Monday, 22 May 2023

KAMATI MPYA MUHAS YATAKIWA KUTOA MAONI NA USHAURI KUBORESHA MITAALA NA UANDAAJI WA MITAALA MIPYA


KAMATI mpya ya Ushauri wa Kisekta ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) imetakiwa kutoa maoni na ushauri utakaowezesha kuboresha mitaala na uandaaji wa mitaala mipya itakayoendana na wakati, kutilia mkazo mahitaji ya soko, ujuzi na kuboresha usimamizi wa mafunzo kwa vitendo.

Agizo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akimwakilisha Waziri wa Elimu kuzindua Kamati hiyo pamoja na mafunzo ya uaandaji mitaala ambapo amesema kufanya hivyo kutasaidia Chuo kuendelea kutoa wahitimu bora na wenye ujuzi stahiki.

Prof. Mdoe pia ameitaka Kamati hiyo kuangalia mahitaji ya taaluma na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na kushauri maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho ili kujumuisha maarifa ya kisasa, umahiri, kujenga ubunifu, kukuza stadi za kazi na viwango vya kimataifa.

“Nimefarijika kujulishwa kuwa wajumbe wateule wa Kamati wanatoka katika makampuni/Taasisi ambazo majukumu yake yanaendana na fani zinazofundishwa hapa MUHAS. Kwa msingi huo sina wasiwasi na weledi, ujuzi na uzoefu wenu. Ni matumani yangu kuwa ujuzi na uzoefu wenu mkubwa utakuwa na manufaa katika kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kitaaluma hapa chuoni,” amesema Prof. Mdoe.

Ameongeza “kupitia Mradi wa HEET tumetenga Shilingi bilioni 18.23 ambazo zitatumika kuhuisha na kuandaa mitaala mipya zaidi ya 300 ya Taasisi za elimu ya juu lengo ni kuhakikisha elimu inayotolewa inaendana na kujibu mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi,”

Akizungumzia utekelezaji wa Mradi wa HEET kwa MUHAS amesema utajikita katika kukarabati na kujenga Kampasi ya Mloganzila (Ndaki ya Tiba) na Kigoma, kuboresha miundombinu ya kujifunza na kufundishia, kuhuisha au kuandaa mitaala, kusomesha watumishi, kuweka miundombinu ya kisasa ya TEHAMA pamoja na kuweka mifumo ya kidijitali kwa ajili ya kufundishia na utawala.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dkt. Harrison Mwakyembe amemuhakikishia Prof. Mdoe kuwa watasimamia utekelezaji wa mradi huo kwa umakini ili uweze kuwa na matokeo chanya.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Juu ambae pia ni Mratibu wa Taifa wa Mradi wa HEET Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Kenneth Hossea amesema Mradi unaotekelezwa MUHAS ni kati ya miradi mitatu mikubwa katika Taasisi 23 zinazofaidika na mradi huu na kuwaomba ushirikiano ili kuhakikisha pamoja na kuwa mradi umechelewa kuanza utekelezaji wake uweze kufikia malengo.

Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Andrea Pembe amesema Chuo kinajivunia kuwa kitovu cha mafunzo katika nyanja ya afya na kwamba siku zote kitaimarisha ubora wa mafunzo yanayotolewa. Amesema pamoja na mafanikio yaliyoyapatikana ikiwemo ukuaji wa tafiti, Chuo kwa sasa kipo katika kuongeza nguzo kuu mbili ambazo ni kubadilisha ubunifu unaofanyika kuwa bidhaa ambayo itapelekea nguzo ya tano ambayo ni viwanda.
Share:

NILIBEBA UJAUZITO BAADA YA KUITWA MGUMBA

Nilitaka sana na kutamani kwa muda mrefu lakini haikuwezekana kabisa, mwanzoni nilidhania kuwa kizazi change kiko mbali lakini wala ilikuwa tu ni magonjwa yaliyo nishambulia kipindi cha nyuma na kuniacha na makovu yasiyofutika sikuweza kubeba ujauzito hata mara mmoja.

Haya yote niliyajuwa nilipoamfahamu bingwa daktari BAKONGWA  wa https://bakongwadocotors.com na bila msaada wa mama yasinta muuzaji wa mayai nisingepata mtoto yawezekana kabisa ningefariki na ugumba wangu au nisingeolewa kabisa.


Madktari wote wakubwa walioko Tanzania wanao sifiwa niliwatembelea na kuwaeleza shida inayo nisumbuwa lakini wao waiishia kunipea ratiba ya miale na dawa za kutumia ambazo hazikuleta matunda yoyote yale kwangu.

Nimempoteza mwanaume wa ndoto zangu ambaye tumeishi naye kwake pasipo kutambulishana ilikuwa ni kipindi cha kujuana lakini alipo fahamu kuwa mimi sibebi ujauzito hapo ndipo ulikuwa mwisho wa mahusiano yetu na mipango yetu mizuri yote ikayeyuka.

Hospitali nilizotembea waliniambia kuwa kwa sababu za magonjwa yaliyonisumbuwa sana utotoni na kushindwa kujitibu mapema kwa wakati ndio chanzo cha kuniacha mimi niwe mgumba -- yaani  siwezi kubeba ujauzito tena hata kwa dawa ya mtindo gani isingekuwa rahisi.

Imani yangu ikabakia kwenye kuitwa shangazi na watoto wa kaka zangu  tu maana sasa hakuna hata mwanaume ambaye anaweza kuowa mwanamke asiyezaa kamwe hayupo mimi nimeyaona hayo mwenyewe kwenye ndoa zangu.

Nikaanzishiwa tiba mbadala na mama yangu mzazi za kienyeji kwa hau sana ya kuzaa nikazinywa na uchungu wake uleule lakini nalo bado lilikuwa ni jaribu linguine tena kwangu hakuna ujauzito wala dalili yoyote ile kwangu.

 Mama Yasinta jirani sana na mama siku hiyo alikuja kunitembelea nyumbani alikuwa kwenye uuzaji wake wa mayai wa kila siku nilipomweleza shida zangu ndio akaanza kufunga yote anayoyajuwa.

Kwanza alishangazwa kwa kuwa yeye alijuwa tayari mimi nimeolew muda mrefu, nikamjibu niliolewa lakini nimeachika kwa kushindwa kubeba ujauzito na madaktari walikwisha sema mimi ni mgumba siwezi kuzaa kwa sababu ya magonjwa yaliyo wahi kunishika kipindi cha nyuma.

Mama yasinta akapayuka kwa ujasiri mcheki daktari bakongwa wengu wanamsema kuwa anaweza , nilipomuuliza nitampataje aliniandikia nambari zake za whatsapp +243990627777 kisha nikazipokea nakuzipiga moja kwa moja.

Upande wa pili wa simu daktari alipokea na kunielekeza nini shida zilizo nizuia kubeba ujauzito akanipa maelekezo ya kutosha na kisha akanitumia dawa ya matumizi ya masaa saba tu ambaye ilipofika ilikuja na kikaratasi chenye maelekezo ya kufuata.

Nilipopokea dawa nikaaza kutumia na baada ya dawa nilikutana na mwanaume tena ilikuwa ni siku zangu za hatari ghafla tu siku tatu baadaye nikaanza kuona mabadiliko mwilini mwangu nilipoamuwa kupima kila mmoja alishangazwa nilikuwa ni mjamzito, asante daktari kwa uaminifu wa dawa zako.



Share:

PROFESA MKENDA KUFUNGUA MAONESHO YA NANE YA TAFITI NA UBUNIFU UDSM

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda anatarajia kufungua maonesho ya nane ya Utafiti na Ubunifu yanayotarajia kuanza Mei 23 - 25, 2023 katika Viwanja vya Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Akizungumza na Wanahabari Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Utafiti, Profesa Lettice Rutashobya
amesema maonesho hayo yenye kauli mbiu "Utafiti na Ubunifu kwa Ustawi wa Uchumi - jamii nchini Tanzania"


Prof. Nelson Boniface amesema kuwa maonesho hayo yatataguliwa na ufunguzi ambapo wazungumzaji watakuwa ni Leticia Lutashobya ambaye ni mbobezi katika masuala ya biashara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Michael Shirima mwenyekiti na Mwanzilishi wa Presicion Air Tanzania.


Amesema kuwa katika maonesho hayo ya nane wanatarajia kuonesha miradi 99 iliyotokana na maonesho yalifanyika katika ngazi ya vitengo ambapo jumla ya miradi 350 na wakachagua hiyo 99.


"Malengo ya Tafiti hizi ni kuwavutia wanataaluma kutoka chuo chetu na taasisi nyingine zinazohusiana na Taaluma Pamoja na utafiti na watu wote wa serikalini ikijumlisha wenye viwanda kuja kushuhudia tafiti na bunifu zao wanazofanya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam," amesema Prof. Nelson Boniface.


Ameongeza kuwa tafiti zote zinazofanywa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zinalengo la kuboresha maisha ya Watanzania hivyo ni vyema watu wakajitokeza kwa wingi kuhudhuria maonesho hayo ili waweze kujifunza mambo mbali mbali. --
Share:

NIT KUJENGA MAJENGO 8, IKIWA 5 KAMPASI YA MABIBO DSM NA 3 UWANJA WA NDEGE KIA KWA AJILI YA MAFUNZO YA MARUBANI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akisoma hotuba wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara yake kwa Mwaka 2023/24 leo Mei 22,2023 Bungeni Dodoma.

****************

NA EMMANUEL MBATILO

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeendelea kutekeleza mradi wa kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga na Operesheni za Usafirishaji unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Mradi huo utaimarisha miundombinu na ununuzi wa vifaa vya kufundishia ambapo unajumuisha ujenzi wa majengo nane (8) ikiwa majengo matano (5) yanajengwa katika Kampasi ya Mabibo Dar-es-Salaam kwa ajili ya kufundishia Wahandisi wa Ndege na Wahudumu wa Ndani ya Ndege na majengo matatu (3) yatajengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya mafunzo ya Marubani.

Aidha, ujenzi wa majengo matano (5) unaendelea ambapo umefikia hatua ya kusimamisha nguzo za jengo hilo na ujenzi wa majengo matatu (3) upo katika hatua za kumpata Mshauri elekezi wa usanifu.

Hayo yameelezwa leo Mei 22, 2023 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara yake kwa Mwaka 2023/24.

Amesema kupitia kituo cha umahiri cha mafunzo ya taaluma za usafiri wa anga na operesheni za usafirishaji kilichoanzishwa chini ya mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, NIT imenunua vifaa vya mafunzo ambavyo ni Aircraft Engineering System Trainers; Virtual Maintenance Trainer kwa ajili ya mafunzo ya Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege; na Fixed Cabin Crew Mock – Up kwa ajili ya mafunzo ya Wahudumu wa ndani ya Ndege.

"Katika kuimarisha mafunzo ya taaluma za usafiri wa anga, Serikali kupitia NIT imenunua Ndege mbili (2) zenye injini moja (1) kwa ajili ya kufundishia Marubani pamoja na Full Motion Cabin Crew Mock-Up yaani kifaa maalum cha kufundishia Wahudumu wa ndani ya Ndege". Amesema Prof. Mbarawa

Pamoja na hayo amesema NIT kupitia Kituo cha Kikanda cha Umahiri cha Mafunzo ya Usalama Barabarani kilichoanzishwa kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kimeendelea kutekeleza majukumu yake ambapo hadi kufikia Aprili, 2023, tathmini ya kumpata Mshauri Elekezi ambaye ataandaa mitaala na miongozo ya kufundishia pamoja na kupata ithibati ya kimataifa ipo kwenye hatua za mwisho.

Hata hivyo amesema Kituo kupitia ufadhili wa AfDB kinaendelea na hatua za ununuzi wa vifaa vya kufundishia mafunzo ya Usalama Barabarani ikiwemo Teleconferencing System pamoja na Geographic Information System (GIS) and Remote Sensing.

Amesema NIT imeendelea kutoa mafunzo, kufanya tafiti, kutoa ushauri wa kitaalam na machapisho kwa lengo la kufundisha wataalam katika njia za usafirishaji ambazo ni Barabara, Anga, Reli, Maji na Bomba (Pipeline).

Ameeleza kuwa katika mwaka wa masomo 2022/23, Chuo kilitoa mafunzo ya kozi ndefu 34 ikilinganishwa na kozi 33 zilizotolewa katika mwaka wa masomo 2021/22 ikiwa ni ongezeko la kozi moja (1) sawa na asilimia 3. Kwa sasa Chuo kina wanafunzi wa kozi ndefu 14,920 ikilinganishwa na wanafunzi 12,942 katika mwaka wa masomo 2021/22 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,978 sawa na asilimia 15.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akisoma hotuba wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara yake kwa Mwaka 2023/24 leo Mei 22,2023 Bungeni Dodoma.

Share:

MFUKO WA WCF WATOA MAFUNZO YA TATHMINI KWA MADAKTARI KANDA YA ZIWA

Zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wamepewa mafunzo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), ili kuwawezesha kufanya tathmini stahiki kwa wafanyakazi wanaopata majanga kazini.

Akifungua mafunzo hayo yanayofanyika jijini Mwanza kwa muda wa siku tano kuanzia Jumatatu Mei 22, 2022, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amewataka washiriki kuzingatia elimu watakayoipata.

“Mkahakikishe tathmini zinafanyika kwa usahihi na wafanyakazi watakaopata majanga ya ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wapate fidia stahiki na kwa wakati. Hii itaongeza ari kwa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii wakijua wana uhakika wa kinga ya majanga kazini” amesema Masala.

Masala ambaye amefungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla ameongeza kuwa ni vyema waajiri wakahakikisha wafanyakazi wao wanajiunga na mfuko wa WCF ili kuondolewa mzigo wa gharama za majanga mbalimbali yanayoweza kutokea kazini.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omar akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, amesema mafunzo hayo yatawaongezea weledi madaktari hao kufanya tathmini sahihi na kwa wakati hatua itakayosaidia pia wafanyakazi wanaopata majanga kazini kulipwa fidia stahiki na kwa wakati.

Baadhi ya madaktari walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Dkt. Julieth Nkoubi wamekiri kuwa yatawaongezea ujuzi wa kufanya kazi kwa weledi zaidi na hivyo WCF kulipa fidia stahiki.

Mfuko wa WFC ulianza kutoa huduma kwa wafanyakazi wanaopata majanga kazini mwaka 2016 ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanzishwa, ukichukua nafasi ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo ilionekana kutotoa fidia stahiki kwa wafanyakazi waliopata majanga kazini.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kufanya tathmini sahihi kwa wanachama wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wanaoumia wakiwa kazini.
Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia Jumatatu Mei 22, 2023.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omar akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu WCF.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera ili kuwaongezea ujuzi wa kufanya tathmini kwa wafanyakazi wanaoumia kazini (kupata ajali, kuugua ama kufariki wakiwa kazini) ili kupata fidia stahiki na kwa wakati kutoka WCF.
Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia mafunzo hayo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Dkt. Julieth Nkoubi amesema mafunzo hayo ni muhimu na yatawasaidia kufanya tathmini kwa weledi zaidi kwa wafanyakazi wanaoumia kazini.
Daktari kutoka Hospitali ya Magai Kahama, Dkt. Peter Magai akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo ambao ni pamoja na kuwawezesha madaktari kufanya tathmini sahihi kwa wanachama wa WCF wanaoumia kazini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Madaktari walioshiriki mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 22, 2023






Share:

Sunday, 21 May 2023

MCHENGERWA ATOA MIEZI MIWILI KUKAMILISHA MKAKATI ACHIA SHOKA KAMATA MZINGA, AZINDUA MWONGOZO WA USIMAMIZI WA HIFADHI ZA NYUKI


Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka watendaji wa sekta ya Misitu na Nyuki kukamilisha mkakati wa kuongeza uzalishaji wa asali toka tani 35000 za sasa hadi tani 138000 katika kipindi cha miezi miwili alioupa jina la mkakati wa “achia shoka kamata mzinga” huku akitaka eneo la misitu na asali kufanyiwa utafiti wa kutosha ili litumike kama zao jipya la utalii.

Mhe Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 21, 2023 wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yaliyofanyika kitaifa katika Uwanja wa Bombadia mkoani Singida.

Akiwa kiwanjani hapo amezindua Mwongozo wa Usimamizi wa Hifadhi za nyuki, na vibanda maalum vya kuuzia asali pia ametoa Tuzo 5 za wadau wenye mchango mkubwa kwenye Sekta ya nyuki na ametoa vyeti kwa wanafunzi walioandika nsha nzuri kuhusu ufugaji wa nyuki.


Akisoma hotuba yake amesema pamoja na uwepo wa maeneo makubwa yaliyohifadhiwa na yanayofaa kwa ajili ya kuzalisha mazao ya nyuki yenye viwango bora vado takwimu zinaonesha uzalishaji ni 23% ikilinganishwa na uwezo uliopo wa kuzalisha tani 138,000 kwa mwaka.

Kutokana na hali hiyo Mhe. Mchengerwa ameelekeza Wizara ya Maliasili ishirikiane na Wizara ya Kilimo kuanzisha programu za matumizi ya makundi ya nyuki kwenye uchavushaji mimea ili tuweze kuongeza kiwango na ubora wa mazao yanayozalishwa.

Ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mfuko wa Misitu kuhakikisha wanawezesha wananchi hasa wale wanaopakana na maeneo ya hifadhi kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji nyuki pamoja na mizinga ya kisasa. Pia kushirikiana na wadau mbalimbali kuhamasisha jamii kupanda na kuitunza miti katika maeneo yao.

Aidha, amesema pamoja na Serikali kuweka jitihada kubwa kwenye kulinda na kuhifadhi maliasili, bado katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na kasi kubwa ya uharibifu wa maeneo yaliyohifadhiwa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu.

Akitolea mfano amesema mkoa wa Singida umebarikiwa kuwa na uoto wa kipekee ujulikanao kwa jina maarufu kama Vichaka vya Itigi (Itigi Thicket) ambao upatikana katika nchi mbili tu duniani, yaani Tanzania na nchi ya Zambia ambao katika kipindi cha miaka kumekuwa na kasi kubwa ya ukataji na uondoaji wa uoto huu kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu.

Hali hii imesababisha sehemu kubwa ya ardhi iliyokuwa na uoto huu kubaki wazi na pia kumebainika kuwepo kwa mimea vamizi pale ambapo uoto huu ulipoondolewa. Kutokana na hali hiyo ameielekeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha kuwa maeneo yote yaliyobaki ambayo yenye uoto huo yanatambuliwa na kuhifadhiwa kisheria, pia wananchi waliopo kwenye maeneo hayo wanapewa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira na ufugaji nyuki kibiashara.


Ameitaka TFS kuhakikisha vijiji vyote vya maeneo hayo vinakuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi na inatekelezwa ipasavyo.


Pia kutoa elimu kwa wafugaji nyuki ili waweze kutumia vifaa sahihi vitakavyoweza kuendeleza uhifadhi wa maeneo hayo.

Akizungumzia kuhusu zoezi la uwekaji wa mizinga nchi nzima Mhe Mchengerwa ametoa rai kwa wananchi kutumia wataalamu wa ufugaji nyuki waliokwenye maeneo yao kupata elimu sahihi ya namna ya kufuga nyuki kwa tija na kusisitiza wataalamu watoke maofisini na kwenda kuwahudumia wananchi.


Aidha amesema pamoja na faida nyingi tunazopata kutoka kwa mdudu nyuki bado nyuki anaweza kutumika kutupatia zao jipya la utalii ambapo amesema katika nchi ya Solvenia mdudu nyuki hutumika sana kwa ajili ya shughuli za utalii.


Amewataka wataalamu kuangalia namna watakavyoweza kupata sifa za kipekee za asali inayozalishwa hapa nchini ili tuweze kuitangaza Kimataifa ambapo ametoa wito kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine; pamoja na Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha kufanya utafiti huu.


Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akielekeza na kusisitiza kulinda Maliasili na kuendeleza utalii.


Aidha, amempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohammed Mchengerwa (Mb) kwa kutembea takriban nchi nzima kuhamasisha utunzaji wa maliasili, mazingira na uendelezaji utalii.


Share:

KAMATI TENDAJI YA PROJECT ECHO TANZANIA, YARIDHISHWA NA ONGEZEKO LA WASHIRIKI WA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO

Mwenyekiti Bi. Mary Mtui (wa kwanza kulia), akiendesha kikao cha Kamati Tendaji ya Project ECHO Tanzania, Dodoma. Katikati ni Mratibu wa Project ECHO Tanzania Bw. Jacob Lusekelo, ambaye pia ni katibu wa Kamati hiyo. Kulia ni Bw. Victor Muchunguzi, mshauri wa Mafunzo na Machapisho kutoka Mradi wa ECHO, Chuo Kikuu Mzumbe.

***

Kamati Tendaji ya “Project ECHO” Tanzania, iliyo chini ya Wizara ya Afya, imekutana Dodoma katika kikao chake cha 13, kilichofanyika katika Hoteli ya Morena na kuwakutanisha wadau mbalimbali katika Sekta ya Afya wakiwemo wataalamu kutoka TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wataalamu wa Maabara, wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya na wataalam kutoka mabaraza ya wataam (Professional councils), Chuo kikuu Mzumbe na wafadhili wa Mradi (CDC).

Kikao hicho kilifunguliwa na Mwenyekiti Bi. Mary Mtui, Msajili wa Baraza la Wataalamu wa Maabara akimwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali. Akizungumza katika mahojiano maalumu baada ya kikao hicho kumalizika, Bi Mary, amesema Kamati imefarijika kuona ongezeko la wataalamu wa afya wanaoshiriki katika mafunzo kwa njia ya mtandao, yanayotolewa katika vituo 9 (Hubs) zilizofungungiliwa nchini nzima.

“ Inatia moyo kuona idadi ya washiriki wa mafunzo inaongezeka kila siku, na hii inatokana na jitihada kubwa zilizofanywa na wataalamu wa Chuo Kikuu Mzumbe kupitia mradi wa Kuboresha mifumo ya Afya nchini unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia CDC. Kikubwa Mzumbe waongeze kasi ya kutoa CPD Points kwa washiriki” Alisema.

Amesema ongezeko hilo linatokana na kutolewa kwa “CPD point” zinazowaongezea washiriki nafasi ya kuhuisha leseni zao, na baadhi kupanda madaraja; na hivyo kuwataka Chuo Kikuu Mzumbe kuongeza kasi ya kutoa CPD points kwa wakati, ili kuongeza idadi wa washiriki wa mafunzo ambayo yamekuwa yana manufaa makubwa katika kuboresha utoaji huduma za Afya nchini.

Miongoni mwa mafunzo yanayotolewa kwa sasa ni pamoja na kliniki za “Adult HIV, Pediatric HIV, MDR TB, HVL, HIV LAB, Supply Chain na AMS/IPC ECHO”. Hadi kikao cha 13 cha mwaka cha Kamati ya Utendaji, inakadiriwa zaidi ya CPD pointi 1600 zimetolewa kwa watumishi wa afya ambao wamekuwa wakipata mafunzo kwa njia hiyo ya mtandao, huku zaidi ya watumishi na watoa huduma za afya 650 wakishiriki mafunzo nchini nzima kila wiki. Kwasasa Mzumbe kwa kushirikiana na MCT, wanaendelea kuchakata maombi mapya ya CPD’s zaidi ya 2600 kwa washiriki waliokidhi vigezo vya ushiriki kwenye mafunzo.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho, kimekusudia kujadili na kuweka mikakati ya namna ya kuongeza ushiriki wa wataalamu wa Afya katika mafunzo kwa njia ya mtandao “ECHO Platforms” pamoja kutolewa CPD point kwa wakati. Kwasasa mafunzo hayo yanaendeshwa kila wiki kupitia vituo 9 (hubs), na washiriki kufuatilia mafunzo hayo kupitia clinic (Spokes) zaidi ya 399 zilizofungiwa vifaa vya mafunzo nchi nzima.

Wakichangia mkutano huo, wadau wamepongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wadau wa maendeleo CDC, kwa kuwekeza katika mfumo wa mafunzo kwa njia ya mtandao; na hivyo kuwajengea uwezo wataalamu wa Afya wakiwa mahali pa kazi.

Akieleza mikakati zaidi ya Wizara; Mratibu wa Project ECHO Tanzania Bw. Jacob Lusekelo amesema, Wizara inakusudia kuendelea kushirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kupanua wigo wa mafunzo na usimamizi nchini katika kutoa mafunzo, miongozo na usimamizi wa wataalamu wa huduma za afya (immersion training).

Mkutano huo wa siku moja umefadhiliwa na Serikali ya Watu wa Marekeni, kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani katika kupambana na Ukimwi(PEPFAR) kipitia CDC na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Wizara ya Afya, TAMISEMI, wawakilishi kutoka Mabaraza ya Kitaaluma Tanzania, Chuo Kikuu Mzumbe, MDH, THPS, MNH na NBTS. Mradi huu kwa sasa unatekelezwa na Chuo Kikuu Mzumbe.
Bw. Victor Muchunguzi, mshauri wa Mafunzo na Machapisho kutoka Mradi wa ECHO, Chuo Kikuu Mzumbe akichangia jambo wakati wa mkutano.Bi. Osigele Oswald kutoka Wizaya ya Afya, akichangia jambo wakati wa mkutano wa Kamati Tendaji ya Project ECHO Tanzania.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Kamati Tendaji ya Project ECHO Tanzania, wakifuatilia kwa makini wasilisho wakati wa kikao kilichofanyika Hoteli ya Morena, Dodoma hivi karibuni.
Washiriki wa Mkutano wa Kamati Tendaji ya “Project ECHO” Tanzania, iliyo chini ya Wizara ya Afya, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho kumalizika, Dodoma hivi karibuni.
Share:

ONGEZA MAOKOTO UKICHEZA KASINO YA MTANDAONI

 

Ujio wa Meridianbet umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza malalamiko ya ukosefu wa ajira mitaani, kwa sasa vijana wengi wamekuwa wakijipatia kipato kirahisi kupitia ubashiri wa soka na kucheza kasino ya mtandaoni ya meridiannbet.

 

Kuna mchezo mmoja ni rahisi kupiga mtonyo leo nataka nikwambie, Expanse studio wametengenza Pia Premium unaupata kasino ya mtandaoni ya Meridianbet, ili kushinda fuata maelekezo haya:

 

Jinsi ya Kucheza Kasino ya Mtandaoni.

 

Pia Premium ni Mchezo unachezwa kwa mpangilio wa mistari 4×5, na ushindi wote hulipwa kutoka kushoto kwenda kulia isipokuwa kwa alama ya kutawanya ‘scatter’, ambayo hulipa kwa nafasi zote ikiwa idadi fulani ya alama za kutawanya zitakusanywa. Ikiwa na mistari 40 isiyobadilika, toleo hili ni mchezo unaolipishwa kulingana na uwezekano wa kushinda, mchezo huu ni maalum kwa wachezaji wa aina zote.

 

Mchezo huu wa Pia Premium wa kasino ya mtandaoni una Jackpot endelevu za aina tatu, ili ushinde moja ya Jackpoti hizi unapaswa kuzungusha mara kwa mara wakati ukicheza kasino ya mtandaoni. Kila mzunguko unakufanya kuingia kwenye droo ya Jackpoti mpaka pale mshindi atakapo patikana.

 

Bila kusahau mchezo huu una kipengele cha kubashiri (gamble), ambacho huwaruhusu wachezaji kuongeza faida maradufu kwa kukisia kama kadi ifuatayo itakuwa nyekundu au nyeusi. Huku alama ya Wild kwenye Pia Premium ina nafasi nyingi za kujishindia.

 

Kasino ya Mtandaoni kila siku inakuja na matoleo mapya na yenye kuburudisha wachezaji wakiwa mawindoni kusaka utajiri, unaweza kujisajili Meridianbet kama bado ili ufurahisie michezo mingi ya kasino ya mtandaoni na sloti za kijanja kabisa, zawadi ya ukaribisho utaipata kwa mizunguko mingi ya kucheza kasino ya mtandaoni bure.

 

Lakini pia ukiachana na Pia Premium kuna sloti nyingi za Roulette, na michezo ya kasino ya mtandaoni kama Aviator, Poker na mingine mingi inaweza kuongeza kipato chako kama tu utachagua kucheza kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.


Share:

MAYELE NOMAAA...SASA YANGA SC KUKUTANA NA AZAM FC FAINALI ASFC


NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga Sc imefanikiwa kutinga fainali Kombe la Shirikisho la Azam mara baada ya kuichapa Singida Big Stars 1-0 kwenye mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Liti mkoani Singida.

Yanga Sc iliweza kuwapa nafasi wachezaji wengi ambao mara nyingi wamekuwa hawaanzi kwenye mechi akiwemo Mauya, Doumbia, Mzize na mlinda lango Metacha Mnata.

Katika mchezo huo ambayo ilikuwa ya aina yake, timu zote zilitengeneza nafasi za magoli kipindi cha kwanza bila mafanikio, hivyo kwenda mapumziko matokeo yakiwa 0-0.

Yanga ilifanya mabadiliko kadhaa kwa baadhi ya wachezaji, wakaingia Fiston Mayele, Tuisila Kisinda, Dikson Job pamoja na Musonda mabadiliko hayo yalizaa natunda kwani Yanga ilianza kulisakama lango la wapinzani na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Fiston Kalala Mayele na matokeo kuwa 1-0.

Yanga Sc inaenda fainali ambapo inaenda kukutana na Azam Fc ambao walitinga hatua hiyo mara baada ya kuwaondoa Simba Sc.

Mechi hiyo ya Fainali itechezwa katika dimba la Mkwakwani Tanga hivi karibuni.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger