Thursday, 20 April 2023

TAASISI YA GOODWILL&HUMANITY FOUNDATION YALAANI NDOA ZA JINSIA MOJA


MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akizungumza wakati wa hafla ya Iftari aliyoaiandaa kwenye Kituo hicho

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Mwanaidi ambaye ni Afisa Tarafa wa Ngamiani Kati akizungumza

Msimamizi wa Casa Della Giaio Sista Consolata Mgumba akizungumza wakati wa halfa hiyo ambapo aliiasa jamii ipunguze ubinafsi na kurudisha moyo wa kujali kuwaangalia wengine na kuwajaali.






MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya futari

MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya futari

MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya futari






Na Oscar Assenga,TANGA

MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi amesema kwamba taasisi hiyo inalaani vikali ndoa ya jinsia moja ikiwemo vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wakina mama.

Muhdar alitoa kauli hiyo wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kueleza namna walivyopingana na vitendo hivyo na kuitaka jamii kutokubali kushiriki kwenye mambo hayo

Alisema kwamba wanataka kuiambia dunia kwamba taasisi hiyo ina laani ndoa za jinsia moja na inakemea vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikifanywa kwa watoto na wakina mama kwa kuitaka jamii kubadilika na kuachana navyo.

“Taasisi hii tuna laani ndoa za jinsia moja na hatuviungi mkono kwani sisi ni moja ya huduma tunazotoa ni kuhifadhi watoto waliopotea na waliofanyiwa ukatili na Tuna Afisa Ustawi maalumu wa kuambatana na maafisa wa serikali kuwapelekea mahakamani wanaowafanyia ukatili watoto wenye kesi zinayowakandamizi watoto tunaokuwa nao kwenye makazi yetu”Alisema

“Kwani tumekuwa tukipokea watoto wamekatwa masikio,watoto wamekatwa mikono,wamemiminiwa nailoni iliyochomwa moto,waliocopmwa midomoni ,waliovuliwa nguo na kumiminiwa nailioni na kuwababua ngozi hizo ni changamoto kubwa wanazokumbana nazo watoto”Alisema

Aidha alisema kwamba wao wanaungana na kauli ya Serikali ya kukataa ukatili dhidi ya watoto na leo wametoka kuiambia dunia ukatili dhidi ya watoto haiwezekani ikiwemo ndoa ya jinsia moja haikubaliki na hawapo tayari kuwa na taifa ambalo limejaa mashoga na lenye wanawake wasagaji .

“Tumewaita kuja kufuturu pamoja ni kuthamini mchango wenu kwenye taasisi hii ambayo imeundwa kwa lengo la kusaidia mayatima,wazee, walemavu na makundi yasiyojiweza”Alisema

Awali akizungumza Msimamizi wa Casa Della Giaio Sista Consolata Mgumba aiasa jamii ipunguze ubinafsi na kurudisha moyo wa kujali kuwaangalia wengine na kuwajaali.

“Tujiulize watoto yatima kwanini zamani hayakuwepo familia tuacha kukimbia maajukumu yetu na tuwapeleka watoto kwenye vituo hivyo ikiwa hakuna msaada wowte kwenye jamii kwani wana jamii zao “Alisema

Aidha aliwataka wazingatie maadili huku akieleza kwamba mambo ya ushoga inatokana na wakina mama kutokutaka kuishi na wanaume badala yake wanalea watoto pekee yao na hivyo kuwajenga watoto kwenye mitazamo isiyosawa hivyo wao wataendelea kulipigia kelele jambo hilo.

Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa iftari hiyo Mwakilishi wa Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Mwanaidi ambaye ni Afisa Tarafa wa Ngamiani Kati alitoa wito kwa wazazi na walezi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili kwenye jamii zao kutokana na kwamba hali sio nzui

Mwanaidi alisema kwamba wazazi watoe taarifa na wae na kauli kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili kwenye jamii

Share:

JAMAA AMPA TALAKA MKEWE KISA KUDHARAU NDUGU NA MARAFIKI..."HADI MAMA YANGU ANAMUITA MCHAWI"


Mwanaume mmoja raia wa Ghana ametahamaki baada ya kufunguka kuhusu ndoa yake iliyofeli na aliyekuwa mkewe.

Akizungumza katika mahojiano na SVTV Africa kwenye YouTube, Agyei Mensa ambaye anaishi nchini Sweden alisema sababu kubwa iliyomfanya aondoke kwenye ndoa yake ya awali ni kutokana na tabia mbaya ya mkewe.

Akitafakari kwa kina, mlofa huyo alisema sifa moja ambayo hakuipenda kwa mke wake ni jinsi alivyowadharau jamaa na marafiki zake. 

Alieleza kuwa mke wake wa zamani hakuona kosa kuwatusi ndugu zake, marafiki na hata mama yake.

Alitaja jinsi mke wake wa zamani alivyokuwa na kiburi hadi kumshutumu mamaake kuwa mchawi ingawa ndiye aliyemshauri amuoe. 

“Mamangu ndiye alinishauri nimuoe mke wangu wa zamani lakini cha kushangaza baada ya kufunga ndoa mtazamo wake ulibadilika, ilifikia hatua anaweza kuwatukana ndugu, binamu na marafiki zangu waliokuja kunitembelea wakati wowote nikiwa Ghana. Wakati fulani alimuita mamaangu mchawi hivyo niliamua jambo bora zaidi kwangu ni kuvunja ndoa."

Aliongeza "hata nilikuwa nikitayarisha hati zake ili ajiunge nami Sweden ili tuishi kama familia yenye furaha, lakini mtazamo wake uliharibu kila kitu." 

Agyei Mensah alisema pamoja na kwamba ana mtoto wa miaka mitatu na mke wake wa zamani, anakusudia kumruhusu akue nchini Ghana ili apate malezi bora.
Share:

DC LUDIGIJA AWATAKA WAKAZI WA WILAYA YA KWIMBA KUHAKIKISHA WANALALA KWENYE VYANDARUA






Mkuu wa wilaya ya KwimbaJijini Mwanza Ng'wilabuzu Ludigija amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanalala kwenye vyandarua viilivyoyolewa na serikali ili kujikinga na ugomjwa hatari wa Malaria kwasababu ni miongoni mwa Magonjwa yanyasababisha vifo vingi 

Ludigija ametoa maelekezo hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la kugawa vyandarua vyenye viatilifu zaidi ya elf 12 katika mpango wa serikali wa kudhibiti Malaria Kwa watoto wadogo wenye umri chini ya mwaka mmoja na Kwa Makundi Maalumi kama vile Wajawazito wazee wenye umri miaka 60 na kuendelea, watoto wenye umri chini ya miaka 5 wanapoenda kutibiwa malaria, wanaoishi na Virusi vya Ukimw na wanaolazwa kutokana na malaria

Vyandarua hivi vitatolewa kwa mzunguko wa miaka miwili kwa makundi hayp na vina nembo ya MSD ikiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita katika mpango wake wa kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030 na kuongeza umiliki wa vyandarua kwa jamii angalau 80%.

Aidha Amewasihi kuachana na Imani potofu juu ya vyandarua hivyo vinavyotolewa bure na serikali kwasababu Ina lengo la kuwalinda wananchi wake dhidi ya ugonjwa wa Malakeria hivyo amewataka wakazi hao kuwapuuza wanaojaribu kupotosha kuhusu vyandarua hivyo.


Share:

BWANA WANGU ANAFAIDI ASALI NA KANIFUNGULIA BIASHARA KIBAO

Nimedharaulika kwa kuachika kwenye ndoa yangu na kutelekezwa kwenye maisha magumu pamoja na watoto wadogo wawili maisha yangu hayakuwa na mwanzo kila nilipofikiri niliuona mwisho mbaya mume wangu aliniacha na kutukimbia familia bila ya kutoaa taarifa yoyote.


Baada ya kuzunguka na kuamua kuuza kisamvu mitaani nilizoea kazi japokuwa hali ya Shelui Singida haikuwa nzuri ilinigharimu nipambane kwa ajili ya wanangu tu.


Katika harakati zangu za kupambana siku mmoja nilipeleka mboga zangu huko singida mjini kwa oda maalumu nikiwa njiani narudi nilikutana na mwaume mmoja Rukubanshamba aliyenisimamisha kidogo tukaongea kwa muda mfupi kiasi alitaka nambari zangu nikampa tukaachana.


Siku chache alinipigia na kunitaka nipeleke mboga kwa oda tena huko Itigi kwani ndiko anakoishi nilipeleka na kwa kweli kupitia yeye nilipata wateja wengine wengi wakazini kwake.


Sikumjua vizuri Ruku lakini niliziona dalili zote za yeye kuvutiwa na mimi, mwanaume alifanya hivyo akanitongoza na kuniambia kuwa yeye ni mume wa mtu lakini amenipenda sana na anataka niwe wake wa kimya kimya, nami nilimwambia kuwa nimetelekezwa na watoto kwake hilo hakujali tukaanza mahusiano.


Safari hii sikutaka kabisa kumpoteza mwanaume yoyote ambaye alikuwa tayari kuwa na mimi kwani nilikuwa nimekwishapitia msoto mkubwa sana wa kulea watoto mwenyewe tena kwa kubangaiza.

Nilimjulisha dada yangu naye akaniambia sasa ni wakati wa kuwa makini na wanaume tena haswa hawa wanaume wa watu, akaniambia anasikia fununu zinazomzungumzia daktari BAKONGWA akisifiwa sana kwa tiba zake akanipa tovuti zake https://bakongwadoctors.com kusudi nimjue kiundani.


Na mimi sikusita nilipotembelea huko nikachukuwa nambari zake za whatsapp +243990627777 nikanakiri kisha nikampigia nikamuelekeza kila nililopitia na hali ya mahusiano niliyo nayo kwasasa, Alinipatia dawa ya kutumia kwa wakati ninapokutuna na Ruku, nilitumia dawa kwa siku mbili baada ya hapo nilimuona mwanaume kaongeza mapenzi na kunipangia nyumba jirani na ofisini kwake tena akanifungulia mradi wa kuku nikaanza kuuza kuku wa kienyeji na wakisasa wengi huku sikusahau biashara yangu ya kisamvu nikaiboresha zaidi.

Daktari Bakongwa ninasema asante sana sikuwahi kufikiria kama maisha yangu yatarudi kuwa yenye furaha tena kama hivi lakini kwako hili limewezekana.


Share:

Wednesday, 19 April 2023

WAJASIRIAMALI ZAIDI YA 300 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA USALAMA NA AFYA MKOANI MTWARA


Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Agness Hokororo (aliyesimama) akifungua mafunzo ya usalama na afya kwa wajasiriamali wa Mkoa wa Mtwara katika Wilaya ya Tandahimba yaliyowasilishwa na Meneja wa OSHA Kanda ya Kusini, Bw. Wilbert Ngowi (wa kwanza kushoto)
Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Agness Hokororo akizungumza na wajasiriamali wa Wilaya ya Tandahimba wakati wa mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kwa wajasiriamali hao
Wajasiriamali wa Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara wakifuatilia mada ya masuala ya usalama na afya mahali pa kazi inayowasilishwa na Meneja wa OSHA Kanda ya Kusini, Bw. Wilbert Ngowi (mbele)
Meneja wa OSHA Kanda ya Kusini, Bw. Wilbert Ngowi (mbele) akifafanua kuhusu faida za kuzingatia masuala ya usalama na afya mahali pa kazi kwa wajasiriamali Mkoani Mtwara.

*******************

Na Mwandishi Wetu

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani yatakayofanyika Aprili 28, Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakishirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mtwara wametoa mafunzo ya usalama na afya kwa wajasiriamali ziadi ya 300 Mkoani humo kwa lengo la kuwajengea uelewa wa kukabiliana na vihatarishi vya ajali na magonjwa katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza na wanahabari wakati akihitimisha mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika katika wilaya za Mtwara Mjini, Mikindani na Tandahimba, Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Agness Hokororo amesema kuwa mafunzo hayo yatawaongezea tija wajasiriamali hao pamoja na kuwapunguzia gharama za uendeshaji wa maeneo yao ya kazi.

“Elimu hii ya masula ya usalama na afya itawaongezea tija wajasiriamali hawa kwa kiasi kikubwa sana pindi watakaporejea katika shughuli zao, pia itawaepusha dhidi ya ajali na magonjwa yanayoweza kuwakumba katika meneo yao ya kazi na kuwasababishia gharama kubwa za uendeshaji wa miradi yao hivyo basi niwasihi wajasiriamali wote waliopata mafunzo haya kuhakikisha wanazingatia ipasavyo miongozo ya usalama na afya waliyofundishwa kwani kutokufanya hivyo kunaweza kuathiri mlolongo mzima wa shughuli zao za uzalishaji” alisema Mhe. Agness Hokororo.

Kwa upande wake Meneja wa OSHA wa Kanda ya Kusini ambaye pia ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Bw. Wilbert Ngowi amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya kampeni ya kuelekea katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi yatakayo adhimishwa Aprili 28 Mwaka huu huku akiamini kuwa wajasiriamali hao wataitumia ipasavyo elimu hiyo katika kuboresha mifumo ya usalama na afya katika maeneo yao ya kazi.

“OSHA imeona ni vyema katika kipindi hiki tunachoelekea katika maadhimisho ya usalama na afya mahali pa kazi Duniani tuwe na mafunzo haya kwa wajasiriamali kwasababu nao ni sehemu ya uzalishaji mali na katika maeneo yao ya kufanyia kazi wanakumbana na vihatarishi vingi na wengi wao hawakuwa na uelewa mzuri juu ya namna sahihi ya kukabiliana na vihatarishi hivyo, tunaamini kuwa vikundi hivi vilivyonufanika na haya mafunzo vitakuwa chachu ya mabadiliko ya kiusalama katika maeneo mbalimbali ya kazi” alisema Bw. Ngowi.

Aidha Wajasiriamali hao kutoka vikundi mbalimbali Mkoani humo wanaeleza namna ambavyo elimu hiyo itawaletea manufaa katika shughuli zao za kila siku.

“Kabla ya kupata mafunzo haya tulikuwa hatujui namna sahihi ya kufanyakazi zetu kwa kuzingatia miongozo ya usalama na afya lakini sasa tumejifunza vitu vingi na kufahamu kuwa hata eneo kazi lisilofanyiwa usafi au lisilo na mpangilio mzuri wa vifaa linaweza kuwa chanzo cha ajali na magonjwa” alisema Bi.Eva Mhilu

Nae Bi.Rose Luhongo ambaye ni Mjasiriamali katika Wilaya Tandahimba amewasihi wajasiriamali wenzake kufanyakazi kwa tahadhari na kwa kuzingatia sheria na miongozo ya usalama na afya

“Tukifanya shughuli zetu kwa kuzingatia taratibu zote tulizoelekezwa kupitia mafunzo haya basi tunaweza kudumu na kuwa na nguvu kwa miaka mingi sana lakini tusipozijali afya zetu na kukiuka taratibu hizi basi tunaweza kupatwa na magonjwa au ajali zitakazotusababishia ulemavu ambao unaweza kukwamisha shughuli zetu za kiuchumi” alisema Bi. Rose.

Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi hufanyika tarehe 26 hadi 28 mwezi Aprili kila mwaka na katika mwaka huu 2023 yanatarajiwa kufanyika Kitaifa Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku, Kauli mbiu ya maadhimisho ni ; Mazingira Salama na Afya ni Kanuni na Haki ya Msingi Mahali pa Kazi.
Share:

JAMAA ATUPWA JELA MIAKA 30, VIBOKO 6 KWA KUMPIGA MTAMA NA KUMBAKA BIBI


Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Lindi imemhukumu Said Mohamed (49) mkazi wa chikonji Lindi, kifungo cha miaka 30 jela sambamba na adhabu ya viboko 6 na kulipa fidia ya shilingi laki tano kwa kosa la kumbaka bibi wa miaka 62 katika kijiji cha Chikonji manispaaa ya Lindi.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi mfawidhi Maria Batulaine ambapo imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 130(1)(2)(a) na 131(1) cha kanuni ya Adhabu

Inaelezwa kwamba mtuhumiwa alimvizia na kumpiga mtama bibi huyo nyakati za saa 11 Alfajiri wakati ambao bibi huyo alikuwa akielekea shambani na kumbaka.

Upande wake mtuhumiwa ameiambia mahakama kuwa hajatenda jambo hilo hivyo sheria izingatie suala lake kwani amesingiziwa. Huku jopo la mashahidi wanne ambao ni mtaalamu wa Afya (Daktari), mwenyekiti wa kijiji, mgambo aliyeshiriki kumkamata mtuhumiwa na mtendwa mwenyewe, wamekiri kutokea kwa tukio hilo

Baada ya Hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 30 jela, adhabu ya viboko 6 na kumpa fidia ya shilingi laki 5 mtendwa hakimu Maria Batulaine ametoa nafasi kwa mtuhumiwa kukata rufaa.

Share:

MLINZI ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KURUHUSU KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE



Muharami Hassan Nayonga

Mahakama ya wilaya ya Kilwa imemhukumu Muharami Hassan Nayonga, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na hatia ya kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na watu mbalimbali.


Muharami ambaye ni mlinzi wa SUMA JKT na mkazi wa Kata ya Masoko, alikamatwa Aprili 13, 2023, baada ya kumshawishi kwa kutumia simu, kijana anayefahamika kwa jina la Zalafi Selemani ili aweze kumuingilia kinyume na maumbile.

Baada ya kukamatwa, mtuhumiwa alichunguzwa na wataalamu wa Afya ambao walibaini kuwa kijana huyo hushiriki ngono kinyume na maumbile.

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na kukiri makosa yake na ndipo jamhuri ilipomhukumu kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo ya kesi namba 27 ya mwaka 2023 imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Carolina Mtui, ikiwa ni baada ya kumkuta na hatia juu ya kosa hilo ambalo lipo kinyume na kifungu namba 154, kifungu kidogo cha kwanza, sheria ya kanuni ya Adhabu, sura namba 16.

Share:

TET YAZINDUA MAABARA YA TEHAMA NA KUKABIDHI VIFAA VYA MRADI WA KLIC 2022


Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo tarehe 18/4/2023 imekabidhi vifaa vya kielektroniki kutoka nchini Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 (Korean e-learning Improvement Cooperation 2022) pamoja na uzinduzi wa maabara ya TEHAMA kwa shule ya Msingi Tegeta "A" ya jijini Dar es salaam.

KLIC 2022 ni programu ya mafunzo yaliyotolewa na nchi ya Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa njia ya mtandao kwa walimu 20 wa shule ya msingi Tegeta A.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET , Dkt. Aneth Komba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya Elimu nchini ambapo ameeleza kuwa walimu katika shule hiyo wataweza kutekeleza kwa urahisi kazi ya ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya kieletroniki.

Dkt Komba amewataka walimu hao kuhakikisha wanaleta matokeo chanya ambayo yatasaidia katika uboreshaji wa elimu.

"Mkayatumie mafunzo vizuri na vifaa hivyo mlivyokabidhiwa kwa kuleta matokeo chanya na tuone ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa Tegeta A" ,Amesema Dkt.Komba.

Tukio hilo liliambatana na kukabidhi vishikwambi 20 kwa walimu walioshiriki programu ya mafunzo hayo.

Kwa upande wake , Mwalimu Mkuu wa shule ya Tegeta A Bwana. Alistides Ntakire ameshukuru kwa mafunzo hayo pamoja na vifaa vilivyotolewa ambapo amesema ana imani yataleta tija katika shule yake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Bwana Yassin Marijan ameshukuru kwa kuzinduliwa maabara hiyo ya TEHAMA na kukabidhiwa vifaa vyote huku akieleza kuwa atahakikisha vinatumika ipasavyo katika kuboresha elimu.

Vifaa vilivyokabihiwa ni pamoja na 'UPS 26,computure Monitor 25, system Unit 25,Wirless keyboard 35,projector moja, scanner moja,printer moja, wireless mouse 35, headphone 25, electric blackboard moja ,webcamera 26,digital podium moja,wired keyboard 25, ,wired mouse 25,speaker 26,adapter 49 na usb flash disk 50'



Share:

KARIBU TARIME VOCATIONAL TRAINING COLLEGE KWA FANI ZITAZOBADILISHA MAISHA YAKO

 


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 19,2023































Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger