnia hii ya vyombo vya habari nchini hivyo lazima tuje na kitu kinacholeta mabadilko kwa vyombo vyetu vya habari nchini”amesema

Amesema hadi sasa anaridhishwa na kazi ambayo inaendelea kufanywa na kamati hiyo kutokana na kushirikisha wataalam kutoka  nyanja mbalimbali ambao wameongeza tija katika tathimini hiyo.

“Kutokana na ramani ambayo kamati hii imeichora hadi sasa inaonyesha ni kwa jinsi gani inakwenda kuleta mambo ambayo yatakwenda kujibu changamoto mbalimbali zinazo ikabili sekta hii ya habari.

“Hivyo basi nitowe wito kwa waandishi wa habari na wadau wengine wa habari nchini kutoa ushirikiano kwa kamati hii ili ifanikishe jambo hili na kuleta mabadiliko kwenye vyombo vya habari ambavyo vingi hivi sasa vipo hoi”amesema Nape

Katika nyingine waziri hiyo wa Habari amesema wakati jambo hilo likiendele mchakato wa sheria ya vyombo vya habari pamoja na sera utaendelea na kama itaoneka ipo haja kufanyiwa maboresho yatafanywa.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya kutathmini  hali ya uchumi kwa Vyombo vya Habarai na wanahabari,Tido Mhando  ameomba Serikali kuwaongezea muda kutokana na kazi hiyo kuhitaji utafiti wa kitaalam  zaidi.


Amesema kuwa yeye pamoja na wajumbe wote wamelivalia njuga suala hilo ili kusaidia vyombo vya habari na wanahabari nchini.

Kadhalika, Mhando amesema watahakikisha jambo hilo linakamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu kwa mujibu wa muongozo waliopewa ili kulisaidia taifa.

“Matatizo ya vyombo vya habari yapo sehemu nyingi duniani inasikitisha sana kuona wanahabari nchini kuendelea kuwa ombaomba na kutegemea bahasha ili waishi na kutokuwa na uhakika wa kesho yao”alisisitiza Mhando.

Kamati hiyo iliundwa rasmi Januari 23 Mwaka huu ikiwa na Wajumbe tisa  ikiongozwa na Mwenyekiti wake Tido Mhando na Katibu ni Gerson Msigwa ambayo  inatarajiwa kukamilisha kazi yake mnamo Mwezi  Novemba Mwaka huu.


Share:

FOOD LOSS AND WASTE IN FISHERIES SECTOR




Edwin Soko Tanzania

Food loss and waste in fisheries can occur at various stages of the supply chain, from the time the fish is caught to the time it reaches the consumer. Some of the main  causes of food loss and waste in fisheries include:

1. Discards: Fish that are caught but not intended for sale or consumption are often thrown back into the sea. This can happen because the fish are too small, the wrong species, or because the vessel has reached its catch quota.

2. Spoilage: Fish that are not properly handled or stored can spoil quickly, leading to food loss and waste. This can happen if the fish are not properly chilled or if they are stored for too long before being sold or consumed.

3. Processing: During processing, fish can be damaged or lost due to improper handling or equipment failure. This can result in a significant amount of food waste.

4. Distribution and retail: Fish that are not sold or consumed at the retail level may be discarded, leading to food waste. This can happen if the fish are not properly packaged or if they do not meet certain quality standards.

Food loss and waste in the fisheries sector can have significant economic, environmental, and social impacts. It can lead to lower incomes for fishermen, increased pressure on fish stocks, and contribute to greenhouse gas emissions from decomposing waste. In order to reduce food loss and waste in fisheries, improved handling and storage practices, better processing technologies, and more efficient distribution systems may be necessary. Additionally, efforts to reduce discards and improve the utilization of bycatch could help to reduce food loss and waste in the fisheries sector.
Share:

JITU LA MIRABA MINNE LAMEGA TUNDA LA MKE WANGU NA KUONDOKA NA WATOTO....AKUTWA NA BALAA

 

Ilikuwa machi mwaka huu ambapo tulikuwa tumeenda na mke wangu kijijini kwa ajili ya likizo fupi, lakini mke wangu aliitwa kazini ghafla na hapo nikamruhusu arudi mjini kwa shughuli za kikazi kwa kuwa mimi bado nilikuwa na mambo yangu.


Baada tu ya yeye kufika mjini, nami Meneja wangu alinipigia simu akanieleza kuwa ninahitajika kazini ili niweze kusambaza bidhaa flani kwani likizo yangu imesitishwa, sikuwa na budi bali kurejea mjini kwa wakati ule ingawaje nauli ilikuwa juu sana.


Nilifika mjini saa nne usiku na hapo nikafanikiwa kupata teksi iliyonifikisha hadi nyumbani, lakini mazingira niliyoyakuta yalikuwa sio ya kawaida jambo lililo nishangaza.

Haikuwa kawaida ya mke wangu kuzima taa za chumba chetu mapema vile, nilijua lazima kutakuwa na jambo, nilifungua mlango na kukupata watoto wetu  wamelala sebuleni. 

Niliamua kwenda katika chumba chetu, nilipokuwa katika veranda ya chumba chetu, ghafla nilisikia sauti “Endelea kabisa, unanipa raha ajabu" nilipandwa na mori na kufungua mlango kwa kishindo, nikakutana na jitu la miraba minne likishiriki ngono na mke wangu.

Nilipomuuliza yule mwanaume nini alichokuwa akifanya chumbani mwangu alinizaba kofi nikaanguka sakafuni na kunitishia maisha, baada ya muda waliondoka pamoja, pia aliwabeba watoto wote na wakaondoka nao.

Siku iliyofuatia nilielekea kazini lakini kwa ajili ya msononeko niliyokuwa nao moyoni, Meneja wangu alifahamu kwamba sikuwa sawa, kila mara aliniuliza nini tatizo.

Nashukuru Anna ambaye alikuwa Mhasibu kwenye kampuni yetu alinishauri kuwa African Doctors wanaweza kunisaidia kwani aliweza kuirejesha ndoa yake na mume wake ambayo ilikuwa kwenye hali mbaya na sasa wanaishi vizuri.

Nilifunga safari na kuenda kwa African Doctors alinihudumia na kurejea nyumbani, baada ya siku moja nilipokea simu ambapo mke wangu alilalamika kwamba wamenasiana na jitu lile wakati wakifanya mapenzi.

Nilifahamu fika kwamba African Doctors alikuwa keshasababisha mambo yake, baadaye nilifika sehemu waliyokuwa na kumpigia simu African Doctors, alitoa maelekezo ya kufanya ikiwa ni pamoja na jitu lile kulipa faini ya Ksh30,000, baada ya vile waliweza kuachana.

Mke wangu aliniomba msamaha na kujutia kosa lake, tulisameana na kurudi pamoja kama mke na mume jinsi tulivyokuwa zamani. Tangu siku ile ndoa yetu imekuwa yenye furaha kila wakati.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:

BARRICK BULYANHULU YAFIKISHA KAMPENI YA USALAMA YA ‘JOURNEY TO ZERO’ KWENYE JAMII


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare,akitoa zawadi ya jaketi la kinga ya ajali (Reflector) kwa mmoja wa waendesha punda za kubeba mizigo wakati wa mafunzo ya uhamasishaji usalama kwa jamii yaliyoandaliwa na kampuni hiyo na kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kakola wilayani Msalala jana.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare,akiongea na wananchi wakati wa mafunzo hayo ya usalama kwa jamii.

***
Katika jitihada za kuhakikisha jamii inakuwa salama,Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia kauli mbiu yake ya kuhamasisha usalama ya Journey to Zero imeshirikiana na Jeshi la Polisi kutoa mafunzo ya usalama katika jamii wilayani Msalala mkoani Shinyanga.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi ya Kakola yalihusisha viongozi wa vijiji na kata mbalimbali, wananchi, wanafunzi na waendesha pikipiki na mifugo ya kubebea mizigo.

Katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Maofisa kutoka Jeshi la Polisi na wataalamu wa usalama kutoka Mgodi wa Bulyanhulu wananchi walipata elimu kuhusiana na usalama barabarani, kukabiliana na majanga ya moto pia waendesha pikipiki na wanyama wa kubeba mizigo waligawiwa jaketi maalumu (Reflectors) kwa ajili ya kuwawezesha kuonekana kwa urahisi wanapotembea usiku ili wasigongwe na magari.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare, alisema Usalama ni suala ambalo kampuni ya Barrick inalipa kipaumbele kikubwa na ndio maana imeamua kuandaa programu za kuelimisha jamii kuzingatia usalama lengo kubwa likiwa ni kutokomeza vitendo hatarishi kwa usalama wa wananchi.

Sangare, alisema ili kufanikisha suala hili ni jukumu la kila mmoja kuzingatia kujilinda na kuwalinda wenzake sambamba na kuhakikisha anapinga na kukemea matukio yanayoweza kusababisha matukio ya ajali.

”Barrick kupitia kauli mbinu yetu ya Journey to Zero tutaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kutokomeza matukio ya ajali nchini” ,alisema.

Akiongea kwa niaba ya viongozi wa vijiji na madiwani kutoka kata mbalimbali waliohudhuria katika mafunzo hayo,Diwani wa kata ya Bugarama, Prisca Msoma, aliishukuru Barrick Bulyanhulu, kwa kuja na programu ya kuelimisha jamii masuala ya usalama kuanzia wa barabarani hadi majumbani sambamba na kugawa vifaa vya kujikinga na ajali katika makundi mbalimbali kwajamii.

“Kupitia Programu hii ya kuelimisha jamii masuala ya usalama,Barrick mmedhihirisha kuwa mnawajali wananchi katika jamii,kwa maana usalama ni suala la msingi kwa kila mtu na alitoa wito kwa wananchi kuzingatia mafunzo waliyoyapata pia alitoa wito kwa madereva kuanzia wa magari ,Pikipiki na wanyama wanaobeba mizigo kuzingatia usalam na kufuata alama za usalama barabarani”,alisema Msoma.


Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Msalala,Elias Msome, alisema Jeshi hilo litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wanaounga mkono jitihada za kutokomeza ajali na aliwahimiza wananchi kuzingatia kanuni za usalama wakati wote ili kufanikisha mkakati wa Serikali wa kuhakikisha matukio ya ajali zisizo za lazima zitokanazo na uzembe yanatokomezwa.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria mafunzo hayo katika jukwaa kuu
Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Msalala,Elias Masome akiongea na wananchi wakati wa mafunzo hayo.
Diwani wa Kata ya Bulyanhulu,Shija Luyombya akitoa shukrani kwa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuendesha mafunzo ya usalama barabarani.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi wilayani Msalala,John Kahibi akielezea matumizi ya alama za barabarani na sheria za barabarani kwa wananchi waliohudhuria mafunzo hayo.
Mtaalamu wa zimamoto kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu Eric Chacha, akitoa mafunzo ya kuzima moto.
Baadhi ya waendesha punda za kubeba mizigo kutoka vitongoji mbalimbali wilayani Msalala wakifurahia zawadi za jaketi za kinga ya ajali (Reflector) walizozawadiwa na Barrick Bulyanhulu wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya waendesha punda za kubeba mizigo kutoka vitongoji mbalimbali wilayani Msalala wakifurahia na viongozi wao na wafanyakazi wa Barrick baada ya kukabidhiwa zawadi ya jaketi za kinga ya ajali (Reflector) wakati wa mafunzo ya uhamasishaji usalama kwa jamii yaliyoandaliwa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Share:

Monday, 22 May 2023

SERIKALI IKABIDHI NDEGE  ATCL- MTATURU


MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameiomba serikali kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),ili kuchochea shughuli za utalii nchini.

Mtaturu ametoa ushauri huo Mei 22,2023,wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

“Kwenye hili nitaongea mambo mawili ili kukuza utalii nchini,ukiboresha Shirika letu la ndege utachochea shughuli z utalii nchini,watalii wengi watakuja lakini ukiwa na ndege yako mwenyewe biashara zinazofanyika katika maeneo mbalimbali duniani utakuwa na uhakika nazo,

“Niombe sana Mh Mwenyekiti,tunategemea kupata ndege ya Cargo hivi karibuni ambayo itarahisha biashara za mbogamboga na maua nchi za Ulaya na Asia,niombe sana Shirika hili liangaliwe na serikali iendelee kuliwezesha ili kuhakikisha kwamba linapata faida,”amesema.

Aidha,ameeleza changamoto ya madeni inayoikabili Shirika hilo na kuishauri serikali kubeba deni la Shilingi Bilioni 100 ambalo Shirika hilo linadaiwa.

“Awali wakati Shirika halifanyi kazi lilikuwa linadaiwa karibu Bilioni 236 na wamejitahidi kulipa karibu Bilioni 136 na sasa wamebakiwa na deni la Bilioni 100,niombe serikali iangalie namna ya kulipa deni hili ili kuweza kuweka mizania sawa ya hesabu ya shirika hilo na hivyo liweze kuondokana na hasara ambayo imeweza kujitokeza,”amesema.

Changamoto nyingine aliyoitaja ni kukamatwa kwa ndege katika nchi nyingine ambazo zinaidai Tanzania,“Ndege hizi zimekuwa zinashikwa lakini sio kwamba ATCL inadaiwa bali inadaiwa serikali lakini kwa sababu Shirika la Ndege linamilikiwa na Wakala wa Ndege wa Serikali (ATGF),ndio maana deni lolote linalohusu serikali likipatikana ndege inakamatwa na hivyo kuondoa mtiririko wa usafiri,

Amesema ndege kama inaenda Mumbai au nchi nyingine ukiiondoa maana yake unapunguza mtiririko wa abiria hivyo usitegemee kupata faida.

“Leo hii CAG akienda anaona kila siku Shirika linapata hasara kwa sababu ni mpango ambao tumeuweka wenyewe ,niombe sana serikali iangalie uwezekano wa kuhakikisha ndege hizi za ATCL iweze kumilikiwa na Shirika lenyewe ili kuleta faida na kulifanya shirika liweze kufanya kazi vizuri,”amesema.

Amesema kwa sasa ATCL inalipa Shilingi Milioni 700 kwa ajili ya kukodisha ndege ya serikali jambo ambalo linashangaza kwa serikali kukodishana ndege ilhali ni kitu kimoja.

“Kwa mantiki hii Shirika letu haliwezi kuendelea kwa kuwa linakwama na mambo mengi,Waziri akirudi aseme ni mpango gani wa serikali umefikiwa wa kurudisha ndege hizi ATCL kuondoka kwenye wakala wa ndege wa serikali ili kuondokana na changamoto ambazo shirika inazipata,”ameongeza.
Share:

MBUNGE MTATURU AOMBA KILOMITA 10 ZA LAMI


MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amechangia bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya mwaka 2023/2024,huku akitoa ombi kwa serikali kwenye mambo matatu ikiwemo kuanza ujenzi wa barabara ya Handeni-Kiblashi – Kwamtoro –Kiteto hadi Singida ili kuongeza uchumi wa wananchi wa maeneo hayo.

Aidha,ameiomba serikali kujenga kilomita 10 za lami kutoka Ikungi Londoni kwenda Kilimatinde Solya ili kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo eneo la Mang’onyi.

Akichangia bajeti hiyo Mei 22,Bungeni Jijini Dodoma,Mtaturu amesema barabara hiyo ikikamilika itaongeza ufanisi katika bandari ya Tanga.

“Leo waziri ametuambia tunaenda kusaini barabara zenye urefu wa kilomita 2,035,niombe sana mkandarasi apatikane mapema kwenye barabara hii ya Handeni hadi Singida yenye urefu wa Kilomita 460 ili maboresho tuliyoyafanya kwenye bandari ya Tanga yapate majibu,

“Tumeambiwa mwezi wa sita utasainiwa mkataba nimuombe Waziri kwa heshima kabisa tuhakikishe barabara inasainiwa mapema ili wabunge wa maeneo ukitoka pale Handeni ndugu yangu Omary Kigua,ndugu yangu wa Kiteto Edward Ole Lekaita, ndugu yangu Mohammed Monni wa Chemba pamoja na mimi mwenyewe tuweze kufarijika wananchi wetu wakipata lami,”ameeleza.

Akizungumzia ombi la Kilomita 10 za lami katika Wilaya ya Ikungi amesema barabara hiyo ikijengwa itaongeza thamani ya mradi wa mgodi wa madini ya dhahabu wa Shanta.

“Mh Waziri mlinipa kilomita moja ndani ya wilaya yangu ya Ikungi,niombe sana mniongezee kilomita 10 barabara ya kutoka Ikungi Londoni kwenda Kilimatinde Solya kwa ndugu yangu Chaya ili barabara ile ijengwe kwa kiwango cha lami na kwa kuwa tuna muwekezaji pale wa madini ambaye yupo eneo la Mang’onyi,ikiwekwa lami barabara hii itaongeza thamani ya mradi ule,”amebainisha.
Share:

KAMATI MPYA MUHAS YATAKIWA KUTOA MAONI NA USHAURI KUBORESHA MITAALA NA UANDAAJI WA MITAALA MIPYA


KAMATI mpya ya Ushauri wa Kisekta ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) imetakiwa kutoa maoni na ushauri utakaowezesha kuboresha mitaala na uandaaji wa mitaala mipya itakayoendana na wakati, kutilia mkazo mahitaji ya soko, ujuzi na kuboresha usimamizi wa mafunzo kwa vitendo.

Agizo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akimwakilisha Waziri wa Elimu kuzindua Kamati hiyo pamoja na mafunzo ya uaandaji mitaala ambapo amesema kufanya hivyo kutasaidia Chuo kuendelea kutoa wahitimu bora na wenye ujuzi stahiki.

Prof. Mdoe pia ameitaka Kamati hiyo kuangalia mahitaji ya taaluma na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na kushauri maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho ili kujumuisha maarifa ya kisasa, umahiri, kujenga ubunifu, kukuza stadi za kazi na viwango vya kimataifa.

“Nimefarijika kujulishwa kuwa wajumbe wateule wa Kamati wanatoka katika makampuni/Taasisi ambazo majukumu yake yanaendana na fani zinazofundishwa hapa MUHAS. Kwa msingi huo sina wasiwasi na weledi, ujuzi na uzoefu wenu. Ni matumani yangu kuwa ujuzi na uzoefu wenu mkubwa utakuwa na manufaa katika kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kitaaluma hapa chuoni,” amesema Prof. Mdoe.

Ameongeza “kupitia Mradi wa HEET tumetenga Shilingi bilioni 18.23 ambazo zitatumika kuhuisha na kuandaa mitaala mipya zaidi ya 300 ya Taasisi za elimu ya juu lengo ni kuhakikisha elimu inayotolewa inaendana na kujibu mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi,”

Akizungumzia utekelezaji wa Mradi wa HEET kwa MUHAS amesema utajikita katika kukarabati na kujenga Kampasi ya Mloganzila (Ndaki ya Tiba) na Kigoma, kuboresha miundombinu ya kujifunza na kufundishia, kuhuisha au kuandaa mitaala, kusomesha watumishi, kuweka miundombinu ya kisasa ya TEHAMA pamoja na kuweka mifumo ya kidijitali kwa ajili ya kufundishia na utawala.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dkt. Harrison Mwakyembe amemuhakikishia Prof. Mdoe kuwa watasimamia utekelezaji wa mradi huo kwa umakini ili uweze kuwa na matokeo chanya.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Juu ambae pia ni Mratibu wa Taifa wa Mradi wa HEET Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Kenneth Hossea amesema Mradi unaotekelezwa MUHAS ni kati ya miradi mitatu mikubwa katika Taasisi 23 zinazofaidika na mradi huu na kuwaomba ushirikiano ili kuhakikisha pamoja na kuwa mradi umechelewa kuanza utekelezaji wake uweze kufikia malengo.

Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Andrea Pembe amesema Chuo kinajivunia kuwa kitovu cha mafunzo katika nyanja ya afya na kwamba siku zote kitaimarisha ubora wa mafunzo yanayotolewa. Amesema pamoja na mafanikio yaliyoyapatikana ikiwemo ukuaji wa tafiti, Chuo kwa sasa kipo katika kuongeza nguzo kuu mbili ambazo ni kubadilisha ubunifu unaofanyika kuwa bidhaa ambayo itapelekea nguzo ya tano ambayo ni viwanda.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger