Thursday, 18 May 2023

TCRA YAZIPIGA STOP MALULA TV, DELLAH ONLINE TV & MISALABA BLOG......DC SAMIZI ATAKA WAANDISHI WATUMIE VIZURI KALAMU ZAO


                    
                   Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) imeadhimisha Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ kwa kufanya mkutano na wadau wa vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga.


Maadhimisho hayo yamefanyika leo Alhamisi Mei 18,2023 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.


Mhe. Samizi amewapongeza waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kwa kazi nzuri wanayofanya katika utekelezaji wa majukumu yao huku akiwataka kutumia kalamu zao za vizuri.

“Wito wangu kwa waandishi wa habari tutumie kalamu zetu na matamshi yetu katika kuhabarisha ili habari iliyokusudiwa ifike kwa maksudi yaliyokusudiwa ikiwemo kuhabarisha na kuburudisha”,amesema Samizi.


“Nitoe rai kwa watu wanaopenda uandishi wa habari watambue kuwa uandishi wa habari ni taaluma siyo utashi tu wa kuandika hivyo kama wanamatamanio ya kuwa waandishi wa habari basi waende darasani kusoma”,ameongeza Mhe. Samizi.


Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Francis Mihayo amewataka watoa huduma za maudhui kuhakikisha wanazingatia sheria na kuwa na leseni za utoaji huduma za mawasiliano.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Francis Mihayo

“Niwaombe wale ambao wana Blogs na Online Tv ambazo hazina leseni muombe leseni, andikeni vizuri vichwa vya habari vizuri. Unakuta mtu hajasomea uandishi wa habari , hana taaluma na hawa leseni ya TCRA lakini anatoa huduma za maudhui, acheni hayo”,amesema Mihayo.


“Lakini hivi sasa tuna Wimbi la ku Copy na Ku Paste, unakuta habari imekosewa imesambaa kila chombo cha habari ikiwa na makosa yale yale, kuweni makini lakini pia nendeni shule,mkaongeze ujuzi kwani sheria inawataka msome. Hakikisheni mnazingatia sheria na mnafuata sheria”,amesema Mihayo.


“Waandishi wa habari msichanganye uandishi wa habari na siasa, uanaharakati. Kama unataka uanaharakati achana na uandishi wa habari, kama unataka siasa jipambanue achana na uandishi wa habari”,amesema.

Meneja huyo wa TCRA pia amewataka waandishi wa habari kuandika habari zenye tija na yeyote ambaye hana leseni akae pembeni.

Mhandisi Mihayo ametumia fursa hizo kuziagiza baadhi ya Blogs na Online TV ikiwemo Dellah Online Tv, Misalaba Blog na Malula TV kusitisha mara moja huduma za utoaji za maudhui mtandaoni mpaka pale watakapopata leseni kutoka TCRA.

“Kuanzia leo Dellah Online Tv, Malula Tv na Misalaba blog na wengine wote wanaotoa huduma bila leseni wasitisishe shughuli za kuchapisha habari. Kwanini mnanichokoza? Kuanzia sasa naagiza msitishe uchapishaji wa habari kwenye mitandao yenu mpaka pale mtakapopata leseni kutoka TCRA”,amesema Mhandisi Mihayo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
 Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Ali Lityawi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya habari ‘Media Day’ mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023


Share:

RAIS SAMIA ATEUA MAJAJI SITA WA MAHAKAMA YA RUFAA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewateua Majaji sita wa Mahakama ya Rufaa.


Amemteua Jaji Zainab Goronya Muruke kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Kabla ya uteuzi huo, Jaji Muruke alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi cha Mashauri ya Ndoa, Talaka na Mirathi - Temeke, Dar es Salaam

Amemteua Jaji Dkt. Benhajj Shaaban Masoud kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Masoud alikuwa Mkuu wa Shule ya Sheria Tanzania

Amemteua Jaji Amour Said Khamis kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Khamis alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora;

Amemteua Jaji Leila Edith Mgonya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgonya alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Masijala Kuu Dar es Salaam

Amemteua Jaji Gerson John Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mdemu alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma

Amemteua Jaji Agnes Zephania Mgeyekwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgeyekwa alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Uteuzi huo wa Majaji wa Mahakama ya Rufani umeanza tarehe 28 Aprili, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.
Share:

Wednesday, 17 May 2023

BENKI YA NMB KANDA YA KASKAZINI YAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA MKOANI TANGA

 



Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Praygod Godwin akizungumza na wafanyabiashara mkoani Tanga jana kuhusu namna walivyojipanga kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wafanyabiashara pamoja na ,kuwaelezea fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye benki hiyo kushoto n i Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga



Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa Halfa hiyo

Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa Halfa hiyo


Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe akizungumza wakati wa kikao hicho


Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe akizungumza wakati wa kikao hicho


Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe akizungumza wakati wa kikao hicho

Sehemu ya Washiriki wa Kikao wakifuatilia kikao hicho





Na Oscar Assenga,Tanga

BENKI ya NMB Kanda ya Kaskazini leo wamefanya kikao na wafanyabiashara mkoani Tanga (NMB Business Club) huku wakieleza kwamba wamekuwa wakitoa zaidi ya Bilioni 60 kila mwezi kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo hapa nchini

Hatua hiyo inatajwa kama juhudi za benki hiyo kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu kuwawezesha wajasiriamali wadogo wasogo ili waweze kujikwamua kiuchumi na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji maendeleo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho na wafanyabiashara ambao wanawahuduma na Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe ambapo alisema kwamba walianza kutoa mikopo hiyo kwa wajasiriamali tokea mwaka 2000.

Mashaga alisema kwamba hatua hiyo imewajengea uzoefu mkubwa namna ya kuwahudumia wajasiriamali hao na kwamba kutokana na utoaji wa mikopo hiyo umewawezesha kuongeza nguvu kwenye mitaji yao na hivyo kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Leo hapa Tanga tulikutana na wateja kuwaambia kitu gani wamekianzisha na wakifanye ili kuweza kuboresha huduma zao kwa sasa wana huduma waliyoanzisha kwa ajili ya wateja wanaofanya huduma kwenye masoko yanayosimamiwa vizuri na serikali yana vizimba na wateja wameandikishwa”Alisema

Alisema kwamba ili kuhakikisha nao wananufaika na mikopo hiyo wameanza kutoa mikopo kuanzia 100,000 mpaka 1000000 bila dhamana na baadae milioni 1 hadi 2 mteja anaweka dhamana na wana mikopo mengine zaidi ya hapo inakwenda mpaka Milioni 5 kwa wateja wao.

“Lakini pia tumeanzisha mikopo kwa ajili ya vijana wanaojihusisha na bodaboda ambapo kitu ambacho kinahitajika ni kujiandikisha kwenye vyama vyao ambavyo vinatambulika na serikali na yeye ni kutafuta asilimia 20 ya chombo anachokitaka akishapata benki inaongzekja kiasi kilichobaki ili kumpatia”Alisema Meneja huyo Mwandamizi wa mikopo NMB Makao Makuu.

Hata hivyo alisema kwamba baadae wanafanya biashara na kufanya marejesho kila wiki kumaliza deni kwa kipindi cha miezi sita hadi 12 mpaka watakapoikamilisha ili kuwezesha na wengine kunufaina nayo.

Awali akizungumza Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya NMB-Playgod Godwin alisema kwamba leo wamekutana na wafanyabiashara kuweza kutengeneza mtandao na kubadilishana uzoefu ikiwemo kuwapa mafunzo ya vitu mbalimbali na mwaka huu wamewafundisha vitu vitatu.

Alisema kikao hicho kilikuwa ni mahususi kuwakutanisha wafanyabiashara (Bussness Club) kuwakutanisha ili kuwaeleza kwamba mteja anatakiwa kuaangalia mfano anafanyabiashara ya usafirishaji anatumia petrol lakini dunia inabadilika magari mengi yanabadilika kwenye matumizi ya gesi na mama lishe anatumia mkaa lakini dunia ya leo wanatoka kwenye mkaa kwenda kwente gesi hivyo watawafundisha mbinu mbalimbali na mambo ya kurekodi taarifa za mapato na matumizi na umuhimu wake na wapo wataalamu wazuri.

Hata hivyo alisema pia wataalamu hao watawafundisha jinsi mfanyabiashara kuangaa ikitokea amepata changamoto za kiafya,uzee nani atasimamia biashara zake pia wataangalia namna ya kuwafudnisha katika mambo hayo muhimu.

Katika kikao hicho kiliwakutanisha wafanyabiashara 150 wa mkoa wa Tanga wenye matawi 12 kwa mkoa ambapo inaelezwa kwamba kitakuwa na tija kwa siku zijazo katika kuendeleza biashara zao na hatimaye kukuza mtaji wao.

Naye kwa upande wake Mfanyabiashara wa Hotel Celina Ndumbaro alisema kwamba alichojifunza katika mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kuweza kuona namna ya kufanya biashara zao kwa tija na kuweza kupata mafanikio.

Share:

WIZARA YA AFYA YAWATAHADHARISHA WANANCHI DHIDI YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU


Na Dotto Kwilasa, Dodoma.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tatizo la ugonjwa wa shinikizo la juu la damu nchini bado ni kubwa ambapo kwa wagonjwa waliotibiwa katika Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI)tangu ilipoanzishwa Septemba 2015 hadi Aprili 2023 kati ya wagonjwa 619,102 waliotibiwa asilimia 66 kati yao walikuwa na shinikizo la juu la damu.

Ameeleza hayo leo Jijini hapa kwenye maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu duniani ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Mei 17 na kueleza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kwa kila wagonjwa 10 wanaoumwa hospitalini hapo, wagonjwa 6 wana ugonjwa wa shinikizo la damu.

Amesema katika uchunguzi uliofanywa katika jamii kwenye mikoa ya Pwani, Arusha,Geita, Mtwara,Lindi, Zanzibar,Iringa na Dar Es Salaam takwimu zinaonesha watu 3 hadi 4 kati ya 10 wana shinikizo la damu la juu .

"Shinikizo la juu la damu ndio sababu kubwa ya kiharusi,shambulio la moyo,moyo kushindwa kufanya kazi,kutuna kwa kuta za mishipa ya damu ,moyo,uharibifu kwenye chujio za Figo,ganzi miguuni na mikononi,upofu na kupunguza nguvu za kiume,"amesema

Pamoja na hayo Waziri huyo wa afya amefafanua kuwa kwa takwimu za Tanzania kutoka mfumo wa ukusanyaji taarifa za afya zinaonesha kuwa jumla ya wagonjwa 2,535,281 walitibiwa magonjwa yasiyoambukizwa kwenye vituo vya afya kwa mwaka 2017.

Amefafanua kuwa wagonjwa hao wameongezeka hadi kufikia wagonjwa 3,440,708 Kwa mwaka 2021 ambapo ongezeko hilo wako wagonjwa 905,427 Kwa kipindi cha miaka mitano ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 9.4.

"Kati ya hao ugonjwa wa shinikizo la juu la damu ndio ulioongoza miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza ambapo waliongezeka Kutoka wagonjwa 688,901 Kwa mwaka 2017,hadi kufikia wagonjwa 1,345,847 kwa mwaka sawa na ongezeko la asilimia 95.4 katika kipindi hicho;

Kwa takwimu hizo inaonyesha kwamba wagonjwa Wenye shinikizo la damu wameongezeka takribani mara mbili zaidi Kwa kipindi cha miaka mitano,"alisema Waziri Ummy 

Kutokana na hayo Waziri Ummy alisema Serikali inaendelea na utekelezaji wa Sera ya afya ya mwaka 2007 ambayo inalenga kutoa huduma kwa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo shinikizo la damu Kwa umahiri zaidi.

Kwa upande wake Prof. Pasco lubajo Mkurugenzi wa kinga Wizara ya afya ametumia nafasi hiyo kuhimiza wananchi kubadili mtindo wa maisha Kwa kufanya mazoezi, kuepuka tabia bwete, kupunguza ulevi, matumizi ya tumbaku na bidhaa zake .

Prof.Lubajo ameutaja ugonjwa wa shinikizo la juu la damu kuwa unasababishwa na nguvu ya msukumo wa damu Katika mishipa kuwa kubwa kuliko kawaida Kwa muda mrefu ambapo ongezeko hilo huulazimu moyo kufanya kazi kupita kiasi.

Akieleza kipimo cha kawaida cha shinikizo la juu la damu alisema ni 100 hadi 140 milimita za zebaki upande wa kipimo Cha juu na milimita za zebaki 60 Hadi 90 upande wa kipimo cha chini.

"Kuna aina mbili za shinikizo la juu la damu ambazo ni asili na linalosababishwa na magonjwa mengine,kadiri ya asilimia 90 hadi 95 za watu wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu linalosababishwa na magonjwa mengine kama Figo,kisukari,mapafu na mfumo wa homoni,"amesema

Siku ya shinikizo la juu la damu duniani huadhimishwa Kila mwaka ifikapo Mei 17 ambapo kwa Tanzania kitaifa inafanyika mkoani Manyara huku kaulimbiu ya maadhimisho kwa mwaka huu ni Pima shinikizo la damu kwa usahihi,idhibiti ,ishi kwa muda mrefu .

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger