Monday, 17 April 2023

SHUWASA YAWAFUTURISHA WADAU WA MAJI SHINYANGA, DC SAMIZI ATAKA VIONGOZI WA DINI KUTILIA MKAZO MAADILI


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) ambayo inatoa huduma katika Manispaa ya Shinyanga na Miji ya Didia, Tinde na Iselamagazi halmashauri ya Shinyanga imewafuturisha Wateja na Wadau wa SHUWASA Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa utamaduni wa Mamlaka hiyo kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoishiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Hafla ya Futari imefanyika leo Jumatatu Aprili 17,2023, katika ofisi za SHUWASA na imekuhudhuriwa na wateja na wadau wa SHUWASA wakiwemo Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Buhangija kilichopo Mjini Shinyanga ambapo SHUWASA pia imekabidhi zawadi kwa watoto hao.


Akizungumza wakati wa Iftar hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ambaye alikuwa mgeni rasmi ameishukuru na kuipongeza SHUWASA kuandaa Futari hiyo huku akiwaomba viongozi wa dini na jamii kuungana kupiga vitendo vya ukatili katika jamii.

“Vitendo vya ukatili ukiwemo ubakaji na vimeongezeka katika jamii, ni jukumu la kila mmoja wetu kupiga vita ukatili lakini pia kuhakikisha tunawalea watoto wetu ili kulinda maadili yetu na kuepuka mmomonyoko wa maadili kwa matendo maovu yanatupa taswira mbaya. Naomba viongozi wa dini mtilie mkazo suala la maadili ili tulinde jamii”,amesema Mhe. Samizi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akichukua Futari.

Akikabidhi zawadi ya sabuni, mafuta ya kupikia, sukari na juisi zilizotolewa na SHUWASA kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga, Mkuu huyo wa wilaya amesema ni jambo jema kwa kila mwananchi pale anapopata chochote kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji.


Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi amesema SHUWASA imekuwa na utamaduni wa kuandaa Futari kwa ajili ya wateja na wadau kutokana na kwamba waumini wa dini ya kiislamu ni sehemu ya wadau muhimu wa SHUWASA.

Amewaomba wananchi na wadau wote wa maji kuendelea kushirikiana na SHUWASA katika kulinda miundombinu ya maji sambamba na kutoa taarifa mbalimbali ili kuboresha huduma ya maji.
Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Kategire na viongozi wa dini ya kiislamu na wadau wakichukua Futari.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya amewashukuru wadau wote walioshiriki katika futari hiyo na kuahidi kuwa SHUWASA itaendelea kuboresha zaidi huduma zake.


Naye Katibu wa Kamati ya Amani Wilaya ya Shinyanga Sheikh Shaban Katundu ameishukuru SHUWASA kuandaa Futari hiyo na kwamba viongozi wa dini ya kiislamu wataendelea kushirikiana na SHUWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) leo Jumatatu Aprili 17,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Katibu wa Kamati ya Amani Wilaya ya Shinyanga Sheikh Shaban Katundu akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
 Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mfanyakazi wa SHUWASA Kimbira Mtebe akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Viongozi wa dini ya Kiislamu wakiomba dua wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Viongozi wa dini ya Kiislamu wakiomba dua wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  akichukua Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  akichukua Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Kategire na viongozi wa dini ya kiislamu na wadau wakichukua Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  akichukua Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney akichukua Futari
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) akipata Futari
Waumini wa dini ya kiislamu na wadau wakichukua Futari
Waumini wa dini ya kiislamu na wadau wakichukua Futari
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija na wadau wakichukua Futari
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija na wadau wakichukua Futari
Wadau wakichukua Futari

Wadau wakichukua Futari
Wadau wakichukua Futari
Watoto wakipata Futari
Wadau wakipata Futari



Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi zawadi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi zawadi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga
Zawadi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga

Wafanyakazi wa Benki ya NBC wakipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi 
Wadau wakipiga picha ya kumbukumbu 
Meneja wa Benki ya CRDB Luther Mneney akibadilishana mawasiliano na mkazi wa Shinyanga Bw. Issa Mkondo (kushoto).

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

SHABIKI WA YANGA AFARIKI KWA PRESHA SIMBA SC IKIIKANDA YANGA KWA MKAPA


Baadhi ya wananchi waliofika msibani kwa Jeni


Shabiki wa Yanga aliyejulikana kwa jina la Jane, mkazi wa Kata ya Bwilingu wilayani Chalinze mkoa wa Pwani, amepoteza maisha wakati akiangalia mchezo wa jana wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga.


Imeelezwa kuwa alipatwa na presha na kuanguka ghafla.

Mechi ya jana Aprili 16, 2023, Simba waliondoka na ushindi wa magoli mawili kwa nunge dhidi ya Yanga.

SIMBA SC  iliendelea kupunguza gape la Pointi dhidi ya Yanga SC na kuendelea na mbio za Ubingwa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba SC walianza kwa kasi ya ajabu na mnamo dakika ya 2 Beki Kisiki Henock Inonga aliwanyanyua mashabiki wake akifunga bao safi kwa kichwa akimalizia Krosi ya Shomari Kapombe.

Baada ya kupata bao hilo Simba waliendelea kuishambulia Yanga na dakika ya 32 Kiungo mshambuliaji aliyekubalika kwa mashabiki Kibu Denis alipigilia msumari wa pili kwa shuti kali lililomshinda Diarra.


Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 63 na kupunguza gape la Pointi na kubaki alama tano huku kila timu ikibakiwa na mechi nne Ligi imalizike.


Yanga wanabaki na Pointi zao 68 ili wawe mabingwa wa Ligi msimu huu wanahitaji kushinda mechi tatu ili wafikishe Pointi 76 ambazo Simba akishinda mechi zake zote atakomea pointi 75 .
Share:

NHC KUJENGA JENGO LA KISASA LA KIBISHARA MANISPAA YA KAHAMA


Meneja wa Shirika la Nyumba (NHC) Angelina Magazi (kushoto) akimkabidhi nyaraka mbalimbali ikiwemo ramani ya ujenzi wa jengo la kisasa la kibiashara linalojengwa katika eneo la kiwanja cha shirika hilo kilichopo eneo la uwekezaji la Bukondamoyo , Halmashauri ya Manispaa ya Kahama anyepokea ni Mhandisi Mburuga Matamwe na Mshauri wa mradi wa Shirika Godfrey Mkumbo na kulia anayeshuhudia ni mkandarasi Mhandisi Masumbuko Majaliwa na kushoto ni Msanifu wa mradi NHC ,Robert Kintu.
Mshauri wa mradi wa Shirika la Nyumba Tanzania ( NHC) Godfrey Mkumbo akiwaonesha eneo mradi wa ujenzi wa jengo la kisasa linalojengwa eneo la uwekezaji la Bukondamoyo , Halmashjauri ya Manispaa ya Kahama , litakalokuwa na vyumba vya maduka vya kisasa, Migahawa, Super Market , sehemu ya kuosha magari , wengine ni meneja wa NHC mkoa wa Shinyanga , Angelina Magazi, meneja Mradi wa NHC , Mhandisi Mburuga Matamwe na Msanifu wa Mradi NHC ,Robert Kintu.
Msanifu wa Mradi wa NHC Robert Kintu wa katikati akiwaonesha maafisa wa NHC ramani ya ujenzi wa jengo la kisasa litakalokuwa na vyumba vya maduka 84 , Migahawa, Super Market na eneo la kuonsha magari ambalo linajengwa katika eneo la uwekezaji lililopo Bukondamoyo , Manispaa ya Kahama.
Meneja wa NHC wa mkoa wa Shinyanga , Angelina Magazi wa katikati akiongoza maafisa wa Shirika hilo katika mradi wa ujenzi jengo la kisasa litakalokuwa na vyumba vya kisasa vya maduka , migahawa , super market , sehemu za kuonya magari ambalo mradi huo umeanza kutekelezwa katika eneo lao la Bukondamoyo , Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Msanifu wa Mradi wa NHC ,Robert Kintu wa ujenzi wa jengo la kisasa katika eneo la uwekezaji la Bukondamoyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama unaotekelezwa na shirika hilo ambalo jengo hilo litakuwa na vyumba vya kisasa vya maduka 84 , Super Market , Migahawa na sehemu ya kuonya magari akiwaonesha maafisa wa NHC ramani ya mradi huo ulioanza kutekelezwa wilayani Kahama


Na Patrick Mabula , Kahama .


Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) limeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la kisasa katika eneo la uwekezaji lililopo Bukondamoyo katika Halamashauri ya Manispaa ya Kahama kwenye eneo lake ambako wanajenga vyumba vya kisasa vya maduka , migahawa, Super Market pamoja na sehemu ya kuoshea magari.


Akiongea katika eneo la mradi huo leo, Meneja wa Shirika la Nyumba wa Mkoa wa Shinyanga , Angelina Magazi amesema mradi huo umeanza kutekelezwa katika kiwanja cha shirika hilo kilichopo eneo la viwanda la Bukondamoyo maarufu kwa jina la Dodoma Manispaa ya Kahama.


Magazi amesema NHC katika mradi huo kutakuwa na vyumba vikubwa vya kisasa vya maduka vipatavyo 84, Migahawa, Super Market na sehemu ya kuosha magari na watapangisha kwa wateja watakao kidhi masharti kwa gharama nafuu kwa lengo la kusaidia ajira kwa watu.


Meneja Mradi wa Shirika la Nyumba Tanzania , Mhandisi Mburuga Matamwe amesema ujenzi wa mradi huo wa majengo ya kisasa ni uwekezaji mkubwa unategemea kugharimu kisasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja na tayari mapema utekelezaji wake umeshaanza.


Mshauri wa mradi huo , Mhandisi Godfrey Mkumbo amesema ujenzi wa jengo hilo litakalokuwa na vyumba vikubwa vya maduka vya kisasa utekelezaji wake unatarajia kukamilika katika kipindi cha miezi sita ijayo na hiyo itakuwa ni fursa kwa watu kupangishwa kwa gharama nafuu.


Kwa upande wake mkandarasi wa mradi huo , Mhandisi Masumbuko Majaliwa amesema tayari ameanza utekelezaji wa maradi huo na kuahidi kukamilisha ndani ya kipindi atakachokuwa amepewa kadri ya mkataba unavyosema.

Naye Msanifu wa mradi huo Arch Robart Kintu amesema mradi huo upo eneo zuri lililopo karibu na stendi ndogo ya magari ya abiria ya Bukondamoyo , katika eneo la viwanda la Manispaa ya Kahama ambapo watu watapata fursa ya kujiajiri na pale utakapokamilika katika kipindi cha miezi sita na utachochea maendeleo katika manispaa ya Kahama.


Share:

MFUNGWA AFARIKI KWA KUSHAMBULIWA NA KUNGUNI WENYE NJAA KALI GEREZANI


Familia moja nchini Marekani inataka uchunguzi wa uhalifu ufanyike kuhusu kifo cha jamaa wao aliyefariki akiwa jela baaa ya kudaiwa kung'atwa na kunguni.


LaShawn Thompson, 35, alipatikana akiwa amefariki katika seli chafu ya jela baada ya kuliwa akiwa hai na kunguni mnamo Septemba 2022.

Wakili wa familia hiyo alitoa picha zinazoonyesha mwili wa Thompson ukiwa umejaa kunguni. 

“Jela alilowekwa Thompson halikufaa hata kwa mnyama mgonjwa. Hakustahili kutendewa hili,” ilisoma taarifa ya wakili huyo kwa vyombo vya habari.


Kulingana na ripoti ya Mkaguzi wa Matibabu wa Kaunti ya Fulton, Thompson alipatikana akiwa hana fahamu akiwa jela miezi mitatu baada ya kukamatwa.

 Alithibitishwa kufariki kufuatia majaribio ya polisi wa eneo hilo na wafanyikazi wa matibabu kutaka kumuamsha, kwa mujibu wa ripoti ya USA Today.

 Wakili Harper anasema rekodi za jela zinaonyesha maafisa wa kizuizini na wafanyikazi wa matibabu waligundua kuwa Thompson alikuwa akidhoofika lakini hawakufanya chochote kutoa msaada au kumsaidia vinginevyo.


“Mwili wake ulipopatikana mmoja wa maafisa wa kizuizini alikataa kumfanyia CPR kwa sababu kwa maneno yake ‘alichanganyikiwa.’ Jela alilowekwa Thompson halikufaa hata kwa mnyama mgonjwa. Hakustahili hili.” 

Ripoti ya mchunguzi wa matibabu ilisema kulikuwa na “uvamizi mkali wa kunguni” katika seli yake katika wodi ya wagonjwa wa akili lakini akaongeza hakuna dalili za wazi za kuonyesha kwamba alipata mfadhaiko wa akili kwenye mwili wa Thompson. 

Picha za kutisha zilizoambatanishwa na taarifa ya Harper zinaonyesha seli ya Thompson, ambayo ni chafu mno.


Moja ya picha hizo zinamuonyesha Thompson, ambaye uso na kiwiliwili chake vinaweza kuonekana vikiwa vimefunikwa na wadudu. 

Ripoti ya mchunguzi wa afya wa Kaunti ya Fulton inaorodhesha sababu ya kifo cha Thompson kama haijabainika lakini anabainisha kulikuwa na "uvamizi mkali wa kunguni" kwenye seli yake.

 Kulingana na mtaalamu wa wadudu katika Chuo Kikuu cha Kentucky, ambaye ni mtaalamu wa kunguni, kuumwa na kunguni kwa kawaida hakusababishi kifo.


Hata hivyo, katika baadhi ya matukio nadra, Potter alisema, kuwa katika mazingira ya mrundiko wa kunguni kwa muda mrefu kunaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini yaani anemia kali, ambayo inaweza kuwa mbaya ikiwa haitatibiwa.
Share:

JAMAA ASABABISHA MSONGAMANO WA MAGARI BAADA YA KURUSHA MAMILIONI YA FEDHA BARABARANI


Mwanaume mmoja kutoka Oregon amesababisha msongamano wa magari kwa kurusha rundo la pesa kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi. 

Tukio hilo lilitokea kwenye barabara kuu ya I-5 mjini Eugene katika jimbo la Oregon, Marekani.

Kulingana na Fox 2, walioshuhudia tukio hilo walisimamisha magari yao na kukimbilia kuchukua kima cha $100 (KSh 13,000) zilizotawanyika kando ya barabara. 

Watu kadhaa walipiga simu kuarifu maafisa wa polisi wa Jimbo la Oregon kuhusu tukio hilo.

 Polisi waliwasiliana na mtu huyo, Colin Davis McCarthy, mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Eugene, ambaye alisema kuwa alitaka kutoa pesa hizo kama zawadi na kukadiria kuwa alitoa $200,000 sawa na takribani Milioni 460 za kitanzania

Japo hapakuwa na njia ya kudhibitisha kiasi halisi cha pesa kilichotolewa.

Ukarimu wa McCarthy ulisababisha msongamno mkubwa wa magari na hivyo kuwachochea maafisa wa usalama kumkanya kutupa pesa nje ya dirisha lake. 

McCarthy alitii na kukubali kuacha kurusha pesa barabarani. 

Jamaa wa McCarthy waliwaambia polisi kwamba hiyo ilikuwa tabia yake ya kawaida na kwamba alipata pesa hizo kwa kutumia akaunti ya benki ya pamoja ya familia yake, na kuwaacha bila senti.

"Madereva wanaosimama kando ya barabara kuu na kuingiza trafiki ya watembea kwa miguu kwenye barabara kuu huleta hatari kwa waendeshaji magari na watembea kwa miguu wenyewe," Kapteni Kyle Kennedy alisema. 

Aliongeza: “Njia za dharura zimekusudiwa kwa ajili ya dharura, hivyo kuegesha magari pembezoni mwa maeneo hayo si salama kwa ujumla, tunawaomba wananchi waepuke eneo hilo ili kuepusha hali ya hatari na pia kwa sababu hatuamini kuwa hakuna kitu kinachoweza kutokea kwa wakati huu."
Share:

NAIBU KAMISHINA TIRA APONGEZA MKAKATI WA BENKI YA CRDB KUCHOCHEA UJUMUISHI WA BIMA KUPITIA CRDB WAKALA

Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Khadija Said (watatu kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya “10 na Kitu” ya Benki ya CRDB inayolenga katika kuadhimisha miaka 10 ya huduma za CRDB Wakala. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Wateja Wago na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul (Wapili Kushoto), Mkuu wa Kitengo cha CRDB Wakala, Ericky Willy (watatu kuli), Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al Barakah, Rashid Rashid (wakwanza kuli), Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya CRDB, Badru Idd, na Meneja wa Ubora na Udhibiti wa Viatarishi TIRA, Zakaria Muyengi.Picha zote na Othman Michuzi.
Dar es Salaam 17 April 2023 – Ikitimiza miaka 10 tokea uanzishwaji wa mfumo wa utoaji huduma wa CRDB Wakala, Benki ya CRDB leo imetangaza kuanzisha huduma za bima kupitia mawakala wake ikiwa ni mkakati wa kusaidia jitihada za Serikali kukuza ujumuishi wa bima nchini.


Mkakati huo umepongezwa na Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Khadija Said, akisema utakwenda kusaidia kufanikisha lengo la Serikali la kuongeza ujumuishi wa bima kutoka asilimia 15 hivi sasa kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.


“Natambua kuwa Benki ya CRDB ndio kinara kwa idadi ya Mawakala katika sekta ya benki ikiwa na CRDB Wakala zaidi ya 25,000 nchi nzima. Kwa idadi hii nidhahiri kuwa kasi ya ufikishaji na ufikiaji wa huduma za bima itakwenda kuongezeka kwa Kiasi kikubwa,” alisema Naibu Kamishina TIRA huku akiwataka mawakala kufuata miongoz iliyowekwa.


Naibu Kamishina pia aliipongeza Benki ya CRDB kwa mapinduzi makubwa ambayo imeyafanya katika sekta ya fedha nchini katika kipindi cha miaka 10 ya CRDB Wakala. Alisema CRDB Wakala imetoa mchango mkubwa katika kufikisha huduma za fedha kwa wananchi.
Aidha, alipongeza Benki hiyo kwa kuboresha huduma zinazopatikana kupitia CRDB Wakala ambapo sasa hivi wateja wanaweza kupata zaidi ya asilimia 95 ya huduma kupitia mfumo huo ikiwamo huduma ya kufungua akaunti zote za benki ikiwamo akaunti za Al Barakah zinazofuata misingi ya sharia.

“Niwapongeze pia kwa uzinduzi wa kampeni ya ‘10 na Kitu’ ambayo inakwenda kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma zinazotolewa kupitia CRDB Wakala ikiwamo huduma za bima. Niwaombe Mawakala tukashiriki kikamilifu”, aliongezea Naibu Kamishna.
Akielezea kuhusu kampeni ya “10 na Kitu”, Mkurugenzi wa Wateja Wadogo, na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul alisema mbali na kusherehekea maiaka 10 ya CRDB Wakala, kampeni hiyo pia inalenga katika kuhamasisha Mawakala kuongeza kasi ya utoaji huduma kwa kufanya miamala mingi zaidi ili kuchochea ujumuishi wa kifedha.

“Kila mwezi tutakuwa tukitoa zawadi kwa CRDB Wakala ambao watakuwa wamefanya miamala mingi, kufungua akaunti nyingi, na kuuza huduma za bima. Jumla ya zawadi zote katika kampeni hii ni Pikipiki 40, Bajaji 5 na gari aina ya Toyota Alphad kwa mshindi wa jumla,” alibainisha.
Katika kipindi cha maiaka 10, CRDB Wakala imekuwa na mchango mkubwa katika ufikishaji wa huduma za Benki ya CRDB kwa wateja. Bonaventura alisema kuwa takwimu za Benki hiyo zinaonyesha kuwa hivi sasa CRDB Wakala inatoa huduma za kifedha kwa Watanzania zaidi ya milioni 3 kwa mwezi ambapo asilimia 40% ni wateja wa Benki hiyo na asilimia 60 ni wananchi wengine.

Pamoja na mafaniko hayo, taarifa za utendaji za Benki ya CRDB zinaonyesha zaidi ya miamala milioni 100 yenye thamani ya shilingi Trilioni 50 imekua ikifanyika kupitia CRDB Wakala kwa mwaka. Lakini pia, CRDB Wakala imetoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 35,000.




Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd akuzungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya huduma za CRDB Wakala iliyoenda sambamba ya uzinduzi wa kampeni ya “10 na Kitu” ya Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbu wa. Golden Memory, Sinza jijini Dar es salaam leo.



Mkuu wa Kitengo cha CRDB Wakala, Erick Willy akuzungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya huduma za CRDB Wakala iliyoenda sambamba ya uzinduzi wa kampeni ya “10 na Kitu” ya Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbu wa. Golden Memory, Sinza jijini Dar es salaam leo.



Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Barakah, Rashid Rashid akuzungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya huduma za CRDB Wakala iliyoenda sambamba ya uzinduzi wa kampeni ya “10 na Kitu” ya Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbu wa. Golden Memory, Sinza jijini Dar es salaam leo.















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger