NA ANDREW CHALE
MWALIMU wa Dance na mcheza dance mjini Arusha ambaye picha zake zimekuwa gumzo mitandao kuanzia Aprili 29, 2023, Kilumbo Steven amefunguka juu ya uwezo wake wa aina mbalimbali ya 'break dance' akiwa amepiga picha akiwa kichwa chini na miguu juu akiwa na Mke wake wa ndoa pembeni.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mwandishi Andrew Chale, Break Dancer huyo kupitia mpango wake wa B Boy Kilumbo anasema kuwa amepata simu nyingi ikiwemo pia kuona wadau wakiposti picha zake hizo mitandaoni.
"Nimefanya densi ndani ya harusi yangu.
Lakini pia picha nyingi tulipiga sema hizo mbili za kusimama kwa kichwa chini ndo imesambaa zaidi mitandaoni, ila tumepiga picha nyingi " amesema Kilumbo.
Aidha, amefafanukuwa B Boy Kilumbo ni kwamba B imesimama kwenye Break, Boy imesimama kama yeye mwenyewe na Kilumbo ni jina lake.
"Watu wengi wameona picha zile lakini wamekuwa na maoni tofauti, Mie ni kijana ambaye nina malengo makubwa kupitia kipaji changu.
Nataka kuendeleza uwezo wangu huu na hata kuwarithisha wengine."Amesema Kilumbo.
Ambapo lengo kubwa ni kuanzisha Shule maalum ya Break Dance kwa vijana wote wa kiume na kike ilikuongeza vijana wengine zaidi.
"Hapa Tanzania najulikana kwa vijana wengi na nimekuwa nikiwafunza kwenye Break Dance.
Lakini pia nimekuwa nikishiriki mashindano tofauti, ikiwemo shindano la Hip-hop Hasili na mwaka juzi nilikuwa mshindi wa kwanza.
Pia nimekuwa nikifanya mashindano kwa njia ya mtandao 'Online' Marekani na pia nchi zingine hivyo kwa sasa malengo ni kuona nafika mbali na pia kuacha alama.
Kilumbo anasema kuwa, yeye ni Mngoni aliyeamua kufanya maisha yake Arusha ambapo pia mbali na kufanya Break Dance, lakini pia anajihusisha na masuala ya Utalii akifanya program ya 'Ngondi ya mtembezi' akitembeza Watalii maeneo mbalimbali.
Mwisho.