Sunday, 21 May 2023

WIZARA YA ARDHI BARA NA ZANZIBAR ZAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA ARDHI

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akibadilishana Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta ya ardhi na Dkt. Mngereza Mzee Miraji, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 20 Mei 2023.

*************

Na Munir Shemweta, WANMM

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na ile ya Makaazi Zanzibar pamoja na Taasisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na lile la Zanzibar (ZHC) zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi na Nyumba.

Hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa mwongozo wa ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Ofisi ya Makamu wa Pili SMZ kuhusu taasisi zisizo za muungano kukutana na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa majukumu yao na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utekelezaji majukumu yao.

Utoaji saini makubaliano hayo ya pande hizo ulifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anthony Sanga na yule wa Makaazi Zanzibar Dkt Mngereza Mzee Miraji wakati Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likiwakilishwa na Mkurugenzi wake Hamad Abdalah na lile la ZHC Mwanaisha Ali Said mbele ya Mawaziri wa wizara hizo Dkt Angeline Mabula na Rahma Kassim Ali

Maeneo yanayokwenda kutekelezwa katika ushirikiano huo ni kukusanya, kuchakata na kubadilishana taarifa za ardhi baharini, kubadilishana uzoefu kwenye maendeleo na matumizi ya mifumo ya habari na teknolojia kwa sekta ya ardhi pamoja na kuandaa na kutekeleza sera, sheria na miongozo mbalimbali ya sekta ya ardhi .

Maeneo mengine ni kushirikiana kitaalamu na kubadilishana uzoefu katika mfumo wa usimamizi na maendeleo ya sekta ya milki kuu inayojumuisha makaazi na nyumba, utafiti na maendeleo kwenye sekta ya ardhi, utatuzi wa migogoro ya ardhi pamoja na ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika usimamizi na maendeleo ya mji Mkongwe.

Akizungumza katika hafla fupi ya utiaji saini makubaliano hayo yaliyofanyika jijini Dodoma tarehe 20 Mei 2023, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema, makubaliano yaliyofikiwa yaingie katika utekelezaji nay awe fursa kwa kwa kila mmoja kuona namna ya kuboresha mahusiano katika sekta ya ardhi kwa kuwa, upande wa Tanzania Bara sekta ya ardhi ni wezeshi na inapofanya vibaya inakwaza sekta nyingine.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, changamoto anayoina ni kuwa makubaliano hayo yamechelewa sana kutokana na kila upande kuwa na mambo mazuri iliyofanya na kusisitiza ushirikiano huo utakuwa njia bora za kutatua migogoro lakini pia kuleta salama ya milki, ufanisi na kikubwa kuona namna ya kuisimamia sekta ya ardhi.

‘’Msisitizo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ni sekta ya ardhi kuwa kinara katika kuongoza na kuifanya ardhi kupangika vizuri na kuleta manufaa kwa wananchi. Sekta hii inaleta maisha bora na hatuwezi kuwa na maisha bora wakati kila siku kuna migogoro na hatuwezi kutoa fursa watu wawekeze’’ alisema Dkt Mabula

Ametaka makubaliano yaliyofikiwa yasimamiwe kwa vitendo sambamba na kuwa na vikao vya mara kwa mara vya ufuatiliaji na tathmini katika kutekeleza makubalinao.

Ametoa rai kwa makatibu wakuu kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa yanatekelezwa kwa kuwekewa utaratibu mahsusi sambamba na kusimamiwa kwa kuwa na vikao vya mara kwa mara ili kujua kinachoendelea.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Rahma Kassim Ally amesema, katika utekelezaji wa makubainao ipo haja kwa wataalamu kuweka mpango kazi utakaoainisha vitu vya kuanza navyo na iwapo zipo changamoto basi ziwasilishwe kwa mawaziri kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Amesema, makubaliano yaliyosainiwa yakifanikishwa serikali zote mbili za SMT na SMS zitakuwa zimepiga hatua kubwa sana na kuwafanya viongozi wake kuwa salama kwa kuwa wizara hizo zinahudumia na kutoa huduma bora kwa wananchi.

‘’Katika makubaliano haya sote tunabadilishana uzoefu lakini wenzetu mmetuzidi mtuone kama watoto, sisi tuna yetu na ninyi mna yenu ila mmetuzidi kwa hiyo tutakuwa tunahitaji msaada zaidi kwenu kuliko sisi’’ alisema Rahma Kassim Ally.



Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (nyuma kulia) na mwenzake wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Rahma Kassim Ali wakishuhudia utiaji saini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara hizo uliofanywa na makatibu wakuu wa wizara hizo kwenye hafla iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 20 Mei 2023.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Hamad Abdallah (Kulia) na mwenzake wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) Mwanaisha Ali Said wakionesha Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa mashirika hayo mara baada ya kusaini katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 20 Mei 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa utiaji saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara yake na ile ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 20 Mei 2023.
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Rahma Kassim Ali akizungumza katika hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara yake na ile ya Tanzania Bara iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 20 Mei 2023.
Sehemu ya washiriki katika hafla ya utiaji saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ile ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 20 Mei 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ile ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 20 Mei 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Share:

Saturday, 20 May 2023

NYUKI SAFARI YAPAMBA MAADHIMISHO YA SIKU NYUKI DUNIANI MKOANI SINGIDA, VIVUTIO VYA UTALII VYAPAA




Na Mwandishi Wetu-SINGIDA

Programu maalumu ya kuhamasisha Utalii wa Ndani maarufu kama 'Nyuki Safari' imefana kwenye Maadhimisho ya siku ya Nyuki Duniani mkoani Singida ambapo wadau wa Misitu na Ufugaji Nyuki wametembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo mkoani humo.

Programu hiyo mahsusi imeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuhamasisha Utalii wa ndani sambamba na kuunga mkono juhudi za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hasa kupitia Filamu Maarufu ya ' The Royal Tour'

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Mhifadhi Historia kutoka Mkoa wa Singida, Moses Msai amesema mkoa huo umebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambapo Wadau hao wamepata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vivyopo mkoani humo ikiwemo maeneo ya Malikale.

" Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yamechagiza vivutio vya utalii vya mkoani Singida kujulikana hivyo ni imani yangu kuwa ziara hii imeacha alama kubwa" amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Ufugaji Nyuki (TABEDO) Rudia Hamudu Issa aliyeshiriki ziara hiyo amesema ziara hiyo ni muhimu kwani imeutangaza mkoa wa Singida kiuwekezaji.

" Nimeifurahia sana ziara hii kwani Mimi na Wenzangu tumejifunza mengi, Singida imebarikiwa kuna vivutio vingi sana hasa vya Malikale" Amesema

" Tumeona Vivutio vya Malikale vizuri, Tumepata Historia ya Mtemi Senge Mughenyi ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa Wanyamapori Saadani, Haya ni mambo ambayo Watanzania wanatakiwa kuyafahamu na kuyaendeleza kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi cha baadae" amesema Hamudu

Katika ziara hiyo ya Wadau wametembelea maeneo mbalimbali ya vivutio ikiwemo eneo la Malikale la Bomani, eneo la Ziwa la Kitalii la Singidani, eneo la Makumbusho lililopo katika Chuo Kikuu Huria cha Singida, Jengo la Bohari ambalo kichwa cha Mwanamama aliyepigana na Wajerumani kwa kutumia Nyuki Maarufu kama Jengo la Bohari pamoja na Makazi ya Mtemi Senge Mughenyi, Kiongozi aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Wakazi wa Singida kwa ujumla

Share:

PROF.MKENDA AZINDUA MAONESHO YA PILI NACTVET JIJINI ARUSHA


Serikali imesema kuwa maonesho ya elimu yanayolenga kuunganisha Vyuo vya ufundi, juhudi za ubunifu, sayansi na teknolojia pamoja na shughuli za uzalishaji kuanzia sasa yatakuwa yakifanywa kwa pamoja.

Hayo yamesemwa na Waziri w Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Mei jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Pili ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET)

Prof. Mkenda ameongeza kuwa kuunganishwa kwa maonesho hayo kutasaidia wananchi kupata taarifa na huduma za elimu kwa wakati mmoja pamoja na kuwakutanisha waajiri na vyuo vinavyotoa mafunzo ili kuweza kufahamu soko la ajira linataka nini.

"Tutahakikisha maonesho haya yanaunganisha Vyuo vya ufundi, juhudi za ubunifu, sayansi na teknolojia pamoja na shughuli za uzalishaji na huduma kwa ajili ya kutengeneza uwezo wa kutambua mahitaji na kuimarisha utoaji mafunzo kwa vitendo kwa vijana wetu," amesema Prof. Adolf Mkenda.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko ameishukuru Wizara kwa kuishirikisha Kamati hiyo katika shughuli zote za Wizara na kuahidi kwamba itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mageuzi makubwa ya elimu yanayotarajiwa yanatokea.

Akizungumzia maonesho ya NACTVET Makamu Mwenyekiti huyo amesema kuwa maonesho hayo ni mazuri huku akiwataka wananchi kujitokeza kuona namna kazi kubwa ya ubunifu na ufundi zinazofanyika katika Vyuo na Taasisi mbalimbali zinazotoa mafunzo ya ufundi.

Naye mmoja wa wadhamini Deogratius Haule kutoka Geita Gold Mine amesema wataendelea kudhamini maonesho hayo ili vijana wa Vyuo vya kati na Taasisi mbalimbali zinazotoa mafunzo zipate fursa ya kuonyesha uwezo, vipaji na ubunifu wanaofanya na hivyo kuleta maana halisi ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu la Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt Adolf Rutayuga amesema kuwa nchi nyingi Duniani zinatambua kuwa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ni nyenzo muhimu katika kuchochea maendeleo ya viwanda, hivyo inapaswa kuzingatia umahiri wa kutenda na mahitaji ya soko la ajira kwa wahitimu.

Ameongeza kuwa ili kuwepo na elimu yenye tija inayojibu changamoto za jamii ni lazima kuwepo kwa ushirikiano kati ya watoa mafunzo na waajiri.

Maonesho ya Pili ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayoendelea jijini Arusha yameshirikisha zaidi ya Taasisi 200 zikiwa ni Vyuo vya elimu ya ufundi, ufundi stadi, Vyuo vikuu, Taasisi na Makampuni ya waajiri, wajasiliamali na vikundi mbalimbali vinavyofaidika na elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
Share:

MRINDOKO : HATUTAKUBALI KUONA MTU ANALETA MGOGORO CCM....TUKEMEE USHOGA, USAGAJI

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini imekemea makundi ndani ya chama na migogoro ikisisitiza kuwa kamwe haitakubali kuona mtu yeyote analeta mgogoro katika chama hicho.


Akizungumza leo Jumamosi Mei 20,2023 wakati wa ziara ya kamati hiyo katika kata ya Chamaguha, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko amewataka wanaCCM kupendana na kushikamana na kuwa na umoja ili kujenga chama.

“Naomba wanaCCM tupendane na kama hatutaelewana tutapoteza dola. Mkiona mtu analeta mgogoro, heri aondoke kuliko kupoteza dola, sisi tumezoea kuwa na dola hatuwezi kukubali dola ipotee. Mtu yeyote unayeona analeta longolongo ya kutaka tupoteze dola aondoke CCM”,amesema Mrindoko.

Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wazazi pia amekemea vitendo vya ushoga na usagaji katika jamii akisema hayo ni mambo ya aibu na ya ajabu hivyo kuwataka wazazi kusimama imara katika malezi ya watoto ili kukabiliana na mmonyoko wa maadili.


“Tuwalindeni watoto, tuwalindeni wajukuu zetu tuepuke tabia mbovu zinazoletwa na mataifa ya nje. Mtoto akirudi kutoka shule mkague maana dunia imeharibika. Tuwe makini kwa watoto wetu, tuwe makini kwa mabinti zenu mambo yameharibika. Huu mchezo ukiendelea tutakuwa na viongozi kweli?.

“Hawa wamama wanaosagana wametukosa sisi wanaume?? Mababa tupo akina mama msihangaike kusagana.  Eti wanaume wanalawitiana mna akili kweli”,amesema Mrindoko.


Naye Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi amewataka wanandoa kupendana na kushirikiana katika malezi ya familia.


“Kupigana siyo dili wanandoa pendaneni, furaha ya ndoa inatakiwa iwepo kila siku na tuachane na vitendo vya ubakaji na ulawiti ndani ya famila zetu.Ukiona babu anamuita mjukuu wake mke, shtuka , kwani wapo wababu wanawafanyia ukatili watoto”,amesema Kibabi.


“Tukemee ushoga , siku hizi unakuta mme wako kumbe naye ni mke wa mwanaume mwenzake, mambo ya ajabu sana haya, lazima tuyakemee”,ameongeza Kibabi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko ambaye ni diwani wa kata ya Chamaguha akizungumza kwenye kikao cha wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha



Share:

MERIDIANBET YAIFIKIA MABIBO BOYS NDANI YA MABIBO


 

Timu ya mpira wa miguu wa miguu ya Mabibo Boys inayopatikana Mabibo imefikiwa na wababe wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet ambao walipofika hadi ya mitaa ya Mabibo na kugawa vifaa vya michezo ambavyo ni jezi na mipira, Hii ni kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za vijana wa mtaani ambao wanapambana katika michezo.

Mkuu wa kitengo cha Masoko na mawasiliano kutoka Meridianbet Bwana Matina Nkurlu aliiongoza timu nzima ya ya kampuni hiyo mpaka kufika Mabibo na kugawa vifaa hivo, Kitu ambacho wamekua wakikifanya mara kwa mara kuhakikisha wanasaidia jamii ambayo inawazunguka pale ambapo itawabidi kufanya hivo.

Meridianbet wanaendelea kurudisha kwa jamii kila siku kwani kufanya hivyo ni kuwajali vijana hasa katika soka. Meridianbet “CHAGUA TUKUPE”.

Sub-Heading:

Pata mizunguko 50 ya bure kucheza sloti na michezo ya kasino ya mtandaoni ukijisajili na Meridianbet. Jisajili kupitia link hii

 

Bwana Matina Nkurlu alisema kuwa Meridianbet iliamua kuwafikia Mabibo Boys kwasababu,

“Meridianbet tunaamini michezo ni Afya na ni Ajira hivyo kuwapa vifaa  vya michezo ndugu zetu wa Mabibo Boys ni katika kuhakikisha vijana hawa wanakua na afya njema lakini pia kupata ajira kupitia michezo, na tunatoa wito kwa makampuni mengine kushiri kikamilifu kuvisaidia hivi vituo vidogo vya michezo ili kuzalisha watu wengi wenye mafanikio kwenye michezo”

Vilevile baada ya kupokea vifaa hivyo michezo katibu wa timu ya Mabibo Boys alisema “Kiukweli msaada huu umekuja wakati sahihi kabisa kwakua timu yetu ilikua na uhitaji mkubwa wa vifaa vya michezo na mipira hivyo hii itakua ni sehemu ya kutatua changamoto za timu kuelekea kwenye mashindano

 

Meridianbet imekua na utaratibu wa kutoa misaada katika sehemu mbalimbali bila kujali tasnia hii imekua ni kawaida kwao pale ambapo wataona jamii ina uhitaji wao wamekua mstari wa mbele kuhakikisha wanatoa msaada katika eneo hilo.

 Pia Meridianbet imeleta mchongo wa  hela kila siku. Kuna hii bonasi ya ukaribisho kwa wateja wapya wote wanapata Tsh 25,000/= ya kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Ingia mchezoni www.meridianbet.co.tz

Basi nakwambiaje pesa zipo hapa Meridianbet kama hujajiunga huu ndio muda sasa ingia na uweze kupata hiyo bonasi na ubashiri mechi zako kadhaa unazoamini kuwa zitakupa ushindi ndani ya Mabingwa wa ODDS KUBWA.

 Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.

Kampuni zingine ziige mfano kutoka Meridianbet kwa kurudisha kwa jamii kwani kuwaunga mkono vijana hasa katika soka itasaidia sana kuleta chachu ya maendeleo katika sekta ya michezo kwani vijana ndio Taifa la leo.

 

Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.

 

NB: Habari njema kwako, Meridianbet imesikia ombi la wengi imekuja na Jackpot kubwa ya mechi 13 kwa dau dogo la kuanzia 1,000/=TZS mshindi atajinyakulia donge nono la Tsh 85,000,000/= PIGA *149*10#

#MERIDIANBET CHAGUA TUKUPE



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger