Tuesday, 18 April 2023

Picha : KANISA LA WASABATO LAFUTURISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU SHINYANGA...WAKEMEA USHOGA, USAGAJI NA UKATILI , WAOMBEA NCHI



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu (Nyanza Gold Belt) limewafuturisha Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni Mwendelezo wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo viongozi wote wa dini wametumia fursa hiyo kuiombea nchi ya Tanzania amani, utulivu na mshikamano pamoja na kuombea viongozi wa taifa wakiongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Hafla hiyo ya Futari iliyoandaliwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando imefanyika leo Jumanne Aprili 18,2023 katika Hoteli ya Karena Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando ametumia fursa hiyo kukabidhi zawadi ya Mbuzi na Mchele kwa ajili ya Eid kwa Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya pamoja na Vitabu vya ‘Jipatie Amani ya Moyo’ kwa Sheikh huyo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.


Akizungumza wakati wa Iftar hiyo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando amesema Kanisa la Waadventista Wasabato linaamini juu ya mahusiano baina yao na wenza walio katika dini mbalimbali, madhehebu mbalimbali ya Kikristo lakini pia linaamini katika mahusiano na hata wale wasiomjua Mungu kwa sababu ni binadamu wenzao


 "Kwa hiyo kwa muktadha huo kwa kutambua kwamba wenzetu, ndugu zetu Waislamu wamekuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na sisi tunafurahishwa sana kwa kuona kujitoa kwao katika kumtafuta Mwenyezi Mungu ndani ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ikizingatiwa kuwa wamekuwa wakikisisitiza umoja nasi tunafurahishwa na hilo",amesema Askofu Sando.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati wa Hafla ya Futari.

"Mwezi huu Waislamu wanaamini kuwa mioyo yao katika Mwezi huu inachipuka upya na baada ya hapa wanaenda kuendeleza maisha ya uadilifu katika jamii na kwa sababu hiyo kwa sababu kanisa la Waadventista Wasabato tunaamini katika hayo ambayo Waislamu wanayaamini tukaona basi ni vyema katika kipindi hiki tuandae Iftar hii iwe ni sehemu ya kusema nyinyi ni ndugu zetu lakini iwe sehemu ya kuungana nanyi kumuomba Mwenyezi Mungu ili aweze kutupa amani katika maisha yetu, jamii zetu, taifa letu la Tanzania na kuomba Mwenyezi Mungu amjaalie Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wa nchi hii amani ya bwana itawale. Tutakiane heri, Baraka za bwana ziwe juu yenu",amesema Askofu Sando.


Askofu huyo amesema Kanisa la Waadventista Wasabato linaungana na Waislamu na ameomba wawe kitu kimoja kulaani kabisa vitendo viovu vinavyoendelea katika ulimwengu hasa vitendo vya Ushoga na Usagaji na vitendo vingine ya ukatili yakiwemo mauaji ili kuwa na jamii na taifa lenye amani.

Kwa Upande wake Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya amelipongeza na kulishukuru Kanisa la Waadventisa Wasabato kwa kuandaa Futari hiyo akisisitiza kuwa hilo ni jambo la heri na wasisite kuandaa tena.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu.

“Sisi ni ndugu wa damu moja, hivyo leo ndugu wamefuturishana. Jambo hili la sisi Waislamu kukaribishwa na ndugu zetu kwa ajili ya chakula ni jambo adhimu sana. Naomba jambo hili ambalo limehudhuriwa pia na viongozi wa Serikali liendelee kwani lina manufaa makubwa. Umoja huu ni mzuri na unapendeza kwani hapa tunatengeza umoja, mshikamano, upendo na ushirikiano”,amesema Sheikh Makusanya.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amelipongeza na kulishukuru Kanisa hilo kuandaa futari huku akitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa dini kukemea vitendo vya ukatili wa aina zote akieleza kuwa inaleta taswira mbaya mkoa wa Shinyanga kuwa na sifa ya matukio ya ukatili.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani leo Jumanne Aprili 18,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Viongozi wa Dini ya Kiislamu wakichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando
Viongozi wa Dini ya Kiislamu wakichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 
Viongozi wa Dini ya Kiislamu wakichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando (kushoto), Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Hamis (kulia) wakipata futari






heikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiomba dua wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akiomba wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya (kulia) Vitabu vya ‘Jipatie Amani ya Moyo’ 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya (kulia) Vitabu vya ‘Jipatie Amani ya Moyo’ 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya  zawadi ya Mbuzi na Mchele kwa ajili ya Eid
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akishikana mkono na Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya ishara ya kukabidhi zawadi ya Mbuzi na Mchele kwa ajili ya Eid
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) Vitabu vya ‘Jipatie Amani ya Moyo’.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

 
Share:

MSHINDI WA KAMPENI YA SIMBANKING AKABIDHIWA GARI AINA YA TOYOTA CROWN


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Kimweri (mwenye kanzu) akimkabidhi mshindi wa kampeni ya Benki ni SimBanking, Mayani Yahaya Hassan mkazi wa Dodoma funguo ya gari baada ya kuibuka kidedea katika droo iliyochezwa mapema mwezi huu. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Benki ya CRDB ambao walishiriki katika hafla hiyo ya kukabidhi gari kwa mshindi iliyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 14 Aprili 2023. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Kimweri (wapili kulia) na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati, Chabu Mishwaro (kulia) wakishuhudia mshindi wa kampeni ya Benki ni SimBanking, Mayani Yahaya Hassan mkazi wa Dodoma akikata utepe kama ishara ya kukabidhiwa gari baada ya kuibuka kidedea katika droo iliyochezwa mapema mwezi huu. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Benki ya CRDB ambao walishiriki katika hafla hiyo ya kukabidhi gari kwa mshindi iliyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 14 Aprili 2023.

============ =========== ===========


Benki ya CRDB imekabidhi gari aina ya Toyota Crown kwa mshindi wa kampeni ya “Benki Ni SimBanking” kwa mwezi Februari na Machi anayejulikana kwa jina la Mayani Yahaya Hassan mkazi wa Dodoma.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi huyo iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, Dodoma, Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya CRDB, Chabu Mishwaro alisema mshindi huyo alipatikana katika droo ya kwanza ya kampeni hiyo iliyofanyika tarehe 6/04/2023.

“Mayani ni moja ya wateja ambao wamekuwa wakitumia SimBanking kufanya miamala yao ya kifedha, jambo ambalo lilimpelekea kuingia katika kinyang’anyiro cha ushindi, na kuibuka kidedea baada ya droo kuchezeshwa,” alisema Chabu.

Chabu alibainisha kuwa katika kusaidia jitihada za Serikali za kuchochea uchumi wa kidijitali nchini, kampeni ya “Benki Ni SimBanking” imekuwa ikihamasisha wateja kufanya miamala kidijitali kupitia SimBanking na kuachana na matumizi ya pesa taslimu.

Akielezea kampeni hiyo inaendeshwa, Chabu alisema kampeni ya “Benki Ni SimBanking” inaendeshwa kwa muda wa miezi 10 hadi Desemba 2023, ambapo kila siku wateja wamekuwa wakijishindia zawadi, huku pia kukiwa na zawadi za mwezi, miezi miwili, na zawadi kubwa ya Toyota Vanguard ambayo itatolewa mwishoni wa kampeni.

“Hadi kufikia sasa tayari tumeshatoa zawadi mbalimbali ikiwamo pesa taslimu, simu janja, na laptop kwa washindi 79. Zawadi bado zipo nyingi sana, hivyo niwasihi wateja na wale wasio wateja waendelee kufanya miamala kupitia SimBanking ili waweze kujishindia,” alisema chabu huku akiwakaribisha wale ambao sio wateja wa Benki ya CRDB kufungua akaunti ili waunganishwe na SimBanking.

Akikabidhi zawadi hiyo ya gari kwa mshindi, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Kimweri aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa kampeni hiyo ambapo alisema sio tu inachochea matumizi ya mifumo ya kidijitali ya utoaji huduma, bali pia inachochea ujumuishi wa kifedha kwa wananchi.

Kimweri alisema Serikali imekuwa ikitilia mkazo katika matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma kwa wananchi ili kuendana na kasi ya maendeleo kote duniani, hivyo aliwasihi wateja na wananchi kutoa ushirikiano kwa Benki ya CRDB na kushiriki katika kampeni hiyo ya “Benki ni SimBanking”.

“Nimefurahi kuona Dodoma tumetoa mshindi katika kampeni hii, inaonyesha ni namna gani wananchi wa Dodoma wanaendelea kujenga uelewa juu ya umuhimu wa matumizi ya mifumo ya kidijitali ya kibenki. Niwasihi na wananchi wengi tujenge utamaduni wa kutumia mifumo hii si tu kwasababu ya zawadi bali tufanye hivyo tukitambua huko ndipo dunia ilipo sasa hivi,” aliongezea.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo Mayani Yahaya Hassan aliishukuru Benki ya CRDB kwa zawadi hiyo ya gari huku akibainisha siri ya ushindi ni kujenga utamaduni wa kutumia SimBanking kufanya miamala yake yote ya kifedha.

“Ninafurahia sana kufanya miamala kupitia SimBanking iliyoboreshwa, imekuwa rahisi na nafuu sana kutumia. Sasa hivi miamala yangu yote nakamilisha kupitia SimBanking, iwe kufanya malipo kupitia CRDB Lipa Namba, kutuma pesa, kulipia bima, kulipia kodi na kutoa fedha kwa CRDB Wakala/ ATMs na Tawini bila ya kadi,” alibainisha Mayani.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 18,2023




Share:

BENKI YA EXIM YAANDAA HAFLA YA FUTARI DODOMA NA TANGA,VIONGOZI WA DINI,SERIKALI WAGUSWA

Maofisa wa Benki ya Exim Tanzania akiwemo Mkuu wa kitengo cha Hazina na Masoko ya Dunia Bw Nelson Kishanda (katikati) wakikabidhi msaada wa chakula na mahitaji muhimu kwa mmoja wa wananchi wenye uhitaji jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuwa karibu zaidi na wateja wake katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw Hashim Mgandilwa (wa tatu kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga Sheikh Juma Luwuchu (kushoto)
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu ( wa tatu kushoto) sambamba na wageni waalikwa akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw Hashim Mgandilwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga Sheikh Juma Luwuchu wakipata futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed abbas akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wageni wengine waalikwa waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa kitengo cha Hazina na Masoko ya Dunia Bw Nelson Kishanda (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa chakula na mahitaji muhimu kwa wananchi wenye uhitaji jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuwa karibu zaidi na wateja wake katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya wageni waalikwa wakipata futari wakati hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Rasilimali watu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Fredrick Kanga akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw Hashim Mgandilwa (wan ne kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga Sheikh Juma Luwuchu (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya Exim wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu ( wan ne kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Hafla zote mbili zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Na.Mwandishi Wetu-Tanga na Dodoma

Benki ya Exim Tanzania imehitimisha rasmi zoezi la uandaaji wa futari kwa wateja wake katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar, Dodoma na Tanga kwa msimu huu wa mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani huku wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, viongozi wa dini na serikali wakionyesha kuridhishwa na utaratibu wa benki hiyo wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalum katika mwezi huo.

Katika kuhitimisha zoezi hilo ilishuhudiwa viongozi waandamizi wa serikali na dini katika mikoa ya Tanga na Dodoma wakishirikiana na viongozi waandamizi wa benki hiyo akiwemo Afisa Mtendaji Mkuu Bw Jaffari Matundu pamoja na Mkuu wa Rasilimali watu wa Benki hiyo Bw Fredrick Kanga katika kuongoza hafla mbili tofauti zilizoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wenye imani ya Kiislam katika mikoa hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Sambamba na hafla hizo benki hiyo pia kupitia Mkuu wake wa kitengo cha Hazina na Masoko ya Dunia Bw Nelson Kishanda pamoja na baadhi ya wateja wake iliweza kukabidhi msaada wa chakula na mahitaji muhimu kwa familia zenye uhitaji kupitia taasisi ya Maawal Islamic ya jijini Tanga, zoezi ambalo liliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw Hashim Mgandilwa aliemuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, sambamba na Sheikh Mkuu wa Mkoa huo Sheikh Juma Luwuchu.

Wakizungumza kwenye matukio yote mawili ya jijini Tanga DC Mgandilwa pamoja nae Sheikh Luwuchu walionyesha kufuruhishwa na mtazamo wa benki hiyo wa kutokutazama mwezi wa Ramadhani kama ni mwezi wa kujenga mahusiano na wateja wao pekee bali pia kuutumia vyema mwezi huo kwa kuyakumbuka makundi yenye uhitaji bila kujali kama si wateja wa benki hiyo.

“Hiki kinachofanywa na benki ya Exim ni mfano haswa wa kuigwa. Wangeweza tu kukutana na wateja wao na kufuturu pamoja lakini wameona kitendo hicho pekee hakitoshi kuuheshimisha mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani hivyo wameona ni vema wawakumbuke pia wenye uhitaji maalum. Kupitia Taasisi ya Maawal Islamic wameweza kukabidhi futari kwa watu wenye uhitaji…hongereni sana,’’ alipongeza DC Mgandilwa.

Akizungumzia matukio hayo Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu alisema ni muendelezo wa utaratibu wa benki hiyo kwa zaidi ya10 miaka sasa ikilenga kujumuika na wateja wake kama hatua ya kuonyesha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema benki hiyo inaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba wake kupitia mfungo na kufanya maombi.

“Kwetu sisi mwezi huu tunautazama kiimani zaidi ndio sababu tunazama makundi yote wakiwemo wateja wetu pamoja na watu wenye uhitaji maalum. Tumeweza kuandaa matukio kama haya mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar na leo tunakamilisha na mikoa ya Tanga na Dodoma.’’

“ Zaidi tutaendelea kutoa zawadi za Sikukuu ya Eid al-Fitr katika maeneo mengine pia. Lengo ni wote tufurahie mwezi huu muhimu huku pia tukikumbushana kufanya kilicho chema mbele za Mungu wetu.” Alisema Matundu.

Hafla zote mbili zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger